Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja
Sunday, November 4, 2012
Afisa Elimu avuliwa madaraka
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma,
limemvua madaraka ofisa elimu wa shule za sekondari, Bilungama Nyalinga,
kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Akitoa taarifa ya kuvuliwa madaraka hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Juma Maganga, alisema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya tume kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili ofisa huyo.
Maganga alizitaja tuhuma zilizokuwa zikimkabili kuwa ni kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, matumizi mabaya ya fedha za ofisi, kuwa na mahusiano mabaya na walimu anaowaongoza, na kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani hapo.
“Nyalinga hatakuwa na cheo cha ofisa elimu katika wilaya hii kuanzia sasa, na anaruhusiwa kukata rufaa mahali popote tangu pale atakapokuwa amepokea barua ya kumtaarifu juu ya suala hili,” alisema Maganga.
Alisema kuwa kabla ya kuvuliwa madaraka, alisimamishwa kazi na baraza hilo kwa miezi mitatu iliyopita na kuundwa kwa tume ya uchunguzi iliyokuja na ripoti ya kubaini madudu hayo yaliyokuwa yakimkabili.
Akitoa taarifa ya kuvuliwa madaraka hayo wakati wa kikao cha baraza la madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Juma Maganga, alisema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya tume kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili ofisa huyo.
Maganga alizitaja tuhuma zilizokuwa zikimkabili kuwa ni kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, matumizi mabaya ya fedha za ofisi, kuwa na mahusiano mabaya na walimu anaowaongoza, na kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani hapo.
“Nyalinga hatakuwa na cheo cha ofisa elimu katika wilaya hii kuanzia sasa, na anaruhusiwa kukata rufaa mahali popote tangu pale atakapokuwa amepokea barua ya kumtaarifu juu ya suala hili,” alisema Maganga.
Alisema kuwa kabla ya kuvuliwa madaraka, alisimamishwa kazi na baraza hilo kwa miezi mitatu iliyopita na kuundwa kwa tume ya uchunguzi iliyokuja na ripoti ya kubaini madudu hayo yaliyokuwa yakimkabili.
Mikoa vinara biashara ya binadamu yatajwa, Mkoa wa Singida ukiwemo
SHIRIKA la mtandao wa vijana linalojishughulisha na uzuiaji wa vitendo vya
kikatili dhidi ya wanawake (Y2Y Movement), limeitaja mikoa ya Mara na Singida
kuwa bado inakabiliwa na janga kubwa la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake,
ikiwa ni pamoja na biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Mbali na mikoa hiyo, mikoa mingine iliyotajwa kuendeleza vitendo hivyo vya
kinyama, ni pamoja na Mwanza na Shinyanga, ambapo imeelezwa kwamba zaidi ya nusu
ya wanawake na wasichana wamekuwa wakitendewa ukatili huo, huku asilimia 40 ya
kundi la vijana wa kuanzia miaka 10 hadi 24 bado wanaamini kuwa mwanamke anayo
haki ya kuteswa.
Akitoa mada katika semina ya kupambana na ukatili iliyofanyika jijini hapa,
Mkurugenzi wa shirika hilo, Hellen Mahindi, alisema vijana wa mikoa ya Mara,
Singida, Shinyanga na Mwanza wamekuwa wakijihusisha na ukiukwaji wa haki za
binadamu kwa kumnyanyasa mwanamke.
Mahindi alisema baadhi ya jamii ya Mkoa wa Singida wamekuwa wakijihusisha na
biashara haramu ya kusafirisha watoto wa umri mdogo kwenda mkoani Tabora kwa
ajili ya kuwatumikisha katika baadhi ya shughuli, ikiwa ni pamoja na kutega na
kufuga nyuki, kulima na kufanyishwa kazi ngumu za majumbani.
Aliitaka serikali kupitia vyombo vyake vya dola kufanya uchunguzi wa kina
katika suala hilo, kisha hatua kali zichukuliwe mara moja kwa watu wote
watakaobainika kuhusika na biashara hiyo haramu ya binadamu.
Alisema kuwa, lazima wanaharakati, mashirika na serikali washirikiane kwa
pamoja kudhibiti hali hiyo na kujenga taifa lenye mtazamo chanya wa
kimaendeleo.
“Asilimia 40 ya kundi la vijana bado wanaamini haki ya kunyanyaswa mwanamke.
