WATU WENGI WAJITOKEZA KUMSIKILIZA.
ASEMA ATAMALIZA KERO YA MAJI MANYONI.

Kabla mgombea huyo hajapanda
jukwani, viongozi mbalimbali wa chama hicho walihutubia. Sumaye akiwahutubia
wananchi wa Manyoni, alishangaa ndani ya miaka 50 ya utawala wa CCM Hospital ya
Manyoni haina dawa, wagonjwa kulala chini huku akina mama wajawazito wakiagizwa
kuleta vifaa vya kujifungilia ili hali huduma hiyo inatolewa bure. Akihutubia
kwa njia ya kuuliza maswali, sumaye aliuliza, “tuliweka misingi kwamba watoto
chini ya miaka 5 watibiwe bure. Je wanatibiwa bure?” alijibiwa na umati wa
watu, “Hapana!”. “Hospitali yetu kuna dawa?” alijibiwa “hakuna.” Aidha
aliendelea kuwaeleza wananchi kwamba, chama cha mapinduzi kimeshindwa kuwaletea
maendelea ndani ya miaka 50 kitaweza ndani ya miaka 5? “Sasa tumewaletea rais
anayeweza kuwaletea maendelea naye si mwengine ni Edward Lowassa.”

Mapema kabla ya kuzungumza
Sumaye, aliyekuwa naibu waziri wa Ajira na Vijana, Mh. Makongoro Mahanga,
alisema, “Ndugu zangu nimekuwa naibu waziri wa Ajira na Vijana kwa muda mrefu, CCM
wasiwadanganye hakuna ajira huko, ajira zitakuwepo chini ya serikali ya UKAWA.”
Aidha Tundu Lissu akiwazungumzia Mawaziri hao wastaafu, aklisema kwamba,
mawaziri hawa hawana shida ya maisha, wangeamua kukaa kimya kama alivyokaa
kimya Msuya (Waziri Mkuu Mstaafu), ama wangeamua kutumika na CCM kama
anavyotumika Warioba licha ya madhambi waliyomfanyia. “Ndugu zangu, Lowassa
analipwa asilimia 80 ya mshahara wa sasa wa Mizengo Pinda...Sumaye naye
analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, hawana
shida ya maisha wameamua kuungana na sisi ili kuwaletea maendeleo...” Alisema
Lissu.
Lowassa apanda jukwaani

Akiendelea kujinadi alisema
kwamba, atashughulikia matatizo yote ya afya, maji, elimu, na miundo mbinu.
Anachohitaji wamchagulie wabunge na madiwani kutoka vyama vya ukawa ili
kuwaletea maendeleo wananchi wa Manyoni. Ukafika muda akampandisha mgombea
Ubunge wa Jimbo hilo bwana Emmanuel Mpandagoya kueleza matatizo
yanayowakabiliwa Wanamanyoni. Akizungumzia kero za Wanamanyoni, Mgombea huyo
alisema, Manyoni inakabiliwa na tatizo la maji, walimu wa hususani walimu wa
masomo ya Sayansi, umeme, “Kuna vijiji hapa manyoni havina huduma ya maji wala
umeme, tunaomba Mh. Rais utakapochaguliwa tu tunaomba utusaidie kuondoa kero hii.”
Alisema mgombea huyo. Aidha aliongeza kuwa kumekuwa na kero za michango na kodi nyingi kwa wananchi wa Manyoni.
Mgombea huyo wa urais mara baada
ya kupokea kipaza sauti kwa mgombea ubunge, aliwauliza wananchi kama mbunge
huyo anaweza kuwa mbunge na kuitikiwa na umati wa watu kuwa anaweza huku
wengine wakiimba Imma! imma! Imma. “Ndugu zangu Wanamanyoni tuchagueni tumalize
kero hizi.” Alisema Lowassa ambaye alitumia dakika 12 kuongea na Wanamanyoni.
Wanamanyoni wanasemaje?
Wakiongea na mwandishi wa Baba D
Blogy, wakazi wa Manyoni walikuwa na maoni tofautitofuati kuhusiana na ujio huo
wa Lowassa. “Ndugu yangu nilikuwa nasikia kuwa wanaojitokeza katika mikutano
yake wanabebwa na malori ili kujaza mikutano yake, leo nimeshuhudia mwenyewe
hawa watu wamekuja kwa mapenzi yao tu.” Alisema kijana mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la Shaban. Mkazi mwingine wa Manyoni ambaye hakupenda kujitambulisha
alisema kuwa wakati wa ujio wa Maghufuli hapa Manyoni alivyokuja kujitambulisha
watu hawakujitokeza kama hivi leo, tena wengine tulibebwa kutoka vijijini kuja
kumshuhudia lakini leo licha ya kuchelewa kupata taarifa za ujio huu nimekuja
kwa mapenzi yangu kutoka Kintiku.”
Dereva bodaboda aliyejitambulisha
kwa jna la Rama, “alienda mbali zaidi na kusema kuwa haijawahi kutokea chama
cha upinzani kwa historia ya Manyoni kukusanya watu wengi kiasi hiki. Huyu
jamaa CCM wakicheza anapita.”
Kwenye vijiwe vya madereva tax na
boda boda stori za leo ni Lowassa tu, wengine walisikika wakisema huu ni wakati
wa mabadiliko, wengine ambao walionekana kuwa wachahce walionekana bado wana
imani na CCM na mgombea wake Maghufuli. “Maghufuli ndiyo kila kitu hamuoni
barabara?” alisikika dereva mmoja wa tax na kushambuliwa na wenzake ambao
wanaonekana kumzidi nguvu. “CCM imeshindwa kwa miaka 50 ni wakati wa kuwapima
wengine.” Alijibiwa na mwenzake na kushangiliwa na wenzake.
Wengine waponda
Wakazi wengine waponda, wadai
umati uliojitokeza si kwamba wanampenda Lowassa ila walikuja kumuona tu
anafananaje. “Wala hakuna jipya alilolizumza leo.” Alisema mkazi mmoja ambaye
hakupenda kutaja jina lake.
Mgombea huyo anaendelea na
mikutano mingine katika majimbo mengine ya Mkoa wa Singida.
Simu: 0715 33 55 58