Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, December 21, 2014

NGANO ZETU : HADITHI YA JOKA JEUPE

Hadithi ya Joka Jeupe

     Katika enzi za kale, kwenye Mlima wa Emi kulikuwa na majoka mawili yenye umri wa miaka elfu moja, moja jeupe, moja jeusi. Majoka hayo mawili yalipenda sana mandhari ya watu wanapoishi, basi yalijibadilisha kuwa wasichana wawili warembo, moja lilijipa jina la Bai Suzhen , jingine liliitwa Xiao Qing. Siku moja walifika kwenye sehemu maarufu yenye mandhari nzuri, ziwa la Xihu mjini Hangzhou.Mandhari ya ziwa la Xihu kweli ilivutia sana, walipofika kwenye daraja moja la ziwa hilo ghafla mvua ilianza kunyesha, wakakimbia mvua na kujificha chini ya mti mmoja mkubwa. Wakati huo alikuja kijana mmoja mwenye mwamvuli aliyeitwa Xuxian, ambaye alikuwa akirudi nyumbani baada ya kusafisha makaburi. Alipoona wasichana chini ya mti aliwasaidia kwa mwamvuli wake na baadaye aliwasaidia kuwapeleka nyumbani kwa mashua. Bai Suzhen alianza kumpenda kijana huyo, alipoagana na kijana huyo alimwambia kesho aje kuchukua mwamvuli wake.

Siku ya pili kijana Xuxian alifika nyumbani kwa Bai Suzhen karibu na ziwa kuchukua mwamvuli wake. Bai Suzhen alimshukuru sana na kumwuliza habari za familia yake, akafahamu kuwa alifiwa na wazazi wake mapema tokea alipokuwa mtoto na sasa anaishi kwa dada yake na kufanya kazi katika duka moja la dawa. Msichana Bai Suzhen aliomwomba aolewe naye. Hakika Xu Xian alikuwa na furaha isiyo kifani. Kwa kuongozwa na Xiao Qing walifanya sherehe ya ndoa. Baada ya ndoa walianzisha duka la dawa. Bai Suzhen alifahamu matibabu, kila siku aliwatibu wagonjwa wengi.
Kulikuwa na sufii mmoja wa dini ya Buddha aliyekuwa anaitwa Fa Hai. Fa Hai alikuwa anajua siri ya Bai Suzhen kuwa alikuwa joka mwenye miaka elfu moja, na hakika angewadhuru watu, hivyo alidhamiria kumwokoa kijana Xu Xian.

Siku moja Fa Hai alikuja nyumbani kwa Xu Xian, alimwambia, mkewe ni zimwi. Xu Xian hakuamini. Basi Fa Hai alimwambia, kama haamini, ajaribu kumshawishi anywe pombe tarehe 5 Mei, siku ya mashindano ya mbio za mashua, na kama akinywa atarudia asili yake.

Tarehe 5 Mei ilifika, kila familia hunywa pombe kusherehekea siku hiyo. Majoka yanaogopa pombe, Bai Suzhen alitaka kwenda mlimani kukwepa, lakini alikuwa na wasiwasi kuwa mumewe Xu Xian atamshuku, alikuwa hana budi ila kubaki nyumbani akijidai anaumwa.

Ingawa Xu Xian hakuamini aliyoambiwa na sufii Fa Hai, lakini kila mmoja katika siku hiyo hunywa pombe, hivyo alimshawishi mkewe anywe pia. Mkewe Bai Suzhen alishindwa kukataa, alikunywa glasi moja, mara akaanza kuona kizunguzungu. Xu Xian alimsaidia hadi kitandani, kisha akaenda jikoni kumtengenezea supu ya kuondoa ulevi. Akaja na bakuli moja la supu kitandani, alipofungua chandarua akaona joka kubwa jeupe limelala kitandani, Xu Xian alikufa kwa mshtuko.

Joka jeupe lilipozinduka likaona mumewe amekufa kwa mshtuko, alihuzunika sana, alimwomba Xiao Qing amtunze mumewe, na yeye akatoka haraka na kwenda kwenye mlima mmoja ulioitwa Xianshan ambako kulikuwa na aina moja ya jani la dawa ambalo lingeweza kumwokoa mumewe.

