Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Tuesday, December 3, 2013

KUFUATIA TIMKA TIMKA YA WATU WANAOJIITA WENYEVITI WA CHADEMA, NAO WATOA KAULI YA MSIGWA NA JOSEPH SELASINI

Kutokana na watu wanaojitambulisha kuwa ni viongozi wa Chadema kutoa matamko au kujiuzuru nafasi zao,wakipinga kile maamuzi ya chama chao kuwavua akina Zitto na Kitila nafasi zao,  Mch. Peter Msigwa (Mbunge wa Iringa Mjini-Chadema) katika ukurasa wake wa facebook ameandika hivi:

 "Safari hii Kila mtu akijita mwenyekiti wa CHADEMA HATA KAMA CHEO CHAKE HAKIPO KIKATIBA ,IMEKUWA DILI . ILIMRADI NDOTO ZAO ZA KUONA CHADEMA INAKUFA. LET ME BE CLEAR ON THIS, OUR PARTY IS MORE STRONGER LIKE NEVER BEFORE, WE ARE NOT DYING WE ARE HERE TO STAY. ingawa ni wakati mzuri wa kupembua mchele. Huwezi sema eti kwa sababu umepanga na kupamba vizuri sebule yako,nyoka akiingia.,unaogopa kumtoa kwa kisingizio cha kuvuruga sebule. NI mwehu tu anayeweza kufikiri au kufanya hivyo. Mwerevu Atamsaka nyoka kwa gharam yoyote ikibidi hata kuvunja sofa, viti, redio,n.k, kwani gharama ya kuvunja vitu hivyo ni ndogo ukilinganisha na gharama ya kukaa na nyoka, ambaye anaweza kutoa uhai wako."


Naye mbunge wa Rombo Joseph Selasini ameandika hivi:

Kwa wenye uwezo wa kufikiri na kuamua kwa maslahi ya wengi, wasingeweza kukurupuka na matamko ya hovyo huku wakikimbilia CCM!. Huko ni kujidhalilisha kisiasa,na kuonyesha wazi kuwa mtu/watu hao hawana wala hawakuwa na nidhamu kwa chama.
Pia wanaowakaribisha huko CCM ni udhihirisha wazi kuwa lilikuwepo jambo nyuma ya pazia tangu awali. Nisingependa nimzungumzie Mhe.Zitto kwa sababu bado hatujapata majibu ya Tuhuma zake, kwasasa ngoja niendelee kuweka funda la maji kinywani.
Ifike mahali tujitambue kuwa sisi (Individual) si zaidi ya chama.

Joseph Selasini,
Mb.Rombo (CHADEMA)

No comments:

Post a Comment