Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Saturday, December 7, 2013

WATAFUTA HURUMA YA UMMA KWA KUTENGENEZA WARAKA FEKI DHIDI YA CHADEMA

Watu wasiojulikana wametengeza waraka feki, wakidai kuwa umechomolewa katika laptop ya mmoja wa viongozi wa red brigade Makao makuu, baada ya juhudi za kumpata John Mnyika kuuzungumzia waraka huo kushindakana, mwandishi wetu aliwasiliana na kiongozi mwengine wa Chadema makao makuu ambaye hakutaka jina liwekwe hewani kwa kuwa si msemaji wa chama, alisema, "Kaka kuhusu huo waraka hata mimi nimeuona katika mitandao ya kijamii, huu ni upuuzi unaoendelezwa na wasiokitakia mema chema chetu,...tena ningependa watanzania wajue, katika kipindi hiki watasikia mengi tu, tutapakaziwa mengi sana, kiufupi chama chetu hakina mawasiliano ya aina hiyo, miundo ya barua zetu inafahamika, hatuna muhuri wa siri sisi wala hilo linaloitwa baraza maalumu la maamuzi hatuna katika chama chetu...hata maudhui ya barua yenyewe hayawezi kuandikwa na katibu mkuu." Alimalizia kwa kusema kuwa, "Chama chetu kiko imara wasaliti wote tutawatimua bila kuangalia sura zao au wamekitumikia chama kwa muda gani."

Waraka wenyewe huu hapa chini, kwa kuwa hauonekani vizuri, tumekuwekea namna waraka huo unavyosomeka. 

Mheshimiwa mwenyekiti, wajumbe wa baraza maalum la mapinduzi ya chama ni vema sasa tujipongeze kwa kazi nzuri tuliyoifanya.
Tangu tulipomalizana na CHACHA WANGWE harakati na mikiki mikiki yake kuanzia 2008 sasa tumekomesha.


Tuwapongeze sana makamanda LEMA na MNYIKA kwa kuandaa waraka wa siri unaoonyesha namna anavyolipwa mamilioni ya fedha. Hata kama atakwenda kushitaki mahakamani tutasingizia kuw...a amebebwa na mahakama kwa kuwa agenda yetu ya kumshusha na kutumiwa na CCM imefanikiwa sana kama ilivyokuwa kwa WANGWE, hivi sasa kila kona ananuka, hakuna anayeweza tena kumuamini kuwa hatumiwi na CCM, mpaka ukweli utapokuja kugundulika kuwa na mchezo nafikiri itakuwa tayari tumeshatimiza malengo yetu.


Pamoja na pongezi lakini pia hatutakiwa kulala, ni lazima tuendeleze mapambano ya kumchafua mpaka aone aibu kutembea, mpaka ajivue uanachama na ubunge.Huyu sio mtu mzuri hata kidogo,amevamia chama ambacho hajui waasisi wetu mlikianzisha kwa malengo gani, eti demokrasia, shauri yake


Tumdhibiti sasa na agenda yao ya kwamba sisi ni chama cha wahagga na wakristo, kuwaajili watu wa mikoa mingine kama vile Marcus,Kibatala na wengineo inaweza kuwa utetezi kwetu. Hoja ya ubunge wa viti maalum kuwa ni upendeleo haina mashiko tena shida ni hili la uchaga na ukristo kidogo, japo la ukristo linatubeba kwa kuwa tunapata sapoti ya wakristo wengi.

Nimesikia fununu kuwa watazunguka nchi nzima kutusema vibaya lakini hawatafanikiwa kwa kuwa makamanda wetu wameshatangulia huko tangu usiku wa siku tuliyomchinja.
Nimewaagiza pia makamanda wetu wa RED BRIGED wazuie na ikiwezekana kuwadhuru na hata kuwaua kabisa dawa ya hawa watu ni kuwashughulikia mpaka mwisho
NAWASILISHA USIRI UENDELEE KWENYE MAWASILIANO YETU

No comments:

Post a Comment