Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Thursday, July 4, 2013

STORY NZIMA NA PICHA ZA JOYCE KIRIA KWENDA GEREZANI TABORA KUMUONA MUME WAKE AMBAYE PIA NI KAMANDA WA CHADEMA HENRY KILEWO

SAFARI YANGU YA KWENDA TABORA.

 
S
[Joyce.jpg]afari yangu kuelekea mkoani tabora ilikuwa na changamoto nyingi, Ila kubwa namshukuru Mungu nilifika salama na kurudi salama. Najua kuna FANS wangu wengi wananipa support haswa katika maombi ya familia yangu. So najua itakuwa vizuri kama nitashare na nyie jinsi safari yangu nzima ilivyokuwa.
Nimetumia siku tano so nitakuwa naielezea kwa day after day ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka naenda mpaka narudi.
 
 
 
I
la wakati naipanga hii safari ili kwenda kumuona mume wangu, iliniweka katika wakati na maamuzi magumu sana kama fans zangu mnavyofahamu nina watoto wadogo akiwepo mdogo wa miezi mine 4,  Tabora ni mbali sana ni mwendo wa karibia masaa 14 kutokea Dar Es Salaam watoto ni wadogo nikisafiri nao nikaona nitakuwa nawatesa,  Nikafanya maamuzi magumu mno ya kuwaacha wanangu kwa wadada wasaidizi wangu wa nyumbani. Hizi ni changamoto za maisha inapofika wakati mgumu kama huu ulionifikia mimi inabidi ufanye maamuzi mazito, so nikawaacha wanagu Lincon na Linstone.
 
Lincon na Mdogo Wake Linston.

DAY1. IJUMAA 28/06/2013
 
S
iku ya Ijumaa tarehe 28/June Tulikutana Ubungo, Tukitumia usafiri binafsi na tulikuwa watu 5. Tukaanza safari yetu na tunamshukuru mungu tulifika salama Mkoani Morogoro, Tukaendelea na safari  Ila tukiwa kati ya Morogoro na Dodoma gari yetu kidogo ikaleta tabu,
 
 hapa ni kati ya Moro na Dom
Baridi ya hapa ilikuwa ni balaa.
hapa baba mkwe akicheki tatizo la gari.
Baada ya dk kadhaa gari ikawa iko poa.
 Baada ya gari kuwa poa tukaendelea kwa safari tukaingia Dodoma, Tukapata chai kidogo 
Tukisubiria Chai hapa ni Dodoma.
 Baada ya chai tukirudi garini kuendelea na safari.
 na gari nayo ikapata lishe/mafuta. then tukaendelea na safari. 
 
Tulipofika Ikungi  Kabla hatujafika Singida mjini gari ikaharibika tena , dereva akasema ni tatizo dogo linarekebishika fasta then tutaendelea na safari,
 Tukapata Fundi pale pale Ikungi, hapa akitazama tatizo.
 dah ikawa vise versa tatizo likawa kubwa, it was around saa tisa hivi alasiri tupo Ikungi, mpaka saa 6 usiku gari haikufaa ikabidi tutafute hotel kulala hapo.
 Mida ya saa sita hivi gari ikawa bado haijatengamaa.

   DAY2.JUMAMOSI 29/06/2013
 
S
iku ya pili tukaamka na kujiandaa, ila mpaka tunamalizia kujiandaa gari ilikuwa bado haijatengamaa, ili wote tusiwe tumestuck sehemu moja tukaamua kugawana wengine wabaki na gari na wengine tutangulie. Kutokea hapo Ikungi tukapata usafiri wa NOAH mpaka Singida Mjini si Mbali sana ilikuwa mwendo kama wa dk 20 ama 30 hivi, Tulipofika Singida Mjini tukapata HIACE ambayo tulianza safari kuelekea Igunga.
 hapa ilibidi tufanye safari za kuunga unga mana usafiri pia ulikuwa wa tabu, 
mwendo wa masaa kama mawili na nusu ama matatu tukawa tumefika Igunga, tukakata tiketi za kuelekea Tabora mjini..
 Hapa ni stendi Igunga tukisubiria basi.
 
