Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, October 7, 2013

RAGE ATAKA YANGA WAHAMISHIWE MABWEPANDE

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick kuhakikisha anawahamisha watani zao Yanga katika eneo la Jangwani kwa kuwa ni hatarishi kwa maisha yao.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe jijini Dar es Salaam jana, Rage mbali ya kumsifu Sadick kwa kuwaondoa baadhi ya watu na kuwapeleka Mabwepande, anamuomba awaondoe na Yanga kwani ni eneo hatarishi kwa maisha yao.
 
Alisema, yeye kama mtani wa Yanga, hahitaji kuwapoteza watani zake, hivyo basi anamuomba ahakikishe anawaondoa katika eneo hilo kama alivyofanya kwa watu wengine.
 
“Mimi nitahakikisha napeleka muswada huo bungeni, kwani wale wengine walitoka, hivyo basi namuomba Mkuu wa Mkoa awaondoe na Yanga eneo hilo kwani ni hatarishi pia kama walivyoondolewa wengine,” alisema Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini na kuwavunja mbavu mashabiki wa Yanga waliokuwepo katika eneo hilo.
 
Wakati Rage akimtaka Sadick kufanya hivyo, wiki iliyopita mkuu huyo wa mkoa aliwaruhusu Yanga kuwahamisha watu waliovamia eneo lao kwa kuwa walishawaondoa siku nyingi toka kipindi cha mafuriko, huku Manispaa ya Ilala ikiwataka kukagua mipaka na kujiridhisha kwanza
 
Via-Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment