Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, August 31, 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA IV NA VI KUPANGWA KI-GPA

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limetangaza mfumo mpya wa upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa kutumia wastani wa pointi (GPA) ambao utaanza kutumika katika mtihani wa kidato cha nne 2014 na cha sita 2015.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema kuwa mfumo huo umekuwa ukitumika katika kupanga madaraja ya ufaulu katika baadhi ya mitihani inayosimamiwa na baraza hilo.
Alisema manufaa yake ni kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa ina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu; matokeo yaliyo katika mfumo huo kwenye cheti yatarahisisha kazi ya udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na NACTE katika ngazi za juu za mafunzo.
Pia aliongeza kuwa mfumo wa GPA ni rahisi kuelewa kwa wadau wa kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na GPA kubwa ndiye aliye na maokeo mazuri.
Kwa mujibu wa Dk. Msonde, madaraja katika mfumo wa GPA hupangwa katika utaratibu wa Distinction, Merit, Credit na Pass ambapo daraja la juu ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass.
Kulingana na utaraibu huo, daraja la Distinction litakuwa na alama kati ya 3.6-5.0, Merit 2.6.3.5,Credit 1.6-2.5, Pass 0.3-1.5 na Fail 0.0-0.2 kwa matokeo ya kidato cha nne wakati wa kidato cha sita Distinction ni kati ya 3.7-5.0, Merit 3.0-3.6, Credit 1.7-2.9, Pass 0.7-1.6 na Fail 0.0-0.6.
“Ukokotoaji wa wastani wa pointi (GPA) ya mtahiniwa hufanywa kwa kuzingatia masomo ambayo mtahiniwa amefaulu. GPA anayopata mtahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne hutokana na wastani wa pointi alizopata katika masomo saba aliyofaulu vizuri wakati kwa kidato cha sita ni masomo matatu,”alisema
Via: Tanzania Daima

Wednesday, August 27, 2014

HATARIIII! MFANYAKAZI WA NDANI {HOUSE GIRL} ACHOMWA MOTO SEHEMU ZA SIRI KISAAAA!



Huko mkoani Arusha mfanyakazi wa ndani (House Girl)  amechomwa moto na bosi wake kwa kosa la kukojoa kitandani. Jionee mwenyewe unyama aliofanyiwa huyu dada, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA....



Chanzo: wanawakelivetv.com


Monday, August 18, 2014

KUFUATIA MALALAMIKO YA BAADHI YA WATU BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA (NECTA) KUTOJUMUISHA MASOMO YA DINI KUPANGA MADARAJA, HUU NDIYO UFAFANUZI WA NECTA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA


UFAFANUZI KWA UMMA KUHUSU KUTOJUMUISHWA KWA ALAMA ZA MASOMO YA HIARI KATIKA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2014


Baadhi ya wadau wamekuwa wakitaka kujua utaratibu uliotumika kukokotoa pointi za madaraja katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2014. Hii imetokana na kuona kuwa kuna baadhi ya masomo hayakujumuishwa katika kupata idadi ya pointi kwa watahiniwa wa Tanzania Bara na wale wa Zanzibar.

Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha wadau wote kuwa ukokotoaji wa pointi za madaraja kwa watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Sita huzingatia masomo ya Tahasusi (Subject Combinations) aliyoyasoma mtahiniwa kama ilivyobainishwa katika Kanuni za Mitihani (The Examinations Regulations) Toleo la mwaka 2013 kifungu cha 23(1) kinachosomeka:

 “The Advanced Certificate of Secondary Education shall be awarded in four Divisions to both schools and private candidates who have conformed to entry requirements and have fulfilled the conditions of the awards. Calculations of points shall be done based on Subject Combinations approved by the Ministry of Education”,

Masomo ya Tahasusi (Subject Combinations) yanayotumika kukokotoa alama za madaraja  yamebainishwa katika Waraka Namba 1 wa mwaka 2006 wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na Waraka Kumb. Namba P33/8/53/Vol.I/44 wa mwaka 2012 wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar.

Baadhi ya Tahasusi zinazotumika Zanzibar zinatofautiana na zilizopo Tanzania Bara, ambapo kwa Zanzibar zipo baadhi ya Tahasusi zenye kuhusisha masomo ya hiari. Masomo ya hiari ambayo husomwa na baadhi ya watahiniwa ni  pamoja na General Studies (GS), Islamic Knowledge, Basic Applied Mathematics (BAM), Divinity, Computer Studies na Arabic Language. Hata hivyo, Baraza la Mitihani hufanya tathmini na kutunuku ufaulu kwa masomo yote ya hiari ya mtahiniwa katika cheti chake ili kimsaidie katika udahili wa ngazi mbalimbali za mafunzo kulingana na matakwa ya sifa za mafunzo husika.

Taarifa za kina kuhusu utaratibu wa kutunuku matokeo ya Kidato cha Sita zipo katika kitabu cha Mwongozo wa Matumizi ya Viwango vya Ufaulu na Utaratibu wa Kutunuku Matokeo ya Kidato cha Nne na cha Sita kilichotolewa mwaka 2014. Aidha, kitabu hicho kilikabidhiwa  kwa Wakuu wa Shule zote za sekondari Tanzania Bara na Zanzibar. Pia kitabu hicho kinapatikana kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania (www.necta.go.tz).

Baraza la Mitihani la Tanzania linawaomba wadau wasipotoshwe na taarifa ambazo zinasambazwa  katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambazo zina lengo la kupotosha Umma.



Imetolewa na,

AFISA HABARI NA UHUSIANO


Sunday, August 10, 2014

KIBONDE ALIVYOJIFANYA MBABE KUMBE NI KIBONDE TU! INGIA HAPA KUSOMA NA KUTAZAMA PICHA AKIPEWA KIBANO


Watangazaji wawili wa Clouds FM, Ephrahim Kibonde na Gadna Habash wamekamatwa na polisi kwa madai ya kusababisha ajali na kutoa lugha ya matusi kwa polisi.
Kibonde na Gadna wanadaiwa kusababisha ajali hiyo jana katika eneo la Makumbusho, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kibonde ndiye alikuwa dereva wa gari linalodaiwa kusababisha ajali hiyo kwa kugonga gari la raia wa kigeni na kukimbia wakati askari wa usalama barabarani (trafiki) walipofika kupima ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alithibitisha kukamatwa kwa watangazaji hao, “Ni kweli tunawashikilia watangazaji hao kwa kosa la kukaidi amri ya polisi, bado tunawashikilia mpaka sasa.”

Ilidaiwa kuwa gari la Kibonde iligonga gari hilo kwa nyuma na trafiki walipofika ili kupima alikimbia, ndipo trafiki walipotumia gari lililogongwa kumfukuzia na kufanikiwa kumkamata.

Akisimulia kisa hicho polisi wa kike katika Kituo cha Oysterbay ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema Kibonde alikataa kutii sheria bila shuruti kwa kivuli cha umaarufu alionao.

“Hawa wanashikiliwa kwa kosa la kuvunja sheria za barabarani, Kibonde alikuwa anaendesha akiwa amelewa na kusababisha ajali, kama haitoshi walikimbia na kuwatolea polisi lugha chafu za matusi jambo ambalo  ni kinyume na sheria,” alisema askari huyo.

Alisema walipoanza kuwafukuzia waliwakamata Kituo cha Mwenge na trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake, trafiki naye akagoma kushuka.

“Kibonde alikaidi tena na kuondoa gari na kuendelea na safari yake wakati trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo, walipofika eneo la Ubungo mataa, trafiki mwingine aliisimamisha gari na Kibonde alikaidi kusimama, akiwa katika hali hiyo kuna gari ilitokea ikakatisha kati ya trafiki na gari hiyo ndiyo kikawa kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa mbaroni,” alisema polisi huyo.

Baada ya kukamatwa, Kibonde na abiria wake walifikishwa katika Kituo cha Polisi Urafiki Ubungo saa 7:00 asubuhi na baadaye saa 8:00 asubuhi walihamishiwa katika Kituo cha Oysterbay.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Osterbay, Victor Samata aliliambia gazeti hili kuwa suala hilo lipo juu ya uwezo wake kulizungumzia kwani yeye siyo msemaji, hivyo kumtaka mwandishi amtafute msemaji wa kituo hicho.
“Sidhani kama hili ni suala la kulijadili, isitoshe mimi siyo msemaji wa hapa ingefaa atafutwe msemaji kulizungumzia hili,” alisema Samata.

Habari kutoka: www.mwananchi.co.tz picha kwa hisani ya mitandao ya kijamii 

Thursday, August 7, 2014

SHIBUDA, ARFI NA LETICIA SAFARI HIYO YA KUTIMKIA ACT-TANZANIA, CHABATIZWA 'CHAMA CHA WASALITI TANZANIA'

Kwa sasa wanachama wa CHADEMA wanaoonekana ni wasaliti wakitimuliwa CHADEMA hujiunga na ACT-Tanzania ambacho kimbatizwa jina la 'Chama cha wasaliti-Tanzania' kwa haliinavyoelekea huenda hawa nao akina Shibuda, Arfi na Leticia wakatimkiwa huko au watakuwa wanachama wa Mahakama.