 Usafiri ni wa Tabu mno tukapata basi ila tulikosa siti takasimama ,
 
 it was a very rough road kutokea hapo Igunga mpaka Tabora mjini na ni mwendo karibu wa masaa 3 na nusu hivi, Ila Mungu alisadia tukafika salama Tabora mjini mida ya saa 11 kama na dk 20
 Mwenyeji wetu akitusaidia kutuonyesha hoteli.
Kutoka stendi ya mabasi mpaka ilipo hoteli ni mwendo wa dk 2 tu kwa miguu.
na kuanza tafuta hotel. By the way nilitamani sana nikiingia Tabora nielekee Gerezani Ila nilikuwa nilishachelewa kwa uliza uliza niliambiwa Kutembelea gerezani mwisho ni saa 9 alasiri.
 Uchovu wa safari.
 
 
K
atika kuulizia ulizia hoteli tukapelekwa Hotel inaitwa Mwafrika Hotel, Pale Tulikosa nafasi ila meneja wa pale akachukua jukumu la kututafutia sehemu nyingine , tukapata sehemu nyingine lakini tukapanga next day wakitoka watu tutarudi pale.
 Aliyevaa Jezi ni Meneja Wa Mwafrika Hoteli, Anayenielekeza ni Mmiliki wa Mwafrika Hotel.
Huyu ni shemeji yangu kabisa kabisa, ni mume wa dada yangu"post ya changamoto na Opportunity" mtamfahamu vyema. Hapa ndo alituchukua na kutupeleka hotel nyingine kwa usiku huu.

DAY3. JUMAPILI
Tuliamka asubuhi tukajiandaa kuelekea gereza Kuu Uyui, ila tulipitia Mwafrika hotel kuacha mizigo yetu mana kwa siku hiyo tutakuwa pale.
Then safari ya kuelekea Gereza Kuu la Uyui,
 
S
i mabali kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5 hivi kwa Gari, tukawa tumefika gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata kujiandikisha na kila kitu halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana pia tulikuta watu wengine ambao nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na sie tukaitwa katika listi tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria zao za kuzima simu na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko kijichumba kidogo tu.
 
K  
 
iukweli it was a very SAD moment, nilipomuana mume wangu, akiwa kwa upande wa pili na sikuwa namuona vizuri mana hiyo nyavu iliyotenganisha hapo ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa Kujizui MACHOZI yalianza kunitoka, Ila mume wangu alikuwa MORE THAN STRONG akinisihi nisilie ye yuko poa, Kiukweli Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na mie Napata nguvu. Swali la Kwanza aliniuliza Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako wako salama , Kutokana na umbali wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia Naendelea Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko Upande Wetu, Misukosuko niliyoipata njiani nawaza ningekuwa na watoto ingekuwaje”?? .Tukaongea mawili matatu kama dakika tano hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka. Kuna nguo nilibeba tukaambiwa zikakaguliwe kwanza then ndo atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka then tukaondoka.
 
 
K
iukweli after  kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia kuwa yuko mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache sana na nilikuwa na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale wakatuambia kwa waliotoka mbali huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at least hata dk kumi, so nikipanga kurudi tena siku ya Jumatatu.
 Jioni Baada ya Kutoka Gerezani, Nilikutana na Sister Wangu ambaye hatujaonana zaidi ya miaka 20. Kwenye post ya changamoto na opportunity nae mtamfahamu.

