Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Thursday, May 30, 2013

SHEREHE YA SEND OFF YA REGINA S. MAFFA ILIYOFANYIKA BASHNET-MANYARA TAR. 25/05/2013

Hii ni kwa ajili ya rafiki zangu na rafiki wa Regina ambao walipenda kuhudhuria sherehe za kuagwa [Send off] kwa Regina S. Maffa lakini kwa namna moja ama nyingine wakashindwa kuhudhuria. Basi tumeamua kuwaletea baadhi ya picha za sherehe hizo ili kujua kilichojili. Sherehe hii ya 'Send off' ilifanyika Nyumbani kwao Regina katika kijiji cha Bashnet-Babati mkoani manyara tarehe 25/05/2013

 Hapa tukiwa tumepumzika kabla hatujaelekea 
ukweni ambako send off itafanyika

 Hapa nikiwa na mama mzazi katika
viwanja vya ukweni tukisubiri shuguli kuanza

Hapa nikiwa na mpambe wangu Bw. Joreth kushoto

Nami nikiingia na wapambe wangu

Mama mkwe kulia, akimpokea mama mzazi kushoto
katikati wanaonekana kukumbatiana ni mzee wangu

 
Tukiendelea kuingia

 
Bi. Harusi mtarajiwa akiingia na wapambe wake

 
 Bi. Harusi mtaarajiwa {kulia} na mpambe
wake wakiingiia uwanjani

 
Muagwa aliyeshika mic, akitambulisha ndugu na jamaa


 Mdogo wangu, Waziri akitambulisha ndugu na jamaa
Baba mkwe akipiga cheers

Cheers ikiendelea



       
 Bi. Harusi mtarajiwa akikata keki huku mpambe wake
akihakikisha vipande vinakatwa kwa size ya
 midomo ya wageni wahudhuriaji

       
Baba mkwe akikabidhiwa keki na binti yake


 Mzee wangu akikabidhiwa keki na mkwe wake

         
Bi. harusi na mpambe wake wakimtafuta
Bw.Harusi mtarajiwa ambaye alifichwa kwelikweli

      
Hapa wamemuona jamaa, fataki inaandaliwa kulipuliwa
kama ishara ya kumuona wa moyo wake

Hapa tukilishana apple baada ya kuniona

Hao tukitoka mafichoni!

  
Tunaendelea kutoka

Tukielekea kwenye msosi

Bado tunaendelea kuelekea kwenye msosi

Tumefika tunapakia menu kama kawaida

Show kama kawa ilikuwepo ya kutosha tu

Show inaendelea
 Walinogesha ile mbayaa na show za kijanja

 Hapa baada ya kumaliza kula

 Hapa akiniambia jambo!

Nami nikitoa ya moyoni

      
 Wageni wakitoa zawadi zao

                                    
Baada ya hapo tulifunga na muziki kama kawaida

Mwenye suti, mdogo wangu Waziri, Katikati mzee mzima
mwenyewe, nyuma wife, pembeni hapo mama mzazi

********
MWISHO: Harusi itakuwa jijini Dar-es-salaam tarehe 15/6/2013, kama kawaida nawakumbusha michango  yenu ya hali na mali, kwa mawasiliano au kutuma mchango wako, Tigo Pesa : 0715 33 55 58 naM- Pesa : 0755 44 06 99. Tuwashukuru wote ambao wametuunga mkono kwa michango yenu na kushirikiana nasi hadi kukamilisha shughuli hii ya Send off, MUNGU awabariki sana.

