Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Thursday, October 31, 2013

KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE, MADARAJA YA UFAULU YAPANGULIWA, DARAJA SIFURI LAFUTWA

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imefanya marekebisho katika upangaji wa viwango vya alama za matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne kwa kufutwa daraja sifuri na kuwekwa daraja la tano, ambalo litakuwa la mwisho katika ufaulu.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome [Pichani kushoto]  alitangaza mageuzi hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu.
 
Alisema kwa muundo mpya, daraja la kwanza litabakia kuanzia pointi 7 hadi 17 kama ulivyokuwa muundo wa zamani, ambalo ni kundi la ufaulu uliojipambanua na bora sana, daraja la pili litaanzia pointi 18 hadi 24, badala ya pointi 18 hadi 21 kama zamani na likiwa ni kundi la ufaulu mzuri sana.
 
Pia daraja la tatu pointi zake zitaanzia 25 hadi 31, badala ya zile za zamani za 22 hadi 25 na kundi hili litakuwa la ufaulu mzuri wa wastani.
 
Kwa mujibu wa Prof. Mchome, daraja la nne litaanzia pointi 32 hadi 47, badala ya zile za zamani za kuanzia pointi 26 hadi 33, na kundi hilo litajulikana kama la ufaulu hafifu.
 
Daraja jipya lililoongezwa ni lile la tano, litakaloanzia pointi 48 hadi 49, litakalofuta daraja sifuri la zamani, lililokuwa na pointi 34 hadi 35, na sasa litajulikana kama kundi la ufaulu usioridhisha.
 
Prof. Mchome alifafanua kuwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wa elimu na kuweka wazi taratibu mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine.
 
Pia alisema wataalamu wa mifumo ya mitihani wataufanyia kazi zaidi muundo huo wa madaraja ili uweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
 
“Yapo mambo mengi mengine ambayo hayana budi kuendelea kuimarishwa, ukiwamo mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na vitabu na vifaa vingine muhimu katika elimu,” alisema.
 
Awali alisema kuwa wizara imekusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu upangaji wa viwango vya alama katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na cha sita pamoja na matumizi ya alama za tathmini endelevu ya mwanafunzi.
 
Alisema maoni hayo ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake katika mitihani hiyo yote ni vya elimu ya sekondari.
“Sera ya elimu na mafunzo ya 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, alama za tathmini endelevu ya mwanafunzi zitachangia asilimia 50 na mtihani wa mwisho asilimia 50.
 
“Kwa upande wa Zanzibar alama hizo zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia 40 na mtihani wa mwisho asilimia 60. Pamoja na kwamba baraza halijawahi kuitumia mifumo hii tokea ilipowekwa, kumekuwa na mitazamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya alama hizo,” alisema.
 
Vilevile alisema kuwa wadau wengi walishauri muundo uliopo sasa wa madaraja uimarishwe ili kuanza kutumia muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (GPA), kwa kuwa ni rahisi kueleweka na kuuandaa kuliko muundo wa madaraja.
 
Pia kwa kutumia muundo huo wa GPA inakuwa rahisi katika kukadiria uwezo wa mwanafunzi kielimu na kufanya uamuzi mbalimbali ikiwamo kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali za elimu.
 
Wakati huo huo, Prof. Mchome alisema kuwa mtihani wa kidato cha nne na mtihani wa maarifa mwaka huu unatarajiwa kufanyika nchini kote kwa siku 18 kuanzia Novemba 4 hadi 21.
 
Alisema jumla ya watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani huo ni 427,906, ambapo kati yao 367,399 ni watahiniwa wa shule na 60,507 ni wa kujitegemea.
 
Kwa mujibu wa katibu mkuu huyo, hadi sasa maandalizi na usafirishaji wa mitihani hiyo hadi ngazi ya mkoa yamekamilika.
 
Alitoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa yote kuhakikisha kuwa taratibu zote za utunzaji, uhifadhi na usafirishaji wa mitihani hiyo zinazingatiwa.
 
Via: Tanzania Daima

UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA, LAKINI PIA HUARIBU MUONEKANO WA SURA YA MTU, TAZAMA MUONEKANO WA SURA ZA MAPACHA WANAOFANANA SANA MMOJA AKIWA ANAVUTA SIGARA NA MWENGINE HAVUTI.

Uvutaji wa Sigara ni hatari kwa afya, lakini pia uvutaji wa sigara huaribu muonekano wa mtu, mtu anaweza kuonekana kuwa ni mzee au ana umri mkubwa kutokana na athari za uvutaji wa sigara, utafiti watafiti wamefanya utafiti wa pacha 70 zinazofanana lakini mmoja akiwa anavuta sigara na mwingine akiwa hatumii, majibu yamejionesha kuwa yule anayevuta sigara anaonekana ana umri mkubwa kuliko umri wa pacha mwenzake asiyevuta. picha hiyo juu inathibitisha hilo, tazama mwenye muonekana wa pacha asiyevuta na mwenzake anayevuta.

Chanzo: Mail Online

Wednesday, October 30, 2013

MTIKISIKO BUNGENI, SPIKA MAKINDA KUNG'OLEWA, SAINI ZAKUSANYWA ZA KUMNG'OA

Dodoma. Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, (CCM), leo anatarajiwa kuanza kukusanya saini za wabunge akitafuta kuungwa mkono katika hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa madai kwamba amekuwa akikiuka kanuni za Bunge.
 
Dk Kigwangalla aliibua hoja ya kutokuwa na imani na Spika katika kikao cha wabunge wote cha kuelezea shughuli zitakazofanywa na Bunge katika mkutano wa 13, kilichofanyika juzi jioni kwenye ukumbi wa Pius Msekwa.
 