DAY4.JUMATATU
 
N
iliamka asubuhi na kujiandaa, Baada ya kumaliza nikatoka kwenda kutafuta baadhi ya vitu alivyoniagiza, So nilipokamilisha vyote nikaanza safari ya kwenda Gereza Kuu Uyui kwa siku nyingine tena, Leo nikiwa nimeongozana na mwanasheria  ambaye yeye anafanya shughuli zake kule kule kwa ajili ya mambo mawili matatu. 
T
ukafuata taratibu zao kama kawaida kuandikisha, na baada ya muda tukapata nafasi  ya kwenda kumuona, Leo Kidogo ikawa  nafuu kwa vile tunatoka mbali” ipo sheria kabisa kwa mtu mfano anayetoka mbali na Tabora kuwepa nafasi kidogo zaidi mana ametokea mbali “. Kama Kawaida ya pale tukatakiwa kuacha kila kitu na siimu kuzizima, tulichoruhusiwa kupita nacho leo hii ilikuwa ni pesa tu,
 Nikiwa na mwanasheria.
T
ukapelekwa katika chumba cha wazi ni pa kuonea wafunga tulikuwa  chini ya ulinzi mkali wa uangalizi wa askari si chini ya 7, akiwepo askari mmoja wa kike , na masharti makubwa mawili hakuna kulia na hakuna kuongea kwa kunong’ona “WHISPER”. Dah kweli ilikuwa ni wakati mgumu hali ambayo nilikuwa naisikia uchungu then napewa masharti hakuna kulia, Ila narudia kusema Mungu hawezi Kuniacha , Nilipata Ujasiri wa ajabu na kuacha kulia na kuanza kuongea mawili matatu kuhusu familia na kuhusu maswala ya kazi, Ila pia napo kama after dakika kumi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka . Tukatoka na kurudi zetu hotelini. Usafiri wa Tabora kwa sasa ni tabu tukakosa usafiri wa kurudi Dar kwa siku ya Jumanne.
 Hapa Nikiagana na Mwanasheria.

DAY5.JUMANNE
 
 
B
aada ya kukosa usafiri wa kurudi Dar Siku ya Jumanne, nikitazama Tabora ni mbali nikasema ngoja niende Gerezani kuomba hata dakika moja ya kumuaga mume wangu, nikaelekea gerezani Uyui, Ila dah nikaomba sana wanilikatalia, nikaamua kurudi zangu kiunyonge hotelini, kuja kusubiria Jumatano kusafiri kurudi zangu Dar.
 

DAY6.JUMATANO
 
N
ikaanza safari ya kurudi dar, Tuliondoka Tabora saa 12 asubuhi, After Masaa Mengi njiani by saa 2 na nusu hivi nikafika salama Dar, nilikuwa So excited kuwaona wangu, Thanx God Nilifika salama na niliwakuta wanangu wako salama.
NYONGEZA
Jumatatu tarehe 8/Julai/2013, mume wangu anapandishwa tena mahakamani huko Tabora, Bado nahitaji msaada wenu katika kunisaidia maombi.
SHUKRANI.
 
N
apenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote wote ambao mpaka sasa mko pamoja na familia yangu, Kiukweli ni wengi mno sitaweza kuwataja wote na naomba msinihukumu kwa hilo ni wengi mno, Ila kwanza kabisa naendelea kumshukuru Mungu naamini yuko pamoja na familia yangu, naamini hatatuacha , pili kwa wasaidizi wangu wa kazi nyumbani kwangu niliwaachia wanangu mikononi mwao na nikawakuta wako salama, Ndugu wote wanaonisupport, marafiki wote wanaonisupport, Ila Shukrani zangu za dhati pia ziwaendee FANS wangu woteeeeee popote walipo kwa kunisaidia kwenu katika maombi inatia moyo.
 

HIVI NDIVYO KALA JEREMIAH ALIVYOANZA GAME LA MUZIKI NA HAWA NDIYO WALIOMFANYA AINGIE KWENYE GAME



 

