Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Wednesday, November 27, 2013

ETI UV-CCM NDO WALIOMWANDALIA ZITTO KABWE MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI

UVCCM wamchafua ZittoUMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umeutia doa mkutano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, na waandishi wa habari uliofanyika juzi katika hoteli ya Serena baada ya maandalizi na uratibu wake kusimamiwa na vijana wa umoja huo.

Kwa hatua hiyo imeelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitia umoja wao wa vijana kwamba ndio walioratibu, kusimamia na hata kuugharimia mkutano wa mbunge huyo pamoja na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) Dk. Kitila Mkumbo.


Vijana hao wa UVCCM ambao ndio waliosimamia mkutano huo, walipata kuwa wanachama na viongozi wa CHADEMA lakini baadaye walienguliwa kwa makosa ya usaliti na baadaye kujiunga na UVCCM.
Vijana hao ni pamoja Juliana Shonza aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA), Tanzania Bara, Mtela Mwampamba, na Habib Mchange waliokuwa wanachama wa kawaida.


Mwampamba na Machage ndio waliokuwepo ukumbini juzi na ndio waliosimamia mkutano huo wa Zitto na Dk. Kitilla ambao waliutumia kufafanua na kujisafisha tuhuma zilizoelekezwa kwao na Kamati Kuu ya CHADEMA, iliyoamua kuwavua nyadhifa zao za uongozi na kubaki wanachama.


Vijana hao waliofukuzwa uanachama wa CHADEMA kisha wakajiunga na CCM kwa kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete, mjini Dodoma mapema mwaka huu.

Kisha wakaanza kuzunguka maeneo mbalimbali  nchini wakiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, ambapo wamekuwa wakisimama majukwaani na kwenye mitandao ya kijamii wakikiponda chama chao cha zamani pamoja na viongozi wake.


Katika siku za hivi karibuni, Mwampamba amekuwa akijiita kuwa ni msemaji wa UVCCM. Mchange yeye ingawa hajawahi kuonekana wala kutamka hadharani kuwa amehamia CCM, anajulikana kwa kuisema vibaya CHADEMA na viongozi wake, hasa mitandaoni.

Katika mkutano wa juzi wa  Zitto na Dk. Kitila, Habib Mchange ndiye alikuwa anafanya uratibu wa masuala mbalimbali ukumbini ikiwemo wakati wa maswali na majibu kutoka kwa waandishi wa habari na wadau wengine waliohudhuria.


Mwampamba ambaye ni mwanachama wa CCM, yeye alikuwepo ukumbini ambapo alionekana akizunguka na kutimiza majukumu fulani fulani, kisha baadaye inadaiwa alipeleka mkanda wa video wa mkutano wote ili urushwe katika kituo cha televisheni cha  Star tv.

Uwepo wa vijana hao, unamtia doa Zitto ambaye katika moja ya tuhuma zinazoelekezwa kwake ni pamoja na madai ya kutumiwa na CCM kuisaliti CHADEMA.

Katika moja ya tuhuma zake ambazo hata hivyo juzi alizipangua, Zitto anadaiwa kuandika barua kwa baadhi ya wagombea ubunge wa CHADEMA katika majimbo kadhaa, wajitoe ili kuiwezesha CCM ishinde bila kupingwa katika majimbo hayo.

Katika mkutano na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, Zitto ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, ameapa kuwa hayuko tayari kuondoka ndani ya chama hicho na atakuwa mtu mwisho kuondoka kwa hiari.


Wakati Zitto akiapa kwamba hayuko tayari kuondoka CHADEMA, Dk. Mkumbo, ambaye amekuwa mshauri mkuu wa chama hicho maarufu nchini, amesema kuwa kile kinachoitwa uhaini ndani ya CHADEMA ni wasiwasi wa siasa za ushindani kwa watu wasiotaka mabadiliko.


Akieleza sababu za kutokujitoa CHADEMA, Zitto alisema zaidi ya nusu ya maisha yake yamekuwa CHADEMA kwani alijiunga nacho tangu alipokuwa na miaka 16 hadi sasa ana miaka 37 na amekabiliana na vitisho mbalimbali dhidi ya wasiotaka mageuzi kwa wakati ule.

Mbunge huyo ambaye amepata umaarufu mkubwa tangu alipoingia bungeni, alieleza kuumizwa na shutuma nyingi ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kwa muda mrefu.