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, jana alithibitisha kuwapo kwa mjadala huo katika kikao cha wabunge, lakini hakuwa tayari kueleza kwa undani na badala yake alisema kwamba leo ataanza kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kukamilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika Makinda
 
Chanzo chetu kutoka katika kikao hicho cha wabunge kilibainisha kuwa Kigwangalla alihoji kuhusiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge (CCM-Bariadi Magharibi) kuteuliwa na Spika wakati katika kamati nyingine wenyeviti na makamu huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika.
 
Pia Dk Kigwangala alisema Spika Makinda alivunja kanuni kwa kuwapa posho ya Sh430,000 kwa siku wajumbe wa kamati inayoongozwa na Chenge wakati wajumbe wa kamati nyingine wamekuwa wakipewa Sh130,000.
 
“Anachokifanya Spika ni matumizi mabaya ya fedha za umma, inakuwaje wengine wafanye kazi hata bila posho lakini wao (Kamati ya Bajeti), walipwe posho ya Sh430,000 kwa siku?” chanzo hicho kilimkariri Dk Kigwangalla akihoji. Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah akizungumza na gazeti hili jana alisema mazingira ya kamati fulani kupata malipo ya ziada tofauti na viwango vya kawaida hutokea pale uongozi wa kamati husika unapoomba kwa Spika.
 
“Si kweli kwamba Kamati ya Bajeti inalipwa fedha za ziada kila wakati, hapana, ni pale tu wanapoomba malipo hayo kutokana na sababu ambazo lazima Spika aridhike nazo. Ieleweke kuwa siyo kamati hiyo tu, kwa sasa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ambayo inachambua miswada mingi nayo imekuwa ikiomba na baada ya Spika kuridhia basi nao wanapewa,” alisema Dk Kashililah.
 
Katibu huyo wa Bunge alieleza kuwa zaidi ya kamati nane zimewahi kuomba malipo ya ziada kwa maana ya kutaka posho zaidi, ulinzi, usafiri na hata chakula, ikiwa zinakabiliwa na majukumu ya ziada pia katika mazingira tofauti nje ya utaratibu wa kawaida.
 
“Kimsingi, kamati nyingi zinapewa malipo tofauti, watu wanaweza kuwa na kazi mpaka saa saba au nane usiku, au wanakwenda kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida, taratibu zinamruhusu Spika kama akiridhika na maelezo ya kazi husika, basi anaruhusu kutekelezwa kwa maombi hayo,” alisema Dk Kashililah.
 
Kuhusu Serukamba
Aidha, Dk Kigwangalla alinukuliwa akisema Spika amekiuka kanuni kwa kumchagua Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM), kuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
 
“Hakuna mbunge yeyote aliyepo katika kamati mbili lakini hata kungekuwa na sababu maalumu basi wa kuteuliwa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini-CCM) ambaye TRA (Mamlaka ya Mapato Nchini) ipo chini ya kamati yake,” kilisema chanzo hicho.
 
Chanzo hicho kilisema Dk Kigwangalla alisema badala ya kumweka karibu katika ushiriki, Mgimwa alipokwenda katika kamati hiyo aliambulia kufukuzwa.

Akizungumzia suala hilo, Dk Kashililah alisema Serukamba pamoja na wabunge wengine kadhaa waliteuliwa na Spika kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kamati hiyo wakati wa kipindi cha Bajeti Kuu ya Serikali.
 
Aliwataja wabunge wengine walioteuliwa kushiriki katika Kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa ni John Cheyo (Bariadi Mashariki-UDP), Salahe Pamba (Pangani - CCM) na Hamadi Rashid Mohamed (Wawi - CUF).
 
Kanuni za Bunge
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge katika toleo la mwaka 2007, kifungu cha 137(1), ili kumwondoa Spika madarakani, mbunge anayetaka kuwasilisha hoja hiyo atatakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi ya kusudio hilo kwa Katibu, akieleza sababu kamili ya kutaka kuleta hoja hiyo.
 
Kifungu kidogo cha pili kinasema baada ya kupokea taarifa ya maandishi ya kusudio la kumwondoa Spika kwenye madaraka, Katibu atapeleka taarifa hiyo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa.
 
Kifungu cha tatu kinabainisha kuwa endapo kamati hiyo itaridhika kuwa zipo tuhuma mahususi dhidi ya Spika zinazohusu uvunjaji wa masharti ya ibara husika za Katiba, sheria au kanuni zinazoongoza shughuli za Bunge, basi kamati hiyo itaidhinisha hoja hiyo ipelekwe bungeni ili iamuliwe.
 
Kanuni zinasema Naibu Spika, atakalia Kiti cha Spika wakati wa kujadili hoja ya kutaka kumwondoa Spika madarakani na Spika atakuwa na haki ya kujitetea wakati wa mjadala na kwamba ili kumwondoa zinahitajika kura zisizopungua theluthi mbili ya idadi ya wabunge wote.
 
Via MCL

SITTA: HATUJAOLEWA EAC, TUTAWAMWAGA KAGAME, MUSEVENI NA KENYATA

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema Tanzania itatoa talaka kwa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambazo zimeamua kuanzisha Jumuiya ya hiari nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Sitta alisema kutokana na nchi hizo kuonekana kuitenga Tanzania na Burundi ambazo ni wanachama wa jumuiya hiyo, wameshaanza mazungumzo ya kushirikiana kiuchumi, kisiasa na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC).
 
Kauli hiyo ya Sitta inatokana na mikutano ya mara kwa mara inayofanywa na marais Uhuru Kenyata wa Kenya, Paul Kagame (Rwanda) na Yoweri Museveni (Uganda) kuzungumzia masuala mbalimbali ya kushirikiana nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Waziri Sitta alibainisha msimamo wa Tanzania kutengwa na nchi hizo tatu jana bungeni, alipokuwa akijibu maswali ya wabunge mbalimbali waliokuwa wakitaka kujua kauli ya serikali juu ya vikao vinavyofanywa na marais hao watatu.
 