H

AWA NI KATI YA WATU WALIONISUKUMA MIMI KUINGIA KWENYE MUZIKI WA HIP HOP KAMA MSANII.MIMI SIKUWA NAJUA KAMA NINA KIPAJI MPAKA NILIPOANZA KUUPENDA MZIKI WA HIP HOP.NILIANZA KUUPENDA MUZIKI WA HIP HOP MIAKA YA 90 MWISHONI. NIKAENDELEA KUWA SHABIKI MZURI SANA MPAKA MWAKA 2004 AMBAPO NILIZIDI KUUPENDA ZAIDI NA KUAMUA KUANDIKA UBETI WANGU WA KWANZA MWISHONI MWA MWAKA 2004. WAKATI NAANDIKA UBETI HUO SIKUWA NA JUA KAMA NINA KIPAJI NILIANDIKA TU KWA KUWA NAUPENDA MUZIKI HUO. NA LENGO LA KUANDIKA ILIKUWA NI KWA AJILI YA KUJIFURAHISHA TU.BAADA YA KUANDIKA WIMBO HUO ULIOKUWA UNAITWA DUNIA YA MATANGAZO. NIKAWA SIWEZI KUANDIKA KIITIKIO CHA WIMBO HUO MPAKA NILIPOMUOMBA RAFIKI YANGU ANIANDIKIE KIITIKIO NA KUFANYA HIVYO.HUYO RAFIKI YANGU ANAITWA BULLET.MWANZONI MWA MWAKA 2005 NILIINGIA STUDIO ZA UJUMBE RECORDS ZILIZOKUWA JENGO LA CCM MWANZA.WIMBO HUU NILIURECORD KWA KUTUMIA MDUNDO WA MSANII MWINGINE.YANI NILIFANYA KWA AJILI YA KUSIKILIZA MIMI MWENYEWE.BAADA YA KUUCHUKUA STUDIO NILIWASIKILIZISHA RAFIKI ZANGU AMBAO WALINIAMBIA NI MZURI NA KUNISHAWISHI KUINGIA RASMI KWENYE GAME.
 


K
WA KIFUPI MIMI NISINGEKUWA MSANII KAMA NISINGEKUWA NAAUPENDA MZIKI WA HIP HOP.KWA HIYO HAO JAMAA HAPO KWENYE PICHA WAMECHANGIA SANA LEO HII KUWEPO KALA JEREMIAH.
 
BY. Kala jeremiah

Wednesday, July 3, 2013

TAZAMA PICHA WAMISRI WAKISHEHEREKEA KUPINDULIWA KWA RAIS MORSI



 
 
 
 
Picha kwa msaada wa www.jpost.com

HII NDO NGOMA YA VINEGA INAYOMCHANA LIVE RUGE JAMAA HADI WANAMUOMBEA JAMAA MABAYA

 
 
Hii ni ngoma kwa ajili ya Ruge na Crouds FM, humu kuna mistari ambayo jamaa wanamuombea RUGE afe, katika ngoma hii kuna mapacha, Dani Msimamo na jamaa mmoja ambaye nimeshindwa kujua ni nani aliyechana vesi ya kwanza. wametambaa kwenye beat ya X-plastaz song la ni Dhambi kwa mwenye dhiki na hili song ni dedication kwa RALPH NELLY wa X-Plastaz, jamaa wa mapacha humu anamwambia Nelly
 
 "Ukiwa karibu na Mwenyezi Mungu, Jaribu kumchana,
   kuwa huyu jamaa huku duniani anatugawa kifala..."
 
katika mstari mwingine jamaa wanaendelea,
 
 "..Mwambieni kama vipi amchukue tu Ruge
   Tatizo kubwa ni yeye kama vipi amuue.."




Kama vipi upakue hapa ngoma yenyewe, ili ujue kuwa jamaa wafunguka kivipi kuhusu Ruge, ni track kali kinoma, track nzima ni Ruge tu, hii hapa ;
 
                                        http://www.hulkshare.com/hassbaby#/0a75gou9y52t

BURUDIKA NA KATUNI NNE ZINAZOHUSIANA NA ZIARA YA OBAMA TZ

 
 
 

Tuesday, July 2, 2013

MAHAKAMA YA SINGIDA YATUPILIA MBALI KESI YA VIONGOZI WA CHADEMA



Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida leo imetupilia mbali kesi iliyokuwa inanawakabali viongozi wawili wa CHADEMA Ndugu Mwita Waitara [Pichani kulia]  ambaye ni afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo [Pichani kushoto]. Katika hukumu yake aliyeiosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao Tundu Lissu Hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa.


Aidha, hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri. Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa, alisema hakimu huyo. 
 
 
Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago
wilayani Iramba ambapo Chama cha Mwita Waitara Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara. Kesi hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.
 