Wakati huo Bai Suzhen alikuwa amepata mimba ya miezi saba. Alipofika mlima Xianshan watoto waliokuwa wananlinda mlima walipojua kuwa anataka kuiba jani la ajabu walipambana naye. Mungu wa mlima huo alipoona jinsi Bai Suzhen alivyohangaika kumwokoa mumewe alimpa jani la ajabu.

Xu Xian alifufuka, lakini bado alikuwa ameshikwa na hofu. Bai Suzhen alipatia mzungu wa kumdanganya, alitumia kitambaa kirefu cheupe na kukigeuza kuwa joka kuzunguka kwenye boriti la dari na kumwita mumewe aone. Kwa kuona joka hilo, Xu Xian aliondoa mashaka yake juu ya mkewe, na waliendelea kuishi kwa mapenzi.

Sufii Fa Hai hakukufa moyo. Siku moja alimdanganya Xu Xian kwenda kwenye hekalu lake na kumzuia asirudi nyumbani. Baadaye mkewe na Xiao Qing walikuwa kwenye hekalu wakitaka kumrudisha nyumbani, wakagombana na sufii. Wakati walipopurukushana, Bai Suzhen alisikia maumivu ya uja uzito, kwa haraka alirudi nyumbani na Xiao Qing, alipofika kwenye daraja alikumbuka jinsi alipokutana na mumewe na kuanza na mapenzi, alihuzunika sana. Xiao Qing alimlaumu Xu Xian kwa kumsikiliza sufii, alimshawishi Bai Suzhen amwache mumewe.

Kwa kusaidiwa na sufii wengine, Xu Xian alitoroka kutoka hekalu na kwenye daraja alimpata mkewe. Mkewe alimwambia ukweli wa mambo, kwamba kweli alikuwa joka. Wakati huo Xu Xian alikuwa ameelewa kwamba mapenzi ya mkewe ni ya kweli na makubwa, akamwahidi kuwa hatajali akiwa ni kitu gani, lakini ataishi naye mpaka kufa.
Baada ya kurudi nyumbani, muda mchache baadaye Bai Suzhen alizaa mtoto. Katika siku ya kutimiza mwezi mzima kwa mtoto walifurahi sana, lakini wakati huo sufii Fa Hai alikuja tena nyumbani, alimkamata Bai Suzhen na kumtia chini ya mnara wa Leifong kando ya ziwa la Xihu.

Xiao Qing alitorokea mlimani Emei, alijitahidi kuinua uhodari wake wa mapambano, mwishowe alimshinda Fa Hai, na alimwokoa Bai Suzhen.

