Katika kipindi hiki kuelekea siku kuu ya Christmass au Pasaka, ni jambo la kawaida kukuta nyumba za waumini wa dini ya Kikristo zikiwa zimepambwa na picha mbalimbali za Yesu. Lakini pia kama wewe ni muumini wa dini hiyo, unapotajiwa au kulisikia jina la Yesu, kuna picha fulani inakujia mawazoni, kuna sura fulani inakujia mawazoni, si picha au sura nyingine, bali ni sura ya Yesu.
Wapo wanaodhani kuwa picha hiyo au sura hiyo ndiyo Yesu mwenyewe aliyezaliwa yapata miaka 2000 iliyopita. Hapana, hakuna anayejua sura ya Yesu ikoje, anaonekana vipi, bali mtu huyo ambaye ulimwengu umezoea kumwona kama ndiyo Yesu wa Nazareti, huyu ni jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Brian Deacon. Ndiye jamaa aliyeigiza ile filamu maarufu ya Yesu, inayojulikana kwa jina la ‘Jesus Film’ mwaka 1979. filamu hiyo iliigizwa na watu mbalimbali ambao wengine wapo hai mpaka leo, picha za filamu hiyo zilipigwa nchini Israeli.
Kutoka kushoto ni Dalia Shapira aliyeigiza kama Mary Magdalene,
Babi Neeman aliyeigiza kama Yakobo, Niki Mitai aliyeigiza kama Petro
na Brian Deacon aliyeigiza kama Yesu katika filamu hiyo
Katikati ndiyo Brian Deacon aliyeagiza kama Yesu,
Kushoto ni mmoja wa watoto wa waigizaji katika filamu hiyo
aliyeigiza kama Yesu mtoto na kulia alieyeigiza kama Yesu mwenye umri wa miaka 12
Je Brian Deacon ni nani?
Brian Deacon ndio jina halisi la mwigizaji huyo ambaye ni raia wa Uingereza alizaliwa tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza ni mtoto wa pili katika familia yao, baba yake alikuwa ni fundi makenika huku mama yake akiwa akiwa ni Muuguzi.
Brian Deacon aliyegiza kama yesu katika filamu ya Yesu
Maisha yake ya Ndoa
Brian alifunga ndoa yake ya kwanza na binti aliyejulikana kwa jina la Rula Lenska mwaka 1977 na kufikia mwaka 1987 ndoa hiyo ilivunjika, huku wakiwa wamefanikiwa kupata mtoto wa kike ajulikanaye kwa jina la Lara Deacon,
Mwaka 1998 alifunga ndoa nyingine baada ya kuachana na Rula, alimuoa Natalie Bloch ambaye yupo naye mpaka sasa.
Brian Deacon katika filamu ya Yesu
Filamu
Alipata nafasi ya kuigiza filamu ya Yesu baada ya kupita mchujo, katika mchujo huo walijitokeza waigizaji zaidi ya 1000. Brian Deacon aliwahi kunukuliwa akisema kuwa, filamu hiyo ya Yesu ilimfanya yeye kuokoka baada ya kuitamaza kwani kabla ya kuigiza filamu hiyo hakuwa ameokoka. ilichukua miezi saba Mpaka filamu hiyo inakamilika
Hapa chini ni baadhi ya filamu alizocheza.
A Zed & Two Vamyres The Triple Echo Lillie (1978)
Noughts (1974) (1972)
(1985)
Unaweza iangalia hapa chini filamu yenyewe
Imeandaliwa na Furaha Venance, Habari na picha kwa msaada wa Mtandao.
Mawasiliano: 0715 33 55 58 (whatsapp)
0755 44 06 99
Nifollow instagram: fullraha17
Facebook: Furaha Venance
Nifollow instagram: fullraha17
Facebook: Furaha Venance
No comments:
Post a Comment