Mbunge wa Viti Maalumu Rukia Ahmed (CCM), aliitaka serikali ipeleke pendekezo bungeni la kujitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla haijapewa talaka kutoka kwa Rwanda, Uganda na Kenya ambazo zimekuwa zikifanya mikutano inayojadili masuala ya jumuiya bila kuihusisha serikali ya Tanzania.
 
Akijibu hoja hiyo Sitta, alisema ni mapema kwa Tanzania kupeleka bungeni hoja ya kujitoa katika jumuiya hiyo kwa kuwa kinachofanywa na nchi hizo kimeshafikishwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama ambaye atakitolea ufafanuzi katika kikao kitakachofanyika wiki mbili zijazo.
 
Sitta alifafanua kauli ya Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hivi karibuni ya kwamba Tanzania inasubiri talaka akisema yenyewe ndiyo yenye uwezo wa kutoa talaka kwa jumuiya hiyo kwa kuwa inamiliki asilimia 52 ya eneo lote huku nchi zilizobakia zikigawana asilimia 48 iliyobakia.
 
“Hawa wenzetu wanafanya utoto wa kutuzunguka, sisi tunatumia hekima za mzee Mwinyi aliyesema ‘mwongo, mwongoze’. Kama wao wana hila zozote juu yetu, siku si nyingi tutazibaini, kama ni ndoa kwenye jumuiya basi sisi ndio tutakuwa tumeoa…hivyo tutatoa talaka wakati wowote,” alisema.
 
Naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela (CCM), aliitaka serikali isiendelee na hatua zozote kwenye jumuiya hiyo ambayo inaonekana kuelekea kuvunjika.
 
Akijibu swali hilo, Sitta alisema serikali haijakaa kimya bali imeamua kutoshiriki vikao vyote ambavyo nchi za Kenya, Rwanda na Uganda zitakuwa zimeshayazungumzia masuala husika na kuamua kuwa na msimamo wa pamoja nje ya jumuiya.
 
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alihoji serikali inangoja utafiti gani juu ya kutengwa kwao kiuchumi na nchi hizo tatu wakati Kenya wameshaingia makubaliano ya kibiashara na Ethiopia na Sudan.
 
Katika jibu lake, Sitta alisema Tanzania imeshafanya mazungumzo na nchi za DRC na Burundi kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
 
Alisema kuwa DRC ndiyo yenye manufaa makubwa kiuchumi kwa Tanzania kuliko Rwanda, Uganda, Kenya na Burundi kwa sababu mizigo mingi hutegemea bandari ya Dar es Salaam.
 
“Burundi nao wanatengwa kama tunavyofanyiwa sisi, lakini tumeamua kushirikiana kikamilifu na DRC pamoja na Burundi ambao tuna imani wana manufaa makubwa kwetu,” alisema.
 
Hivi karibuni Tanzania iliingia kwenye mgogoro na Rwanda baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ushauri kwa Rais wa Rwanda, Kagame kuketi chini na waasi wa nchi hiyo ili kuzungumzia masuala ya amani kwa nchi yao.
 
Tanzania Daima

TANZANIA: TUNAWEZA JITOA AFRIKA MASHARIKI

Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
 
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
 
Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.
 
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.
 
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.
 
Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
 
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
 
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.
 
Via- bbc
 
Tuesday, October 29, 2013

SAMSON MWIGAMBA: SIKUPIGANA NA MBOWE WALA HAKUWEPO WAKATI UGOMVI UNATOKEA, LAPTOP YAKE INA SIRI NZITO

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha ambaye amesimamishwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, Samson Mwigamba, amesema kuwa hakupigana na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, kama ilivyodaiwa na baadhi ya magazeti.
 
Mwigamba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuelezea kile kilichojiri mwishoni mwa wiki hadi akapigwa na baadhi ya wajumbe wa kikao, wakimtuhumu kwamba aliandika taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums akizungumzia masuala ya uongozi ndani ya chama.
 
Mwigamba alisema kuwa hata wakati akivutana na walinzi wa chama Mbowe hakuwa ndani ya chumba cha mkutano, hivyo akadai kuwa anashangazwa na wale waliosambaza taarifa hizo kwamba alipigana na kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.
 
Aliwataja wale aliodai walimpiga kuwa ni Katibu wa Bavicha Wilaya ya Arusha, Noel OLovaroya, walinzi wa chama pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba alijaribu bila mafanikio kumpiga na kitofali ambapo alikikwepa kwa kujiangusha chini na kujigonga kisogoni.
 
“Wakati vurugu zikianza Mbowe hakuwa ukumbini, nilimuona akija Lema na Olevaroya, ambapo Lema alishikwa kabla hajanifikia huku Olevaroya akiruka juu ya meza na kuja kunipiga ngumi, mimi kwa kujitetea ilibidi nimpige ngumi kabla hatujaamuliwa,” alisema.
 
Mwigamba alimtuhumu Lema kuwa amekuwa akimtishia kumuua kwa kipindi kirefu, ambapo siku ya tukio alirudia kauli hiyo kabla hajaenda kuchukua kitofali na kujaribu kumpiga nacho ambapo alikikwepa.
Alisema kuwa tayari alishatoa taarifa polisi na kupewa kumbukumbu: AR/RB/1759/2013 aliyoifungua Februari 12, mwaka huu, baada ya kuwa anapokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa Lema kupitia simu yake ya kiganjani.
 
Kuhusu kusimamishwa uongozi, Mwigamba alisema kuwa ametii licha ya kuwa kikao kilichomsimamisha hakina mamlaka kisheria, huku akiweka wazi kuwa hayuko tayari kukihama chama hicho, kwani bado anaamini ndicho chenye uwezo wa kuleta mabadiliko nchini.
 
