Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Friday, October 31, 2014

NI SHIIIIIIIIIIIIIIDA!!! MASOGANGE AZIDI KUJIANIKA MITANDAONI


Katika ukurasa wake wa facebook, Masogange ametupia picha hii hapa huku ikiambana na ujumbe wa , sijui lengo lake lilikuwa nini?

Photo: ITS FURAHIDAY

Kutazama picha zaidi za Masogange bofya HAPA

Friday, October 24, 2014

MAELFU WAMZIKA FR. MAKWANDA, ATHIBITISHA KUWA ALIKUWA KIPENZI CHA WATU, MKUU WA MKOA SINGIDA AMPA TANO.


Na.Venance Furaha-Manyoni

Wakazi wa Manyoni na vitongoji vyake na wageni mbalimbali kutoka Mkoa wa Singida na mikoa mingine nchini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone, wamejitkeza kwa wingi leo kumzika Fr. Makwanda aliyefariki kwa ajali ya gari wakati akitokea Itigi kwenda Manyoni. ajali hiyo iliyotoa uhai wa Fr. Makwanda ilitokea eneo la Mabondeni usiku wa jumatatu, tarehe 20/10/2014. ajali hiyo huenda ilitokea kati ya Saa nne au tano usiku hivi. Mji mzima wa Manyoni ni kama ulikumbwa na simanzi baada ya taarifa za kifo cha Padri huyo kuanza kusambaa. Baadhi ya wakazi wa Manyoni wakiongea na BabaD Blog.wakimuelezea Padri huyo, walisema kuwa   alikuwa mtu mcheshi, mkarimu, na aliyependa kujichanganya na kila mtu bila kujali dini ya mtu.
"Kusema kweli ndugu yangu huu msiba ni pigo kubwa sana si kwa Wakatoliki pekee bali kila mtu aliyekuwa akimfahamu huyu jamaa atakuwa ameguswa na tukio hili" Alisema Mzee Juma aliyejitambulisha kuwa anatokea maeneo ya Majengo. 

Mkazi mwingine wa Manyoni ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake, alidai kuwa Padri Makwanda ni kama alijitabiria kifo, "Ujue padri wetu ni kama alikuwa anajua kuwa hivi karibuni hatakuwa nasi, ni juzi juzi tu alikuwa anatuonesha  eneo ambalo kama akitangulia kufa mwili wake utapumzishwa na hapo na ndipo alipopumzishwa siku ya leo (Jana) kweli huyu  padri alikuwa kipenzi cha watu ona umati wote huu!"

Akimzungumzia marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Parseko Kone, alisema kuwa Fr. Makwanda alikuwa mtu wa watu, mara nyingi nikiwa hapa manyoni Fr. Padri Makwanda alinipa sehemu ya kulala, alinihudumia chakula hakika nilikuwa nahudumiwa kama mtoto...katika hali ya kibanadamu Fr. Makwanda alikuwa kama kijana wangu, lakini kiroho alikuwa ni baba yangu." Alisema Mkuu wa Mkoa.

Wageni wengine waliohudhuria ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi. Fatuma Tawafiq, vingozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu na dini mbalimbali, wawakilishi mbalimbali kutoka Parokia na majimbo mbalimbali.

Mwili wa marehemu kabla ya kupumzishwa katika nyumba yake ya milele, misa ya kumuombea marehemu  ilifanyika katika kanisa la RC Manyoni, Parokia ya Kupaa Bwana na baada ya shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu yalifuatiwa na maandamano kuelekea makazi ya Mapadri ambako ndiko Mwili wa Fr. Makwanda ulipolazwa.

Mpaka mauti inamkuta Padri Makwanda alikuwa ni Msaidizi wa Paroko parokia ya Kupaa Bwana Manyoni.