CHADEMA kuwatosa Shibuda, Arfi, Leticia

  • Lissu asema hawavumiliki, CUF yawakana waasi
  • Bunge lawatilia shaka, lazuia wasilipwe posho
John Shibuda, Leticia Nyerere na Said Arfi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kitawafukuza wabunge wake, John Shibuda (Maswa Magharibi), Said Arfi (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere (Viti Maalum) baada ya kujiridhisha kwamba wameshiriki vikao vya Bunge Maalum.
Hatua hiyo inakuja baada ya wabunge hao kuripotiwa kujisajili na kushiriki vikao vya Bunge hilo kinyume na msimamo wa CHADEMA kupitia kundi lao la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambalo wamesusia wakidiai CCM imechakachua rasimu yenye mapendekezo ya wananchi.
Msimamo wa CHADEMA ulitolewa jana na Mwanasheria wake, Tundu Lissu akisema kuwa Kamati Kuu ilishatoa maelekezo kwa wabunge wote, hivyo hawamuogopi wala hawataki kumwonea mtu, kwamba ndio maana wanajiridhisha kwanza.
“CHADEMA kama mshirika wa Ukawa, tuliwazia wabunge wetu wasishiriki Bunge hilo wala vikao vya kamati zake, sasa hawa waliokwenda huko Dodoma lazima waseme wako Ukawa au CCM.
“Hawa watu ni mamluki, kwa hili wala hatutahitaji kuwaita wajieleze. Tulisema wasiende, wao wakaenda. Sasa tutuchukua hatua na kama wanataka ubunge wa mahakama wataupata,”alisema.
Lissu alisisitiza kuwa wabunge hao wameonesha njaa ya ajabu ya kukimbilia posho kwani hata kama ni shida ya kukosa fedha si kwa njia hiyo ya usaliti wanaojaribu kuufanya wakidhani watakidhoofisha CHADEMA.
“Hivi nani asiyemjua Shibuda…nani hamjui Arfi tangu ajiengue umakamu mwenyekiti wa chama au nani asiyejua mwenendo wa Leticia? Sisi hatumwogopi wala hatutamwonea mtu bali siku ya kufanya hesabu ikifika, kila mmoja ataoneshwa zake na kama kuna wengine acha waende tutawashughulikia bila kujali,”alisema

Posho
Bunge Maalum la Katiba, limeamua kuzuia malipo ya posho za kujikimu kwa baadhi ya  wajumbe wa Ukawa waliojisajili bila kushiriki vikao.

Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Hamis Hamad, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kubaini wajumbe hao wanafanya hila ya kujipatia fedha bila kufanya shughuli inayotakiwa.

Alisema kuwa utaratibu huo wanaufanya kujenga uhalali wa kulipwa posho ya kujikimu ya sh. 230,000 inayotolewa kila siku kwa mjumbe aliyeko Dodoma.

Kwa mujibu wa utaratibu wa malipo ya Bunge Maalum kila siku mjumbe aliyejisajili hulipwa sh. 230,000 na atakayehudhuria kikao hulipwa sh. 70,000, hivyo kufanya sh. 300,000 kwa siku.

Hamad alisema mpaka jana asubuhi wabunge wawili wa CHADEMA, John Shibuda na Leticia Nyerere ndiyo waliojisajili lakini hawakuhudhuria vikao.

Alibainisha kuwa mjumbe mwingine kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Clara Mwaituka naye alijisajili lakini hakushiriki kwenye vikao.

Alisema wamebaini kuwa licha ya wabunge hao kujisajili lakini walikuwa hawajalipwa fedha za siku saba kama walivyolipwa wenzao wanaoshiriki vikao.

Alisema kuwa alipokwenda kwa wahasibu kuangalia walivyolipwa Ukawa, alibaini kutofanyika kwa malipo, hivyo akaagiza yoyote atakayekuja asilipwe mpaka kuwe na uhakika wa kuhudhuria vikao.
“Kwa bahati nzuri watu wa uhasibu waliandika pembeni majina ya wajumbe wa Ukawa….hata Shibuda na Nyerere hawakulipwa, sasa tunataka tubane zaidi kukwepa ujanja ujanja,”alisema.
Katibu aliongeza kuwa Shibuda alitoa taarifa  kuwa hatoweza kushiriki kwenye vikao vya kamati kwa madai ana matatizo ya kiafya.
“Shibuda alikuja ofisini kwangu huku mguu wake ukionekana kuwa umevimba hivyo akaomba ruhusa kwenda kupatiwa matibabu, lakini hao wengine wamejiandikisha tu na kuondoka hata hivyo hawajaonekana tena,”alisema.

Hamad aliwataja wajumbe wengine kutoka Ukawa waliojiandikisha na kuhudhuria vikao vya kamati kuwa ni Fatma Mohamed Hasan na Ally Omary Juma aliodai ni wa CUF.
Tanzania Daima, liliwasiliana na mmoja wa wajumbe wa Ukawa, Ismail Jussa Ladhu, ambaye alisema wajumbe waliotajwa na Hamad, hawatoki CUF.
“Mimi naona Katiba hafuatilii vema taarifa za wajumbe wake maana aliowataja mmoja natoka kundi la 201 mwingine anatoka chama kingine cha upinzani kisichokuamo Ukawa,” alisema.
Hamad alimtaja mjumbe mwingine aliyeonekana kuwa na msimamo wa Ukawa akitokea kundi la 201 kuwa ni Jamila  Abeid, ambaye hakutaja anawakilisha kundi lipi.

Arfi awasili bungeni
Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (CHADEMA) jana alijisajili kushiriki vikao vya Bunge Maalum huku akidai amefanya hivyo kwa kutimiza haki yake ya kimsingi.
Arfi aliwasili majira ya asubuhi na mara baada ya kukamilisha taratibu za kujisajili alisema anawawakilisha Watanzania Bara.

Alisema amepata fursa na haki ya kuwemo kwenye Bunge hilo kutokana na kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Arfi alisema licha ya viongozi wa CHADEMA kuwataka wanachama wake wasihudhurie vikao, yeye ameamua kushiriki kwa lengo la kutimiza wajibu wake kwa wananchi waliomchagua.
Alipinga msimamo wa chama chake huku akidai kuwa vyama vinataka kupokonya mamlaka ya wananchi, kwamba iwapo wataendelea kukubali hali hiyo watakuwa wanawanyima wananchi haki yao ya msingi na kikatiba.

TAMKO LA CHADEMA KUFUATIA WABUNGE WAKE KUONEKANA DODOMA



Kumekuwepo na madai yanayosambazwa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari kuhusu baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuonekana mjini Dodoma au kujisajili kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini humo.
Chama kupitia Idara ya Habari kingependa kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;

1. Uamuzi wa kuwataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaotokana na CHADEMA kushirikiana na wenzao wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kutoshiriki vikao vya bunge hilo ili kuepuka kunajisi mchakato wa Katiba Mpya, ulitokana na maazimio ya kikao cha Kamati Kuu iliyoketi Julai 18-19 na kuazimia kwamba;
Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na CHADEMA, kama sehemu ya UKAWA, watarudi kwenye vikao vya Bunge Maalum endapo tu mamlaka ya Bunge hilo yatafafanuliwa kuwa ni ya kuboresha, na sio kuibomoa au kuifuta, misingi mikuu (basic features) ya Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi na kuandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoteuliwa na Rais kwa ajili hiyo;
Wajumbe wa Bunge Maalum wanaotokana na CHADEMA, kama sehemu ya UKAWA, watarudi kwenye vikao vya Bunge Maalum endapo tu, na baada ya, ufafanuzi uliotajwa katika aya ya 2 utahusisha marekebisho ya kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, inayohusu mamlaka ya Bunge Maalum, pamoja na Kanuni husika za Bunge Maalum;
Wajumbe wote wa CHADEMA katika Bunge Maalum hawatashiriki katika kikao chochote cha Bunge Maalum au Kamati zake hadi hapo ufafanuzi wa mamlaka ya Bunge Maalum uliotajwa katika aya za 2 na 3 utakapofanyika kwa mujibu wa maazimjo ya Kamati Kuu;
Hadi wakati huu, hakuna jambo hata moja kati ya hayo lililofanyika, huku mazungumzo yaliyotarajiwa kuokoa mchakato yakiwa yamevunjika, kwa sababu CCM na Serikali yake wameamua kudharau na kupuuza maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba badala yake kuweka maslahi ya chama hicho kwenye katiba.

2. Iwapo kuna mjumbe/wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaotokana na CHADEMA wameonekana wakijisajili kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma au watashiriki vikao vya bunge hilo au kamati zake, wataandikiwa barua ya kujieleza kisha chama kitachukua hatua kwa mujibu wa taratibu zake kupitia vikao.

3. Tunapenda pia kuwakumbusha wanachama wa CHADEMA na umma mkubwa wa Watanzania kuwa, mji wa Dodoma mbali ya kuwa Makao Makuu ya Nchi pia inapatikana Ofisi Kuu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba ambako hakujaridhiwa na Watanzania wengi, hakujazuia shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanyika ikiwemo kutoa huduma kwa watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wabunge. Suala hilo linakwenda sambamba na ukweli kwamba sehemu kubwa ya watumishi wa Bunge Maalum la Katiba ni wale wale ambao wanatakiwa kuwahudumia wabunge wa Bunge Maalum la Katiba.

Hivyo kuonekana kwa mbunge yeyote wa CHADEMA mjini Dodoma au kwenye viwanja au Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuwezi kutafsiriwa moja kwa moja kuwa mbunge husika amehudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba, kinyume na msimamo wa UKAWA.