Hata hivyo, tuhuma za Mwigamba zilikanushwa na Katibu wa CHADEMA wa mkoa, Amani Golugwa, akisema ni uongo dhidi ya Lema, kwani kwenye taarifa yake aliyowasilisha juzi kwenye kikao cha uongozi wa kanda alimsifu mbunge huyo kwamba ameongoza harakati mbalimbali za ujenzi wa chama kwa mafanikio makubwa, zikiwamo kampeni za ushindi wa kata nne zilizofanya uchaguzi mdogo hivi karibuni.
“Kwa kipindi chote ambacho amekuwa hayuko kazini Lema amekuwa akimsaidia hata kukamilisha ujenzi wa nyumba yake maeneo ya Sokon 1, hata anavyokwenda kwenye kesi zake Dar es Salaam ni Lema amekuwa akimsaidia gharama.
 
“Hicho alichokizungumza kwenye mkutano wake juu ya malalamiko ndiyo anatudhihirishia kuwa amekuwa nyoka na mnafiki ndani ya kundi letu,” alifafanua katibu huyo huku akisema hakuna malalamiko yoyote juu ya suala hilo ndani ya chama.
Golugwa aliongeza kuwa baada ya kupitia kompyuta ya Mwigamba wamebaini mambo mengi machafu na ya hatari kwa mustakabali wa chama ambayo yanawagusa watu wengi.
 
Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani wala kuyafafanua akisema yatakisaidia chama katika uchunguzi wake zaidi, na kwamba tayari kikao cha Baraza la mkoa kimeshakaa na kimemwandikia Mwigamba barua ya ajieleze ni kwa nini asivuliwe uongozi ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kulifikisha suala hilo mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Taifa.
 
Chanzo: Tanzania Daima
 
Monday, October 28, 2013

SHULE NYINGI ZA SEKONDARI ZA SERIKALI ZINANGOZWA NA WAKUU WA SHULE WASIOKUWA NA SIFA

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kuikalia ripoti ya Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mapema mwaka huu, baadhi ya wajumbe wake wameanika madudu mengi yaliyobainika katika uchunguzi huo.
 
Mmoja wa wajumbe waliounda Tume hiyo ameliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa waligundua mambo mengi yanayodhihirisha udhaifu mkubwa katika uendeshaji wa sekta ya elimu nchini, ikiwa ni pamoja na kubaini kuwa idadi kubwa ya wakuu wa shule hawana elimu ya shahada.
 
Alieleza kuwa kiutaratibu mkuu wa shule anatakiwa kuwa na elimu isiyopungua shahada pamoja na mafunzo ya uongozi na usimamizi. “Kumbukumbu zilionyesha kuwa elimu ya sekondari ya kawaidaina jumla ya shule 4,528. Wakuu wa shule 1,498 wana shahada ya kwanza au zaidi, 1,703 wana stashahada, 33 wana sifa nyingine” alisema.
 
Sehemu kubwa ya matokeo ya uchunguzi huo inasemekana yamejikita zaidi katika kuzitupia lawama taasisi za Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE).
 
Udhaifu wa kiutendaji kati ya taasisi hizo mbili unadaiwa umechangia kwa wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka jana, kiasi cha kuilazimisha Serikali kuunda tume kuchunguza tatizo kutokana na kilio kikubwa cha wadau wa elimu na wananchi.
 
Matokeo hayo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 walipata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakiwa wamepata daraja la nne.
Katika mtihani huo, watahiniwa 397,136 walikuwa wa shuleni na 68,806 wa kujitegemea.
 
Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu Pinda aliamua kuunda Tume iliyoanza kufanya kazi kuanzia Machi hadi Juni mwaka huu. Tume hiyo iliyokuwa inaongozwa na Profesa Sifuni Mchome ilimkabidhi Waziri Mkuu ripoti Juni 15, mwaka huu.
 
Hata hivyo, ripoti hiyo haijawahi kutolewa hadharani baada ya Tume kumaliza kazi yake, huku Profesa Mchome ambaye alikuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Vyuo Vikuu Tanzania akipandishwa cheo na kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
 
Kauli ya Profesa Mchome 
Profesa Mchome alipotafutwa jana kuzungumzia kuhusu upatikanaji wa wakuu wa shule alisema, “Mimi hivi sasa ni katibu mkuu wa wizara siwezi kuzungumzia hilo, kwanza sijaiona hiyo ripoti. Ukitaka ufafanuzi mzuri mtafute Kamishna wa Elimu.”
 
Gazeti hili lilimtafuta kamishna huyo pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo bila mafanikio kwani simu zao zilikuwa zikiita bila majibu.
 
Akifafanua zaidi kuhusu viwango vya elimu, uzoefu na uwezo wa wakuu wa shule za sekondari mjumbe huyo alisema, “Mkuu wa shule anatakiwa achaguliwe kwa vigezo maalumu na apewe muda wa miaka mitano katika nafasi hiyo na kila baada ya miaka mitano apimwe utendaji wake kabla ya kumuongezea kipindi kingine.”
 
Alisema kuwa bado malengo ya sera ya kuwa na wakuu wa shule wenye kiwango cha shahada ya kwanza au zaidi haujafanikiwa.
 
“Hivi sasa kuna shule za sekondari 4,528 wakati rekodi zinaonyesha jumla ya wakuu wa shule ni 3,238 hivyo kuwa na tofauti ya shule 1,294. Wakuu wa shule wengi hawajaandaliwa katika fani ya utawala na hawapati mafunzo yenye tija ya kujenga umahiri wakiwa kazini” alisema na kuongeza;
“Baadhi yao kubaki wakiogelea na kufanikiwa kwa juhudi zao wenyewe. Kukosekana kwa utaratibu wa upimaji kwa wakuu wa shule za umma kumewafanya walimu hao kukosa motisha na hivyo kutojitahidi katika kuifanya shule yake kuwa ya kwanza au ya mfano katika elimu.”
 
Alisema kuwa utaratibu wa kuteua na kutokuwapima wakuu wa shule umekuwepo kwa muda mrefu tangu wakati idadi ya shule, wanafunzi na walimu ilipokuwa ndogo.
 
“Kwa hali ya sasa, kuna ongezeko la idadi ya shule, walimu na wanafunzi hivyo mkuu wa shule hawezi kuchaguliwa na kuachwa bila kujengewa umahiri na akategemewa kufaulu katika kazi yake” alisema.
 
Alisema kuwa vigezo vya kumchagua mkuu wa shule vitumike, wapimwe weledi wao kila mara na wapate motisha pale wanapofanya vizuri na kuleta maendeleo katika shule zao.
 
Alisema kuwa utaratibu wa kupata wakuu wa shule katika shule za binafsi na tofauti na shule za umma, kusisitiza kuwa sasa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) inatakiwa kuandaa na kutekeleza utaratibu wa kupima utendaji wa wakuu wa shule na taarifa za utendaji wao zijadiliwe katika vikao husika vya Halmashauri.
 
“Shule za Serikali za sekondari zinapata wakuu wa shule kutokana na mfumo wa uteuzi. Shule nyingi za binafsi hasa zile zinazofanya vizuri katika masomo na mitihani zina mifumo endelevu ya kumpata mwalimu mkuu,” alisema na kuongeza:
 
“Baadhi ya shule za binafsi pia bado hazina uwezo wa kupata Wakuu wa Shule kwa mfumo wa aina hii kwa sababu ya uwezo mdogo wa kulipa mishahara kwa Wakuu wa Shule wenye sifa za juu na wanaoleta matokeo yanayotarajiwa na mwajiri.”
 
Alisema kwa kiasi kikubwa sekta binafsi imekuwa ikiitegemea sekta ya umma katika kupata Wakuu wa Shule walio mahiri.
 
Alisema kutokana na mazingira kubadilika, ualimu mkuu sasa ni fani na siyo cheo tu, kwamba hauna kipindi maalumu na hivyo mtu anaweza kuwa mwalimu mkuu kwa muda wake wote wa ajira.
“Mfumo wa aina hii hautoi fursa ya ubunifu katika maendeleo ya shule. Shule nyingi za binafsi zinaendeshwa kwa misingi ya mkataba wakati za serikali zina mfumo wa ajira ya umma wa kudumu. Mifumo hii ni tofauti na inahitaji mifumo ya uwajibikaji tofauti” alisema
 
Alisema walimu katika sekta ya umma ni wengi na hivyo huhitaji umahiri mkubwa katika kuwasimamia, kuwaendeleza na kushughulikia masilahi yao kuliko kwenye sekta binafsi.
Alifafanua kwamba hali hiyo inatokana na shule binafsi kulipa mishahara mikubwa kuliko ya Serikali na hivyo walimu wa Serikali kuhamia huko kwa sababu ya tofauti katika masilahi.

Via: MCL

Sunday, October 27, 2013

HAYA NDO MAJIBU YA MNYIKA JUU YA TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA ARUSHA ALISIMAMISHWA UONGOZI

Ni kweli nilikuwa mjumbe kwenye timu zilizohusika na kuandikwa kwa katiba mpya ya CHADEMA ya mwaka 2006, aidha nilikuwepo kwenye mkutano mkuu wa chama uliopitisha katiba mpya tarehe 13 Agosti 2006.

Tuhuma ya kwanza toka kwa Mwigamba :

“Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano.

"Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela”.

Majibu ya John Mnyika:

Madai hayo hayana ukweli kwa kadiri ya ufahamu wangu.

Mosi, mwaka 2006 hatukufanya marekebisho ya katiba bali tuliandika upya katiba ya chama kutoka ile ya mwaka 2004. Waraka uliandikwa nchi nzima kwa wanachama kutoa maoni na kuwasilisha makao makuu kuanzia kwenye ngazi zao za chini za kikatiba.

Baada ya kukusanya maoni kulikuwa na timu tatu, timu moja ilihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Profesa Baregu na katibu wake nilikuwa mimi.

Sehemu hiyo ya katiba niliandika neno kwa neno mapendekezo ya awali kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa, tulifanya mapitio pamoja na Profesa Baregu na hatimaye ikaingia kwenye vikao vya kikatiba vya chama na kupitishwa.

Sehemu ya falsafa kwa sehemu kubwa tulinukuu kwenye katiba kama ilivyokuwa mwaka 2004, sehemu ya itikadi tuliandika upya kabisa haikuwepo katika katiba ya CHADEMA ya zamani.

Sehemu zingine katika katiba kwa sehemu kubwa kazi ya kuunganisha maoni mapya na kufanya pia rejea kwenye katiba ya zamani ilifanywa na timu ya watu watatu tukiongozwa na muasisi wa chama Mzee Victor Kimesera pamoja na Mkurugenzi Benson Kigaila na mimi.

Kulikuwa na timu nyingine ya kuandaa miongozo ya mabaraza ya chama: Baraza la Wazee, BAVICHA na BAWACHA ambao nao walifanya kazi kwa upande wao na nilishiriki katika kupendekeza mwelekeo na mapitio ya kulinganisha rasimu ya miongozo yao na rasimu ya katiba ya chama.

Kwa ninavyokumbuka hicho kinachoitwa “kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano” hakijawahi kuingizwa kwenye katiba ya CHADEMA.

Baada ya timu zote kufanya kazi yake; rasimu ya katiba ilipita katika vikao vyote vya kikatiba yaani sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hatimaye mkutano mkuu. Katika vikao vyote hivyo, iwapo kipengele hicho kingekuwa kimeondolewa ‘kinyemela’ kama inavyodaiwa, mwandishi wa tuhuma hiyo angehoji toka Agosti 2006.

Aidha, baada ya katiba kupitishwa na kuanza kutumika kifungu hicho kingekuwa kimeondolewa kinyemela kati ya mwaka 2006 mpaka 2008 mtoa madai au mtu mwingine yeyote ndani ya chama angekuwa amehoji wakati wa matumizi. Kumekuwepo pia mchakato wa kufanya marejeo kwa ajili ya kushughulikia makosa ya uchapaji (errata) kwa nyakati mbalimbali, suala hili si kati ya mambo yaliyoibuliwa.