Chanzo cha habari: chademablog.blogspot.com
 

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAR. 02/7/2013 HABARI KUBWA ZIARA YA OBAMA TZ

DSC 0157 db3db
DSC 0163 0cc83
DSC 0162 fd06c
DSC 0161 a3658
 
DSC 0164 0d0d6

DSC 0158 c75a3
DSC 0159 22c0d
DSC 0160 bc092
DSC 0169 be795
 
 
DSC 0167 00bcc
 
DSC 0168 92847
 
DSC 0166 40372
 
Soma hapa chini habari nzima iliyobebwa na  gazeti laTanzania Daima
 
 
DSC 0163 0cc83HAYAWI hayawi sasa yamekuwa baada ya Rais wa Marekani, Barack Obama, kuwasili nchini jana kuanza ziara yake ya kiserikali ya siku mbili akitokea Afrika Kusini.
 
 
Rais Obama ambaye alipata mapokezi makubwa ya wananchi na viongozi mbalimbali, walioongozwa na Rais Jakaya Kikwete, aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere saa 8:36 akiongozana na mkewe Michelle pamoja na watoto wao wawili, Sasha na Malia.
 
 
Mara baada ya kuteremka kwenye ndege yake ya Air Force One, Rais Obama, alikumbatiana na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso E. Lenhardt na mkewe, kisha akasalimiana na mwenyeji wake, Rais Kikwete na Mama Salma.
Rais Obama alikwenda moja kwa moja kwenye jukwaa dogo kisha kupigiwa nyimbo mbili za Tanzania na Marekani zilizoambatana na mizinga 21, kisha akakagua gwaride na vikundi vya ngoma za asili.
 
 
Huku akishindwa kujizuia kutokana na burudani hiyo, Rais Obama alijikuta akisakata ngoma na mwenyeji wake, Rais Kikwete na baadaye alisalimiana na viongozi kadhaa wa kiserikali na mabalozi kisha viongozi hao walielekea Ikulu kwa mazungumzo.
 
 
Wakati wote ulinzi mkali wa maofisa usalama wa Marekani kwa kushirikiana na wale wa nchini uliimarishwa kila kona, ambako wananchi wengi walifurika mitaani kumlaki kiongozi huyo.
Baada ya mazungumzo mafupi ya faragha, viongozi hao walikuja mbele ya waandishi wa habari kwa ajili ya kuulizwa maswali mbalimbali.
 
 
Waandishi na maswali
Kinyume cha matarajio ya wengi, waandishi wa habari wa Tanzania walionekana kutopewa nafasi ya kutosha kufanya kazi zao kwa uhuru kutokana na kupangwa katika eneo moja wakati wote wa matukio.
 
 
Hata ilipofika mkutano wao na marais hao, waandishi walipigwa butwaa kuona watu wanne pekee wakitajwa kuuliza maswali ambapo ni swali moja tu liliruhusiwa kwa waandishi wa Tanzania.
Pia maswali yaliyoulizwa hayakuwa na manufaa sana kwa Tanzania, kwani ukiachilia mbali swali la Mtanzania Peter Ambirikile wa gazeti la Jambo Leo, aliyeuliza kama marais hao wanaridhika na misaada ya miradi ya MCC inayotolewa na Marekani, waulizaji wengine walijikita kwenye migogoro ya mataifa ya Afrika.
 
 
Katika hotuba yake Rais Obama alisema maendeleo katika nchi za Afrika ikiwamo Tanzania yataletwa na Waafrika wenyewe, kwani Marekani inachofanya ni kuchochea miradi ya maendeleo.
Pamoja na hayo, alipongeza Tanzania kuwa na utawala bora, Bunge bora na hata kuendesha siasa za upinzani kwa amani.
 
 
Pia alipongeza Tanzania kuingia katika mchakato wa kupata Katiba mpya pamoja na kumpongeza Rais wa Zanzibar kwa kufanikisha kupata Katiba mpya.
 
 
Alisema anafurahi kusikia kuwa misaada wanayotoa imekuwa na matokeo chanya kwa Watanzania kutokana na kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria na maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupungua.
 
Pia alisema mradi wa MCC umefanikiwa kwa Tanzania na kwamba itaingia katika awamu ya pili ya mradi huo.
 
Kuhusu mradi wa umeme wa Power Africa, alisema nchi nne ndizo zitafaidika na kwamba wametenga dola za Marekani bilioni saba kufanikisha mradi huo.
 