Imetolewa  Alhamis Agosti 7, 2014 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari - CHADEMA

NAFASI ZA KAZI





CHUO KIKUU CHA DAR-ES-SALAAM KIMETANGAZANAFASI ZA KAZI KWA KADA MBALIMBALI, NAFASI ZA KAZI ZLIZOTANGAZWA BONYEZA HAPA---> NAFASI ZA KAZI

Sunday, August 3, 2014

TAHAKIKI TAMTHILIYA YA KILIO CHETU KIDATO CHA 3&4


JINA LA TAMTHILIYA: Kilio Chetu
MWANDISHI: MEDICAL  AID FOUNDATION
MCHAPISHAJI: TANZANIA PUBLISHING HOUSE (TPH) MWAKA 1995
JINA LA MHAKIKI: Mwl. Furaha Venance
Mawasiliano 0715 33 55 58

Mwaka 2014
                                                          UTANGULIZI
Kilio Chetu ni tamthiliya inayojikita kuzungumzia umuhimu wa elimu ya jinsia na ukimwi kwa vijana, Tamthiliya hii inaonesha namna ukosefu wa elimu ya jinsia na ukimwi kwa jamii hususani vijana inavyochangia mimba za utotoni au mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana.
Katika tamthiliya hii, mwandishi anaonesha namna ambavyo jamii ikiangaika kujielimisha kuhusu elimu hii ya jinsia na ukimwa na kuwaacha vijana wakiangamia kwa kukosa elimu hiyo, hali hii inaifanya jamii kugawanyika, wapo wanaoona kuwa suluhisho la janga hili la Ukimwi, ni jamii nzima wakiwemo na vijana kupewa elimu hii lakini wapo wazazi wanaopinga wakiamini vijana umri wao wakupewa elimu hii haujafika bado. Je ni nini hatima ya vijana hawa? Basi tafuta kitabu hiki cha Kilio chetu kisome utajifunza mambo mengi sana ni kitabu kinachotakiwa kusomwa na watu wa rika lolote.
WAHUSIKA
Katika kazi ya fasihi wahusika wanaweza kuwa watu, wanyama au vitu, na wahusika ndiyo wanaobeba dhamira za msanii, na katika kazi ya fasihi wahusika tunawagawa katika makundi mawili, wahusika wakuu na wahusika wasaidizi/ wahusika wadogowdogo


(a)  Wahusika Wakuu
Katika tamthiliya hii, ina wahusika wakuu wawili, ambao ni Suzi na Joti.
1.     SUZI
ü Ni binti anayesoma shule ya msingi
ü Ni binti asiyekuwa na elimu ya jinsia na ukimwi, Mama yake anashindwa kumpa elimu hiyo akiamini kuwa umri wa Suzi haujafikia kupewa elimu hiyo.
ü  Anajiingiza katika mapenzi akiwa mdogo.
ü Anakuwa na mahusiano ya kingono na mwanafunzi mwenzake anayeitwa Joti.
ü Ni binti wa pekee wa Mama Suzi.
ü Anapata mimba akiwa mwanafunzi na anafikiria kuiotoa mimba hiyo.

2.     JOTI
ü Ni kijana wa kiume anayesoma shule ya msingi.
ü Ni kijana asiyekuwa na elimu ya jinsia na ukimwi, baba yake anashindwa kumpa elimu hiyo akiamini kuwa umri wa joti haujafikia kupewa elimu hiyo.
ü Anajiingiza katika mahusiano ya kingono akiwa mdogo huku akiwa mwanafunzi.
ü Anajihusisha na mahusiano ya kingono na wasichana wengi, akiwemo Suzi, Chausiku, Gelda n.k.
ü Ni mvulana mlaghai, anawalaghai wasichana ili tu kutimiza haja zake za kingono.
ü Anaambukizwa virusi vya ukimwi
ü Anafariki kwa ugonjwa wa ukimwi.

(b) Wahusika wadogo wadogo
1.     MAMA SUZI
ü Huyu ni mama yake Suzi
ü Anamlea Suzi bila baba
ü Anajishughulisha na biashara ndogondogo kama vile kuuza vitumbua ili kujipatia kipato.
ü Anaamini kuwa mtoto mdogo hawezi kuambukizwa virusi vya ukimwi.
ü Anakumbatia mila na desturi zililozipitwa na wakati zinazokataza watoto/vijana kupewa elimu ya jinsia na ukimwi.
ü Anakataa katakata mtoto wake, Suzi kupewa elimu ya jinsia na ukimwi akiamini kuwa umri wake ni mdogo, na kufanya hivyo ni sawa na kumfundisha umalaya.
ü Anamwadhibu mtoto wake (Suzi) baada ya kukuta vidonge vya kuzuia mimba katika mfuko wa sketi yake.

2.     BABA JOTI
ü Ni baba yake na Joti.
ü Anaamini kuwa ukali wa mzazi na viboko ndiyo suluhisho la kuwazuia watoto kujiingiza katika mambo mabaya.
ü Anakataa katakata elimu ya jinsia na ukimwi kutolewa kwa watoto/vijana.
ü Anaangaika kuokoa uhai wa mtoto wake, Joti, kwa kutafuta tiba yake kila mahali.
ü Anampoteza mtoto wake(joti) baada ya kufariki kutokana na ukimwi.

3.     MAMA JOTI
ü Huyu ni mama yake Joti.
ü Mke wa Baba Joti
ü Rafiki yake Mama Suzi
ü Anahisi mume wake ana uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine, hali inayomlazimu kuwanunulia kanga zenye maandishi ya mafumbo ili kuwapasha wezi wake.
ü Yeye na mumu wake (Baba Joti) wanashindwa kumpa Joti elimu ya jinsia na ukimwi.
4.     BABA ANNA
ü Huyu ni baba yake Anna.
ü Anaamini kuwa elimu ya jinsia na ukimwi ni muhimu kwa vijana ili kuwanusuru na janga la ukimwi.
ü Kwa kushirikiana na mke wake wanafanikiwa kuwapa watoto wao elimu ya jinsia na ukimwi, elimu inayowasaidia kupambana na vishawishi.

5.     MAMA ANNA
ü Huyu ni mama yake Anna.
ü Ni mke wa Baba Anna
ü Kwa kushirikiana na mume wake wanafanikiwa kuwapa watoto wao elimu ya jinsia na ukimwi, elimu inayowasaidia kupambana na vishawishi.
6.     ANNA
ü Mtoto wa kike wa Baba Anna na Mama Anna
ü Ni mwanafunzi wa Shule ya msingi.
ü Amepewa elimu ya jinsia na ukimwi, elimu inayomsaidia kupambana na vishawishi vya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mdogo
ü Ana mkatalia Mwarami kuwa naye kimapenzi

7.     MJOMBA
ü Huyu ni kaka yake na Mama Suzi
ü Mjomba wake na Suzi
ü Anasisitiza elimu ya jinsia itolewe kwa vijana wote ili kuwanusuru na maambukizi ya virusi vya ukimwi na mimba zisizotarajiwa.
ü Anamshauri Baba Joti kutoangaika kwenda kwa waganga na kumaliza rasilimali zake kwa ajili ya kutafuta tiba ya UKIMWI kwa mtoto wake Joti  kwani ukimwi hauna dawa

8.     JIRANI
ü Huyu ni jirani yake na Baba Joti.
ü Anamshawishi Baba Joti kwenda kwa mganga wa kienyeji kutibiwa ukimwi.

9.     MWARAMI
ü Huyu ni rafiki yake Joti, Choggo na Jumbe
ü Ni mwanafunzi wa shule ya msingi
ü Hana elimu ya jinsia na Ukimwi anaamini ukimwi unawapata wakubwa tu
ü Wenzake wanamshawishi kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na hata kumtishia asipofanya hivyo watamfukuza katika kundi lao la urafiki
ü Anashindwa kumshawishi Anna

10.                     CHOGGO
ü Huyu ni rafiki yake Joti, Mwarami na Choggo
ü Ni mwanafunzi wa shule ya msingi
ü Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mtoto mdogo tena mwanafunzi
ü Yeye na rafiki zake wana tabia ya kwenda katika vibanda vinavyoonesha video za ngono (sinema za X) kuangalia

11.                     JUMBE
ü Huyu ni rafiki yake Joti, Mwarami na Choggo
ü Ni mwanafunzi wa shule ya msingi
ü Anajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi akiwa mtoto mdogo tena mwanafunzi
ü Yeye na rafiki zake wana tabia ya kwenda katika vibanda vinavyoonesha video za ngono (X) kuangalia

12.                     CHAUSIKU
ü Huyu ni mwanamke mtu mzima jirani na akina Joti.
ü Anajishughulisha na biashara ndogondogo hususani biashara ya vitumbua ili kujipatia kipato.
ü Anakuwa na mahusiano ya kimapenzi  na kijana mdogo tena mwanafunzi (Joti)
ü Ana mahusiano ya kimapenzi na Mpemba muuza duka.

13.                     FAUSTA
ü Huyu ni msichana anayesoma darasa  la tano
ü Anafariki kwa ukimwi

14.                     MPEMBA
ü Huyu ni mfanyabiashara wa duka
ü Anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Chausiku

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Wahusika na hasa mhusika mkuu katika tamthiliya  ndiye anayeifikishia jamii ujumbe uliokusudiwa. Tumia tamthiliya mbili kutetea hoja yako.
2.     Chagua wahusika watatu wa kike kutoka kila tamthiliya kati ya tamthiliya mbili ulizosoma, kasha onesha kukubalika kwao kama kielelezo cha maisha katika jamii.
                               