Alisema amekuwa akiitwa msaliti, mnafiki, mla rushwa akihongwa kwa ajili ya kukisaliti chama.
Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema  akiwa mwanasiasa kijana na binadamu anaamini ana makosa kwa kuwa hakuna binadamu aliye mkamilifu na kwamba upungufu wake unapaswa kupimwa na mema aliyoyafanya.

Kwa upande wake Dk. Kitilla Mkumbo alikiri kuuandaa waraka huo kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, ambaye naye kwa sasa amesimamishwa.


Alisema waraka huo uliandaliwa kwa siri bila kumshirikisha Zitto na kwamba hajui lolote kwani walipanga kumpelekea baada ya kukamilika na baada ya chama kutangaza tarehe ya uchaguzi.

Via: Tanzania Daima

Wednesday, November 20, 2013

SUMAYE AIPONDA DIVISION 5, APINGA ZERO KUFUTWA, AIPONGEZA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII KUIPIGA STOP SERIKALI KUTUMIA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU

                          
                           Na. Furaha Venance. Manyoni-Singida 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick T. Sumaye amesema kuwa, nchi yoyote kama inataka kuboresha elimu yake njia nzuri si kushusha viwango vya ufaulu, inachotakiwa ni kuhakikisha inaboresha utoaji wa elimu bora. Waziri Mkuu huyo mstaafu ameyasema hayo jana {Jamatano} katika mahafali ya 11 ya wahitimu wa kidato cha IV katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Amani [Amani Girls] iliyoko wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.

Akionekana kutokubaliana na viwango vipya vya ufaulu vilivyotangazwa na wizara ya elimu, aliema, “Tusitengeneze viwango vya ufaulu ambavyo vinatiliwa shaka…” aliendelea kusema kuwa, kwa viwango vipya vya ufaulu maana yake ni kuwa wanafunzi watafanya bidii ya kufeli kuliko kufaulu kwa kuwa kufaulu kutaoneka kuwa ni rahisi kuliko kufeli akasisitiza kuwa, hakuna nchi yoyote duniani ambayo haina alama za kufeli.


"Ndugu zangu, kama badiliko hili litapitishwa maana yake ni kuwa mwanafunzi atafanya bidii ya kufeli…na kama hakuna kufeli ufaulu hauna ulazima. Kwa sasa mwanafunzi anasoma kwa bidii ili asifeli, viwango vipya vinafanya kufeli kuwa kazi kuliko kufaulu” Alisema Sumaye.


Pia ametumia fulsa hiyo kuipongeza Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, inayoongozwa na Mh. Magreth Sitta, kwa kupinga hivyo viwango vipya vya ufaulu na kuishauri serikali kutumia viwango vya zamani.


Kuhusu ubora wa elimu unaopatikana katika shule za serikali na zile za binafsi, Sumaye alisema kuwa, utoaji wa elimu na ubora wa elimu umekuwa tofauti sana kati ya shule binafsi na za serikali, na hata zile za serikali pia kuna utofauti mkubwa wa utoaji wa elimu bora kati ya shule kongwe na hizi za kata.


“ Siyo kwamba nazipinga hizi shule za kata, hapa sizipingi kwa sababu ni sera ya serikali, lakini upanuaji wa elimu huenda sambamba na upatikanaji wa walimu, vitabu na vifaa vingine vya kufundishia, kujenga shule bila walimu ni sawa na kujenga hopitali bila madaktari." Alisema Mh. Sumaye


Awali kabla ya mgeni rasmi hajaanza kuzungumza, Mkuu wa shule, akisoma risala ya shule hiyo, alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, imekuwa ikipiga hatua kitaaluma katika mitihani ya taifa kidato cha nne, kwa mfano mwaka 2003 shule ilikuwa ya 60 kati ya shule 180, 2004, ilikuwa ya 41 kati ya shule 187, 2005 ya 28 kati 174, 2006, ya 22 kati ya 144, mwaka 2007 ya 75 kati ya 143, miaka mingine ni, mwaka 2008 ilikuwa ya 70 kati ya shule 1643, mwaka 2009 ilishika nafasi ya 83 kati shule 2261, 2010 shule hiyo ilishika nafasi ya 80 kati ya shule 3197, mwaka 2011 nafasi ya 26 kati ya shule 3908 na mwaka 2012 ilishika nafasi ya 48 kati ya shule 3396.

Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne mwaka huu ni wanafunzi 54, ambao walianza kidato cha kwanza mwaka 2010 wakiwa wanafunzi 72, kwa mujibu wa mkuu huyo wa shule, idadi hiyo imepungua kutokana na matatizo mbalimbali, kama vile ugonjwa, kuhama shule na wengine kutofikisha wastani wa shule hiyo kutoka kidato kimoja kwenda kingine ambani wastani wa 50%.