Aidha, alisema wataongeza fedha katika nchi za Afrika katika kukabiliana na magendo na ujangili.
Alisema ingawa ni mara yake ya kwanza kufika Tanzania, amefurahishwa na mapokezi maalumu aliyopata.
 
 
Rais Obama katika kujibu maswali ya migogoro hiyo ya Afrika katika nchi za Congo (DRC) na Misri, aliwaasa watawala kuheshimu wapinzani na kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.
 
 
Awali, Rais Kikwete, alisema Tanzania inaendelea kufurahia uhusiano wake na Marekani na kwamba misaada inayopata katika sekta mbalimbali imekuwa na faida kwa Watanzania.
 
 
Alitoa mfano kuwa misaada katika sekta ya afya imesaidia kupunguza vifo na misaada katika sekta ya elimu imesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi shuleni.
 
 
“Misaada mingine tunayopata ni katika usalama wa chakula, umeme na maji,” alisema.
Alisema Marekani imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kulingana na mahitaji ya Tanzania na kutoa mfano katika miradi ya barabara, upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na umeme vijijini.
“Tunaridhika na misaada tunayopata kupitia mradi wa MCC…nikisema hatujaridhika rais atakataa maombi mengine,” alisema.
 
 
Alisema misaada ya Marekani kwa kiasi kikubwa imesaidia kuboresha maisha ya Watanzania na kumuomba ikiwa anaweza kuendelea kuisaidia Tanzania afanye hivyo.
 
Kuhusu swali la ofisa wa ubalozi, Allan Mzengi, anayetuhumiwa kumdhalilisha kijinsia msichana wa Kitanzania, hatua iliyoilazimu Tanzania kulipa fidia alisema:
 
“Nalijua suala hilo, lilihusu msichana mdogo wa ofisa wetu wa ubalozi, walimchukua vizuri kwa lengo la kumsaidia kielimu, lakini kulitokea tofauti za kifamilia, yule msichana akashtaki akasema anafanyiwa vitendo vya unyanyasaji.
 
“Nakubali kulikuwapo na suala hilo ila faini iliyotolewa ilikuwa ni kubwa sana, hata kwa pensheni yangu ambayo nitalipwa baada ya kustaafu urais isingetosha kumlipa huyo, hata hivyo sehemu ya malipo hayo imekwisha kufanywa,” alisema Kikwete.
 
Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC One) ambacho pekee ndicho kilikuwa kikirusha matangazo hayo, mawasiliano yake yalikuwa yakikatika mara kwa mara, hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakifuatilia ziara hiyo kupitia runinga hiyo au nyingine zilizokuwa zimejiunga na kituo hicho.
 
 
Tanzania yakosolewa
Katika hatua nyingine, wakati Rais Obama akipokewa kwa bashasha, gazeti maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
 
 
Habari hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
 
 
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
 
 
Anasema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
 
Kwamba kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
 
Alisema kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
 
 
Ananukuu kuwa waandishi wamekuwa wakishambuliwa na mmoja aliuawa akiwa anatekeleza kazi yake ya uandishi wa habari.
 
Aliongeza kuwa Julai mwaka jana, serikali ililifungia gazeti huru la uchunguzi la kila wiki la Mwanahalisi, ambalo lilikuwa likiandika kwa undani kuhusu tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka, ambalo lilihusisha uhalifu huo na serikali ya Rais Kikwete.
 
 
Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari yenye makao makuu yake New York nchini Marekani, wiki jana ilimtaka Rais Obama kuliibua suala la uhuru wa vyombo vya habari atakapokutana na Rais Kikwete jijini Dar es Salaam.
 
 
Gazeti hilo pia limetaja vurugu za kisiasa kuwa zilichukua sura mpya na ambayo haikutegemewa wakati bomu la kurushwa kwa mkono lilipolipuliwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa madiwani wa CHADEMA na kusababisha vifo vya watu wanne mkoani Arusha.
 
“Hivi ni vitisho” ananukuliwa Dk. Willibrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA. “Watu wataogopa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura na wale jasiri watakuwa wameuliwa”.
 