Tuesday, May 14, 2013

SAFARI YANGU YA BABATI MKOA WA MANYARA KULIPA MAHARI KWA BINTI WA KIIRAQ

 
Tarehe 04/05/2013 nilikuwa safarini Babati mkoa wa Manyara, huko nilienda kulipa mahari, maana nimechoka kuwa 'bado nipo nipo kwanza' zifuatazo ni baadhi ya picha za safari hiyo; 
 
Huyu ndo Mzee wangu, Mzee Venance Kaguo
akiwa ukweni akiangalia mandhari
 
Mama Mkwe [Mama Regina] akimtembeza mzee wangu
kumuonesha mazingira ya ukweni
 
Baba akifurahia jambo, huku mdogo wangu
anayenifuata, Waziri akiwa pembeni
 
Tukipata chai nzito kabla ya kikao cha kupangiwa mahari hakijakaa
 
Nikiwa na Mshenga wangu Mzee Gobret (Baba Kalay)
 
Nikiwa na Mshenga na Mzee wangu kulia
 
Huyo wa kulia ndo alikuwa Mkalimani maana Mshenga alikuwa full Kiiraq
 
Mshenga, Mkalimani, Mzee na Bwana harusi mtarajiwa
tukijadili kabla hatujaingia ndani
 
Hapa mi na Mzee wangu tukijadili jambo baada ya kupata maelezo na taratibu
tunazotakiwa kuzizingati, si unajua ukikosea kidogo mafaini
 
Mshenga akikazia jambo fulani
 
Hapa wameingia ndani, Mkalimani akimfafanulia Mzee jambo
 
Hapa Mzee akionekana kufurahia jambo
 
Mshenga akiwa kazini
 
Huyo mwenye koti na kofia  rangi damu ya mzee  ndiyo Baba mkwe mwenyewe,
anayefuatia ni baba mkubwa wa wife, na aliyevaa kofia nyeusi na mgorori wenye miraba miekundu ni uncle wa wife
 
Hapa Baba mkubwa wa wife  akiandika koo tatu akishirikiana na uncle
maana hayo majina ya Kiiraq yalitushinda kuandika wakati wakizitaja
 
 
 
                                        


Mahari imeshapangwa, wamemalizana Mzee ananipa kilichojili ndani
maana mi sikutakiwa kuingia ndani kwa mujibu wa mila na desturi za Kiiraq

Mjomba mtu naye akatokea, hapo ananiambia
 "Si unaona nilikwambia mjomba ndo kila kitu, tumemaliza bwana
 kuwa na amani mjomba wangu"
 
Huyo ndo aliyenipeleka Manyara, mtoto wa Kiiraq ndo Bibi Harusi Mtarajiwa
 
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, naishukuru sana familia yangu Baba na Mama kwa kufunga safari ndefu toka Dar. mpaka Babati Manyara kwa ajili ya kwenda kulipa mahari ya kijana wao, pia namshukuru  Mdogo wangu Waziri Venance naye kufunga safari na kuacha kazi zake kuja kunipa 'suport' kaka yake kutoka Mwanga Kilimanjaro hadi Manyara.
 
 
Pia namshukuru sana Kipenzi changu Regina S. Maffa kwa kunikubali kuwa mimi kuwa wake, kunikubali mimi kijana ninayetoka familia ya kawaida kabisa, hakuwa kama wale wengine. Namshukuru pia Mshenga wangu kwa ngumu na nzito aliyoifanya, namshukuru pia Denis Chirimi pamoja na Mr. Kalay kwa kuniunganisha na Mshenga Mzee Gobret maana bila wao sijui kama ningepata mshenga mzuri, na ukizingatia huko sikuwa mwenyeji wala mtu ninayefahamiaana naye huko ambaye angeweza kufanya kazi hiyo.
 
Mwisho naishukuru familia yake Regina kwa kunikubali nami kuwa kijana wao wa kiume, wasiwe na hofu binti yao atatunzwa vizuri sanaaaaa.
 
Ndoa itafungwa Tarehe 15/06/2013 DSM, kwa wale ambao nimewapa kadi za michango na wengine nilishindwa kuwafikia wapo nilio wa in-box nawakumbusha bado napokea michango, michango yenu muhimu kufanikisha jambo hili jema. unaweza tuma kwa M-pesa: 0755 44 06 99 na Tigo Pesa 0715 33 55 58 na Airtel money: 0787 33 55 53