Chanzo:http://swahili.cri.cn/chinaabc/chapter19/chapter190305.htm

NGANO ZETU


HADITHI YA SIRI NYANI KUKOSA MANYOYA YA MUHIMU




Hadithi hadithi, hapo zamani za kale kulikuweko na sungura aliyekuwa na familia yake ya mke na mtoto mmoja, akawa ana hamu sana ya kujenga nyumba ya kuishi na familia yake. Akazunguka akitafuta mahala pazuri pa kujenga nyumba hatimae akapapata, akapasafisha siku nzima akajitayarisha kwa kuweka nguzo za awali za nyumba yake. Kumbe simba nae alikuwa na tatizo hilo hilo, nae akazunguka kwa mshangao akakuta mahala pazuri alipapenda pamekwisha safishwa akaamua kuanza kujenga alifanya kazi nzuri siku hiyo ikabakia kuweka paa. Sungura alipokuja baada ya siku moja akashangaa pameshajengwa hivyo akamshukuru Mungu na kuamua kuweka paa, nyumba ikawa tayari. Siku alipokuja kuleta familia yake akashangaa kukuta simba nae yupo na familia yake, wakasalimiana na baada ya majadiliano wakakubaliana kuwa nyumba ile waliijenga pamoja wakagawana vyumba. Mapema kabisa sungura alijua ujirani huu ni wa hatari sana, hivyo akapanga na mkewe njia ya kumtoa simba. Usiku wa manane akamuamsha mkewe kwa sauti,’Mke wangu ile mifupa ya simba tuliyemla wiki iliyopita iko wapi?’ Mkewe akajibu, ‘Si ulisema niiweke utampa mbwa wetu?’. Sungura,’Ahh okay, nilidhani imekwisha nikamtafutie mbwa wangu simba mwingine’. Simba kusikia vile alimuamsha mkewe na wakakosa raha kabisa kiasi cha kuhama jua la kwanza kwa kuogopa kuliwa na sungura. Wakiwa wanahaha porini, mvua ikaanza wakajikunyata chini ya mti kwa baridi, nyani akapita, akamuuliza Simba,’Mzee vipi tena mbona uko kwenye mvua huna raha?’, Simba akamwambia nyani kuwa hana nyumba kwa kuwa amekimbia nyumba kukwepa kuliwa na sungura, nyani akacheka sana,’Sungura kumla simba? sijawahi kusikia hebu nipe mkasa mzima’. Simba akahadithia mkasa wote na kumuwacha nyani anacheka  sana,’Sasa mzee, sungura kakudanganya, twende naenda kumtandika mikwaju mbele yako hana adabu kutisha wakubwa’. Msafara ukaanza kurudi alikokuwa sungura. Sungura alikuwa nje ya nyumba yake akamuona nyani akiongoza msafara wa simba na familia yake, akajua dili limebumbuluka. Walipofika karibu sungura akwahi kumkaribisha nyani,’Aise bradha nyani, aksante sana sikutegemea kama ungeweza kuwaleta kama ulivyoniahidi’. Simba kusikia hivyo akapaniki,’Haaa nyani kumbe umeniuza?’ Alichofanya ni kumkwangua nyani ngozi ya makalioni nakukimbia na kupotea. Na ndio maana mpaka leo nyani hana ngozi makalioni.
VIA:http://sundayshomari.com

Monday, November 10, 2014

KUMBE MAWIGI NI MANYOYA YA MBUZI

Nywele bandia ambazo wanawake wanapenda kuvaa siku hizi.
Nchini China nywele za bandia ni biashara kubwa sana , wanunuaji katika maduka ya urembo na saluni huambiwa kuwa nywele hizo ni za kweli, lakini ukiziangalia kwa karibu zaidi, wakati mwingine hazionekani hivyo.
Katika kiiji kimoja, jimbo la Hunan, katikati ya China,Katika mitaa ya kijiji hicho inaonekana kuwa na nywele hizo , baadhi ya nywele hizo ni za kweli lakini nyingine si nywele za binaadamu isipokua manyoya ya mbuzi.
Mtu mmoja anafanya kazi ya kukusanya nywele, anasema anapogonga kengele wanawake hutoka kisha mtu huyo huwakata nywele kwa ajili ya kuuza.Mwenyewe anasema anawapa hela nzuri.
Nywele za bandia zinazoelezwa kuwa za binadamu huchanganywa na manyoya ya mbuzi bila mteja kujua
Baada ya kukusanya nywele,huzipeleka kwenye kiwanda kidogo ambacho kuna wanawake ambao huzitengeneza na kuwa nywele za bandia.
Nikitazama ninaona baadhi ya nywele zinazosukwa pamoja ni za binaadamu lakini nyingine sio kabisa, na mtu huyu huuza nywele hizo kwa viwanda vikubwa ambapo huwekwa dawa za kemikali kabla ya kuuzwwa madukani na nchi nzima.
Nywele hizo hufikishwa mpaka mjini Guazngzhou,mji ulio maarufu kwa shughuli za biashara.
Katika eneo hilo hakuna mteja wa asili ya kichina wanunuaji wengi wanatoka Afrika , Nigeria, Ghana,Congo, Afrika kusini,Angola na Uganda
Chanzo: bbc