Kwa sasa shule ina mpango wa kujenga shule katika eneo lingine hapa hapa Manyoni, shule hiyo itakuwa ni kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita.

Tazama picha mbalimbali za sherehe hiyo.


                               Mgeni rasmi akiingia kwa gwalide lililoandaliwa na wanafunzi waaga

                                              Burudani waaga wakicheza wimbo wa twist
 Wanafunzi waaga wakisoma risala

Baadhi ya wahitimu na wageni waalikwa

Comedy nayo ilikuwepo,  

                                                     Meneja wa shule akitambulisha wageni

                                                          Wahitimu wakisoma risala

Mkuu wa Shule akisoma risala

                                                                   Baadhi ya wahitmu

                                     Mgeni rasmi, Mh. Sumaye [Waziri Mkuu mstaafu] akihutubia
   

                                       Wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi

                                       Viongozi wa dini wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi

                                                     Mgeni rasmi akiendelea kuhutubia
                               Baadhi ya wahitimu na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi
                                                    
                                              Mgeni rasmi akitunuku vyeti kwa wahitimu

Mgeni rasmi akitoa zawadi kwa wahitimu

                                                       Baadhi ya wahitimu wakiangalia vyeti vyao

                                                          Picha ya pamoja na wahitimu

                                             Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Amani Girls

                                                              Mgeni rasmi akikata keki

                                                     Mgeni rasmi akilishwa keki na wahitimu


Imeandaliwa na Furaha Venance
Anapatikana kwa barua pepe: venancefuraha@gmail.com                                                                     Simu: 0715 33 55 58 au 078733 55 53

Monday, November 4, 2013

HAKUNA DIVISION 5 WALA ZERO, SPIKA AAGIZA SERIKALI ILETE KAULI YAKE BUNGENI

WIKI moja tangu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome, atangaze mfumo mpya wa upangaji alama za matokeo ya wanafunzi wa sekondari kwa kufuta daraja sifuri na kuanzisha daraja la tano, naibu waziri ameibuka na kupingana naye.
 
Naibu waziri huyo, Philipo Mulugo, aliibua mkanganyiko huo bungeni jana, akisema si kweli kwamba serikali imefuta daraja la sifuri katika mitihani ya kidato cha nne kama ilivyoeleweka.
 
Kutokana na kukinzana huko, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliiagiza serikali kuleta bungeni mabadiliko ya madaraja hayo ya ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne na sita yaliyotangazwa hivi karibuni.
 
“Naibu Waziri nenda mtuletee kauli ya Serikali kuhusiana na utaratibu huo ili kuweza kupata majibu ambayo yanaridhisha,” alisema.
 
Awali akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige (CCM), Mulugo alisema taarifa zilizoenea kwamba daraja la sifuri limefutwa si za kweli.
 
Katika swali lake, Magige alitaka kujua kama uamuzi wa serikali wa kushusha madaraja katika mitihani ya kidato cha nne lengo lake ni kuwaokoa wanafunzi wanaofeli.
 
“Serikali haijafuta divisheni sifuri na wala hakuna daraja la tano, yaliyopo ni la kwanza, pili, tatu, nne na sifuri kama kawaida,” alisema.
 
Alisema unamuzi wa kushusha madaraja uliofanywa haukuwa na lengo la kuwaokoa wanafunzi wanaofeli bali ni kuondoa mrundikano wa alama katika daraja moja.
Alisema serikali imeweka madaraja mapya kwa kutofautisha alama kumi kumi kutoka daraja moja kwenda jingine na kwamba hata hivyo alama za ufaulu bado ni 40 ambazo ni daraja la C.
Awali akijibu swali la msingi la Magige, Mulugo alisema serikali haina mpango wa kuanzisha programu maalumu hasa za ufundi kwa wanafunzi waliofeli katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.
“Kwa mwaka 2013, jumla ya wanafunzi 60,507 wa kujitegemea, wamejisajili kufanya mtihani huo, watahiniwa 3,578 wakiwamo wasichana 2,020 na wavulana 1,558 waliofeli katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamejisajili kurudia mtihani huo,” alisema.
 
Alisema kwa sasa katika vyuo vya Ufundi Stadi kuna programu za fani mbalimbali za muda mfupi na muda mrefu ambazo wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi na sekondari wanaweza kujiunga kwa vile mafunzo yatolewayo katika vyuo hivyo huzingatia stadi moja tu.
 