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Fr. Makwanda enzi za uhai wake


Fr. Makwanda enzi za uhai wake

Jinsi ilivyokuwa maeneo ya makaburini
















Hii ndiyo gari aliyopata nayo ajali

Baba D. blog inaungana na Wanamanyoni wote kuipa pole familia ya Fr. Makwanda, Paroko wa Parokia ya Kupaa Bwana na waumini wote wa parokia hiyo. R.I.P Fr. Makwanda.

Picha kwa hisani ya Sylvery Hussein, Edga Madeje na wadau wengine.

Tuesday, October 21, 2014

LUNDENGA AMKIMNGIA KIFUA MISS TZ 2014 ADAI UMRI WAKE NI SAHIHI, CHETI CHA KUZALIWA CHA MISS HUYO CHAZUA UTATA




Kamati ya Miss Tanzania yakata mzizi wa fitna Kwa Sitti Mtemvu? Cheti cha kuzaliwa kilichooneshwa chazua utata

Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga hii leo amezungumza na waandishi wa habari  juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu. Kujua zaidi alichosema Lundenga BOFYA HAPA

Sunday, October 19, 2014

NAMNA YA KUMPIGIA KURA DIAMOND KATIKA TUZO ZA MTV INGIA HAPA

Kumpigia kura DIAMOND ni rahisi saana Bonyeza HAPA  itakupeleka moja kwa moja hadi kwenye picha hii

halafu utabonyeza ilo Neno VOTE chini ya jina la Diamond 

FID Q AJITOKEZA KUMTETEA MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU KUHUSU KUDANGANYA UMRI



Fid Q 1
Fid Q 2
KUHUSIANA NA HABARI ZA MISS HUYO SOMA ZAIDI HAPA

BOFYA HAPA PIA KWA USHAHIDI WA UMRI WA MISS HUYO

HUU NDO USHAHIDI MWINGINE UNAONESHA KUWA MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU ALIDANGANYA KUHUSU UMRI

               JUU, LESENI YA UDEREVA INAONESHA KUWA ALIZALIWA TAR. 31/5/1989


HII NI PASSPORT YAKE YA KUSAFIRIA NAYO INAONESHA ALIZALIWA TAR.31/5/1989

Kumbuka kwamba miss huyo alidai kuwa anamiaka 18 na elimu yake ni kiwango cha shahada ya pili yaani Masters SOMA HAPA ZAIDI

Wednesday, October 15, 2014

HUYU NDIYE MISS TZ MWENYE AKILI KULIKO WOTE, AVUNJA RECORD, ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MWAKA 1

MISS TANZANIA 2014 Sitti binti Mtemvu ambaye ni mtoto wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu wakati akijinadi alisema kuwa ana miaka 18 na elimu yake ana shahada ya Uzamili (Masters) mfumo wa elimu yetu jinsi ulivyo haiwezekani kijana wa miaka 18 akawa na elimu ya kiwango hicho,
Name:  wpid-mmgm0157.jpg
Views: 133
Size:  89.0 KB

HEBU TUPIGE HESABU;
Masters(Shahada ya uzamili)  miaka  2
Shahada ya kwanza                 miaka  3
Sekondari                                 miaka  6
Shule ya Msingi                       miaka 7
Chekechea  (kama alisoma)     mwaka 1
                                                               
IJUMLISHE HIYO MIAKA, YAANI: 2 + 3 + 6 + 7 + 1 = 19

Maana yake ni kuwa, mrembo huyo alianza shule akiwa na mwaka 0 kama alianzia chekechea, lakini kama alirukia moja kwa moja darasa la kwanza itakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na mwaka mmoja.

Hapa inawezekana, mrembo huyo alidanganya miaka yake ya kuzaliwa au alidanganya kiwango chake cha elimu. lakini kama alichosema kitakuwa na ukweli basi maajabu haya yatakuwa yanapatikana Tanzania tu.

Ila ukitaka kujua kuwa aliudanganya umma BOFYA HAPA UTAJUA MIAKA YAKE HALISI


Julius S. Mtatiro's photo.
Julius S. Mtatiro's photo.