Hivi ni vitendo vibaya na tunatakiwa sote kwa pamoja tuunganishe nguvu
kutokomeza kabisa ukatili wa namna hii, maana binadamu wote ni sawa,”
alisema.
Mahindi alisema kuwa wamelenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 asilimia
kubwa ya vijana nchini watakuwa wameelimika na kuachana kabisa na unyanyasaji
huu wa kijinsia.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili 04 Nov. 2012
CHILIGATI AWAONYA WANAOTAKA MUUNGANO UVUNJWE
Asema: Kama muungano ungekuwa ni sumu inayojaribiwa, tungethubutu kuuvunja kwa muda kidogo...
Katika kuchangia maoni yake kwa tume ya mabadiliko ya katiba. Mh. Chiligati amenukuliwa akisema.; “Kama muungano ungekuwa ni sumu
inayojaribiwa, tungethubutu kuuvunja kwa muda kidogo, kule Zanzibar Watanzania
elfu 15, na Wanzanzibari walioko bara laki 2.5 waonje adha ya kutafuta hati ya
kusafiria au waambiwe wahame, tungejaribu kufanya hivyo.”
Aliendelea kukosoa mfumo wa serikali tatu ambao baadhi ya wabunge walikuwa wakiupendekeza, Chiligati alisema kuwa, unaongeza gharama kwa
sababu utahitaji Baraza la Mawaziri na rais mwingine, na kwamba Tanganyika
iliyokufa itabidi ifufuliwe.
Maoni hayo ya Mh. Chiligati yametolewa jana ikiwa ni siku tatu kabla ya ukusanyaji wa maoni kwa wakazi wa Manyoni kuanza rasmi siku ya jumanne tar. 06 Nov. Je wanamanyoni tunasemaje? tunataka katiba ijao iweje? basi tujitokeze kwa wingi siku hiyo ili kushiriki kutoa maoni yetu na hivyo kuwa sehemu ya mabadiliko ya Katiba hayo.
Saturday, November 3, 2012
WABUNGE WATOA MAONI YAO KUHUSU KATIBA MPYA
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, pamoja na mambo mengine..Wataka Umri wa mgombea uraisi upunguzwe toka miaka 40 hadi 35...Wataka Mawaziri wateuliwe nje ya wabunge...Uteuzi wa viongozi wa juu uthibitizhwe na Bunge...Idadi ya Wizara ijulikane kikatiba na ziwe chache...
Wataka matokeo ya rais yapingwe mahakamani...Muungano wa kimkataba (treaty-based union)...Rais wa Zanzibar awe Makamu wa rais...Majina matatu ya jaji mkuu yapendekezwe kwa rais kwa uteuzi na jaji athibitishe na Bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwaondoa mpaka ridhaa ya wabunge, Hapa inahusu pia uteuzi wa CDF,IGP, Mkuu wa TISS, Magereza, Uhamiaji nk....
Wataka pia ubunge na udiwani uwe na kikomo...Viti maalumu vifute na badala yake majibo yawe ni wilaya na kuwe na mgombea ubunge na mgombea mwenza wake..Kama mgombea ni mwanaumwe, mgombea mwenza awe mwanamke na akichaguliwa mmoja wote wameshinda kama kwa rais...Uraisi uwe wa Kipindi kimoja cha miaka 7.....
...
Pia uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship)...Kuwe na tume kikatiba itakayo shunghulikia kero za Muungano...Chiligati ataka Articles of Unioni zirejee kama ilivyokuwa mwanzo mambo 11...Mafuta gesi visiwe vya Muungano (hapa ni wabunge wa CCM na CUF bara na Visiwani waliungana)....Ubunge na Udiwani uwe na kikomo cha vipindi viwil (Miaka mitano kila kipindi)
Na Zitto Kabwe na Moses Machali wataka vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa viondolewe, Esther Bulaya ataka Muungano wa Serikali Tatu.