“Serikali imekuwa ikiongeza na kuboresha vyuo vya ufundi na kuweka mazingira rahisi kwa wanafunzi ili waweze kupata stadi mbalimbali,” alisema.
 
Mulugo aliongeza kuwa kati ya mwaka 2010 hadi 2012, serikali kupitia VETA imesajili jumla ya vyuo vya Ufundi Stadi 75 sawa na asilimia 75 na asilimia 10.8 ya vyuo 618 vilivyokuwapo.
 
Naibu waziri huyo alifafanua kuwa katika kipindi hicho, jumla ya vyuo vinane sawa na asilimia 3.2 ya vyuo 248 vilivyokuwepo vilisajiliwa na NACTE.
 
Via : Tanzania Daima

SHIBUDA ATIMULIWA, CHADEMA KANDA YA ZIWA HAWAMTAKI

MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA), ametimuliwa katika kikao cha ndani ya chama hicho Kanda ya Ziwa Mashariki kwa madai ya usaliti.
 
Uamuzi wa kutimuliwa kwa mwanasiasa huyo ulifikiwa juzi jioni mkoani Shinyanga wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipokutana na viongozi wa kanda hiyo katika kikao cha ndani kwa ajili ya mikakati ya ujenzi wa chama.
 
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki, Silvester Kasulumbai, alisema kuwa katika mkutano huo uliowahusisha viongozi wa mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara, kabla ya Shibuda kutimuliwa, Mbowe alimpa nafasi ya kutetea tuhuma zilizotolewa dhidi yake ikiwamo sababu ya kuhudhuria majukwaa ya mikutano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
“Mmoja wa wajumbe alisimama na kutoa hoja ya kuwa kikao hicho hakiwezi kuendelea kujadili masuala ya msingi ya chama ilhali kukiwa na watu wanaotoa taarifa kwa CCM na ghafla akamtaja mtu huyo kuwa ni Shibuda,” alisema.
 
Kasulumbai aliongeza kuwa mtoa hoja alisisitiza kuwa Shibuda alipanda katika jukwaa moja na viongozi wa CCM na kudai kuwa vyama vya upinzani havina kitu, kwamba CCM ndicho chama tawala, hali aliyoeleza kuwa hata mikakati itakayopangwa katika mkutano huo anaweza kuivujisha na hivyo kumtaka Mbowe amtoe nje ya kikao hicho.
 
Kwa mujibu wa Kasulumbai ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Mashariki, baada ya hoja hiyo Mbowe aliwataka wajumbe wasiwe na jazba na wampe nafasi Shibuda ili aweze kujitetea dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake.
 
Alisema baada ya Shibuda kupewa nafasi alieleza kuwa yeye kupanda katika jukwaa la CCM si jambo la ajabu katika masuala ya kisiasa na kutolea mfano hatua ya wenyeviti wa vyama vitatu vya CHADEMA, NCCR-Mageuzi na CUF kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu huku wakijua kuwa ni mwenyekiti wa CCM.
 
Kasulumbai alisema katika utetezi wake, Shibuda alisema kwamba mtu mzima anapokuwa na shida yoyote hukimbilia kwa baba yake na kumaainisha baba huyo ni chama kinachotawala yaani CCM.
 
Aliongeza kuwa kauli ya Shibuda iliwakasirisha wajumbe na kuwaudhi zaidi, hivyo kuanza kumshambulia kwa maneno hali iliyomfanya Mbowe kuingilia kati na kuwataka wajumbe kupiga kura kwa ajili ya kufikia hitimisho juu ya uwepo wake katika kikao hicho.
 
“Zilipigwa kura akapata kura 38 zilizotaka aendelee kubaki ndani, tano ziliharibika na 90 zilitaka aondolewe katika kikao na wajumbe wakamuomba Mbowe afanye utaratibu wa kumuondoa kwa amani,” alisema Kasulumbai.
 
Alipotafutwa kwa simu jana kuzungumzia tuki hilo, Shibuda alisema wanachama na wafuasi wa CHADEMA walimuelewa vibaya alipopanda jukwaani katika mkutano wa CCM mjini Geita.
 
Alisema wakati alipopanda jukwaani na kuonana na viongozi wa CCM, alikuwa akiwakilisha kilio cha wakulima wa pamba wa Kanda ya Ziwa.
 
