Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Tuesday, September 23, 2014

HIVI NDIVYO TULIVYOSHEREHEKEA KATIKA BIRTHDAY YA MTOTO WETU DAVID

My son, David alizaliwa tarehe 22/09/2013, mwezi huu wa 9, tarehe 22 alikuwa ndo anafunga mwaka, hivyo kama wazazi tuliamua kuandaa chakula cha jioni ili kujumuika na ndugu, marafiki na jamaa zetu ili kwa pamoja tuweze kuadhimisha siku hii muhimu katika familia yetu. Kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao hawakuweza kufika kutoka na umbali au matatizo ya hapa na pale ambao walipenda wajumuike nasi lakini haikuwezekana, tumuona tuwaletee tukio zima katika picha, basi jumuika nasi kwa kuangalia picha hizi


 David na mama yake

                Baba D.


 Mwabeza akisoma neno la Mungu




 Baba David akiwakaribisha wageni


 Mama David akiwapungia mkono wageni 


 Mr. Prosper, ndiye alikuwa Dj. wa shughuli yenyewe


                                                                                       








 David akimlisha keki yake wa baba wa ubatizo, John Kimolo
         David akimlisha keki mama yake

   Akimmlisha keki baba yake

 Akimlisha keki bibi yake

 Akimlisha keki baba Enosh, (Mwl. Mwabeza)

















  Hii ndo familia, mama, dady, son












Tunakuombea kwa Mungu mtoto wetu David,uendelee kukua vizuri, akupe maisha mazuri na marefu, wazazi wako tunakupenda sana. Mungu akulinde.

Tunapenda kuwashukuru wote waliohudhuria katika shughuli ya kumpongeza mtoto wetu kwa kutimiza mwaka mmoja. Janeth Lubasi, Boniface Manyasa, Steven Mandia, familia ya Mwabeza, familia ya Madata, Moris Nyamwale, familia ya John Kimoro, familia ya Gwamaka, Sarah Mgulula, Maria Ntandu, Edward Mbuya, John Maghway, Mama Schola, Sylvery Hussein, Stewart Prosper, Elizabeth, Agnes, n.k. Tunawashukuru hawa wote kwa kuweza kutupa kampani ya kutosha katika siku hii muhimu ya mtoto wetu kutimiza mwaka mmoja. Mungu awabariki sana na awazidishie pale walipopungukiwa.

