Nitapambana kutetea uanachama wangu
Huu ndo ujumbe aliouandika Zitto Kabwe kupitia akurasa wake wa facebook,

Ninarudia kuwaambia ndugu zangu kwamba sitoki CHADEMA. Chama kina jasho langu na nitapambana mpaka dakika ya mwisho kutetea haki ya uanachama wangu.
Mimi ni CHADEMA toka ujana. Niliingia CHADEMA kwa kuchagua na sio wengine walioingia kwa Mazingira Ya kupata fursa za kugombea. Wengine wangepitishwa na chama walichokuwa kuwa wagombea Leo wasingekuwa upinzani na inawezekana wangekuwa mawaziri mizigo au waendesha operesheni tokomeza!"
No comments:
Post a Comment