Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Wednesday, November 20, 2013

SUMAYE AIPONDA DIVISION 5, APINGA ZERO KUFUTWA, AIPONGEZA KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII KUIPIGA STOP SERIKALI KUTUMIA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU

                          
                           Na. Furaha Venance. Manyoni-Singida 

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick T. Sumaye amesema kuwa, nchi yoyote kama inataka kuboresha elimu yake njia nzuri si kushusha viwango vya ufaulu, inachotakiwa ni kuhakikisha inaboresha utoaji wa elimu bora. Waziri Mkuu huyo mstaafu ameyasema hayo jana {Jamatano} katika mahafali ya 11 ya wahitimu wa kidato cha IV katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Amani [Amani Girls] iliyoko wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.

Akionekana kutokubaliana na viwango vipya vya ufaulu vilivyotangazwa na wizara ya elimu, aliema, “Tusitengeneze viwango vya ufaulu ambavyo vinatiliwa shaka…” aliendelea kusema kuwa, kwa viwango vipya vya ufaulu maana yake ni kuwa wanafunzi watafanya bidii ya kufeli kuliko kufaulu kwa kuwa kufaulu kutaoneka kuwa ni rahisi kuliko kufeli akasisitiza kuwa, hakuna nchi yoyote duniani ambayo haina alama za kufeli.


"Ndugu zangu, kama badiliko hili litapitishwa maana yake ni kuwa mwanafunzi atafanya bidii ya kufeli…na kama hakuna kufeli ufaulu hauna ulazima. Kwa sasa mwanafunzi anasoma kwa bidii ili asifeli, viwango vipya vinafanya kufeli kuwa kazi kuliko kufaulu” Alisema Sumaye.


Pia ametumia fulsa hiyo kuipongeza Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, inayoongozwa na Mh. Magreth Sitta, kwa kupinga hivyo viwango vipya vya ufaulu na kuishauri serikali kutumia viwango vya zamani.


Kuhusu ubora wa elimu unaopatikana katika shule za serikali na zile za binafsi, Sumaye alisema kuwa, utoaji wa elimu na ubora wa elimu umekuwa tofauti sana kati ya shule binafsi na za serikali, na hata zile za serikali pia kuna utofauti mkubwa wa utoaji wa elimu bora kati ya shule kongwe na hizi za kata.


“ Siyo kwamba nazipinga hizi shule za kata, hapa sizipingi kwa sababu ni sera ya serikali, lakini upanuaji wa elimu huenda sambamba na upatikanaji wa walimu, vitabu na vifaa vingine vya kufundishia, kujenga shule bila walimu ni sawa na kujenga hopitali bila madaktari." Alisema Mh. Sumaye


Awali kabla ya mgeni rasmi hajaanza kuzungumza, Mkuu wa shule, akisoma risala ya shule hiyo, alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, imekuwa ikipiga hatua kitaaluma katika mitihani ya taifa kidato cha nne, kwa mfano mwaka 2003 shule ilikuwa ya 60 kati ya shule 180, 2004, ilikuwa ya 41 kati ya shule 187, 2005 ya 28 kati 174, 2006, ya 22 kati ya 144, mwaka 2007 ya 75 kati ya 143, miaka mingine ni, mwaka 2008 ilikuwa ya 70 kati ya shule 1643, mwaka 2009 ilishika nafasi ya 83 kati shule 2261, 2010 shule hiyo ilishika nafasi ya 80 kati ya shule 3197, mwaka 2011 nafasi ya 26 kati ya shule 3908 na mwaka 2012 ilishika nafasi ya 48 kati ya shule 3396.

Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne mwaka huu ni wanafunzi 54, ambao walianza kidato cha kwanza mwaka 2010 wakiwa wanafunzi 72, kwa mujibu wa mkuu huyo wa shule, idadi hiyo imepungua kutokana na matatizo mbalimbali, kama vile ugonjwa, kuhama shule na wengine kutofikisha wastani wa shule hiyo kutoka kidato kimoja kwenda kingine ambani wastani wa 50%.


Kwa sasa shule ina mpango wa kujenga shule katika eneo lingine hapa hapa Manyoni, shule hiyo itakuwa ni kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita.

Tazama picha mbalimbali za sherehe hiyo.


                               Mgeni rasmi akiingia kwa gwalide lililoandaliwa na wanafunzi waaga

                                              Burudani waaga wakicheza wimbo wa twist
 Wanafunzi waaga wakisoma risala

Baadhi ya wahitimu na wageni waalikwa

Comedy nayo ilikuwepo,  

                                                     Meneja wa shule akitambulisha wageni

                                                          Wahitimu wakisoma risala

Mkuu wa Shule akisoma risala

                                                                   Baadhi ya wahitmu

                                     Mgeni rasmi, Mh. Sumaye [Waziri Mkuu mstaafu] akihutubia
   

                                       Wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi

                                       Viongozi wa dini wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi

                                                     Mgeni rasmi akiendelea kuhutubia
                               Baadhi ya wahitimu na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi
                                                    
                                              Mgeni rasmi akitunuku vyeti kwa wahitimu

Mgeni rasmi akitoa zawadi kwa wahitimu

                                                       Baadhi ya wahitimu wakiangalia vyeti vyao

                                                          Picha ya pamoja na wahitimu

                                             Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Amani Girls

                                                              Mgeni rasmi akikata keki

                                                     Mgeni rasmi akilishwa keki na wahitimu


Imeandaliwa na Furaha Venance
Anapatikana kwa barua pepe: venancefuraha@gmail.com                                                                     Simu: 0715 33 55 58 au 078733 55 53

No comments:

Post a Comment