Sunday, November 9, 2014

ZITTO KABWE ASHUSHIWA TUHUMA 7, MWENYEWE AZIPANGUA, LENGO NI KUMUONDOA KWENYE MSTARI SAKATA LA WIZI WA MABILIONI YA PESA AKOUNTI YA TEGETA ESCRO


kia sintofahamu kuhusu sakata la IPTL hususani Ile akaunti Ya Tegeta Escrow kushikiliwa Kidete Rangi PAC inayoongozwa Rangi Zitto Kabwe, watuhumiwa wa wizi Huo wamezusha tuhuma kibao kwa Zitto Kabwe ILI kumpunguzia kasi Ya kupambana Rangi wezi Hao, hizi ndizo tuhuma saba (7) ambazo Zitto anazitolea ufafanuzi katika ukurasa wake wa facebook ikiwa Rangi Kichwa cha Habari  Nashambuliwa, tunashambuliwa! PAC tunasema "Hatutetereki" Nasi tumechukua Rangi tunakuletea KAMA ulivyo Bila kuongeza Wala kupunguza Kitu, JISOMEE ​​MWENYEWE


"Zikiwa zimebaki siku chache Kabla Ya Kamati ninayoongoza Ya PAC kuwasilisha Bungeni Taarifa Maalumu kuhusu ukaguzi maalumu wa akaunti Ya Tegeta Escrow, kumekuwa Rangi kampeni za Chini Chini zinazoendeshwa kwenye korido za Bunge Rangi kwenye mitandao dhidi Yangu binafsi Rangi baadhi Ya wabunge waliosimama Kidete dhidi Ya wizi Wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania akaunti Ya Escrow.

Baadhi Ya tuhuma nimezipeleka kwenye vyombo vya DOLA ILI zichunguzwe Kwani Zina vielelezo vya Latest pa kuanzia (KAMA leseni Ya udereva Ya mwanamke anajulikana KAMA Vivian Sirikwa Emmanuel Rangi MUHURI wa kampuni Ya uwakili inayomilikiwa Rangi Bwana Joseph Mkandege).
Baadhi Ya Tuhuma 
Baadhi Ya Tuhuma


Baadhi Ya tuhuma nitazijibu moja baada Ya moja.
Waziri Mmoja ambaye nai mtuhumiwa wa wizi wa fedha za Tegeta Escrow anazunguka to wabunge akisema tuhuma hizi kupikwa KAMA kutumia kutumia kutumia njia YAKE Ya kuhamisha mjadala kutoka uporaji wa Shilingi bilioni 200 Kwenda kwenye masuala binafsi.

Tuhuma hizi zenye Kichwa cha Habari "Zitto Rangi Filikunjombe wanatumiwa Rangi Kenya Rangi Uingereza kuvuruga Rangi kudhoofisha Uwekezaji nchini mwetu" zinajibiwa HAPA Chini. Utaona Ndugu Filikunjombe ametajwa to Kichwa cha Habari ILI kumtaja Tu Bila Sababu yeyote Ile.

Tuhuma # 1:
Zitto anaye Rafiki YAKE Mkenya aitwae Rapahel Ongangi ambao to PAMOJA wameanzisha Gombe Washauri Co Ltd (iliyosajiliwa tarehe 24 Novemba 2011, Cheti No 87,387) to ajili Ya kufanya biashara Rangi Makampuni Ya Gesi Rangi Mafuta yanayofanya Kazi nchini HAPA.

Majibu:
Gombe Washauri nai kampuni binafsi isiyofanya Faida yaani 'Company Limited Rangi Dhamana'. Haina Kazi Rangi kampuni yoyote Ya Gesi Rangi Mafuta Rangi Wala yenyewe haijuhusishi Rangi biashara hiyo. Gombe washauri haijafanya Kazi yoyote Ile Rangi kampuni Nyingine Zaidi Ya kusaidia wasanii wa kundi la Kigoma All Nyota. Upotoshaji HAPA unalenga kupindisha mjadala.
Tuhuma # 2:
Zitto amemsaidia Ongangi kupata Uraia wa Tanzania Rangi to Sasa nai raia wa pasipoti. Zitto Rangi Ongangi walimtafutia Mkurugenzi Mtendaji wa Shell aitwae Axel Knospe Nyumba Rangi Gari Ya kukodi.
Majibu:
Raphael nai mwavuli binafsi ambaye anafanya shughuli zake nchini HAPA, amesoma HAPA nchini Rangi ameoa Rangi ana Mtoto. Tuhuma hizi hazina Msingi wowote ule maana nai uwongo. Wanaotoa tuhuma hizi waonyeshe hiyo pasipoti Ya Bwana Ongangi kuthibitisha Madai Yao.