MAELFU YA MAGARI YA TOYOTA YANA HITILAFU, YATAKIWA KURUDISHWA

Kampuni kubwa zaidi ya kuunda magari, Toyota, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni moja nukta saba kote duniani kutokana na hitilafu ya breki za magari hayo.
Kampuni hiyo imesema hitilafu tatu zimetambulika kwenye breki katika miundo mbali mbali za magari ya Toyota ikiwemo muundo wa Lexus.
Magari yaliyo ndani na nje ya Japan yote yameathiriwa na hitilafu hizo.
Hata hivyo kampuni yenyewe imesema haina habari yoyote kuhusu ajali za magari au watu kujeruhiwa kutokana na hitilafu hizo.
Wadadisi wanasema hili ni jambo la kuabisha sana kwa Toyota ambayo imelazimika kuagiza magari yake kurejeshwa kiwandani zaidi ya mara moja kutokana na hitilafu mbali mbali. 
CHANZO: BBC

Monday, October 13, 2014

TAZAMA PICHA 96 SIKU YA MWALIMU DUNIANI ILIVYOFANA KIMKOA WILAYANI MANYONI

Siku ya Mwalimu Duniani hufanyika kila mwaka Octoba 5, kimkoa ilifanyika tarehe 10/10/2014, katika Wilaya ya Manyoni na Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick Sumaye. Pata tukio zima katika picha

 Baadhi ya walimu wakijiandaa kwa maandamano

MAANDAMANO YAKAANZA



















 Waziri Mkuu akipokea maelezo kutoka kwa Mwalimu namna 
ya kutumia vifaa mbalimbali kufundishia masomo ya sayansi 




                       Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Manyoni akiteta jambo na mwalimu                                         
 Walimu wakijadili jambo


 Mgeni rasmi na viongozi wengine wakisubiri maandamano

 Maandamano yakiingia viwanja vya Jumbe














 Walimu wakijipanga kuimba wimbo wa mshikamano

 Mkuregenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni 
akifuatilia burudani kwa makini

BURUDANI IKIENDELEA





 Shehe akipiga dua kuombea sherehe

Mama Msongo akipiga sala kufungua sherehe

 Walimu wa Manyoni wakiingia kwa ajili ya kutoa burudani

 Wakijipanga vizuri

 Wakiimba




 Walimu wa wilaya ya Manyoni wakiimba shairi

 Mgeni rasmi akisikiliza kwa makini shairi likiimbwa

 Mwalimu akitoa burudani ya shairi

 Bendi nayo ilikuwepo kutoa burudani

 Huyu naye alikuwepo 

 Bendi ikiendelea kufanya yake

                                 Wanafunzi wa shule ya msingi Tambuka reli wakitoa burudani                                              

 Meza kuu wakiwasikiliza kwa makini buradani

 Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Singida akitoa neno

 Mwakilishi wa R.A.S akitoa neno



 Mkurugenzi wa wilaya ya Manyoni akitoa neno

 Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Manyara akitoa salamu za Manyara

 Mwenyekiti wa CWT  Mkoa wa Dodoma akitoa salamu kutoka Dodoma


 Afisa Elimu Secondari Manyoni, Bw. Timoth Benard 
akiwasalimia wananchi 

BURUDANI



 Kikundi cha sanaa cha maalbino kutoka Dar. wakitoa burudani

                                                                  PICHA YA PAMOJA



 Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Frederick Sumaye na
 Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mama Fatuma Tawafiq na viongozi
 wenine wa CWT katika picha ya pamoja na kikundi cha sanaa cha albino

BURUDANI IKIENDELEA


 Kikundi cha sanaa cha akina mama kikitoa burudani

 MC Mwl. Salumu Mkuya akiwa na Katibu wa CWT Manyoni







 Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Sumaye akiwahutubia
 walimu na wananchi wengine

 Mwenyekiti wa CWT Manyoni akisalimia walimu na wananchi
Katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
 Wilaya ya Manyoni Bw. Supeti, kushoto kwake ni 
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Fatuma Tawafiq

Picha na Furaha Venance Soma zaidi HABARI HAPA