Mwaka 2009 CHADEMA kilifanya uchaguzi mkuu wakae mkuu nchi nzima ambapo vifungu vya masuala ya uchaguzi wa ndani ya chama vilifanyiwa rejea mara kwa mara. Mwandishi wa madai hayo alikuwepo wakati huo, suala hili la kwamba kuna kifungu kimeondolewa kinyemela sikulisikia likilalamikiwa kwenye vikao vyovyote vya kikatiba iwe ni sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na mkutano mkuu.

Kwa vyovyote vile kwa historia ya chama toka mwaka kilipoanzishwampaka wakati huo wa uchaguzi wapo viongozi ambao walikuwa wanagombea wakiwa na vipindi viwili wakati huo kwenye cheo kimoja cha ngazi moja.

Kifungu hicho kingekuwepo toka 2006 kingetumika kuwawekea mapingamizi. Na kama kingekuwa ‘kimeondolewa kinyemela’ kungekuwa na malalamiko mengi kiko wapi kwa kuzingatia ‘joto’ la uchaguzi wa wakati huo.

2010 mpaka 2013 madai hayo hayajawahi kutolewa kwenye kikao chochote cha kikatiba katika ngazi ya taifa kwa kuwa mimi ni mjumbe wa vikao vyote vya kitaifa ambavyo yeye amesema kwamba ni mjumbe.

Madai kama hayo yangetolewa na asiye mwanachama au walau mwanachama wa kawaida tungesema tu ni maoni ya kawaida yaheshimiwe na aelimishwe. Lakini madai kama hayo yakitolewa na kiongozi wa chama mwenye nafasi ya kuujua ukweli wote huo yanaacha maswali kuhusu dhamira yake.

Naamini mamlaka zinazohusika za chama zitatumika katiba, kanuni, maadili na itifaki kuchunguza na kuchukua hatua kuanzia kwenye ngazi yao huko tukio lilipotokea.

Hata hivyo, kwa maoni binafsi (yasichukuliwe kuwa ni kauli ya nafasi ninazoshikilia kwenye chama), dhamira ya haya inajionyesha kwenye andiko lenyewe la muhusika kuanzia aya ya kwaza:( nimeinukuu hapo chini)

“ Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwawana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.

Mtoa madai anaendelea kuandika kwamba :( nimenukuu hapo chini )

“ Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti.

"Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.

"Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu balikwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu."

Anaendelea kuandika madai mengine mengi lakini mwishoni anamalizia kwa dhamira yake ile ile :( nimenukuu hapo chini )

“ Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.”.

Kwa hiyo, dhamira yake ni uchaguzi na mabadiliko ya uongozi;dhamira yeyote njema ifuate mkondo wa katiba, kanuni, maadili na itifaki; kinyume chake ni ‘njama ovu’ na ‘utovu wa maadili”.

Nimekuwepo chaguzi mbili kuu za CHADEMA 2004 (nikiwa mtazamaji sio mwanachama) na 2009 nikiwa katikati ya chaguzi hizo kama kiongozi.

Naamini uchaguzi huu wa chama ulioanza kuanzia mwaka huu 2013 utakamilika mwaka 2014 CHADEMA ikiendelea kusimamia dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.

John Mnyika

HII NDO TAARIFA ALIYOISAMBAZA MWENYEKITI WA CHADEMA ARUSHA NA KUSABABISHA KUSIMAMISHWA UONGOZI NA KUPEWA KICHAPO

HUU NI UONEVU CHUKUA MUDA SOMA ALICHOKUWA AMEKIANDIKA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA JF NA KUFUKUZWA HALAFU UPIME USITOKWE POVU HUYU NI KIONGOZI NDANI YA CHAMA ANAKIJUA CHAMA WEWE MFUASI PIGA KIMYA:

"Wito kwa wana CHADEMA wote!

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari namadhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwawana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama. 

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio. 

Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari. 

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika. Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo? 

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwinginekidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kilamwanachama. 

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tenakatika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. Kakichukua kikiwana wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49. Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzitoza kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk. 

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao. Leo nitaainisha mambo machachetu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripotiza fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa: 

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama. 

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu balikwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi yakakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, Kkatibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwambakiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo. 

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michangoya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwamfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni 
questionable.

3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tuniliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watututafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, nahivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndotoya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari napikipiki zote za M4C.

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazomwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. Na mwenyekiti anafanya mambo hayoyote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendajiambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake yatenda. Huu si ufisadi ni nini?

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi namauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu.

Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama upinzani. 

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko ziHii ndiyo taarifa inayodaiwa kusambazwa katika mitandao ya kijamii na mwenyekiti wa Chadema Arusha akiwa katika kikao, taarifa hiyo aliyoipa kichwa cha habari "Wito kwa wana CHADEMA wote! baada ya kugundulika kuwa ni yeye aliyeandika na kukiri baada ya kupekuliwa katika 'laptop' yake, Baraza la uongozi mkoa huo wa Arusha uliamua kumvua uongozi, taarifa hiyo inasomeka hivi:

"Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari namadhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwawana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.

Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetuwakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli piakwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapondipo mtakapojua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.

Nitaendelea kuwadondolea ili muonekwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.

Ahsanteni kwakunisoma!"

MWENYEKITI CHADEMA ARUSHA ASIMAMISHWA KWA KUKISALITI CHAMA

HUU NI UONEVU CHUKUA MUDA SOMA ALICHOKUWA AMEKIANDIKA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA JF NA KUFUKUZWA HALAFU UPIME USITOKWE POVU HUYU NI KIONGOZI NDANI YA CHAMA ANAKIJUA CHAMA WEWE MFUASI PIGA KIMYA:

"Wito kwa wana CHADEMA wote!