Tuhuma # 3:
Mikataba Ya Statoil iliyokuwa inarushwa kwenye mitandao Ya Jamii Rangi kuchapishwa kwenye magazeti Ya Kenya Ya HAPA nchini (Citizen Rangi Mwananchi) mwandishi mkuu alikuwa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Shell.

Majibu:
Mkataba uliovujishwa wa Statoil ulivujishwa Rangi waandishi wa habari wa Norway. Uchambuzi wa mkataba Huo nimeufanya mwenyewe to kutumia utaalamu Wangu niliosomea wa kuchambua mifumo Ya Kodi kwenye sekta Ya mafuta Rangi gesi. ILI namna yoyote Ile, huyo anayetajwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Shell Ya Ya Ya hahusiki. Tuhuma hii wanaoitoa watoe Ushahidi usio Rangi chembe Ya Mashaka.
Ikumbukwe kuwa mkataba wa Statoil utaipotezea Tanzania mapato Ya DOLA za Marekani bilioni 12 (takribani Shilingi 20,400,000,000,000 / =) katika kipindi cha miaka 15 baada Ya gesi kuanza kuchimbwa.
Uamuzi wa Kamati Ya PAC kutaka mikataba yote Ya Gesi kuwa wazi Una kuamini katika Sisi wenyewe la kuchambua kuona KAMA mikataba yote nchini haipotezi mapato to nchi. Uamuzi Huo umewakasirisha Sana baadhi Ya waliohusika kuingia mikataba Serikalini maana wanajua KUNA madudu kwenye mikataba Rangi wanataka umma wa watanzania usijue!

Tuhuma # 4:
Kampuni Ya SHELL imechukizwa Sana kucheleweshwa to kupata kibali cha kutafuta gesi Rangi mafuta kule Pemba. Vilevile SHELL Haina uwekezaji mkubwa Tanzania Bara Kwani ilishindwa kwenye tenda zenye vitalu vyenye gesi nyingi upande wa Bara.

Majibu:
Ukweli nai kuwa Kampuni Ya Shell mmojawapo vitalu 4 Huko Zanzibar Rangi tayari mmojawapo makubaliano Rangi Serikali Ya Zanzibar kuhusu Utafutaji mafuta Huko katika vitalu namba 9,10,11 Rangi 12. Shell inafanya Kazi Rangi kampuni Ya Petrobras Ya Brazil kwenye kitalu namba 6 Rangi namba 8 . Taarifa hizi zipo wazi kwenye tovuti Ya TPDC. Tuhuma nyepesi namna hii dhidi Ya kampuni Kubwa KAMA Shell zinaonyesha dharau Rangi kiburi kinachotokana Rangi uelewa mdogo wa Mambo wa watu wanaotuhumu.

Tuhuma 5:
Ongangi anapokea maelekezo kutoka Serikali Ya Kenya kuhujumu uwekezaji nchini mwetu.

Majibu:
Nazifahamu Mbinu nyingi zinazotumika kufanya propaganda, lakini Mbinu hii imeshindwa ikiwa mapema Sana. Ni vema wanaotoa tuhuma hizi wazithibitishe vinginevyo nai mwendelezo wa propaganda zisozingatia diplomasia Ndani YAKE dhidi Ya jirani zetu wa Kenya. Hizi nai propaganda Hatari ambazo Hata Hao wanaotuhumiwa wakisikia watatudharau Sana.