DHAMIRA
Hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Na katika tamthiliya hii kuna  dhamira kuu na dhamira ndogondogo ambazo zimejitokeza, kwa kuanza tunaanza na;

(a)  Dhamira Kuu
Dhamira kuu katika tamthiliya ni umuhimu wa elimu ya jinsia na ukimwi, mwandishi anaamini kuwa, ili jamii iweze kunusurika na matatizo yatokanayo na kujamiana kama vile mimba za utotoni (mimba zisizotarajiwa) magonjwa ya zinaa kama vile kasendwe, kisonono gono na ukimwi, sharti vijana wapewe elimu ya jinsia na ukimwi, mwandishi anathibitisha hili akimtumia muhusika Mjomba anaposema, “Upepo umebadilika sasa. Hawa vijana wetu wapewe elimu ya familia ikiwepo ya jinsia. Watoto waambiwe wazi juu ya mambo haya ya mapenzi na hatima yake.” Uk. 9

Vilevile, mwandishi anaonesha namna ambavyo vijana wanapukutika, wanaangamia na ukimwi kwa sababu ya kukosa elimu hii ya jinsia na ukimwi, hali hii inasababisha vijana kuwa gizani kabisa wanashindwa namna ya kujikinga na wengine hata kushindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu , rejea ukurasa wa 13, Mwandishi akimtumia muhusika Mtambaji anaposema, “Kisiwa kizima kipo gizani. Watoto ndio kabisa. Wapo katika giza nene. Wanashindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu.”

Si hivyo tu, mwandishi anaendelea kutuonesha kuwa, ukosefu wa elimu hii ya jinsia na ukimwi kwa vijana/watoto inawafanya watoto/vijana kujitenga na mapambano dhidi ya ukimwi kwakuwa wao wanaamini kuwa ugonjwa huu wa ukimwi ni wa wakubwa tu kwani watoto hawawezi kuambukizwa virusi vya UKIMWI kama mwandishi anavyosema akimtumia muhusika Mwarami anapomwabia Anna, “Ukimwi unawapata wakubwa, Anna.” Uk. 25

Si watoto tu, wapo hata wazazi, watu wazima ambao nao wanaamini kuwa watoto wadogo hawawezi kuambukizwa virusi vya ukimwi, kama anavyoamini Mama Suzi, rejea ukurasa wa 4, muhusika Mama Suzi anaposema, “...Lakini shoga, watu wanatafuta laana ya marehemu. Kitoto kama kile; kife kwa ukimwi! Ungeingilia kona gani?” {Uk.4}

Mwandishi anaendelea kutuonesha kuwa, hata mimba za utotoni, mimba zisizotarajiwa kwa vijana husababishwa na ukosefu wa elimu hii ya jinsia, kwa mfano mwandishi anamtumia muhusika Suzi ambaye anaamini kuwa, kwa kufanya ngono mara moja hakuwezi kusababisha mtu akapata mimba, hili tunaliona ukurasa wa 28, Suzi anapomwambia Anna, “Wala sina mimba, kwanza mimi nimefanya mara moja tu na joti.” {Uk.28}

Vilevile, mwandishi anaonesha kuwa, wapo watoto/vijana ambao kutokana na kukosa elimu hii ya jinsia, wanaamini kuwa wao kama watoto hawawezi kupata mimba, mwandishi anamtumia muhusika Joti anapowaambia rafiki zake, “Mara moja tu, hakuna mimba sisi watoto.” {Uk. 16}

Mwandishi hakuishia tu kuonesha madhara ya kukosa elimu hii ya jinsia, kwa upande mwingine ameonesha faida za elimu hii ya jinsia na ukimwi kwa vijana, mwandishi anaonesha kuwa, vijana waliopata elimu hii, huwasaidia sana kupambana na kujizuia na vishawishi vya kingono kutokana na uelewa waliokuwa nao, kwa mfano mwandishi anamtumia muhusika Anna, ambaye kutokana na mafunzo aliyopewa na wazazi wake yanamsaidia sana kupambana na kujizuia na vishawishi hivyo kutokana na kufahamu madhara ya kushiriki ngono kabla ya wakati, hili mwandishi analithibitisha akimtumia muhusika Anna anaposema, “...Hujui kama kuna madhara mengine. Hujui magonjwa ya zinaa wewe: hujui kisonono, kaswende na mengine kedekede. Haya hata UKIMWI hujui?”  {Uk. 25}

Hivyo mwandishi anashauri, elimu hii ya jinsia na UKIMWI, isitolewa kiubaguzi, itolewe kwa watu wote kwani kila mtu yuko katika hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, mwandishi anaonesha namna ambavyo vijana wanateketea kwa kubaguliwa kwao kupewa elimu hii, rejea ukurasa wa 1-2, Mtambaji anaposimulia, “Wakubwa wakaandika mabuku kupeana habari. Wakabandika mabango kupeana tahadhari, lakini watoto wakateketea kwa kukosa habari zozote za kuwaokoa.”

Mwandishi anaonesha kuwa, kama vijana wangeelimishwa kuhusu madhara ya kufanya mapenzi kabla ya wakati, namna ya kujilinda, basi wasingetummbukia katika janga hili, mwandishi anathibitisha kwa kumtumia muhusika  Suzi anaposema, “Naapa kwa Mungu wangu, mimi na Joti tungepata bahati ya kuelimishwa, tusingetumbu...tusi...(Anaanguka chini.)” {Uk. 36}


(b) Dhamira ndogo ndogo
1.     Ukosefu wa elimu
Dhamira hii inajitokeza katika tamthiliya, mwandishi anaonesha kuwa ukosefu wa elimu ya namna ya kupambana na Ukimwi unaifanya jamii kushindwa kulikabili gonjwa hili, ukosefu wa elimu unawafanya wengine kuamini ugonjwa huu ni wa kurogwa, wengine wanaamini ni ugonjwa unaletwa na mizimu na hata wengine kudhani ni majini.

2.     Mapenzi na ndoa
Suala la mapenzi na ndoa pia limepewa nafasi katika tamthiliya hii, tukianza na suala la mapenzi, mwandishi anajadili mapenzi ya namna mbili, mapenzi ya dhati na mapenzi ya ulaghai.
(a)  Mapenzi ya dhati
ü Baba Anna kwa familia yake
ü Mjomba kwa Suzi
ü Anna kwa wazazi wake
ü Anna kwa Suzi
ü Suzi kwa Joti
(b) Mapenzi ya ulaghai
ü Joti kwa Suzi
ü Joti kwa Chausiku
ü Chausiku kwa Joti

        

3.     Malezi kwa vijana
ü Mwandishi pia amegusia suala la malezi kwa watoto, mwandishi anaonesha kuwa, malezi bora kwa mtoto ni malezi ya wazazi wote wawili, yaani baba na mama, na anapokosekana mzazi mmoja huweza kumuathiri mtoto, katika tamthiliya hii tunamuona Suzi akilelewa na mama peke yake bila baba hali hii inachangia mtoto kuingia katika matatizo, hili linathibitishwa na mwandishi akimtumia muhusika Mama Suzi anaposema, “Kila siku ninasema mwanangu mdogo, mwanangu ni mtoto mzuri, leo Suzi unanifanyia hivi? Hivi baba yako angekuwepo ungefanya hivi? Ah Suzi, ungefanya?” {Uk.31}
ü Katika suala hili la malezi, mwandishi anatuambia kuwa kuwa, mzazi ndiyo mwalimu bora kwa malezi mema ya mtoto,rejea ukurasa wa 11, Mjomba na Baba ANNA wanaposema, “Mzazi ndiye mwalimu wa kwanza...Na ndiye bora.” {Uk. 11} hivyo wazazi wawafundishe vema watoto wao, lakini wazazi wasipofanya hivyo, walimwengu watawafundisha na kwa kawaida walimwengu hufundisha katika upotofu, rejea ukurasa wa 10-11, Baba Anna anaposema, “Dunia imeharibika bwana. Mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha tena sasa si maadili mema bali njia potofu.” {Uk.10-11}

ü Mwandishi pia anaonesha kuwa, ili watoto/vijana wawe na maadili mema, wazazi wanatakiwa kukaa na watoto wao kuwaelimisha mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na madhara kwao kama alivyofanya Baba Anna na mke wake, rejea ukurasa wa 10 Baba Anna anapowaambia wenzake, “Hilo ndilo mie nililofanikiwa mwenzenu. Nimemwambia mama Anna akae na mabinti zake name nikae na vijana wangu wa kiume. Tumefanya kazi hiyo kwa makini sana. Tumewaelimisha juu ya madhara ya tabia hiyo kwao binafsi na kwetu sote. Hatukubakiza kitu.” {Uk. 10}


4.     Usaliti
Usaliti ni dhamira nyingine inayojitokeza katika tamthiliya hii, kwa mfano mwandishi anaonesha usaliti unaofanywa na Baba Joti kwa mke wake, Baba Joti anaisaliti ndoa yake kwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, hili linathibitishwa na Mama Anna anaposema, “Lakini leo nimefika kikomo. Ndiyo mwisho wa kumvumilia huyu nguru anayeichimba ndoa yangu.” {Uk. 7}

Usaliti mwingine, tunaona kwa Joti, pamoja na kwamba Joti anakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Suzi anaamua kumsaliti na kuanzisha mahusiano na wanawake wengine, mwandishi analithibitisha hili akimtumia muhusika Suzi anaposema, “Ndiyo maana mie nilikuwa nakataa Joti. Nishaambiwa kwamba unawasichana wengi shuleni na mtaani kwetu.” {Uk. 21}

Usaliti mwingine unajitokeza kwa Joti na Chausiku, mwandishi anaonesha kuwa Joti pamoja na kuwa na mahusiano na Chausiku anamsaliti Chausiku kwa kuwa na mahusiano na wasichana wengine, Joti anapewa vitu na Chausiku naye anawapa wanawake wengine, rejea ukurasa wa  22, Chausiku anaposema, “Toka hapa. Nimesikia habari zako. Kila msichana unamtaka tu. Mie nakununulia fulana ya mazoezi wewe unahonga kinyago chako kile. Bisha...Nikikupa hela ya kununua peni we unanunulia bazooka visichana vyako.” {Uk. 22} lakini si Joti tu ndiye anamsaliti mwenzake, mwanandishi anatuonesha kuwa, hata Chausiku pia, anamsaliti Joti kwa kuwa na mahusiano na wanaume wengine, rejea ukurasa wa 22-23, Mwarami anapomwambia Joti, “Sasa ndiyo kuparamia mpaka wasichana wakubwa wa mtaani? Fikiri juu ya Chausiku, Yule msichana mjuvi wa mji ambaye pia anachukuliwa na Yule mpemba muuza duka.” {Uk. 22-23}

Tukigeukia katika uhalisia wake, suala la usaliti katika ndoa au mapenzi bado ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu, wanandoa wanasalitiana, wapenzi wanasalitiana tabia hii ya usaliti huwa ni kichochea kikubwa sana kwa watu kuambukizana virusi vya ukimwi, kama tunavyoona kwa Joti. Hivyo jamii iache usaliti.

5.     Athari za utandawazi
Mwandishi pia amejadili suala la utandawazi na athari zake, mwandishi anaonesha namna utandawazi unavyochangia kwa kiasi kikubwa kuharibu tabia na maadili ya watoto na vijana, kwa mfano tunawaona akina Joti, Jumbe, Choggo na Mwarami wanajiingiza katika mahusiano ya kingono wakiwa watoto wadogo kutokana na kuathiriwa na video za ngono (sinema za X) wanazozitazama mtaani, mikanda hii ya ngono imekuwa rahisi sana kupatikana kutokana na utandawazi.

6.     Athali za ukoloni na ukoloni mambo leo
Suala la ukoloni na ukoloni mambo leo pia limepewa nafasi katika tamthiliya hii, mwandishi anaonesha namna  wakoloni walivyoharibu utamaduni wetu kwa kuuita ushenzi na hata tulivyopata uhuru, viongoni wetu wakaendelea kushikilia mawazo hayo potofu ya kikoloni ambayo kwa kiasi kikubwa tunaangamia wenyewe, hili mwandishi analithibisha akimtumia Mtambaji anaposema, “Mila zetu hazikukataza kutoa mafunzo ya elimu ya jinsia...Wakoloni na vibaraka wao ndio wanaostahili kulaumiwa wakoloni walipiga vita jando na unyago wakidai eti ni ushenzi.” Mtambaji anaendelea kutuambia tena, “Viongozi wetu nao wakaendeleza mawazo hayo hata baada uhuru bila kutambua kuwa wanajiua wenyewe.” {Uk. 13-14}

7.     Nafasi ya mwanamke katika jamii
ü Mwanamke amechorwa kama mlezi wa familia, mwandishi anatuonesha namna ambavyo mwanamke anakuwa mlezi mzuri wa familia, anaangaika hapa na pale kuhakikisha mtoto au watoto wake wanapata mahitaji yote muhimu kama vile chakula, mavazi na hata elimu, rejea ukurasa 30, Mama Suzi anaposema, “Mimi ninahangaika kukusomesha, wewe unanifanya hivi...Mama yako nimeungua viganja kwa kupika vitumbu ili mwanangu usome.” {Uk. 30}

ü Mwanamke amechorwa kama mtu mwenyemsimamo, mwandishi anamtumia muhusika Anna kumuonesha mwanamke kama mtu mwenye msimamo katika maamuzi yake, tunamuona Anna pamoja na kusumbuliwa mara kwa mara na Mwarami kumtaka kimapenzi bado anashikilia msimamo wake ule ule wa kumkatalia, hata watu wazima wenye uwezo kipesa wanapomtaka Anna bado Anna anaonesha kutoyumba kimimamo kwa kuwakatalia. Rejea wimbo anaoimba Anna ukurasa wa 27,
                             “Anna Anna Anna mie niacheni mie x2
                              Msichana mdogo bado nasoma niacheni mie.
                              Muda wangu kufanya hayo haujafika mie.
                               Pesa zenu, na lifti zenu niacheni mie.
                               Anna Anna Anna mie niacheni x2”

ü Mwanamke amechorwa kama mtu anayepinga mabadiliko katika jamii, mwandishi anatuonesha kuwa mwanamke ni mtu asiyependa mabadiliko katika jamii, asiyependa kwenda na wakati, dunia inabadilika jamii inatakiwa kuwaelimisha vijana wao kuhusu elimu ya jinsia na mahusiano ,Mama Suzi anapinga, rejea Mama Suzi anaposema, “Tena ishia hapo hapo kaka! Huko si kunifundishia mwanangu umalaya? Umfunze mwanangu habari za ngono ilitoka wapi hiyo? {Uk. 9}

ü Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na msimamo, mwandishi anatuonesha kuwa, mwanamke ni mtu asiye na msimamo katika maamuzi yake, mwandishi anamtumia Suzi, kuijadili nafasi hii, richa ya Suzi kuamua kuachana na Joti na hata anapogundua kuwa Joti anamahusiano na wanawake wengine bado anakubali kuendelea naye. (Rejea uk. 17 na 21)
ü Vile vile, mwandishi amemchora mwanamke kama chombo cha starehe, anamtumia muhusika Joti ambaye anawatumia wanawake ili kujistarehesha kingono, lakini pia tunaona namna watu wanavyotumia pesa na vitu vya thamani ili kuwarubuni wasichana wapate kukidhi mahitaji yao ya kingono. {rejea ukurasa 27}

ü Mwanamke amechorwa kama mtu asiye na elimu juu ya mambo ya jinsia na ukimwi, katika kuilezea nafasi hii, mwandishi anamtumia muhusika Mama Suzi, ambaye anaoneka kutokuwa na ufahamu mzuri juu ya masuala ya UKIMWI, kwa mawazo yake anaamini kuwa ugonjwa wa UKIMWI ni ugonjwa unaowahusu watu wakubwa tu, na watoto hawawezi kuambukizwa jambo ambalo si sahihi. Hata katika jamii yetu, wapo watu wanaoamini kuwa ugonjwa huu wa UKIMWI huwakumba watu wazima watoto na watu walio katika ndoa hawawezi kuambukizwa virusi vya ukimwi jambo ambalo si kweli. Hivyo jamii inatakiwa kuelimishwa sana kuhusu ugonjwa huu.

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Taja maadui sita na fafanua jinsi waandishi wa tamthiliya mbili kati ya ulizosoma walivyojitokeza kupambana na maadui hao.
2.     Waandishi wa tamthiliya wamemchora mwanamke katika sura tofauti. Thibitisha kauli hii kwa kutumia waandishi wawili (2) wa tamthiliya mbili (2)ulizosoma.
MIGOGORO
Migogoro ni hali ya kutoelewana baina ya pande mbili, unaweza kuwa mgogoro kati ya mtu na mtu, mtu na kikundi cha watu, kikundi kimoja na kikundi kingine cha watu au unaweza kuwa mgogoro wa mtu na nafsi yake. Katika tamthiliya hii, mwandishi ameweza kuibua na kuonesha migogoro mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa migogoro hiyo imeweza kusaidia katika ujenzi wa dhamira mbalimbali zilizoweza kujitokeza katika kazi hii, migogoro iliyojitokeza katika tamthiliya hii ni:

ü Mgogoro kati ya Mama suzi na mwanaye,(Suzi) chanzo cha mgogoro ni Mama Suzi kukuta kasha la vidonge vya kuzuia mimba kwenye mfuko wa sketi ya Suzi, mgogoro unakua zaidi Mama Suzi kuamua kumuadhibu kwa kumchapa Suzi hadi anapotokea Mjomba na Baba Anna, kuamulia mgogoro huo na kushauri jambo la msingi ni kumpa elimu ya jinsia na si kutumia ukali na viboko, kama ambavyo Baba Anna anasema, “Watoto wajazwe elimu, waone uchafu na hatari ya kufanya haya. Siyo kuwatia hofu tu. Je leo ukifa ama kulazimika kuwa mbali nawe? Si atafanya tu maana mtia hofu hayupo?” {Uk. 13}

ü Mgogoro kati ya Mjomba na Mama Suzi, chanzo cha mgogoro ni kitendo cha Mjomba kumshauri Mama Suzi kuacha kumuadhibu Suzi na badala yake apewe elimu ya jinsia na mahusiano ya kimapenzi jambo linalopingwa na Mama Suzi na hivyo kuibua mgogoro. {Rejea ukurasa wa 8-14}


ü Mgogoro kati ya Suzi na Joti, mgogoro huu unaibuka baada ya Suzi kupigwa na mama yake sababu ya vidonge vya kuzuia mimba alivyopewa na Joti, mgogoro huu unafikia hatua ya Suzi kuamua kuachana na Joti, suluhisho la mgogoro huu, wanaamua kurudiana na kuendelea na uhusiano wao. (Rejea uk. 17 na 21)

ü Mgogoro kati ya Mwarami na rafiki zake yaani Jumbe, Joti na Choggo. Chanzo cha mgogoro ni kitendo cha Mwarami kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana, hatua inayosababisha kumtishia kumfukuza katika kundi lao, rejea ukurasa wa 24, Jumbe anapomwambia Mwarami, “Sasa bwana hapa kwenye grupu letu hatutaki tabia hiyo ya ushamba. La sivyotutakutoa umemba.” Suluhisho la mgogoro huu ni Mwarami kuamua kumshawishi Anna kimapenzi hata hivyo juhudi zake zinagonga mwamba.