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari namadhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwawana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama. 

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio. 

Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari. 

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika. Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo? 

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwinginekidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kilamwanachama. 

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tenakatika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.

Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. Kakichukua kikiwana wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49. Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzitoza kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk. 

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao. Leo nitaainisha mambo machachetu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripotiza fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa: 

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama. 

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu balikwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.

2. Matumizi ya fedha za chama:
Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi yakakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, Kkatibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwambakiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo. 

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michangoya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwamfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni 
questionable.

3. Taarifa za fedha
Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tuniliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watututafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.

4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, nahivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndotoya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari napikipiki zote za M4C.

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazomwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. Na mwenyekiti anafanya mambo hayoyote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendajiambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake yatenda. Huu si ufisadi ni nini?

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama
Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi namauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu.

Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama upinzani. 

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko ziBARAZA la uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini limemsimamisha uongozi Mwenyekiti wake wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.

Uamuzi huo umefikiwa juzi katika kikao cha dharura cha baraza hilo baada ya mwenyekiti huyo akiwa ndani ya kikao kutuma ujumbe katika mtandao wa kijamii unaolenga kuwachonganisha viongozi na wanachama wa chama hicho.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana juu ya uamuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni mbunge wa Karatu, Mchungaji Israeli Natse, alisema wameamua kuchukua uamuzi huo mgumu kutokana na tuhuma zinazomkabili Mwigamba na kuhitaji uchunguzi wa kina.

Natse alisema kuwa Mwigamba ametenda kosa hilo kupitia taarifa yake aliyotuma kupitia mtandao huo kwa jina la ‘Kwanini mabadiliko CHADEMA ni lazima’ na kusema kuwa viongozi wa chama wamechakachua katiba ili kuendelea kubaki madarakani.

Alitaja tuhuma hizo kuwa ni za usaliti, uzushi, uzandiki na uchonganishi kwa viongozi, ambazo zinahitaji uchunguzi makini, na hivyo kulazimu kumsimamisha wakati uchunguzi huo ukiendelea.
Kwa makosa hayo amekiuka Katiba ya CHADEMA sura ya 10 kuanzia kifungu cha 8, 9 na 10 ambavyo vinamzuia kiongozi kuchafua viongozi wenzake na wanachama kwa ujumla.

Alisema licha ya CHADEMA kuendesha uchunguzi, lakini pia uongozi wa Kanda ya Kaskazini ulimfikisha Mwigamba polisi kwa kutumia mtandao wa kijamii kukichafua chama hicho na viongozi wake ambapo ni kosa kisheria.

Naye Katibu wa CHADEMA wa kanda hiyo, Amani Golugwa, alisema baada ya kufikia uamuzi huo wanaandaa barua rasmi kumkabidhi Mwigamba, ikimaanisha kuwa amepoteza sifa ya kuingia katika vikao vyote alivyokuwa akiingia kupitia wadhifa wake wa uenyekiti.

“Tutakapomkabidhi barua inamaanisha kuwa anapoteza sifa ya kuingia katika vikao vya Baraza la Kanda kama mjumbe, vikao vya Baraza Kuu Taifa, Mkutano Mkuu Taifa na vingine vyote vya mkoa alivyokuwa akihudhuria kwa wadhifa wake wa uenyekiti,’’ alisema.

Kuhusu kumfikisha polisi, Golugwa alisema licha ya kumshitaki kwa tuhuma zinazomkabili, lakini ilikuwa ni kwa usalama wake kwa sababu chama kina wanachama wengi na kila mmoja ana hisia zake binafsi juu ya chama, hivyo ingeweza kuhatarisha usalama wake.

“Mimi kama katibu ambaye nimefanya kazi kwa karibu na Mwigamba akiwa mwenyekiti wangu wa mkoa, suala hili limeniumiza sana kwa kuwa sikutegemea kama angeweza kufanya alivyofanya,’’ alisema.
Alisema wakiwa katika kikao, walishangaa kuona ujumbe ukiingia katika mtandao wa kijamii na kushtushwa, hatua iliyowalazimu kufuatilia ili kumbaini aliyeutuma.

“Haikuwa rahisi kwake kukubali kuhusika kutuma ujumbe huo, na alitaka kuzua vurugu kikaoni, lakini baada ya kutakiwa kukabidhisha kompyuta mpakato ‘laptop’ na ilipokaguliwa kitaalamu na kupata uthibitisho ndipo alipobaki ameshangaa na kukiri kutenda kosa hilo,’’ alisema.

Aidha, tuhuma nyingine zilizotajwa ni kitendo chake cha kuwatuhumu mwenyekiti wa taifa na maofisa wengine wa chama kutumia fedha nyingi kuzunguka na kufanya vitu visivyo na msingi.
“Baada ya kutafakari hayo yote, chama kimeona hakiwezi kuendelea kuishi na mayai viza ama kulea mizoga kwa kuwa  tunaamini amedanganywa na watu ambao hawalitakii mema taifa hili,” alisema Golugwa.

Via Tanzania Daima

Saturday, October 12, 2013

MGANGA MKUU HOSPITALI YA MANYONI ATUHUMIWA, MWENYEWE ASEMA NI MAJUNGU TU

KAIMU Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Dk. Rahim Hangai, amezuiwa kuchukua mafuta lita 2,000 baada ya Mtunza Stoo wa hospitali hiyo, Mary Mayombe, kukataa kusaini vocha inayoruhusu kutolewa mafuta hayo kwa madai kuwa haikufuata sheria.

Akizungumza hivi karibuni na mwandishi wa habari hii, Mayombe alisema alizuia vocha ya lita 2,000 za mafuta kwa sababu ilichukuliwa kinyume cha utaratibu.

Alisema hali hiyo imemsababisha kuondolewa katika nafasi hiyo kutokana na mgongano kati yake na bosi wake.

