Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Friday, June 9, 2017

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA V NA VYUO VYA UFUNDI 2017 HAWA HAPA

Waliochaguliwa kujiunga kidato cha V na vyuo vya ufundi 2017 bofya link hapo chini

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA V NA VYUO VYA UFUNDI 2017

Sunday, January 15, 2017

MANYONI: NIMEWAWEKEA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016 YA SHULE ZAIDI YA 20 ZILIZOPO KATIKA WILAYA YA MANYONI. BOFYA HAPA


1.       MWANZI    BOFYA HAPA
2.       MANYONI  BOFYA HAPA
3.       ITIGI     BOFYA HAPA
4.       HEKA  BOFYA HAPA
5.       KILAMATINDE BOFYA HAPA
6.       MLEWA BOFYA HAPA
7.       SASAJIRA BOFYA HAPA
8.       SANJARANDA BOFYA HAPA
9.       KAMENYANGA BOFYA HAPA
10.   MAKANDA BOFYA HAPA
11.   KINTIKU BOFYA HAPA
12.   RUNGWA BOFYA HAPA
13.   IDODYANDOLE BOFYA HAPA
14.   KINANGALI BOFYA HAPA
15.   AMANI GIRLS BOFYA HAPA
16.   ISSEKE BOFYA HAPA
17.   NGAITI BOFYA HAPA
18.   IPAMUDA BOFYA HAPA
19.   MAKURU BOFYA HAPA
20.   MKWESE BOFYA HAPA
21.   ST. JOHN BOFYA HAPA
22.   CHIKUYU BOFYA HAPA
23.   KIZIGO  BOFYA HAPA

MATOKEO YA TAIFA DARASA LA IV 2016 KWA SHULE ZA HALMASHAURI YA MANYONI NA ITIGI HAYA HAPA. PIA YAPO YA MKOA MZIMA WA SINGIDA



MATOKEO SHULE ZA MSINGI LINK HAPA CHINI



KUANGALIA HALMSHAURI ZINGINE ZA MKOA WA SINGIDA BOFYA HAPA 

KUANGALIA SHULE ZOTE TANZANIA 





MATOKEO YA TAIFA KIDATO CHA PILI 2016 NA DARASA LA NNE 2016 HAYA HAPA


TAZAMA SHULE KUMI BORA KITAIFA NA ZA MWISHO KITAIFA KISHA NIMEKUWEKEA LINK ZA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI NA NNE.


KUONA MATOKEO BOFYA LINK HIZI HAPA CHINI

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2016

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2016

Friday, January 13, 2017

MAJINA YA WAHITIMU WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI WALIOMBA AJIRA YA UALIMU NA AMBAO NYARAKA ZAO HAZINA SHIDA HAYA HAPA

Ministry of Education, Science and Technology
TAREHE 12/12/2016 WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILITANGAZA KUWA WAHITIMU WA STASHAHADA NA SHAHADA ZA UALIMU KATIKA MASOMO YA SAYANSI (FIZIKIA, KEMIA, BIOLOJIA) NA HISABATI WA MWAKA 2015 WAWASILISHE VYETI VYAO KWA
AJILI YA UCHAMBUZI WA WAHITIMU WENYE SIFA.

WAHITIMU WALIOKUWA NA MAPUNGUFU KATIKA NYARAKA ZAO WANATAKIWA WAWASILISHE TENA. WAHITIMU HAO NI KAMA IFUATAVYO:-
     (1) WALIOTUMA NAKALA ZA “RESULTS SLIPS” AU “ACADEMIC TRANSCRIPTS” BILA NAKALA ZA VYETI HALISI VYA KIDATO CHA 4, 6, STASHAHADA AU SHAHADA
     (2) WALIOTUMA NAKALA ZA VYETI VYA STASHAHADA ZA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA IN EDUCATION – PGDE) BILA NAKALA ZA “VYETI VYA SHAHADA YA KWANZA PAMOJA NA “ACADEMIC TRANSCRIPTS” ZAKE;
WAHITIMU AMBAO HAWAKUTUMA KABISA NAKALA ZA VYETI VYAO WANAPEWA FURSA YA MWISHO KUTUMA.
WAHITIMU AMBAO NYARAKA ZAO ZILIWASILISHWA MAJINA YAO YANAPATIKANA KATIKA LINK HIZI

Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.

Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli amesema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.

''Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi chini ya utawala wangu hilo halitakuwepo kuna magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu ikizungumzwa habari hii wao wanageuza hii nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia wasikie wasiposikia  wasisikie lakini magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana''.

Rais Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuvumilia kuona amani ya nchi inahatarishwa na magazeti mawili kwani amani ndio chimbuko la maendeleo ya taifa lolote duniani.

Amesema bila kuwepo kwa amani hakuna mwekezaji atakayeweza kuja kuwekeza nchi, hata wawekezaji wa ndani watashindwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Rais Magufuli amesema uwepo wa amani nchini ndio uliowezesha wawekezaji wa Kiwanda cha Fresho cha kutengenezea mifuko ya kubebea bidhaa za chakula nchini na kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga kujengwa mkoani hapo kwani bila amani visingeweza kujengwa.

Aidha ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi nyingine za fedha kutoa mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda badala ya kuwakopesha wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi yasiyowanufaisha watanzania waliowengi

Rais Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili alivyovizindua katika siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.


Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu
Shinyanga
13 Januari 2017.

Saturday, December 10, 2016

RAIS MAGHUFULI AKUTANA NA MMILIKI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE. HAYA NDIYO WALIYOKUBALIANA...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
                                  OFISI YA RAIS,
                                               IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
                   11400 DAR ES SALAAM,
                                         TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu  ambao  walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.
''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais Magufuli.
Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia  kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43  kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora  kuliko kuagiza nje.




Katika kuthibitisha hilo,  tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi  ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya  Tanzania  na kamwe hana  nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).

Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.
10 Desemba, 2016.

Video hapa chini


Friday, December 9, 2016

DARASA KATIKA WIMBO WAKE NI KAMA ANAWACHANA DIAMOND NA KIBA

                           Darasa                                                          Alikiba                                           Diamond

Na. Furaha Venance

1.  Darasa anaanza kuwaponda wasanii ambao wanakomaa katika game lakini mambo yamekuwa magumu kwao. Anawaambia:

Rudi utotoni,
Usipotembea utabebwa mgongoni.

Hapa anawazungumzia wasanii ambao walipata kiki kwa kubebwa na media (kumbuka anayebebwa ni Mtoto). Hivyo anawataka warudi enzi hizo za kubebwa au wawatafute watu wa kuwabeba.

2.      Diamond ni msanii ambaye anajisifu sana kuwa yeye ndiye msanii anayelipwa zaidi kuliko msanii yoyote Bongo, ndiye msanii mwenye nyumba Sauz, ndiye msanii pekee anayelipa kodi zaidi ya mil/ 30 TRA. Mashakibiki wa muziki wanamuonma kama ni msanii mwenye sifa sana na ni kama ameota mapembe kutokana na misifa yake. Darasa anamwambia:

 Wanaoota mapembe waongezee mkia.

3.      Kiba na Diamond wanajisifu kuwa wao ni wakali hadi kufikia kujifananisha na wanyama, Diamond anajiita Mnyama, Simba huku mashabiki wa Kiba wakimwita mfalme huyo Tembo. Darasa anawambia:
Blah blah sitaki kusikia,
siyo Simba, siyo Chui,
siyo mamba, haaha ”

Akiwa na maana kwake hakuna cha samba, chui wala mamba wote hao anawameza ndiyo maana anamalizia na kibwagizo “Haaaaa!” (kumeza).

4.      Diamond ni msanii anayesifika kwa mashauzi, kujigamba n.k. yemwenyewe anajiita mswahili wa uswahilini hasa. Darasa anamwambia:

Pumzi yangu inatosha kujigamba,
Na sina maneno ya kwenye kanga

Hapa anamaana kuwa kazi (pumzi) zake zinatosha kujigamba wala hana maneno ya kwenye kanga (maneno ya uswahili).