ü Mgogoro kati ya Mama Joti na Mwanamke anayedhani anaingilia ndoa yake, Mama Joti anaona suluhisho la mgogoro huu ni kununua kanga zenye maneno ya vijembe ili kumpasha na kumuumiza roho, Rejea Mama Joti anaposema, “Lakini leo nimefika kikomo. Ndiyo mwisho wa kumvumilia huyu nguru anayeichimba ndoa yangu...Ngoja kwanza nimpashe najua litamuuma tu.” {Uk. 7}

ü Mgogoro mwingine ni kati ya Chausiku na Joti, chanzo cha mgogoro huu ni baada ya kugundua kuwa Joti anamahusiano ya kimapenzi na wasichana wengine, mgogoro unafikia hatua ya Chausiku kumtishia kumdhuru Joti, kama anavyosema, “We usinifanye mie bwege mwenzio...wewe ndiyo unajigonga gonga. Wewe na visichana vyako hivyo nitawachoma moto mie! Nyie hamnijui, ohoooo!” {Uk. 22}

ü Mgogoro kati ya ukale na usasa, huu ni mgogoro mwingine unaojitokeza katika tamthiliya, mwandishi anaonesha mgogoro kati ya watu wanaokumbatia mambo ya kale, mambo yaliyopitwa na wakati na wale wanaotaka mabadiliko katika jamii, mwandishi anawatumia wahusika, Mama Suzi na Baba Joti kama watu wanaokumbatia mambo ya kale na kwa upande mwingine anawatumia wahusika, Mjomba, Baba Anna na Mama Anna kama watu wanaotaka mabadiliko katika jamii, wanataka ukuta unaowatenga watoto na wazazi wao wasipate elimu ya jinsia ubomolewa, mwandishi anaonesha kuwa, kukumbatia mambo ya kale kunaweza kuleta madhara kwa vijana kama madhara ya kupata mimba kwa Suzi, rejea Suzi anaposema, “Mama hakuwa radhi kuachana na utamaduni wa kale wa kuweka ukuta baina ya wazazi na watoto katika kujadili mambo haya. Haya ndiyo madhara yake.” {Uk. 36}

ü Mgogoro wa Suzi na nafsi yake, chanzo cha mgogoro huu ni kitendo cha kuambiwa na mama yake kuwa shangazi yake ataenda kumpima mimba, Suzi anaona suluhisho la mgogoro huu ni kutokubali kwenda kupimwa mimba na shangazi yake na badala yake kumtafuta mwanaume anayehusika na mimba hiyo (Joti)  kuzungumza naye, rejea Suzi anaposema, “Oh Mungu wangu! Nifanye nini sasa? Siwezi kumruhusu shangazi akanipime...oh, nifanye nini mie! Nimtafute Joti, lazima niongee naye.” {Uk. 31}


ü Mgogoro mwingine unaojitokeza ni mgogoro wa Suzi na nafasi yake kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi au la, chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Suzi kugundua kuwa ana mimba na kijana aliyempa hiyo mimba ameathirika na virusi vya ukimwi, rejea Suzi anaposema, “Na mie Suzi nina mimba, mimba ya Joti. Kasha ina maana na mie nina ukimwi?” {Uk. 36}

UJUMBE
Ujumbe ni funzo analolipata fanani anaposoma ama kusikiliza kazi za fasihi, pamoja na ujumbe pia kuna maadili mbalimbali hupatikana, katika tamthiliya hii kuna mafunzo mbalimbali ambayo msomaji wa kazi hii anaweza kuyapata, mafunzo hayo ni kama:

ü Elimu ya jinsia na ukimwi ni muhimu kwa vijana ili kuwanusuru vijana na mimba za utotoni(mimba zisizotarajiwa) na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
ü Ukimwi hauchagui rika, mwandishi anatupa ujumbe kuwa gonjwa hili la UKIMWI hauchagui mtu, kila mtu anaweza kuupata, kama tunavyoona kwa Fausta na Joti, ni watoto wadogo lakini wanaathirika na virusi vya ukimwi na kusababisha vifo vyao.

ü Asiyefunzwa na mama yake, hufunzwa na ulimwengu, hili ni funzo linguine tunalilipata katika tamthiliya, mwandishi anatufundisha umuhimu wa wazazi kuwafundishi watoto wao maadili mema na si kuwaacha watoto wakajifunza wenyewe mtaani, wakiwaacha hivyo, huko hujifunza mambo yasiyofaa, tunaona kwa Suzi, Joti, Mwarami, Choggo, Jumbe, wazazi wao hawakuwafundisha elimu ya jinsia na mahusiano watoto wakajifunza wenyewe mambo machafu na hataimaye yakawaletea madhara.


ü Wazazi ndiyo walimu bora kwa malezi bora na maadili mema kwa watoto wao. Mwandishi anaendelea kutufundisha kuwa, ili vijana wetu wawe na tabia njema, mzazi ni mwalimu bora kabisa anayeweza kumfundisha mtoto wake vema, rejea mwandishi akimtumia muhusika Baba Anna anaposema, “Dunia imeharibika bwana. Mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha tena sasa si maadili mema bali njia potofu.”

ü Kinga ni bora kuliko tiba. Ni vizuri jamii ikajikinga na magonjwa mbalimbali, kuliko kutojikinga na baadaye kuanza kutafuta tiba, tiba huwa gharama sana kuliko kujikinga, tunamuona Baba Joti akitumia gharama kubwa kutafuta tiba  ya mtoto wake, kama ambavyo mwandisha anasema, “Mtani ushauza rasilimali zako kuuguza mtoto. Ushajitia umskini kwa kuhangaika...” {Uk. 34} Hivyo basi ni vema jamii ikaamua kujikinga dhidi ya matatizo mbalimbali kwani matatizo hayo pindi yanapokukumba huwa ni gharama sana kuyatatua na wakati mwingine matatizo mengine huwa hayana tiba kama tunavyoona katika ugonjwa wa UKIMWI.

ü Ngono zembe ni chanzo cha maambukizi ya virusi vya ukimwi na mimba zisizotarajiwa, Tunamuona Joti akiambukizwa virusi vya ukimwi kutokana na kushiriki ngono zemba, vilevile tunamuona Suzi akipata mimba na hata kuwa katika wasiwasi wa kuambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na kushiriki ngono zemba. (Rejea ukurasa wa 4 na 34)

Mafunzo mengine tunayoyapata katika tamthiliya hii ni pamoja na:
ü Jamii inatakiwa kubadilika ili kwendana na mabadiliko katika jamii.
ü Mila na desturi zilizopitwa na wakati hatuna mudi kuachana nazo
ü Huwezi kumtambua mtu aliyeathirika na virusi vya ukimwi kwa kumtazama kwa macho tu. Uk. 4-5
ü Vijana waelimishwe namna ya kukabiliana na changamoto za utandawazi.
ü Utandawazi ni chanzo cha mmong’onyoko wa maadili ya vijana.
ü Malezi bora ni muhimu kwa watoto/vijana ili kuwa na maisha bora baadaye.
ü Majuto ni mjukuu, tunamuona Suzi akijuta kutokana na kutopata elimu ya jinsia na hivyo kujikuta akitumbukia katika matatizo.

MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha ya kawaida, sentensi fupifupi na inayoeleweka kwa urahisi,pamoja na hayo mwandishi pia ametumia lugha ya kisanaa yenye mbinu mbalimbali za kisanaa kama vile nahau na tamathari za semi.

(a)  Matumizi ya methali
ü “Mzazi usipomfunza, walimwengu watamfundisha.” Uk.  
ü “Shukrani ya punda mateke.” {Uk. 19}

(b) Matumizi ya misemo na nahau
ü Shoga, mtakatifu wa kwenye mwanga si lazima awe mtakatifu gizani. {Uk. 4}
ü “Kakanyaga nyaya.” {Uk. 4}
ü “Potelea kwao...” uk. 9
ü “Makapera kibao, mume wangu wa nini. Uk. 7
ü “Wembamba wa reli treni inapita, uk 6
ü Kifua simkingii, maana siwi naye. Uk 6
ü “Kwa mashairi nimekuvulia kofia siku nyingi.” Uk.6
ü  “We pita juu mie nipite chini...”uk 19
ü Mbona umetuanika juani. Uk 16
ü “Hakikisha ndege mjanja ananasa katika tundu bovu.” Uk. 24

(c)  Matumizi ya taswira/lugha ya picha
ü Dubwana, Manaa yake ni kitu au mtu mwenye umbo kubwa lisilo la kawaida au la hovyo hovyo, mwandishi ametumia neno dubwana kitaswira kuufananisha ugonjwa wa Ukimwi sawa na jambo linalotisha, kuogopesha. (Rejea ukurasa wa 1-2)
ü Gizani, gizani ni mahali pasipokuwa na mwanga, hivyo mwandishi ametumia neno giza, akimaanisha kukosa maarifa au kutokuwa na ufahamu ya jambo fulani, kwa kifupi kukosa elimu,  Rejea mtambaji anaposema, “Kisiwa kizima kipo gizani...watoto ndio kabisa. Wapo katika giza nene.” {Uk. 13}

(d) Matumizi ya tamathali za semi.
(i)                Tashibiha, hizi ni tamathari ambazo hulinganisha vitu kwa kutumia viunganishi kama, mfano wa, sawa na, mithili ya, kama vile. N.k. baadhi ya tashibiha zinazojitokeza katika tamthiliya hii ni:
ü “Wewe nawe unakuwa nyuma nyuma kama koti.” Uk. 4
ü “Shoga mbona unakuwa mgumu kama mpingo?” uk. 5
ü “Watu walipukutika, wakapukutika kama majani ya kiangazi.” Uk.1
ü “Lile Dubwana limetanda kama utando wa buibui.” {Uk.13}
ü “Miti inayoungua kama mabua.” Uk. 6
  
