Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, October 6, 2013

UCHEZAJI WA SHILOLE WAZUA GUMZO, WENGI WALAANI

Kutokana na style ya Shilole anayoitumia kucheza imezua gumzo kwa watu mbalimbali na hata katika mitandao ya kijamii, wapo wanavutiwa na uchezaji wake lakini pia lipo kundi lingine lisilovutiwa na uchazaji wake wakidai ni kinyume cha maadili ya Kitanzania, wanaochukizwa na aina hiyo ya uchezaji wa Shilole wamefika mbali zaidi na kusema kuwa, wanawake wengi ambao hawana vipaji au hawajiamini kuwa Nyimbo zao zinaweza kubamba huamua kucheza uchi au kwa style hiyo anayoitumia Shilole ili kuwavutia mashabiki.
 
Mdau mmoja aliuliza, " mbona Lady Jay Dee hachezi kama hawa akina Shilole wanavyojianika! na bado anapendwa, hawa akina Shilole wanatumia muziki kujiuza kimwili si vingine."
 
 
Wengine waliishushia lawama Serikali kwa kuacha tabia hii, ambayo kwa kiasi kikubwa ni udhalilishaji kwa wanawake, bila hata kukemea,"tufike wakati viongozi wetu wawe wakali kwa mambo kama haya, we angalia asilimia kubwa ya wanaohudhuria matamasha hayo ni watoto wadogo sana, wanajifunza nini hapo sasa! yaani leo mambo ya chumbani yanaoneshwa hadharani!" alisikika Mzee mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake wakati akihojiwa na www.venancefuraha.blogspot.com.
 
Kwa upande mwingine wale wanaotetea michezo hii ya akina Shilole, wanasema kuwa, huu ni utandawazi tuwaache wafanye wanavyotaka aliendelea kusema kuwa, "Kama mashabiki wanapendelea mambo hayo ya uchi uchi, we unadhani wafanyaje na wao wanataka pesa? "

"Tukitaka kuitokomeza tabia hii inabidi wanawake wenyewe kwa sauti zao na kwa umoja wao wakemee tabia hizi, lakini kama wao wanafurahia unadhani nani ataliona kama ni tatizo na wapenzi wakubwa wa show hizi za kingono ngono ni wanaume!" aliongeza mama mmoja wakati akichangia mjadala huu.

Hivyo tumeamua kukusanya picha mbalimbali za Shilole katika show zake kwa msaada wa mitandao mbalimbali, ambazo zinalalamikiwa na watu mbalimbali, kisha toa maoni yako je uchezaji huo unafaa kwa mazingira ya sasa au la. twende kazi sasa:

No comments:

Post a Comment