5.      Diamond ni msanii anayemiliki wasanii kadha wa kadha. Miongoni mwao kuna Richmavoko, Raymond, Harmonize na Queen Darlin. Kati ya wasanii hawa Harmonize ameonekana kuzua kizaazaa. Wapo wanamuona hatafika mbali, kutokana na kukosa ubunifu wake na kumuiga zaidi Diamond katika muziki hadi maisha yake binafsi. Sasa hapa ni kama Darasa anamuonya Diamond:

Kuzaa unawe kuzaa kizaazaa,
Sinzia na fegi uchome kibanda. 

Akiwa na maana Diamond ni kama amemzaa Harmonize lake badala yake amezua kizaa, akiendelea kumkumbatia (sinzia na fegi) anaweza ua WCB (choma kibanda).

6.     Wapo wanasema kuwa WCB chini ya Diamond hawafanyi muziki zaidi ya kufanya usanii usanii tu. Miongoni wa wasanii wanaosema hivi ni Ommy Dimpoz na Team Kiba. Darasa ni kama anaungana nao na kumwambia Diamond:

Maisha na muziki,
acha maneno weka muziki.

7.  Kwa sasa bila ubishi Diamond ndiye msanii aliyejuu. Huku Kiba akikimbizana kuhakikisha anamshusha msanii huyo. Sasa kaja Ommy Dimpoz naye anataka kuchuana, kukimbizana na Diamond ambaye anaonekana amewaacha, sasa Darasa anawambia wasanii hawa:

Unataka kukimbia na hauna break,
what do you expect?

Hapa ni sawa na kuwaambia wanataka kushindana wakati hawana mbinu za ushindani. Muziki ni kuwekeza mkwanja, ubunifu na kipaji ili ufike unapotaka.

8.     Diamond ni msanii anayesemwa kuwa anajifanya mjuaji sana, mademu anawajua yeye, muziki anajua yeye, maisha anayajua yeye yaani kila kitu anajua yeye. Sasa kuhusu madem, Darasa anamwambia:

Watch yourself, usije ukaji-comfuse…
Vitu vingine havitakagi ujuaji,
utajikuta unatandikia watu jamvi.”

Hapa ni kama anamwambia kungonoka na madem wa kila aina haitaki ujuaji asijejikuta anaaga dunia kwa ngoma. Si unajua tena mtu akifariki kinachofuata ni kutandika majamvi msibani! (pia inaweza kuwa kuwapa watu maneno ya kusema na kukukalia kitako kukusema).

9.  Kuna hili linasemwa na teamkiba hasa Ommy Dimpoz kuwa wapo wasanii wanaonunua views youtube ili ionekana nyimbo zao zinabamba. Hapa ni kama alikuwa analengwa Diamond na timu yake. Lakini hili ni kama watu hawajalielewa kwa maana kwamba Ommy hajaeleweka. Sasa Darasa anawaona watu wasioelewa hili ni kama machizi vile. Anamwambia Ommy na teamkiba, “Kumuelewesha chizi utajipa kazi.” Anaendelea kuwaambia wasanii kupata views nyingi wafunge mkanda, wakaze kamba, kwa maana ya kutoa ngoma kali. Au wafuate nyao za kununua views waone kama hawajachana msamba (kupotea kwenye game) kama asemavyo:

 Funga mkanda na kaza kamba,
Ama ufuate nyayo uchane msamba.

10.  Mwisho anazigeukia media na watu wanaotaka kuipoteza Hip Hip na wasanii wake. Anawambia:
Wanataka tupotee kwenye map,
tunapeleka game to the top top…
We don’t stop.

Huu ni mtazamo tu...inaweza kuwa si kweli
Mwl. Venance
0715 335558 (whatsapp) 
follow me instagram @fullraha17