Tuhuma # 6 (Juu Ya Uingereza):
Uingereza imekuwa inamfadhili Zitto to miaka mingi to Mambo YAKE Ya kisiasa to hiyo Sasa hivi Ubalozi wa Uingereza unamlipa Zitto Rangi Kafulila kuhakikisha kwamba Standard Chartered Ya Uingereza inalipwa Deni ziwa lisilotambulika kisheria nchini mwetu.

Majibu:
Nimetangulia kusema hapo Awali kuwa KUNA propaganda ambazo haziangalii Hata diplomasia, Nyingine nai hii. Pamoja Rangi kukanusha uzushi Huu, nai Vizuri wanaotoa tuhuma za namna hii kuthibitisha. Mimi binafsi sijawahi kufadhiliwa kisiasa Rangi Taifa lolote Lile. Inaelekea KUNA wanasiasa wanaofadhiliwa Rangi mataifa mengine ambao kwakuwa kwao ndiyo Maisha wanaamini Rangi wengine tupo KAMA walivyo.
Kwangu itikadi Yangu nai 'Uzalendo to nchi Yangu', nai Jambo ambalo Halina mbadala wake. Siku zote nasema "Haki AU Makosa, nchi Yangu Ya Kwanza".
Kurudia kurusha tuhuma to Ubalozi wa Uingereza nchini nai kudhihirisha to Mara Nyingine kiburi cha kuwa Rangi mamlaka (kiburi cha nguvu) walicho nacho wanaotuma tuhuma hizi.
Aidha, wanatuhumu kuwa "Kafulila Rangi Zitto wamehaidiwa 15% Ya USD 150 milioni KAMA Deni likilipwa"
Mtanzania anayeweza propaganda dhaifu KAMA hizi Ya Ya ya basi anatakiwa ajitafakari. Hata hivyo nai vema wanaotoa tuhuma hizi wathibitishe Bila chembe Ya Mashaka.

Tuhuma # 7:
Mbunge Mkono Nae ameshikwa hasira kupoteza Kazi Ya uwakili rangi TANESCO. Kafulila Rangi Zitto wanalipwa Rangi Mkono kuvuruga Serikali to hasira za kukosa fedha za kitapeli za TANESCO.

Majibu:
Hizi nai tuhuma ambazo Sasa tumezizoea kutolewa. Mambo mepesi hayawezi kujibu Mambo Ya Msingi KAMA tuhuma za wizi wa fedha Zaidi Ya Shilingi bilioni 200 kutoka Benki kuu ya Tanzania. Kukusanya KILA propaganda ILI kuuhamisha umma nai kupungukiwa hekima Rangi Busara.
Aidha, wanaotuhumu wanadokeza kuwa "naomba tuwe macho Rangi Wabunge wetu achananeni Rangi Madai Ya Zitto Ya wizi. Huyu mwavuli anafanya biashara Rangi Kampuni Ya Shell Rangi inasemekana analipwa Rangi Ubalozi wa Uingereza. Serikali Ya Kenya Rangi tapeli mkubwa Mbunge Mkono Nae anawalipa Zitto Rangi Kafulila" .

Watanzania, Haya nai Maneno Ya hasira Ya watu wanaokaribia kukamatwa to kushiriki wizi wa fedha katika Benki kuu ya Tanzania. Kamwe tuhuma hizi haziwezi KAMA kutukatisha tamaa katika kupambana ILI Ukweli ujulikane. Sisi tutapigana to ajili Ya Taifa, to ajili Ya Mtanzania Rangi tunachotaka nai Umma uujue Ukweli wa Mambo.

Hasira hizi zinatokana Rangi Mambo mawili:
Moja nai uamuzi wa Kamati Ya PAC kuwasweka Ndani baadhi Ya watendaji wa TPDC to kushindwa kutekeleza maamuzi yanayohusu Ya Kamati Uwazi wa mikataba Ya Gesi Rangi Mafuta.