Familia ya Mr. & Mrs Furaha Venance Kaguo

Sunday, September 21, 2014

DIAMOND ALETA BALAA LINGINE UINGEREZA KAMA LA UJERUMANI HAKUTOKEA KWENYE SHOW

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz kwa mara nyingine tena usiku wa kuamkia jana alisababisha vurugu kubwa nchini Uingereza baada ya kushindwa kutumbuiza katika ukumbi wa LaFace Club uliopo jijini London.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kusababisha vurugu nchi za ughaibuni baada ya Septemba 1, kusababisha vurugu katika mji wa Stuttgart nchini Ujerumani aliposhindwa kufika kwa wakati ukumbini.
Akizungumza na gazeti hili, shuhuda wa tukio ambaye ni Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Uingereza, Flora Lyimo alionyesha wazi kukerwa na tukio hilo ambalo alieleza kuwa huenda likaharibu sifa ya nyota huyo ughaibuni.
Lyimo ambaye alihudhuria shoo hiyo alisema Diamond alisubiriwa na zaidi ya watu 200 tangu saa sita usiku bila nyota huyo kutokea na ilipofika saa 10:00 alfajiri, ndipo walipoanzisha vurugu kudai kurudishiwa pesa zao.
Shoo hiyo ambayo ilitozwa kiingilio cha pauni 20 sawa na fedha za Tanzania Sh54,280 iliishia kwa dosari ya aina yake baada ya polisi kulazimika kuingilia kati kusimamia urudishwaji wa fedha hizo.
Alisema waliamuru watu warudishiwe fedha zao, hivyo walipanga mstari na kurudishiwa fedha zao, kila mmoja akiamuriwa kuondoka eneo hilo huku wenye klabu hiyo wakinyang’anywa leseni.
“Ni jambo la ajabu na aibu kwa msanii ambaye Watanzania tunamtegemea atuwakilishe nje ya nchi anakubali vipi kutangazwa kwenye shoo kama hajalipwa pesa zake, watu wanamchukulia kama tapeli kwani yeye mwenyewe amewatangazia mashabiki wake halafu hajatokea.
“Wengi tunapata shaka kama hajashirikiana na huyo promota kwani hata huo ukumbi ambao shoo ilitakiwa kufanyika hauna jukwaa maalumu ambalo msanii anaweza kutumbuiza binafsi nilishangaa haikuwa eneo sahihi, lakini nikasema ngoja niende kumuunga mkono Mtanzania mwenzangu,”alisema Lyimo.
Hata hivyo, pesa zilizopatikana hazikutosha kuwarudishia watu wote ikizingatiwa kuwa wengi walikata tiketi kabla ya siku ya shoo, hapo ndipo vurugu zilipotokea na polisi kulazimika kumshikilia promota wa shoo hiyo ambaye alifahamika kwa jina la Victor.
“Polisi wengi sana waliofika hapa ukumbini kwa ajili ya kulinda usalama, walichokifanya ni kumchukua promota aliyeandaa shoo hii na kumweka chini ya ulinzi kwa kosa la utapeli, kwa sharti kwamba mpaka watakapompata Diamond, lakini mpaka sasa bado haijajulikana alipo,” alisema Lyimo.
Lyimo alionyesha wasiwasi wake na kueleza kuwa kutokana na mfululizo wa matukio hayo huenda Diamond akazuiliwa kufanya shoo katika nchi za Ulaya, kutokana na kuanza kupoteza imani kwa mashabiki wake.
Gazeti hili lilimtafuta balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe ambaye alieleza kwamba hafahamu chochote kuhusu tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kujua undani wake.
“Kama unasema tukio hilo limetokea usiku mimi sijapata taarifa zozote mpaka sasa, lakini ngoja nijaribu kuwasiliana na mtu ambaye anaweza kufahamu chochote,”alisema Balozi Kallaghe.
Kwa msaada wa Balozi Kallaghe gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Rahma Pompy ambaye pia alikuwa kwenye tukio hilo na kufafanua kuwa kasoro hiyo imetokana na uzembe wa promota.
Alisema mwandaaji wa shoo hiyo alitakiwa kumalizana na Diamond kabla ya kuwajaza watu ukumbini, lakini hakufanya hivyo hali iliyosababisha nyota huyo kushindwa kufanya kilichompeleka na kufafanua kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa promota huyo mwenye asili ya Tanzania kufanya uzembe wa aina hiyo.
“Kwa mimi niliyekuwepo eneo la tukio nafahamu fika kuwa Diamond hakuwa na kosa lolote, hakulipwa na wala promota hakumfuata hotelini. Unafikiri angeweza vipi kufanya kazi ya namna hiyo,” alisema.
Ingawa mashabiki wengi hawakumwona, lakini Pompy alibainisha kuwa Diamond alifika eneo hilo saa tisa usiku, hata hivyo alishindwa kuingia ndani ya ukumbi huo kutokana na kutomalizana na promota.
“Watu wengi hawakumwona ila mimi nilimwona Diamond, alifika na alionyesha wazi namna alivyokuwa akihangaika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ili kuwaridhisha mashabiki wake, lakini alishindwa kwa sababu hakuwa amelipwa na muda ulikuwa umekwisha,” alisema.
