Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Wednesday, October 15, 2014

HUYU NDIYE MISS TZ MWENYE AKILI KULIKO WOTE, AVUNJA RECORD, ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MWAKA 1

MISS TANZANIA 2014 Sitti binti Mtemvu ambaye ni mtoto wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu wakati akijinadi alisema kuwa ana miaka 18 na elimu yake ana shahada ya Uzamili (Masters) mfumo wa elimu yetu jinsi ulivyo haiwezekani kijana wa miaka 18 akawa na elimu ya kiwango hicho,
Name:  wpid-mmgm0157.jpg
Views: 133
Size:  89.0 KB

HEBU TUPIGE HESABU;
Masters(Shahada ya uzamili)  miaka  2
Shahada ya kwanza                 miaka  3
Sekondari                                 miaka  6
Shule ya Msingi                       miaka 7
Chekechea  (kama alisoma)     mwaka 1
                                                               
IJUMLISHE HIYO MIAKA, YAANI: 2 + 3 + 6 + 7 + 1 = 19

Maana yake ni kuwa, mrembo huyo alianza shule akiwa na mwaka 0 kama alianzia chekechea, lakini kama alirukia moja kwa moja darasa la kwanza itakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na mwaka mmoja.

Hapa inawezekana, mrembo huyo alidanganya miaka yake ya kuzaliwa au alidanganya kiwango chake cha elimu. lakini kama alichosema kitakuwa na ukweli basi maajabu haya yatakuwa yanapatikana Tanzania tu.

Ila ukitaka kujua kuwa aliudanganya umma BOFYA HAPA UTAJUA MIAKA YAKE HALISI


Julius S. Mtatiro's photo.
Julius S. Mtatiro's photo.

No comments:

Post a Comment