“Mimi ni mlezi wa wakulima wa pamba Kanda ya Ziwa na pale nilimfuata Katibu wa CCM nikamueleza kuwa akamwambie mwenyekiti wake, Rais wa nchi kwamba tunapata taabu na masilahi kidogo kwa kuwa tunanyonywa na wajanja katika kilimo cha pamba,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Shibuda, kitendo hicho angekifanya kwa kiongozi wa chama chochote kilicho madarakani kwa kile alichoeleza kuwa ilani ya wakati itakayokuwa inatekelezwa ni ya chama husika.
 
Aliongeza kuwa kwa nafasi yake ya mbunge anayetokana na CHADEMA hoja yoyote atakayoipeleka serikalini na kufanikiwa zitakuwa ni juhudi za chama badala ya watu kumfikiria kuwa msaliti.
“Kuna waganga njaa ndio wanaendekeza mifarakano ndani ya chama na hii ipo katika vyama vyote, wanafanya hivi si kwa sababu ya masilahi ya chama na nchi bali kuhakikisha matumbo yao yanashiba wakati wote kwa kuendekeza misigano isiyo na ulazima,” alisema.
 
Aliongeza kuwa kama hatua ya kutaka kuwatetea wakulima wa pamba Kanda ya Ziwa ni usaliti atakuwa tayari kuhukumiwa na kufukuzwa kwa hatua hiyo.
 
Via: Tanzania Daima

Sunday, November 3, 2013

HATUA TATU ZA KUMFANYA MSICHANA AKUKUBARI BILA KIPINGAMIZI, INGIA HAPA KUPATA MAUJANJA

 
 
Let’s face it — there is no fool-proof way to get every woman to fall madly in love with you. Or is there?…
Almost ALL women have the same needs when it comes to looking for the right man, so there are ways of catching the eye of almost any woman.
• Would you like to be able to turn the head of any woman?
• Attract that woman you’ve had your eye on for a while?
• Or just want to take your current relationship to the next level?
Find the ANSWER in this video by relationship author, Josh Pellicer. In this video, he reveals to you the same three, life-changing steps he’s taught to thousands of men around the world so you can quickly and easily get the woman of your dreams. Watch now below.
 
 
Source: Mail Online

HABARI MPASUKO: SENGODO MVUNGI AVAMIWA NA KUJERUHIWA NA MAPANGA

Dr. Sengodo Mvungi ambaye ni mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba, mjumbe wa kamati kuu NCCR-Mageuzi na pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Bagamoyo amevamiwa na kushambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi akiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo, kwa sasa Dr. huyo mtalaam wa masuala ya sheria na katiba amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akiendelea kupatiwa matibabu. Dr. Mvungi ameshambuliwa zaidi sehemu ya kichwani. tazama picha Dr. huyo akiwahishwa hospitali kwa matababu.
 
 
 
 
 
 
Picha kwa hisani ya mtandao wa mzuka kamili

Saturday, November 2, 2013

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA MANYONI, INGIA HAPA

 
MATOKEO YA DARASA LA SABA YAMETANGAZWA, SASA TUNAWALETEA MATOKEO YA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA MANYONI, HIVYO KAMA UNA MTOTO, NDUGU JIRANI N.K. INGIA HAPA UTAKUTANA NA SHULE ZOTE ZA MSINGI WILAYANI MANYONI, JICHAGULIE SHULE UNAYOTAKA, BOFYA ANGALIA ALICHOVUNA MWANAO, BOFYA HAPA CHINI SASA:
 

MATOKEO YA DARASA LA SABA OUT! INGIA HAPA KUSOMA ALAMA ALIZOPATA MTOTO WAKO


Matokeo ya darasa la saba yametangazwa, bofya hapa chini kuona shule ya kijana wako na jinsi alivyopa alama kwa kila somo:

                                 http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/psle.htm
 

MATOKEO DARASA LA SABA HAYOOO! UFAULU WAONGEZEKA, HESABU NOMA KISWAHILI WAKIONEA

KIWANGO cha ufaulu katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu kimeongezeka, ambapo wanafunzi 427,606, sawa na ongezeko la asilimia 19.89 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali.
 
Hata hivyo licha ya ufaulu kuongezeka, matokeo hayo yanaonyesha kuwa wanafunzi wengi wamefeli somo la Hisabati na wamefanya vizuri zaidi katika somo la Kiswahili.
 
Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Dk. Charles Msonde, alisema somo la Kiswahili liliongoza kwa asilimia 69.06 huku Hisabati likiambulia asilimia 28.62.
 