Ilikuwaje Diamond akawasili saa tisa usiku?
Kwa mujibu wa Pompy, baada ya Diamond kusubiri kwa muda mrefu hotelini bila kufuatwa na promota, akaamua kwenda mwenyewe kwenye ukumbi alikotakiwa kufanya shoo. Hata hivyo, alikumbana na usumbufu mkubwa njiani kutokana na barabara nyingi kufungwa nyakati za usiku kutokana na matengenezo.
“Kuna matengenezo ya barabara nyingi zinafungwa, hivyo akajikuta anazunguka kwa muda mrefu kutafuta njia mbadala. Mpaka alivyofika ukumbini, ilikuwa tayari imeshafika saa tisa, hata hivyo asingeweza kufanya chochote kwa kuwa hakumalizana na promota na ukumbi aliotakiwa kufanya shoo unafungwa saa 9:30, nadhani hata yeye alikuwa hafahamu,” alifafanua.
Kuhusu taarifa za Diamond kutafutwa na polisi kutokana na tukio hilo, Pompy alisema hana uhakika na uvumi huo kwa kuwa makosa yalionekana wazi kuwa ni ya promota.
Meneja wa Diamond afunguka
Kutokana na tukio hilo, Meneja wa mwanamuziki huyo, Hamis Taletale maarufu Babu Tale ambaye hakuambatana naye, aliliambia gazeti hili kuwa Diamond alipokea mwaliko kutoka kwa promota huyo, lakini hakulipwa fedha hata kidogo, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufanya uamuzi wowote.
“Diamond alipofika Uingereza yule promota alimdaka juu kwa juu kwa kuwa kule alikwenda kwa ajili ya shoo ya Ujerumani itakayofanyika usiku wa leo (jana) akimtaka afanye shoo jijini London, Uingereza, alikubali na baada ya hapo alisema kuwa angemlipa siku ya shoo, lakini kwa wakati wote hakufanikiwa kuonana naye tena, alikuwa akiwasiliana naye kwa simu tu,” anaeleza Taletale.
Alisema Diamond alimsubiri promota huyo kwa muda mrefu, licha ya kufanya matangazo aliamini kuwa kabla muda wa shoo haujafika angemlipa fedha ili aende ukumbini.
“Diamond alishangaa kuona ilipofika saa nne usiku wa kuamkia jana promota yule hapatikani, kwa kuwa hakulipwa hata dola moja (Sh1,600) aliamua kutulia hotelini kwani promota ndiye anatakiwa amfuate msanii, na yeye hakufanya hivyo wala hakumlipa hata kidogo. Msanii wangu hana makosa ndiyo sheria ya kazi ilivyo,” alisema Taletale.
Hata hivyo, Taletale alisema wamiliki wa ukumbi ndio walioamua kuita polisi baada ya kuona viashiria vya vurugu, na hapo ndipo ilipogundulika kuwa promota huyo hakulipia ukumbi pia.
“Licha ya kwamba hakumlipa msanii wangu, pia ukumbi hakuulipia. Alichokifanya mmiliki ni kurudisha fedha kwa watu waliohudhuria mbele ya polisi na promota yule akakamatwa.”
Akizungumzia usalama wa Diamond, Taletale alisema, “Msanii wangu yupo katika mikono salama na hivi tunavyoongea ameshapanda ndege kuelekea Ujerumani kwa ajili ya shoo jioni ya leo. Hana kosa lolote, hakuna mkataba baina yake na promota unaoonyesha kwamba alilipwa,hivyo hakuwa na kizuizi na polisi hawajashughulika naye,” alisema Taletale.
Hata hivyo, alipoulizwa kwa nini anamwacha msanii wake asafiri peke yake na kufanya makubaliano na mapromota kazi ambayo alitakiwa aifanye yeye (Taletale) alisema:
“Ilikuwa nisafiri naye, lakini kwa bahati mbaya kulikuwa na matatizo ya kifamilia ambayo ilinilazimu nibaki nchini. Yeye alikwenda kwa ajili ya shoo mbili zilizofanyika Jumamosi Afronation na hii ya leo itakayofanyika Sturtgart. Huyu promota alimdaka tu,” alisema Babu Tale.
Baada ya kutokea kwa vurugu hizo, mwanamuziki Diamond alisema promota huyo amemtapeli kwa kuwa hayakuwa makubaliano yao awali.
“Tafadhali ndugu zangu wa Uingereza haikuwa dhamira yangu, kuweni makini sana na promota huyu Victor Dj Rule, mnaposikia kaandaa shoo, pati au hafla yoyote ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwa sababu ni tapeli, si unajua aisifiaye mvua imemnyeshea, basi miye nimeloa kabisa,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Akizungumzia sakata hilo, Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba alisema tatizo alilopata Diamond limepokewa kwa masikitiko makubwa na wanamuziki wote nchini.
“Tunasikitika kwani hii ni mara ya pili inatokea tena kwa kipindi cha mwezi mmoja, lakini baada ya kufanya mawasiliano, tumegundua tatizo lilikuwa la promota, mwanamuziki wetu hana hatia na ameshaondoka Uingereza leo (jana) asubuhi na sasa yupo Ujerumani kwa ajili ya shoo nyingine ya usiku wa leo,” alisema Ado.
Chanzo: Mwananchi

