Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, June 27, 2016

MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WALIOACHWA



Wakuu wa Wilaya walioachwa na vituo vyao kwenye mabano ni Halima Kihemba (Kibaha), Betty Mkwasa (Mvomero), Muhingo Rweyemamu (Morogoro), Matthew Sedoyeka (Sumbawanga), Jacqueline Liana (Nzega), Benson Mpesya (Songea), Suleiman Kumchaya (Tabora) na Amani Mwenegoha (Bukombe).

Wengine ni Fatma Ally (Mtwara), Jackson Msome (Bukoba), Ramadhani Maneno (Chemba), Hafsa Mtasiwa (Korogwe), Pilly Moshi (Magu), Paul Mzindakaya (Busega), Shabani Kissu (Kondoa), Baraka Konisaga(Nyamagana), Francis Mwonga (Bahi), Gerald Guninita (Kasulu), Omar Kwaangw’ (Karatu), Novatus Makunga (Moshi), Farida Mgomi (Chamwino), Ponsiano Nyami (Bariadi).
Pia wamo Lephy Gembe (Kilombero), Dk. Jacqueline Tiisekwa (Dodoma), Bituni Msangi (Kongwa), Margaret Malenga (Nyasa), Sheni Ngaga (Mbinga), Chande Nalicho (Namtumbo), Agnes Hokororo (Tunduru), Hawa Ng’humbi (Kishapu), Wilson Nkhambaku (Arumeru), Ernest Kahindi (Longido), Francis Mitti (Monduli), Zainab Mlesi (Rungwe), Nyirembe Munasa (Mbeya) na Ahmed Namhone (Mbozi).

Katika orodha hiyo wamo Ziporah Pangani (Igunga), Estherina Kilasi (Muheza), Jowika Kasunga (Mufindi), Khanifa Karamagi (Gairo), Subira Mgalu (Kisarawe), Nurdin Babu (Rufiji), Crispin Meela (Babati), Abdallah Kihato (Mkuranga), Joshua Mirumbe (Bunda) na Ali Mohamed (Serengeti).
Lembris Kipuyo (Rombo), Manju Msambya (Ilemela), Saidi Amanzi (Singida), Lucy Mayenga (Iramba), Kanali Samuel Nzoka (Kiteto), Mahmood Kambona (Simanjiro), Dk. Michael Kadeghe (Mbulu), Yahya Nawanda (Lindi), Charles Gichuri (Ikungi), Christopher Magela (Newala) na Bernard Ndutta (Masasi).
Wengine ni Zuhura Mustapha Ally (Uyui), Khanifa Sirengu (Sikonge), Daudi Yassin (Makete), John Henjewele (Kilosa), Mariam Juma (Lushoto), Husna Msangi (Handeni), Peter Toima (Kakonko), Saveli Maketa (Kigoma).

Pia wamo Rosemary Kirigini (Maswa), Georgina Bundala (Itilima) na Erasto Sima (Meatu), Amina Lugaila (Mbogwe), Ibrahim Marwa (Nyang’wale), Abdulla Lutavi (Tanga), Ephraim Mmbaga (Liwale), Mariam Mtima (Ruangwa), Mariam Mohammed (Lushoto), Selemani Liwowa (Kilindi) na Mboni Mgaza (Kilindi).

Taratibu za Kupandishwa Vyeo na Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