Alisema kwa upande wa somo la Kiingereza, lilifanya vizuri kwa asilimia 35.52, Maarifa ya Jamii asilimia 53.00 na Sayansi asilimia 47.49.
 
Katika hatua nyingine, wavulana wameng’ara kwa kuongoza kwa asilimia 55.1 na kuwapita wasichana waliopata asilimia 46.68.
 
Alisema wanafunzi 427,606 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari za serikali.
 
Alisema kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 208,227 na wavulana ni 219,379, hivyo kufanya idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kuongezeka kwa asilimia 19.89 tofauti na mwaka jana ambapo kiwango kilikuwa asilimia 8.8 .
 
Dk. Msonde alisema kuwa mtihani huo ulifanyika Septemba 11 na 12 ambapo watahiniwa walitumia karatasi maalumu za ‘optical mark reader’ na kusahihishwa kwa mfumo wa kompyuta.
 
“Matokeo haya yanaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa 9,126 walipata daraja A, wakati wanafunzi 82,293 walipata daraja B.
“Jumla ya wanafunzi 336,187 walipata daraja C, 389,948 daraja D na waliobaki, yaani 27,367 walipata daraja E,” alisema Msonde.
 
Hata hivyo, Msonde, hakuweza kutaja mikoa iliyofanya vema na ile iliyoshika nafasi ya mwisho, zikiwamo shule zilizoongoza na kueleza kuwa baraza limewasilisha matokeo hayo kwenye mamlaka husika.
 
“Tumewasilisha matokeo kwa mamlaka husika ili zifanye uchaguzi wa watahiniwa wa kujiunga na elimu ya sekondari na matokeo hayo yatatangazwa na mamlaka husika mara baada ya kazi ya uchaguzi itakapokamilika,” alisema.
 
Akizungumzia udanganyifu katika mtihani, alisema takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watahiniwa waliofutiwa matokeo kutokana na kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani huo imepungua.
Alisema waliofutiwa matokeo mwaka huu ni watahiniwa 13, ikilinganishwa na watahiniwa 293 waliofutiwa matokeo kwa undanganyifu mwaka jana.
 
Kuhusu tatizo la baadhi ya wanafunzi kutojua kusoma na kuandika, Msonde alisema ni mapema mno kulijua hilo, kwani linahitaji muda.
 
Wanafunzi 844,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wa kumaliza darasa la saba, wengine 23,045 sawa na asilimia 2.66 hawakufanya kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya utoro, vifo, ugonjwa na wasichana kupata mimba.
 
Via Tanzania Daima

MWANANGU DAVID ATIMIZA SIKU 40, TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA JINSI TULIVYOIFURAHIA SIKU HIYO.

Siku ya ijumaa ya tarehe 01/11/2013 mwanagu David, alitimiza siku 40, tazama matukio katika picha jinsi tulivyofurahia siku hiyo, twende kazi sasa!
 
Akina mama wakiandaa msosi


Msosi ukiendelea kuandaliwa

Muda ukafika mtoto Davie akaanza kutolewa nje,
binti aliyesimama hapo mbele akiwa tayari kwa kumpokea mtoto
 

             Mtoto anatoloewa
 
Mama Davie [Wife] mwenye gauni la batiki
akisalimiana na dada [Mwalimu Epimack] atakayempokea mtoto
 mara baada ya kutolewa nje

Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa tayari kwa kumpokea mtoto Davie
 

Mtoto katolewa kila aliyehudhuria alipata nafasi ya kumbeba mtoto
 
Picha zifuatazo mtoto Davie akipitishwa kwa kila muhudhuriaji






 
 

 D akimfurahia D mwenzake 
 
 Sasa mtoto akakabidhiwa mama mtoto
 
MC wa shughuli akisema neno hapo
 
Kutoka kulia  Baba D, mama D na MC Mr. Moris  
 
Kutoka kulia Baba D, mama D na MC Mr. Moris 
 
 
 
 
Burudani
 
baadhi ya wahudhuriaji wakifuatilia matukio kwa makini
 
 
Ukafika muda wa kupata chakula cha pamoja

 


 

 





Davie akiwa na bibi yake mara baada ya kurudi ndani
 
 
Asante Mungu, Asante Mama D kwa kunipa zawadi ya mtoto Davie, nakupenda sana Mwanangu Mungu aendelee kukukuza kiroho na kimwili. wazazi wako tunakupenda sana.
 
Nawashukuru ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika nasi siku hii nzuri kwetu. MUNGU AWABARIKI SANA