Habari kwa msaada wa Dickson Ng'hily
Friday, November 2, 2012
JK KUTUA MANYONI TAR 5 NOV 2012 KUZINDUA BARABARA
RATIBA NZIMA HII HAPA
MH. RAIS atakuwa ziarani ktk wilaya ya Manyoni tarehe 5 nov kwa mujibu wa maelezo ya mbunge wa manyoni Mashariki mh. Chiligati ratiba itakuwa kama ifuatayo, namnukuu kupitia post yake aliyoipost katika faceebook,"... na kwamba asubuhi atakuwa Itigi kuzindua ujenzi wa barabara uliyoitaja ya manyoni-itigi-chaya hadi Tabora kwa kiwango cha lami! na siku hiyo mchana atakuwa manyoni mjini ambako atazindua barabara ya lami iliyokamilika kutoka manyoni hadi Isina (53km) pia atahutubia mkutano wa hadhara! Hivyo wana manyoni mjini tujitokeze kwa wingi kuja kusalimiana na Mhe Rais wetu mpendwa! Barabara hizi ni fursa kwa wana manyoni kuzitumia kuboresha biashara na kilimo kwani zinasogeza masoko karibu yetu!kazi ya serkali ni kujenga mazingira(kuweka fursa) wanaozitumia wanapata maisha bora na wasiozitumia hubaki maskini!Tutumie fursa hizo ili tupate maisha bora! "Inawezekana , kila mmoja wetu atimize wajibu wake"
Hivyo wanamanyoni tuchangamkie fursa hiyo.
Saturday, June 2, 2012
Mfadhili Uamsho Zanzibar mbaroni
| Mfadhili Uamsho Zanzibar mbaroni |
| Jumamosi 02 Juni 2012 |
KIONGOZI Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) ambaye pia anadaiwa kuwa mfadhili wa kundi hilo, Sheikh Azzan Khalid Hamdan amewasili jana jioni katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar kutoka nchini Oman alipokwenda kwa ajili ya matibabu, kisha kukamatwa na polisi. Sheikh Azzan ni miongoni mwa viongoni waliokuwa wakisakwa na polisi akihusishwa na vurugu zilizotokea wiki iliyopita ikiwa pamoja na kufanya maandamano bila kibali. Baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege, Sheikh Azzan alikwenda moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Mfenesini kujisalimisha na kutoa taarifa kuhusu kuvunjwa kwa milango ya nyumba yake wakati akiwa safarini. Kukamatwa kwake kumekuja siku moja tangu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ally Mohamed Shein atoe ahadi ya wahusikawa vurugu hizo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria. Sheikh Azzan alisema hakutoa taarifa za ujio wake huo kutokana na kuogopa mkusanyiko usio rasmi ambao ungeweza kusababisha kutokea vurugu nyingine visiwani humo. “Unajua hamasa za watu ni kubwa hasa vijana wangekuwa wamepata taarifa za kuja kwangu basi wangejaa hapa uwanja wa ndege na jambo hilo lingeweza kuhatarisha shughuli za uwanja huu ndio maana nikaamua kuja kimya kimya,” alisema Sheikh Azzan muda mfupi baada ya kushuka katika ndege ya Shirika la ndege la Oman Air. Wakati Sheikh huyo akiwa safarini Oman, Zanzibar kulitokea maandamano ambayo yaliandaliwa na viongozi wa jumuiya yake yalioanzia Viwanja vya Shule ya Lumumba kupitia barabara ya Kinazini, Michenzani, Biziredi na kuishia katika viwanja hivyo vya Lumumba, kisha kufanyika mhadhara mkubwa uliozungumzia suala la mfumo wa elimu na matokeo mabovu ya mitihani Zanzibar. Hata hivyo, maandamano hayo yalibandikwa jina la matembezi ya amani yalikwisha salama na waandamanaji wakarudi majumbani, lakini baada ya muda, kulizuka ghasia muda mfupi baada ya kiongozi na mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mussa Juma kukamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano. Kiongozi huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Madema Mjini Zanzibar na kusababisha mamia ya vijana kufika katika kituo hicho wakitaka aachiwe, na waliapa kutoondoka kituoni hapo hadi asubuhi, kitendo ambacho kiliwalazimisha polisi kurusha mabomu ya machozi usiku kucha na vurugu hizo kuendelea hadi siku ya pili. Jeshi la polisi bado linawatafuta viongozi wengine wa jumuiya hiyo walioandaa maandamano hayo akiwamo Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Abdallah Said Madawa, Sheikh Fikirini Majaaliwa Fikirini, Sheikh Suleiman Juma, na Sheikh Sadifa Haji Sadifa. Katika vurugu hizo makanisa matatu yalichomwa moto na mali kadhaa kuteketea ikiwamo magari na nyumba za watu. Chanzo: Gazeti la Mwananchi 02 Juni 2012 |
Subscribe to:
Posts (Atom)
.jpg)




