3.0 Utaratibu wa Mafunzo
3.1 Mkakati wa Mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
  • Kwa mujibu wa Mkakati wa Mafunzo kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI waajiri wanapaswa kundaa mpango wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kuwezesha watumshi wao kujengewa uwezo.
  • Hivyo Waajiri wanapaswa kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa watumishi wao kupitia mfumo wa upimaji kazi wa wazi ili mafunzo atakayopangiwa mtumishi yaweze kuziba pengo la utaalam na stadi za kazi lililoonekana kwa mtumishi kutekeleza majukumu yake.
  • Mtumishi atawekwa kwenye Mpango wa Mafunzo wa mwaka kwa kuwa haiwezekani watumshi wote wakaenda masomoni kwa mara moja.
  • Watumshi wataenda mafunzoni kwa utaratibu ulioidhinishwa na Halmashauri bila kukiuka taratibu zilizotolewa na OR-MUU na Wizara za Kisekta kwa mafunzo yanayohusu utaalam.
  • Mpango ulioidhinishwa na Halmashauri ni muhimu uwe wazi kwa watumishi wote ili Watumishi pamoja na wasimamizi wao wa kazi waweze kupanga vizuri ratiba zao za kazi
  • Waajiri chini ya Mkakati wa Mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanapaswa kutoa kipaumbele zaidi katika mafunzo ya muda mfupi ya kuongeza stadi za kazi.
  • Wizara za kisekta chini ya Mkakati wa Mafunzo zinapaswa kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya kitaalam chini ya Sekta zao ili kuwaongezea uwezo wataalam wa Kisekta waliopo katika Halmashauri na Mikoani
  • Mamlaka za serikali za Mitaa hazina budi kuhakikisha kuwa wataalamu wake wanahudhuria mafunzo ya uongozi na kuingizwa kazini yanayotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa, Dodoma
  • Watoaji wa huduma za mafunzo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wataratibiwa na kusimamiwa viwango vya huduma zao na Chuo cha Serikali za Mitaa Dodoma.
3.2 Ruhusa za kwenda mafunzoni:
  • Waajiri wanapaswa kutenga fedha za mafunzo kadri ya mahitaji yatakayobainishwa na kukubaliwa na Halmashauri pale ambapo mpango utakuwa umepungikiwa fedha ni wajibu wa Waajiri na watumishi kutafuta fedha za mafunzo
  • Kabla mtumishi hajaenda mafunzoni atapaswa kupewa ushauri nasaha kuhusu mafunzo anayokwenda kufanya kuhusiana na ukuaji wake katika utumishi wa umma
  • Barua ya ruhusa ambayo atapewa mtumishi kabla ya kwenda mafunzoni inapaswa kujieleza bayana kuhusu masharti ya ruhusa hiyo
  • Pale ambapo mtumishi atalazimika kujigharamia kwa ridhaa ya mwajiri ni vema mwajiri kuwa wazi katika ruhusa atakayoitoa
  • Mtumishi akiwa katika mafunzo ya muda mrefu wakati wa likizo anaweza kurudi kufanya kazi katika kituo chake cha kazi au Mwajiri anaweza kumtaka kuripoti kazini na kuendelea na kazi wakati wa likizo hiyo.
  • Baada ya mtumishi kugharamiwa mafunzo na Halmashauri itamlazimu kuitumikia Halmashauri hiyo kadiri Halmashauri itakavyokuwa imeridhia wakati inatoa ruhusa
3.3 Baada ya mtumishi kurejea kutoka mafunzoni:
  • Mtumishi wa Umma akimaliza mafunzo anatakiwa kuripoti kwa mwajiri kwa kutoa taarifa ya maandishi ikiwa ni pamoja na kuwasilisha matokeo ya kufuzu masomo wakati akisubiri cheti.
  • Mwajiri atapaswa kumpongeza Mtumishi mara tu baada ya kuwasilisha cheti cha masomo na kufanya mchakato wa kumbadillishia kazi iwapo atakuwa na sifa za kubadilishwa kazi hii ni pamoja na mahitaji ya mtumishi mwenye sifa aliyopata mtumishi (Ubadilishwaji wa cheo recategorization utazingatia maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu, Utumishi).
  • Mwajiri atapaswa kufanya ufuatiliaji wa karibu wa utendaji wa mtumishi baada ya kuhitimu mafunzo ili kumwezesha kutumia ujuzi /Elimu aliyopata na kubaini upungufu kwa ajili ya ushauri na mafunzo mengine ikibidi.
Pages: 1              

Taratibu za Kupandishwa Vyeo na Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