“Kwa kawaida ili mafuta yatolewe huwa kuna vocha inaandaliwa ambayo inapitia kwangu naisaini ili mtu akapewe mafuta hayo lakini ikiwa inaeleza kila kitu, nikagundua vocha hiyo ina upungufu, nikazuia isiruhusiwe kwenda kwa mzabuni, yaani kituo cha mafuta ambacho ni mzabuni wa hospitali,” alisema.

Alisema yeye ni mwadilifu na mwaminifu katika kazi yake kwani siku zote hufuata sheria za kazi, ndiyo maana alifanikiwa kuzuia hizo lita 2,000 zilizokuwa zitoke kinyume cha utaratibu.

Nao wafanyakazi wa hospitali hiyo walidai kuwa Dk. Hangai alitoa tenda ya kuweka umeme wa jua wenye thamani ya sh milioni 18 bila kufuata taratibu.

Akizungumzia madai hayo, Dk. Hangai alisema tuhuma zote hizo ni majungu na wala hazina ukweli.

“Mwandishi kuhusu suala la mafuta hayo kuna taratibu zake, isingewezekana kuchukua kiasi hicho kikubwa cha mafuta,” alisema.

Alisema hata suala la zabuni ya umeme kuna dosari, kwa kawaida tenda yoyote inayoanzia sh milioni tatu lazima itangazwe gazetini

Chanzo: Tanzania Daima

Thursday, October 10, 2013

DR. SLAA AIRUSHIA KOMBORA CCM

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekuwa janga la Watanzania.

Amefafanua kuwa CCM inaua ubunifu wa vijana, kwamba asilimia 90 ya wanafunzi wanafeli shuleni huku viongozi wa chama hicho wakiwahadaa wananchi kwamba wanaleta maendeleo.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana alipozuru Shirika la Anga la Marekani (NASA) huko Huntsville nchini Marekani, ambako anaendelea na ziara yake ya kujifunza katika majimbo mbalimbali.

Akiongozana na mkewe, Josephine Mshumbusi, katibu mkuu huyo alilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Charles Frank Bolden Jr. pamoja na watendaji wengine na kupata fursa ya kutembezwa sehemu kadhaa.

Dk. Slaa alifika hapo kujifunza mambo mbalimbali, ikiwamo namna ya kuwashirikisha na kuwapa vijana wa Kitanzania changamoto ili waweke jitihada zaidi kwenye masomo ya sayansi, waweze kuinyanyua Tanzania kutoka kwenye shimo la umaskini.

Taarifa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimnukuu Dk. Slaa akisema kuwa wanasayansi wa Kimarekani walifika mwezini baada ya kupata changamoto kutoka kwa aliyekuwa Rais wao, John F. Keneddy, aliyewaomba wanasayansi hao kufikisha mtu mwezini chini ya miaka 10.

Alisema kuwa wanasayansi hao walimjibu na kufika mwezini chini ya miaka minane. Hali aliyodai ilitokana na Serikali ya Marekani kuipa kipaumbele elimu.

Dk. Slaa alisema kuwa baada ya uhuru, hayati Mwalimu Nyerere aliipa kipaumbele elimu kwa ujumla. Akitolea mfano kwamba aliwachukua vijana watano wanajeshi na kuwapeleka nchini Ireland kusomea mambo ya uhandisi.

“Waliporudi walipelekwa Kibaha ambako walibuni na kutengeneza gari la kwanza lililoitwa Nyumbu, ambalo ni ubunifu wao.

“Baadaye Mwalimu Nyerere aliwabunia wanajeshi hao mradi wa dhahabu wa Buhemba, ambao ungewawezesha kulipia gharama za kutengeneza magari mengi,” alisema.

Katibu mkuu huyo aliongeza kuwa kwa bahati mbaya baada ya Mwalimu kustaafu, mafisadi walijipenyeza na kuuchukua mradi huo. Kwamba huo ndio ufisadi uliozaa Meremeta.

“Mradi wa Nyumbu ukafa na kilichotokea ni ufisadi wa sh bilioni 155 uliohusisha Benki ya Netherlands ya Afrika Kusini. Hadi leo hakuna maelezo licha ya fedha hizo kutumika kwenye kampeni za CCM za mwaka 1995,” alisema.

Dk. Slaa alihoji ni maendeleo gani wanazungumzia CCM wakati watoto hawajui kusoma wala kuandika, huku wanajeshi waadilifu, wabunifu, wazalendo na wanaojituma wamefikia kuishi maisha ya ajabu.

“Ubunifu wao kama mradi wa Nyumbu umeuawa na CCM, imefanya maisha yao kuwa magumu na ya kusikitisha. Wanajeshi waliostaafu wamebaki kama ombaomba.

“Wale wanaoshiriki kulinda amani nje ya nchi wanadhulumiwa hela zao pale wanaporudi Tanzania. Nchi ambayo haiwezi kuwahudumia wanajeshi wake ni nchi isiyofaa kuwa katika ramani ya dunia,” alisema.

Dk. Slaa aliwaomba wanajeshi na vijana kutokata tamaa wala kusikitika kwani CHADEMA inasikia vilio vyao, na kwamba wanatambua kuwa ugumu wao wa maisha umesababishwa na CCM.

“Wakati hao CCM wanajineemesha na hela zetu za kodi, wanajeshi na wananchi kwa ujumla wanashindwa hata kujenga nyumba ya kujisitiri punde wanapostaafu,” alisema.

Aliongeza kuwa CCM imeua ubunifu ndani ya Tanzania na kuamua kuwaweka vijana kuwa mazezeta ili waendelee kuwatawala.

“Wenzetu wanapeleka watu mwezini, lakini Watanzania hata wembe tunanunua kutoka nje kwa sababu ya CCM. Wakiendelea kuwanyima wananchi haki zao za msingi muda utafika watachoka,” alisema.

via-Tanzania Daima