Friday, September 19, 2014

WATU SITA KUTANDIKWA MIJELEDI 91 KWA KOSA LA KUREKODI WAKICHEZA DANSI WIMBO WA PHARRELL WILLIAM 'HAPPY' HUKO IRAN


Washukiwa walisema walihadaiwa kuwa walikuwa wanafanya mtihani wa kuigiza
Watu sita nchini Iran kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa kifongo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.
Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo.
Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjiniTehran.
Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja.
Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.
Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.
Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo
Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar, pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao.
"inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,'' aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Kwa msaada wa: BBC

Wednesday, September 17, 2014

NAWASHUKURU MARAFIKI ZANGU WOTE KWA KUNITAKIA HERI YA SIKU YANGU YA KUZALIWA

Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru watu wote, familia yangu, baba na mama, mke wangu, mtoto wangu, jamaa na marafiki zangu wote kwa kampani yenu mliyonipa hadi kufikia siku hii kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu, Mungu awabariki sana, kampani yenu bado naihitaji sana

















Nawashukuru wote, Mungu awabariki sana

Monday, September 15, 2014

WAJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA HAWA HAPA, MNYIKA NAIBU KATIBU MKUU BARA


Wajumbe wa kamati kuu walichaguliwa leo ni hawa wafuatao kwa makundi yao
Ulemavu mgombea mmoja
Ndiyo 154
Hapana12
Eli marco macha ndiye mshindi
Kundi D zanzibar wanawake(1)
1.zifa Bakari 70
2.zainabu mussa 111
Kundi c wanaume kutoka zanzibar
1.salimu mwalimu 172
2.Nassaro ali 19
Kundi B wanawake kutoka bara
1. Cicelian pareso 75
2.chiku abwao 19
3.angela 86
4.catherine 97
5.susan kiwanga 93
Wajumbe kamati kuu wanaumne bara
1.Baregu 127
2.mpendazoe 20
3.makagenda 28
4.munishi 34
5.mbogoro 71
6.Dr yaled 77
7. Marando 164
Kwa msaada wa Henry Kilewo
NAIBU KATIBU MKUU BARA NI MNYIKA

HAYA SASA WAZEYA WA GOSPEL! MCHECK HUYU MKONGO NA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA LINGALA YA YESU NI NOOMA






Huyu jamaa anaitwa PIT SON Wimbo unakwenda kwa jina la Lingala ya Yesu, jamaa yuko poa vibaya mno. Bofya kwenye video hapo juu au kwenye jina lake kuicheck.

PROF. JAY ft DIAMOND PLATNUMZ----KIPI SIJASIKIA (Official Video)




Hii ni Official Video kutoka kwa Prof J akimshirikisha Diamond, mzigo unakwenda kwa jina la KIPI SIJASIKIA? kuitazama video yenyewe bofya hii link PROF JAY ft DIAMOND-------KIPI SIJASIKIA






Sunday, September 14, 2014

ISLAMIC STATE (IS) WAKATA KICHWA CHA MATEKA MWEINGINE RAIA WA UINGEREZA

Serikali ya Uingereza imesema kuwa inachukua hatua za dharura ili kubaini ukweli wa kanda ya video inayoonyesha mateka wa Uingereza David Haines aliyetekwa nyara na kundi la himaya ya kiislamu akikatwa kichwa.
Mfanyikazi huyo wa misaada aliyekamatwa nchini Syria mnamo mwezi Machi mwaka jana ameonyeshwa akipiga magoti katika jangwa, kando yake akiwa ni mtu aliyeficha uso wake ambaye amebeba kisu.

Atakuwa mateka wa tatu wa magharibi kukatwa kichwa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
katika kanda hiyo ya Video mtu aliyeshika kisu anaonekana akishtumu mataifa yanayounga mkono Marekani,naye Haines ambaye anaonekana kuwa chini ya shinikizo anaonekana akimlaumu waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron kwa hatma yake.
Mwisho wa kanda hiyo mateka wa pili wa Uingereza anaonyeshwa na kutishiwa.

David Cameron

Wakati huohuo Waziri mkuu nchini Uingereza David Cameron ameshtumu kukatwa kichwa kwa David Haines kama kitendo cha kishetani.
Amesema kuwa wauaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria ata iwapo itachukua mda mrefu.
Katika taarifa yake rais Obama pia ameshtumu mauaji ya kikatili ya David Haines.
Amesema Marekani inaomboleza na Uingereza kifo cha mateka huyo na kungezea kuwa itashirikiana na muungano mkubwa wa kimataifa ili kuwakamata washukiwa mbali na kuharibu tishio hilo kwa ulimwengu.
Wanahabari wawili Steven Sotlof na james Foley waliuawa na wapiganaji hao mwezi uliopita.
CHANZO BBC

Saturday, September 13, 2014