1.0 Utangulizi
Usimamizi wa Watumshi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika masuala ya upandishwaji vyeo, mafunzo na uhamisho yameelezwa katika Sheria ya Utumshi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002, ikisomwa pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na Taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na Miongozo na Nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali. Kwa sasa taratibu za kusimamia masuala hayo ni kama ifuatavyo:-
2.0 Kupandishwa Vyeo
Mamlaka ya kupandisha vyeo watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa isipokuwa Walimu kwa mujibu wa Kanuni ya D. (f) na (g) ya Kudumu ya mwaka 2009 ni Halmashauri yenyewe.
2.1 Nini kifanyike kabla na baada ya mtumishi kupandishwa cheo?
  • Mamlaka ya Ajira yaani Halmashauri inapaswa kutenga fedha na nafasi kwa ajili ya nafasi za vyeo vinavyaotakiwa kupandishwa kwa mujibu wa Miundo yao ya Utumishi na sifa za watumishi wanaotarajiwa kupandishwa vyeo.
  • Mwajiri anapaswa kuhakikisha watumishi wake wanapimwa utendaji kazi kwa kutumia mfumo wa Upimaji na tathmini ya wazi �OPRAS� ili kujua hali ya utendaji wao. Mtumishi atakayezembea katika hili asipopandishwa cheo, halitakuwa kosa la mwajiri bali ni kosa la kiutendaji la mtumishi husika.
  • Ukubwa kazini yaani elimu na uzoefu wa kazi pia ni kigezo muhimu katika kuwafikiria watumishi kupandishwa vyeo licha ya kuwa miundo ya utumishi iko kimya katika hili.
  • Ni muhimu idhini ya kupandishwa watumishi vyeo baada ya Kamati za Ajira za Halmashauri kumshauri Mkurugenzi awasilishe taarifa kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri husika ili litoe idhini, vinginevyo vyeo vilivyopandishwa vitakuwa ni batili.
  • Ni muhimu Vyama vya Wafanyakazi mahali pa kazi kupitia Mabaraza ya kazi vikashirikishwa katika maandalizi ya kupandisha watumishi vyeo ili kuepuka manung�niko yasiyo ya lazima mahali pa kazi.
  • Ni muhimu kwa watumishi wote wa Mamalaka za serikali za Mitaa kufahamu kuwa nafasi zozote za kupandishwa vyeo hazitaombwa mpaka pale itakapolazimika Mwajiri kuzitangaza.
2.2 Taratibu za kujaza nafasi za Uteuzi
Katika utumishi wa umma kuna Taratibu na Miongozo inayotumika kujaza nafasi wazi na vyeo vya uteuzi. Taratibu hizo ni kama zilivyofafanuliwa hapa chini:-
  • Nafasi za uteuzi zinapotokea katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ilivyo kwa taasisi zingine serikalini Waajiri watapaswa kutoa taarifa na mapendekezo ya maafisa wanaoweza kufikiriwa kushika nafasi hizo (majina yawe kati ya mawili na matatu) kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua za upekuzi kisha baada ya kupokea majibu ya upekuzi, Mamlaka za uteuzi zitaendelea na uteuzi na kutoa taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
  • Pale inapotokea ni lazima nafasi za uteuzi ikaimiwe, kabla ya kupata kibali cha kukaimu nafasi hiyo, ni muhimu baada ya Mtumishi kukaimishwa na Mamlaka ya Uteuzi, Mamlaka hiyo kuomba kibali cha kuwakaimisha Watumishi wenye sifa za kukaimu na kupata kibali cha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa umma kwa ajili ya malipo ya posho zao za kukaimu na kuwezesha zoezi la upekuzi kuendelea wakati wahusika wanakaimu.
  • Mara baada ya watumishi kupandishwa vyeo Waajiri wanapaswa kuhakikisha kuwa watumishi wanapewa barua zao za kupandishwa vyeo na wanabadilishiwa mishahara yao kwa wakati bila kuzalisha madeni kwa Serikali.
  • Mtumishi aliyepandishwa cheo atapaswa kuwa katika kipindi cha majaribio na atathibitishwa katika cheo alichopandishwa baada ya miezi sita tangu tarehe ya kupandishwa cheo.
  • Iwapo itaonekana mtumishi ameshindwa kumudu majukumu ya cheo alichopandishwa atajulishwa na kupewa sababu na nafasi ya kujieleza kwanini asivuliwe cheo hicho na kulingana na maelezo hayo anaweza kuongezwa muda wa majaribio.
2.3 Nini kifanyike iwapo Mtumishi hajaridhika na utaratibu uliotumika kumpandisha cheo?
Iwapo mtumishi ataona hakutendewa haki na Mamlaka yake ya ajira katika suala la kupandishwa cheo atapaswa kuchukua hatua zifuatazo;
  • Kumjulisha Mwajiri Malalamiko yake kwa barua,
  • Iwapo Mtumishi hataridhika na majibu ya Mwajiri, atapaswa kutoa malalamiko yake kwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa uamuzi ambapo nakala ya barua yake itatumwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Page 1 2