 
Kwamba viongozi wa CHADEMA wamesema wazi wazi kwamba mtu aliyerusha bomu ni polisi au analindwa na polisi. Wamesema chama chao kipo tayari kuutoa mkanda wa video kuthibitisha tuhuma hizo, lakini lazima iwe mbele ya tume huru ya uchunguzi.
 
 
Lakini pia ananukuliwa kamishna wa Polisi anayehusika na operesheni, Paul Chagonja akipuuza tuhuma hizo na kuziita kuwa hazina msingi wowote, na alisema kuwa chama hicho kinapaswa kufikisha mikononi mwa polisi ili ufanyiwe kazi.
 
 
“Kazi ya msingi ya polisi ni kulinda usalama wa watu, hatufungamani na chama chochote cha siasa,” alisema Chagonja.
 
 
Pia ziara hiyo ya Rais Obama imekosolewa na wakazi wengi jijini Dar es Salaam, walidai kuwa imewaathiri katika shughuli zao za kiuchumi kutokana na kuhamishwa kwa muda katika maeneo yao ya biashara.

Monday, July 1, 2013

JULIUS MTATIRO: JWTZ WANATUMIKA VIBAYA NA CCM

 
Haya ni maelezo aliyoyatoa ndugu Julius Mtatiro Naibu Katibu Mkuu TZ Bara-CUF [Pichani  kulia] kupitia ukurasa wake wa facebook, Mtatiro anaelezea namna alivyokuwa akifuatiliwa na maofisa anaodhani kuwa ni wa JWTZ
 
"Eti jana wamekuja na magari yao kwenye hoteli niliyofikia mara tatu. Mara ya kwanza wamefika wanamuuliza muuza duka aliye karibu na hoteli kuwa ati kama nipo hotelini, akawaambia wawaulize wenye hoteli, wakasepa. Baadaye saa 1 jioni wamerudi na magari mawili, moja likapitiliza na lingine likamshusha ofisa aliyevaa kiraia, wakati anashushwa mita 100 kutoka hotelini kwa kificho, bahati nzuri nyuma yake palikuwa na BG wetu, akanipigia simu. Nikaona hawa washenzi lazima tuwaeleze ukweli. Nikafungua mlango ili nisikie ikiwa mgeni atagonga kengele ya mlango wa reception, kweli ikalia, mimi nikatoka chumba...ni moja kwa moja, nikasema liwalo na liwe. Nikamkabili akiwa mapokezi, nikamuuliza.....bila shaka unamtafuta Mtatiro, akashtuka sana, nikavua kofia, nikamwambia ndo mimi.
 
 
Ni kama nilimpa pigo zito, akaniuliza za siku, nikamjibu za siku kwani mara ya mwisho tulionana lini? Akasema tulisoma wote chuo kikuu, nikahamisha mazungumzo, nikamwambia Mbona mmepaki gari mbali hivyo....akachekacheka. Nikamwambia usicheke, karibu chumbani kwangu upaone ili mtakapokuja kunifuata msipate shida. Akakaa kimya na kuguna.
Nikamwambia....sitahama hoteli hii ili kuwakimbia, nyinyi wauaji, nyinyi siyo mungu, mnaweza kudhuru miili tu lakini si roho na siku zenu zinahesabika, mnatumika vibaya, mnatesa raia badala ya kuwalinda......
 
 
Nikakasirika nikarudi chumbani. Nasikia alibaki pale kwa dakika 3, akaomba kiberiti kwa mhudumu ili avute sigara, mhudumu akamwambia pale aliposimama sigara haziruhusiwi.
Walinzi wetu walishafika, akawapigia simu wenzake, gari yao ya jeshi ikasogea hotelini. Akatoka, wakaondoka.
 
 
Dawa ya hawa washenzi si kuwakimbia, ni kula nao sahani moja tu. Kama wao wameshapewa kibali cha "piga tu" nasi lazima tujichunge. Na jana niliapa, wangeniletea ushenzi, kabla hawajaniua, ningemwaga ubongo wa mmoja wao ili niache kumbukumbu. Hatuwezi kuishi katika nchi yetu kama wakimbizi.
 
 
Hatuwezi kuacha raia wateswe na kunyanyaswa eti viongozi tunaogopa kufa. KIFO kipo tu, hata Mahita alistaafu na siku moja atakufa."