Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Saturday, September 12, 2015

LOWASSA AITEKA MANYONI KWA MUDA: AVUNJA REKODI YA MAGHUFULI.

WATU WENGI WAJITOKEZA KUMSIKILIZA. 

ASEMA ATAMALIZA KERO YA MAJI MANYONI.

Na Furaha Venance (Baba D): Manyoni

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Ngoyai Lowassa leo ameuteka mji wa Manyoni kufuati mapokezi makubwa aliyoyapata wilayani. Msafara wa mgombea huyo uliwasili katika viwanja vya shule ya Msingi Tambukareli kwa usafiri wa chopa akiambatana na viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fedrick Sumaye, aliyekuwa Naibu Waziri wa Ajira na vijana, Mh. Makongoro Mahanga, Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu na viongozi wengine. watu wengi waliojitokeza walikuwa wakisukumana kwa lengo la kumshuhudia kwa macho yao mgombea huyo huku wengine wakipigania ili kumshika wengine wakiwabeba watoto wao juu ili wamshuhudie mgombea huyo ambaye anaonekana ni mgombea mwenye mvuto na ushawishi kuliko wagombea wote katika uchaguzi huu. Aidha mara Chopa ilipowasili katika viunga vya Manyoni, ikiwa angani, wakazi wa Manyoni, walianza kukimbilia na wengine wakifunga maduka yao ili tu kumshuhudia mgombea huyo kat.

Kabla mgombea huyo hajapanda jukwani, viongozi mbalimbali wa chama hicho walihutubia. Sumaye akiwahutubia wananchi wa Manyoni, alishangaa ndani ya miaka 50 ya utawala wa CCM Hospital ya Manyoni haina dawa, wagonjwa kulala chini huku akina mama wajawazito wakiagizwa kuleta vifaa vya kujifungilia ili hali huduma hiyo inatolewa bure. Akihutubia kwa njia ya kuuliza maswali, sumaye aliuliza, “tuliweka misingi kwamba watoto chini ya miaka 5 watibiwe bure. Je wanatibiwa bure?” alijibiwa na umati wa watu, “Hapana!”. “Hospitali yetu kuna dawa?” alijibiwa “hakuna.” Aidha aliendelea kuwaeleza wananchi kwamba, chama cha mapinduzi kimeshindwa kuwaletea maendelea ndani ya miaka 50 kitaweza ndani ya miaka 5? “Sasa tumewaletea rais anayeweza kuwaletea maendelea naye si mwengine ni Edward Lowassa.”

“Huko kote tulikopita tumepokelewa na watu wengi sana, wananchi wanataka mabadiliko. Sasa CCM wanaomba huruma ya wananchi. Si mmemsikia Maghufuli, anasema hakuna haja ya kuchoma kitanda kama kina kunguni! Eti unamuua kunguni kitandanda unakiacha. Kwa lugha ya Maghufuli kitanda ni CCM na kama kitanda kina kunguni dawa yake ni kukitoa nje na kukianika kipigwe jua huko nje miaka 50.” Alisema Sumaye na kushangiliwa na umati wa watu waliofurika katika viwanja hivyo.

Mapema kabla ya kuzungumza Sumaye, aliyekuwa naibu waziri wa Ajira na Vijana, Mh. Makongoro Mahanga, alisema, “Ndugu zangu nimekuwa naibu waziri wa Ajira na Vijana kwa muda mrefu, CCM wasiwadanganye hakuna ajira huko, ajira zitakuwepo chini ya serikali ya UKAWA.” Aidha Tundu Lissu akiwazungumzia Mawaziri hao wastaafu, aklisema kwamba, mawaziri hawa hawana shida ya maisha, wangeamua kukaa kimya kama alivyokaa kimya Msuya (Waziri Mkuu Mstaafu), ama wangeamua kutumika na CCM kama anavyotumika Warioba licha ya madhambi waliyomfanyia. “Ndugu zangu, Lowassa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa sasa wa Mizengo Pinda...Sumaye naye analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, hawana shida ya maisha wameamua kuungana na sisi ili kuwaletea maendeleo...” Alisema Lissu.

Lowassa apanda jukwaani

Ukawadia sasa wasaa wa mgombea huyo kupanda jukwaani saa 6:09. Umati wa watu ulilipuka kwa kelele wakiimba Rais! Rais!, rais! Rais! Huku wakinyajua mabango yao yaliyobeba ujumbe mbalimbali. “Kwanza ni washukuru kwa mapokezi makubwa haya, mmejitokeza kwa wingi asanteni sana.” Alisema lowassa akionekana kushangazwa na umati wa watu waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo. Ndugu zangu nimekuja hapa kuwaomba kura, wangapi watanipa kura siku hiyo?” aliuliza na kujibiwa kwa watu kunyoosha mikono juu. Aidha aliwaambia Wanamanyoni kuwa wamchague alimalize tatizo la maji. “Haiwezekani zaidi ya miaka 50 wilaya ya Manyoni ina matatizo ya maji! Haiwezekani kabisa! Nichagueni tufanye mchakamcha wa maendeleo. Mbunge wa hapa namjua vizuri sana, Chiligati amekimbia matatizo.” Alisema.

Akiendelea kujinadi alisema kwamba, atashughulikia matatizo yote ya afya, maji, elimu, na miundo mbinu. Anachohitaji wamchagulie wabunge na madiwani kutoka vyama vya ukawa ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Manyoni. Ukafika muda akampandisha mgombea Ubunge wa Jimbo hilo bwana Emmanuel Mpandagoya kueleza matatizo yanayowakabiliwa Wanamanyoni. Akizungumzia kero za Wanamanyoni, Mgombea huyo alisema, Manyoni inakabiliwa na tatizo la maji, walimu wa hususani walimu wa masomo ya Sayansi, umeme, “Kuna vijiji hapa manyoni havina huduma ya maji wala umeme, tunaomba Mh. Rais utakapochaguliwa tu tunaomba utusaidie kuondoa kero hii.” Alisema mgombea huyo. Aidha aliongeza kuwa kumekuwa na kero za michango  na kodi nyingi kwa wananchi wa Manyoni.

Mgombea huyo wa urais mara baada ya kupokea kipaza sauti kwa mgombea ubunge, aliwauliza wananchi kama mbunge huyo anaweza kuwa mbunge na kuitikiwa na umati wa watu kuwa anaweza huku wengine wakiimba Imma! imma! Imma. “Ndugu zangu Wanamanyoni tuchagueni tumalize kero hizi.” Alisema Lowassa ambaye alitumia dakika 12 kuongea na Wanamanyoni.

Wanamanyoni wanasemaje?

Wakiongea na mwandishi wa Baba D Blogy, wakazi wa Manyoni walikuwa na maoni tofautitofuati kuhusiana na ujio huo wa Lowassa. “Ndugu yangu nilikuwa nasikia kuwa wanaojitokeza katika mikutano yake wanabebwa na malori ili kujaza mikutano yake, leo nimeshuhudia mwenyewe hawa watu wamekuja kwa mapenzi yao tu.” Alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shaban. Mkazi mwingine wa Manyoni ambaye hakupenda kujitambulisha alisema kuwa wakati wa ujio wa Maghufuli hapa Manyoni alivyokuja kujitambulisha watu hawakujitokeza kama hivi leo, tena wengine tulibebwa kutoka vijijini kuja kumshuhudia lakini leo licha ya kuchelewa kupata taarifa za ujio huu nimekuja kwa mapenzi yangu kutoka Kintiku.”
Dereva bodaboda aliyejitambulisha kwa jna la Rama, “alienda mbali zaidi na kusema kuwa haijawahi kutokea chama cha upinzani kwa historia ya Manyoni kukusanya watu wengi kiasi hiki. Huyu jamaa CCM wakicheza anapita.”

Kwenye vijiwe vya madereva tax na boda boda stori za leo ni Lowassa tu, wengine walisikika wakisema huu ni wakati wa mabadiliko, wengine ambao walionekana kuwa wachahce walionekana bado wana imani na CCM na mgombea wake Maghufuli. “Maghufuli ndiyo kila kitu hamuoni barabara?” alisikika dereva mmoja wa tax na kushambuliwa na wenzake ambao wanaonekana kumzidi nguvu. “CCM imeshindwa kwa miaka 50 ni wakati wa kuwapima wengine.” Alijibiwa na mwenzake na kushangiliwa na wenzake.

Wengine waponda
Wakazi wengine waponda, wadai umati uliojitokeza si kwamba wanampenda Lowassa ila walikuja kumuona tu anafananaje. “Wala hakuna jipya alilolizumza leo.” Alisema mkazi mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Mgombea huyo anaendelea na mikutano mingine katika majimbo mengine ya Mkoa wa Singida.

Simu: 0715 33 55 58


Wednesday, September 9, 2015

KAMA HUKUFANIKIWA KUITAZAMA HOTUBA FULL YA GWAJIMA AKIMJIBU DR. SLAA INGIA HAPA



Askofu Gwajima akijibu tuhuma dhidi yake na dhidi ya maaskofu wa Kanisa Katoliki zilizotolewa na mwanasiasa Dr Slaa. 08/09/2015.