JOINING INSTRUCTIONS FORM V

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA DK KITILA MKUMBO ATEMA CHECHE


Katika ukurasa wake wa facebook Dk. Kitila ameandika haya kuhusu nafasi za Ukuu wa Wilaya:

Nimekuwa nikipigiwa simu na ndugu zetu waandishi wa habari wakitaka maoni yangu kuhusu walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya. Kimsingi sina maoni kabisa kuhusu walioteuliwa lakini nina maoni kuhusu nafasi yenyewe ya ukuu wa wilaya katika mfumo wa utawala wetu. 

uDC ni nafasi yenye sura nyingi lakini zote za kisiasa. Kwa uzoefu wa nyuma na utaratibu wa serikali ya CCM uDC ni sehemu ya kwapa nafasi ya kukua kisiasa na kikada vijana wa chama tawala kupitia jumuiya yao ya uvccm. Ni nafasi za kuwahifadhi makada wastaafu. Ni sehemu ya kuwasaidia waliogombea ubunge kupitia chama tawala na kushindwa. Hutumika pia kutoa fadhila kwa watu ambao wamekisaidia chama tawala katika kushinda uchaguzi kwa namna mbalimbali. Ni nafasi ambayo hutumika kuandaliwa kuja kuwa Mkuu wa Mkoa. Mpaka hapo utaona kwamba nafasi ya uDC haina tija ya maana kwa taifa. Tija pekee ni kwa chama tawala. Ni mzigo kwa wapiga kura. Ni mzigo kwa taifa na ni mzigo hata kwa Rais mwenyewe, hasa ikiwa Rais aliyejitambulisha kubana matumizi katika utumishi wa umma. Ni mzigo kwa wakurugenzi wa Halmashauri na ni mzigo mzito kwa uendeshaji wa halmashauri zetu. 

Ndiyo maana vyama vyote makini vya upinzani vimeweka katika ilani zao kufuta nafasi ya ukuu wa wilaya kama sera muhimu ya kubana matumizi na kuzipa mamlaka kamili halmashauri zetu zifanye kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo. Siku nikipata nafasi ya kumsogelea mheshimiwa Rais nitamnong’oneza jinsi ambavyo kufuta nafasi ya ukuu wa wilaya ingemrahisishia kazi ya kuwahudumia maskini kama alivyopania. Njia rahisi ya kudhihirisha azma na nia ya kubana matumizi kwa Rais wetu ni kutumia mamlaka yake kikatiba kufuta hii nafasi ya ukuu wa wilaya haraka. Hii ni muhimu zaidi kuliko kufuta/kuahirisha sherehe za Uhuru na Muungano ambazo ndio alama kuu ya Taifa letu tulipendalo. Watanzania wenzangu tumuombee sana Mheshimiwa Rais wetu ili Mungu amfungulie aione busara ya kufuta hii nafasi ya ukuu wa wilaya katika mfumo wetu wa utawala. Hayo ndiyo maoni yangu.