(i)                Sitiari, hizi ni tamathari za semi ambazo hulinganisha vitu bila kutumia viunganishi, mfano wa tamathali zilizotumika ni pamoja na:
ü We mbwa mweusi.” Uk. 8
ü “Nyoka wee.” Uk.9

(ii)             Mjalizo, hii ni aina ya tamathali za semi ambazo msanii/mwandishi huitumia kutaja vitu au mambo yaliyo katika orodha bila kutumia viunganishi. Mfano:
ü “...Lakini soma maneno yake. Yamejaa kejeli, ushari, uchimvi, kusengenyana na kufumbiana mafumbo ya kila aina.” Uk. 6

(iii)           Nidaa, hizi ni tamathali za semi, zinazoonesha hali ya kushangaa au kushangazwa na jambo Fulani, mfano wa tamathali hizi ni:
ü “Ai, ai, lahaula lakwata...weye, hiki kitoto?” {uk. 9}
ü “Oi, oi, oi, toba! Kile si kitoto kama cha kwangu...” {uk.10}

(iv)            Takriri, hii ni hali ya kurudiarudia maneno, neno, silabi au sauti zinazolingana katika kazi ya fasihi ili kusisitiza au kutia mkazo jambo fulani. Mfano wa takriri zinazojitokeza katika tamthiliya hii ni:

ü “Watu walipukutika, wakapukutika kama majani ya kiangazi.     Wakapukutika.” Uk. 1
ü “Waongo! Waongo wakubwa.” Uk. 3
ü “ Vifo vikawazoa, vikawazoa...vikawazoa.” uk. 2
ü “Piga domo, piga doma, nikashinda.” Uk. 16

(v)              Tanakali sauti Hii ni aina ya tamathali ambayo sauti ya kitu fulani huigwa ili kwa lengo la kuburudisha au kuipa dhamira uzito falani. Mfano wa tanakali sauti zilizotumika katika tamthiliya hii ni:
ü “Wacha moyo unipwite pwi,pwi,pwi...” uk.16

(vi)            Tashititi Hii ni aina ya tamathari ya semi ambayo mtu huuliza swali huku jibu lake akilifahamu, mfano wa tashititi zinazojitokea katika tamthiliya hii ni:
ü “Huyu ni Suzi kweli au nani?” uk.15

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Lugha ni kipengele muhimu sana kwa mwandishi katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii. Jadili kauli hii kwa mifano toka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
MTINDO NA MUUNDO
(a)  Mtindo
Mtindo ni jinsi msanii anavyotumia ufundi, umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo fulani katika kazi ya fasihi, na mtindo ndiyo huweza kumtofautisha msanii/mwandishi mmoja na mwandishi mwingine. Mtindo hutumika kuipamba kazi ya fasihi, baadhi ya mitindo nayotumika katika kazi hii ni pamoja na:

ü Matumizi ya hadithi ndani ya tamthiliya
Mwandishi ametumia mtindo wa hadithi ambao ni utanzu wa fasihi simulizi ndani ya tamthiliya, mtindo huu unajidhihirisha ukurasa wa kwanza, Mtambaji anapoanza kusimulia hadithi anaposema, “Paukwa” na hadhira inaitikia “Pakawaaaaaaa” na Mtambaji anaendelea, “Hapo zamani za kale paliondokea kisiwa kimoja...” {Uk. 1} Ni utanzu wa hadithi pekee ndiyo huwa na mwanzo wa namna hiyo.

ü Matumizi ya wimbo/shairi ndani ya tamthiliya
Mwandishi pia ametumia wimbo kuipamba kazi yake, wimbo unajitokeza ukurasa wa 27 Anna anaimba wimbo unaowataka wanaume wanaomtaka kimapenzi kuacha kumfuatafuata, muda wake wa kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi haujafika bado mwanafunzi.                          
                              “Anna Anna Anna mie niacheni mie x2
                              Msichana mdogo bado nasoma niacheni mie.
                              Muda wangu kufanya hayo haujafika mie.
                               Pesa zenu, na lifti zenu niacheni mie.
                               Anna Anna Anna mie niacheni x2”

ü Matumizi ya lugha ya majibizano/dialojia na masilmulizi
Kama ilivyo ada, mtindo wa lugha unaotumika katika tamthiliya, kwa asilimia huwa ni mtindo wa majibizano, yaani dialojia. Hivyo basi hata katika tamthiliya hii, mwandishi kwa kiasi kikubwa ametumia mtindo wa majibizano na kidogo ametumia masimulizi, (Rejea masimulizi ya Mtambaji ukurasa wa 1-2, 3-4, na 36)

ü Matumizi ya nafsi zote tatu
Pia nafsi zote tatu zinajitokeza katika tamthiliya hii,
ü Nafsi ya kwanza, mfano,Mimi nawashangaa... {Uk. 6} Najua litamuuma tu (uk.7), Tumebomoa ghala imara...” {Uk. 6}
ü Nafsi ya pili, mfano, Utamaliza kanga zilizoandikwa kila aina ya maneno...”
            Wewe unamwona Fausta alikuwa mdogo?
ü Nafsi ya tatu, mfano, ...alikufa kwa ukimwi” uk. 9, atakutafuta tu mwenyewe.” (uk 17), “Wanashindwa kutofautisha kati ya puto na kondomu.” (Uk. 13)

ü Matumizi ya picha, mwandishi pia ametumia michoro mbalimbali inayoonesha matendo/matukio mbalimbali ya wahusika, picha hizi zimesaidia sana kuipamba na kuipendezesha kazi yake, picha hizo zinapatikana ukurasa wa 3,5,8,11,17,20,23,27, 29 na 35.

(a)  Muundo
Muundo ni mfuatano wa masimulizi au visa katika kazi ya sanaa ya fasihi, hivyo basi.muundo wa tamthiliya hii ni wa moja kwa moja, yaani visa vyake vimepangwa kuanzia kisa cha kwanza , kati hadi mwisho, katika kuvipanga visa vyake, mwandishi ameigawa kazi yake katika sehemu sita, ambazo amezipa majina, Sehemu ya kwanza, Sehemu ya Pili, ya Tatu, ya Nne, Tano na Sehemu ya Sita.

Sehemu ya kwanza.
Mtambaji anasimulia habari za Dubwana(Ukimwi), anasimulia namna wakubwa wanavyoelimishana namna ya kujilinda na ugonjwa huo, huku wakiwaacha watoto wakiangamia kwa kukosa elimu ya jinsia na ukimwi.

Sehemu ya Pili
Hapa mwandishi anatuonesha nyumbani kwa Mama Suzi, Mama Suzi na Mama Joti wanapeana habari za kifo cha Fausta kilichosababishwa na ukimwi, Mama Suzi anakuta kasha la vidonge kwenye mfuko wa sketi ya Suzi wakati akifua jambo linalozua mgogoro kati ya Suzi na mama yake, Mjomba na Baba Anna wanamshauri Mama Suzi kuacha kutumia ukali na badala yake anatakiwa kumpa elimu ya jinsia binti yake ili ajitambue jambo linalopingwa vikali na Mama Suzi.

Sehemu ya Tatu
Hapa mwandishi anatuonesha mtaani, Joti anakutana na Suzi, Suzi anaamua kuachana na Joti kwa sababu ya vidonge vya kuzia mimba alivyopewa na Joti kumsababishia kupigwa na mama yake. Joti anawasimulia wenzake namna alivyofanikiwa kumpata Suzi, Joti, Jumbe, Choggo na Mwarami wanaenda mtaani kuangalia sinema za X.

Sehemu ya Nne
Tukio linatendeka njiani, Joti na Suzi wanakutana, Suzi anamlaumu Joti kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasichana wengine, wanaamua kurudisha uhusiano wao, Joti anaanza kujisikia vibaya, Jumbe anaamua kumpeleka nyumbani, Mwarami anaonekana akimshawishi Anna amkubalie ombi lake la kuanzisha mahusiano ya kimapenzi, Anna anaonesha msimamo anamkatalia, mwandishi pia anatuonesha namna Anna anavyoshinda vishawishi vya kingono.

Sehemu ya Tano
Tukio linatendeka chumbani kwa Suzi akiwa na Anna, Suzi anajisikia vibaya, anahisi huenda ana mimba, anataka kuitoa, rafiki yake Anna anamshauri kuachana na mpango huo kwani ni hatari, anaamua kwenda kwa Joti kuzungumza naye suala hilo.

Sehemu ya Sita
Hii ni sehemu ya mwisho, mwandishi anatuonesha nyumbani kwa Baba Joti, tunaona namna Baba Joti alivyoangaika kwa waganga mbalimbali kutafuta tiba ya Joti bila mafanikio, mwisho wanaamua kumpeleka hospitali, huko wanapata wajibu kuwa Joti amethirika na virusi vya ukimwi, Jirani anamshauri Baba Joti kumpeleka Joti kwa mganga mwingine, Mjomba anamshauri Baba Joti kuachana na mpango huo kwani ugonjwa alionao Joti hauna tiba wala dawa. Suzi anawasili kwa akina Joti anagundua Joti ana ukimwi, Joti anafariki dunia, Suzi anakuwa na wasiwasi kama naye atakuwa ameambukizwa virusi vya ukimwi, anabaki akijutia kwa kukosa elimu ya jinsia na ukimwi.  Na mchezo unaishia hapo.

