Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, March 5, 2018

CAMFED YASHUSHA NEEMA KWA WANAFUNZI WA MWANZI. YAGAWA BAISKELI KIBAO NA VIFAA VINGINE



                            
                                                                                    Na. Mwl. Venance. F.K.
Shirika linalowasaidia wanafunzi wa kike litwalo CAMFED limetoa msaada wa baiskeli na mahitaji mengine kama vile magodoro, sale za shule, taulo za akina mama, madaftari, taa za sola na viatu vya shule. Aidha wapo wengine waliopata pesa kwa ajili ya kulipia pango na matumizi.
Akizungumza katika makabidhiano mbele ya wazazi na wageni waalikwa hapo jana (tar. 05/03/2018) Mkuu wa Shule Janeth Lubasi alisema wanafunzi takribani 60 ndiyo wanafadhiliwa na shirika hilo. Ambao kwa utaratibu kila mwaka wanafunzi wanajaza fomu maalumu kuomba ufadhili kwa kuandika mahitaji wanayoyahitaji kwa mwaka mzima. Kila mwanafunzi alitakiwa kuomba mahitaji ya kiasi kisichozidi Tsh. 250,000/=.

“Kati ya wanafunzi 60 wanafunzi 47 waliomba kununuliwa baiskeli, hivyo wazazi msishangae kuona wanafunzi wengine wanapata baiskeli wengine hapati…kila mwanafunzi amepewa kile alichoomba.” Alisema mkuu wa shule.

Aidha aliwataka wazazi kuzingatia kuwa vifaa hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi walengwa tu na si vya wazazi. “Hatutegemei kumkuta mzazi mnadani akiwa na baiskeli ya motto…baiskeli hii ni kwa ajili ya motto tu…na wazazi ambao watoto wao wamepewa magodoro hairuhusiwi mzazi kumbadilishia motto kudoro au kulichukua na kulitumia nyie…” alisema mkuu wa shule. 

Kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mh. Daniel Mtuka, diwani wa kata ya Manyoni, Mh. Machibula aliwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao na kuhakikisha wanasoma kwa bidii.

Mbunge wa Manyoni Mashariki Daniel Mtuka alisema kuwa ni jambo la kujivunia sana shule ya Mwanzi kuwa miongoni mwa shule zinazofadhiliwa na Camfed. “ndani ya mwanamke kuna kitu…ndiyo maana hawa CAMFED wameona umuhimu wa kuwasaidia hawa watoto wa kike…jambo la muhimu hivi vifaa vitusaidie katika kufanikisha malengo yetu ya elimu watoto” alisema.

Aidha mmoja wa wazazi ambaye mwandishi wetu alishindwa kupata jina lake alitoa neno la shukrani kwa niaba ya wazazi, aliushukuru sana uongozi wa shule na CAMFED kwa kuamua kuwasaidia.
jamani sisi wengine hata uwezo wa kununua viatu pea mbili hatuna…leo tumekabidhiwa baiskeli, viatu na vitu vingine tunasema asante asante sana yaani tunasema asante zaidi ya asante yenyewe.” Alisema.

Nisikuchoshe ungana na mwandishi wetu katika matukio katika picha hapa chini:



 Mh. Diwani wa Kata ya Manyoni akitoa salamu zake


Mh. Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki 
akimkabidhi mmoja wa wanafunzi vifaa


Baadhi ya baiskel walizopewa wanafunzi

 Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake ni mnufaika wa Camfed 
akitoa neno la shukrani

 Mmoja wa wanafunzi akipatiwa godoro na vifaa vingine na Mh. Mbunge

 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Mzee Msongo akitoa neno siku hiyo


Picha zimepigwa na Baba D.