Sunday, June 26, 2016

SHULE 12 ZA WILAYA YA MANYONI AMBAZO ZIMETOA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA V


Zifuatazo ni shule 12 za Wilaya ya Manyoni ambazo wanafunzi wake wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali. Chagua shule unayotaka kuangalia majina ya wanafunzi na shule wanazoenda kwa kubofya jina la shule hapa chini.














Uchambuzi yakinifu wa shule nyingine unaendelea. mara baada ya kukamilika tutawaletea shule zilizobaki. 

Na: Mwl. Venance Furaha

Mawasiliano: 0715 335558 (Whatsapp)
                       0755440699

HABARI NYINGINE


SHULE 12 ZA WILAYA YA MANYONI AMBAZO ZIMETOA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA V


Zifuatazo ni shule 12 za Wilaya ya Manyoni ambazo wanafunzi wake wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule mbalimbali. Chagua shule unayotaka kuangalia majina ya wanafunzi na shule wanazoenda kwa kubofya jina la shule hapa chini.














Uchambuzi yakinifu wa shule nyingine unaendelea. mara baada ya kukamilika tutawaletea shule zilizobaki. 

Na: Mwl. Venance Furaha
Mwanzi Sec.
Mawasiliano: 0715 335558 (Whatsapp)
                       0755440699

HABARI NYINGINE


KIZIGO SEC: FORM V SELECTION

SNNAMBA YA MTIHANIJINSIJINA LA MWANAFUNZISHULE ATOKAYOTAHASUSISHULE AENDAYOWILAYA YA SHULE AENDAYOMKOA WA SHULE AENDAYO
1S1825/0008MJuma Amosi NdahaniKizigoHGLMwanziManyoniSingida

MKWESE SEC: FORM V SELECTION

SNNAMBA YA MTIHANIJINSIJINA LA MWANAFUNZISHULE ATOKAYOTAHASUSISHULE AENDAYOWILAYA YA SHULE AENDAYOMKOA WA SHULE AENDAYO
1S0649/0015MDwasi Mnhandi DwasiMkweseHGKMwengeSingida (M)Singida
2S0649/0016MElia Lameck EliaMkweseHGLDakamaUshetuShinyanga
3S0649/0022MMasunga Mlisu MasungaMkweseHGKItigiManyoniSingida

IPAMUDA SEC: FORM V SELECTION

SNNAMBA YA MTIHANIJINSIJINA LA MWANAFUNZISHULE ATOKAYOTAHASUSISHULE AENDAYOWILAYA YA SHULE AENDAYOMKOA WA SHULE AENDAYO
1S2797/0015MIssa Salum AllyIpamudaHKLMwakaleliBusokeloMbeya
2S2797/0016MJulius Richard JacksonIpamudaHGETosamagangaIringa (V)Iringa

MWANZI SEC: FORM V SELECTION

SNNAMBA YA MTIHANIJINSIJINA LA MWANAFUNZISHULE ATOKAYOTAHASUSISHULE AENDAYOWILAYA YA SHULE AENDAYOMKOA WA SHULE AENDAYO
1S0662/0015FFarida Omary KazyowaMwanziHGKIsimilaIringa (V)Iringa
2S0662/0023FHidaya Nasoro HemedMwanziHGKIsimilaIringa (V)Iringa
3S0662/0042FPrisca Aidan MwajaMwanziPCBKondoa GirlsKondoaDodoma
4S0662/0055FSara Salumu NjoghomiMwanziHGKIkungiIkungiSingida
5S0662/0058FTheresia Frolence MpandaMwanziPCBLugobaBagamoyoPwani
6S0662/0059FTheresia Juma MatongoMwanziHKLJikomboeChatoGeita
7S0662/0108MMichael Meshack MalyosiMwanziPCMSameSameKilimanjaro
8S0662/0124MSamwel Bunzu NduroMwanziPCMKigomaKigoma (M)Kigoma