MANDHARI
Mandhari ni sehemu au eneo ambalo visa na matukio hutendeka katika kazi ya fasihi, katika kazi ya fasihi mandhari huweza kuwa mandhari halisi au ya kubuni, katika tamthiliya mwandishi ametumia mandhari ya kubuni, hivyo basi, mandhari ya tamthiliya hii yanaweza kuwa sehemu yoyote ile katika nchi za Kiafrika. Pia mwandishi anatuonesha visa na matukio yakitendeka mandhari ya nyumbani, mtaani, njiani n.k.
Mandhari ya nyumba
Katika mandhari ya nyumbani, tunaona nyumbani kwa Mama Suzi na Nyumbani kwa Baba Joti, kwa Mama Suzi tunaona ukuta uliowekwa kati ya mzazi na mtoto kuhusu elimu ya jinsia kwa mtoto, Mama Suzi anamuadhibu Suzi kwa kukuta vidonge vya kuzuia mimba kwenye mfuko wa sketi ya Suzi, Suzi anaanza kujisikia vibaya, anafikiria kuitoa mimba. Nyumbani kwa Baba Joti, tunaona kuumwa kwa Joti, kugundulika kuwa ana ukimwi na kufariki kwake.
Hivyo mwandishi ametumia mandhari hii, ili kufikisha dhamira ya umuhimu wa elimu ya jinsia kwa watoto, malezi bora ya mtoto, tatizo la ugonjwa wa ukimwi na athari zake katika familia, n.k.
Mandhari ya Mtaani
Katika mandhari haya, mwandishi, anatuonesha Joti na Suzi wakiwa katika mazungumzo ya uhusiano wao wa kimapenzi, pia tunaoneshwa kuwa ni mahali ambapo Joti na wenzake hukutana na kupanga mambo yao ya mapenzi. Mwandishi anatumia mandhari haya, kuonesha namna watoto wanavyoharibikiwa kitabia mtaani, mandhari ya njiani inatuonesha namna watoto wakike wanavyosumbuliwa na wanaume wasiokuwa waadilifu ambao huwataka kimapenzi.

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.      Jadili jinsi fani ilivyotumika kukamilisha kazi za waandishi wawili wa tamthiliya ulizosoma ukizingatia mtindo na mandhari.
FALSAFA, MTAZAMO NA MSIMAMO WA MWANDISHI
(a)  Falsafa ya mwandishi
Falsafa ni mchujo wa mawazo ya mwandishi kuhusu maisha na jamii yake. Falsafa ya mwandishi wa tamthilia hii anaamini kuwa, ili jamii yoyote ile iweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii husika, elimu ni nyenzo muhimu sana ya kupambana na changamoto hizo. Na elimu hiyo isitolewe kimatabaka.

(b) Mtazamo wa mwandishi
Mwandishi ana mtazamo wa kiyakinifu, ana mtazamo kuwa, matatizo yote yanayotokea katika jamii chanzo ni jamii yenyewe na jamii yenyewe ndiyo inayotakiwa kukabiliana na matatizo hayo, na ndiyo maana anaitaka jamii yake ibadilike.

(c)  Msimamo wa mwandishi
Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi, kwani anaitaka jamii yake ibadilike ili kuendana na wakati, na anaitaka jamii kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu au tamthiliya hii ni Kilio Chetu,kilio chetu ina maana ya tatizo, balaa au janga linapoingia katika jamii ni letu sisi sote. Hivyo basi, jina la kitabu Kilio Chetu linasadifu sana yaliyomo katika tamthiliya hii. Tukianza na:

Tatizo la ukimwi
Mwandishi anajadili ukimwi kuwa ni ugonjwa hatari sana, ni ugonjwa usiobagua mkubwa wala mtoto, kama mwandishi anavyosema, “Ukimwi hauchagui mkuwa wala mdogo.” {Uk. 25} hii inathibitisha kuwa tatizo hili la ukimwi ni letu sote tunatakiwa wote kupambana nalo, na hapa ndipo linapokuja suala la Kilio Chetu.
Elimu ya jinsia
Mwandishi pia anaonesha kuwa suala la watoto/vijana kupewa elimu ya jinsia na ukimwi ni kilio cha jamii, jamii inasisitiza na kupigia kelele suala la vijana kupewa elimu ya jinsia na ukimwi, kwa mfano, mwandishi anamtumia muhusika Baba Anna anaposema, “Mimi bwana nitaendelea kusisitiza juu ya elimu hii.” Mwandishi anaendelea kwa kusema akimtumia muhusika Mjomba, “Tutaendelea kuwaelimisha wazazi umuhimu wa elimu hii.” {Uk.12} Hivyo tunaona kuwa Baba Anna na Mjomba wanatoa kilio chao cha kutaka watoto kuelimishwa elimu ya jinsia.

Si vivyo tu, hata vijana wenyewe, wanapaza sauti, wanatoa kilio chao kutaka kupewa elimu hii ya jinsia na ukimwi, mwandishi anatuonesha kuwa kama vijana wangepata elimu hii wasingeatwa na matatizo, kama anavyosema Suzi, ““Naapa kwa Mungu wangu, mimi na Joti tungepata bahati ya kuelimishwa, tusingetumbu...” {Uk. 36} Pia rejea Mtambaji anaposema, “Watoto hawana uwezo wa kukabiliana nalo...Sikieni kilio chetu!” {Uk. 15}
Hivyo basi, kwa ushahidi huu ni wazi kuwa, jina la kitabu linasadifu yale yote yanayozungumzwa katika tamthiliya hii, na kwa hili mwandishi amefanikiwa sana.
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
(a)  Kufaulu kwa mwandishi.
Hapa tunaangalia kufanikiwa kwa mwandishi katika vipengele vya fani na maudhui, Kifani mwandishi amefanikiwa sana, tukianza na:

Wahusika
Mwandishi amefanikiwa kuwajenga wahusika wake vizuri, amewajenga wahusika katika rika tofauti tofauti na kila rika amefanikiwa kuwavisha uhusika unaendana na rika husika, na amafanikiwa kuonesha namna kila rika linavyoweza kuathiliwa na UKIMWI na kuitaka jamii kutoa elimu ya jinsia kwa kila rika.

Lugha
Mwandishi amefanikiwa kuifanyanga lugha yake kiufundi, amefanikiwa kutumia lugha nyepesi inayoeleweka na kila mtu inayoambatana na matumizi ya methali, misemo/nahau na tamathali za semi, matumizi yote haya ya lugha yamesaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha ujumbe uliokusudiwa na kuipamba kazi husika. (Rejea kipengele cha Matumizi ya lugha)
Mtindo, katika suala la mtindo, mwandishi amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, kwani amefanikiwa kutumia utanzu wa hadithi na wimbo kuipamba kazi yake na ikawa kazi ya kuvutia na inayovuta hisia za msomaji kupenda kuendelea kukisoma kitabu hiki zaidi na zaidi. (Rejea kipengele cha Mtindo)
Muundo
Mwandishi ametumia muundo rahisi, muundo unaeleweka kwa urahisi na hivyo kumsaidia mwandishi kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii husika, visa vyake amevipangalia vizuri hali inayomfanya msomaji apende kuendelea kukisoma kitabu hiki ukurasa mmoja hadi mwingine hadi anakimaliza kitabu hiki.

Kwa upande wa maudhui, mwandishi amefanikiwa kuonesha dhamira mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zina uhalisia katika jamii yetu. (Rejea dhamira)

Vilevile, kwa upande wa ujumbe, mwandishi  amefanikiwa kutupa ujumbe au mafunzo muhimu sana ambayo kama jamii itayazingatia basi mafunzo haya yanaweza kuwasaidia sana. (Rejea Kipengele cha ujumbe)

Migogoro, mwandishi amefanikiwa kuibua migogoro, kuonesha chanzo, upeo na hata baadhi ya migogoro amefanikiwa kuitolea suluhisho. (rejea kipengele cha Migogoro)

(b) Kutofaulu kwa mwandishi
Kutofaulu kwa mwandishi tunaangalia mapungufu tunayokutana nayo katika kazi ya fasihi, hivyo basi, kama ilivyo kawaida huwa hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro, hivyo hivyo katika tamthiliya hii, tunakutana na baadhi ya kasoro ambazo si nyingi, baadhi ya kasoro hizo au mapungufu ni pamoja na,
ü Mwandishi ameshindwa kutuonesha mwanamke aliyemuambukiza Joti virusi vya UKIMWI.
ü Mwandishi pia ameshindwa kutuonesha hatima ya akina Jumbe na Choggo kama nao waliathirika na UKIMWI au la, maana hawa wote matendo yao alikuwa yanafanana tu na Joti.
ü Mwandishi ameshindwa kutuambia alipo baba yake, kama amesafiri au amefariki.
ü Mwandishinpia ameshindwa kuonesha umuhimu wa watu kujitokeza kupima afya zao, kwa mfano Suzi anaoenesha kuwa na wasiwasi kama naye ameambukizwa au la, mwandishi alitakiwa aoneshe Suzi anaamua kwenda kupima afya yake.

Mfano wa maswali unayoweza kuulizwa sehemu hii
1.     Ukitumia vitabu viwili vya tamthiliya, jadili jinsi waandishi wa vitabu hivyo walivyofanikiwa kifani na kimaudhui.
Mwisho


Mwandishi ni Mwalimu Shule ya Sekondari Mwanzi-Manyoni (Singida) anapatikana kwa namba zifuatazo:

Mawasiliano: 0715 33 55 58 (whatsapp)
                       0755 44 06 99
Nifollow instagram: fullraha17
Facebook: Furaha Venance