Pili, nai uamuzi wa PAC kuagiza ukaguzi maalumu wa mchakato Mzima ambazo ambazo ambazo wa kuanzishwa Rangi kufungwa to akaunti Ya Tegeta Escrow ambapo Zaidi Ya Shilingi bilioni 200 ziliporwa Rangi Zaidi Ya Shilingi bilioni 12 zinalipwa Rangi TANESCO KILA mwezi Kwenda kampuni Ya BA inayomilikiwa Rangi Harbinder Singh Sethi (50%) Rangi watu wasiojulikana kupitia kampuni Ya Simba Trust iliyosajiliwa Rangi kufichwa nchini Australia (50%).

Ieleweke kuwa BA inalipwa Shilingi milioni 400 Kila Siku kutoka TANESCO izalishe AU isizalishe Umeme! Watanzania, BA itaendelea kulipwa namna hiyo to miaka 20 ijayo. ILI namna ambayo Seth analindwa Rangi baadhi Ya watendaji Serikalini Rangi Hasa Ndani Ya Wizara Ya Nishati Rangi Madini. Aidha, KUNA fununu kuwa KUNA maofisa serikalini wanaomiliki hizo 50% kampuni za Ya BA. Seth Ya Ya ya pia anamiliki kitalu cha gesi Ya Mnazi Bay Kaskazini kupitia kampuni Ya HydroTanz.

Hasira hizi walizo nazo wanaonituhumu Rangi Kamati Yangu zimewapelekea kugushi nyaraka mbalimbali zinazonituhumu Mimi Rangi wenzangu ILI kutuogopesha Rangi kutukatisha tamaa katika kutafuta Ukweli Juu Ya suala la uporaji wa fedha kutoka Benki kuu. Kuamini katika Sisi wenyewe lao nai kututoa kwenye mstari. Mimi Rangi wenzangu hatutatoka kwenye mstari, tutashirikiana Rangi wabunge wenzetu kuhakikisha Ukweli unajulikana Rangi wezi kuchukuliwa hatua Kali.

Harbinder Singh Sethi aliiangusha Serikali Ya KANU nchini Kenya, Sasa anachotaka kukifanya kinaweza kuiangusha Serikali Ya CCM wakiendelea kumkumbatia.

Watanzania Sio mabwege!
Zitto Kabwe
Mwenyekiti PAC
Dodoma, 9 Novemba 2014 "

Wednesday, November 5, 2014

MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA 2014


Matokeo ya darasa la saba yametoka, kuyaona bofya link hapo chini chagua mkoa shule inapopatikana kisha wilaya baada ya hapo utachagua shule unayoitaka hapo utakuwa umepata matokeo

                                  KUONA MATOKEO DARASA LA SABA BOFYA HAPA

MATOKEO DARASA LA SABA 2014 KWA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA MANYONI, SAYUNI YAIBUKA KIDEDEA


Matokeo ya mtihani wa darasa la saba yametoka huku shule ya msingi Sayuni ikiendelea kupeta, katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani nchini inaonesha kuwa Shule hiyo ya Sayuni imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya kati ya shule 102,  kimkoa inashika nafasi ya pili kati ya shule 491 wakati kitaifa shule hiyo imeshika nafasi ya 456 kati ya shule 15867.

                  KUONA  MATOKEO DARASA LA 7 2014 SHULE ZA MANYONI BOFYA HAPA

Sunday, November 2, 2014

MAKONDA ATUMIA VIJANA KUVURUGA MDAHALO WA KATIBA, WENZAKE WAMFANYIA MBAYA KAMA ATARUDIA TENA BASI NI SIKIO LA KUFA


Katika tukio hilo PAUL MAKONDA chuchupu kuangukia katika mikono ya watu wenye hasira mara baada kukimbilia kujisalimisha kwa Jaji Warioba ili asidhurike na watu hao waliokuwa na hasira kama watu kama mbogo mbogo aliejeruhiwa.

Mara baada ya kutokea vurugu hizo, Prof. Kabudi alimfuata Makonda na kumuambia kuwa anachokifanya siyo atakuja kuumia, katika hali ya kujitetea Makonda alidai kuwa amekoja mwenyewe wala hakuja na kundi hilo la watu.

Vijana hao walionekana kuwa wamelewa kutokana na harufu walizokuwa wanazitoa midomoni mwao wakati wakipiga kelele wanadaiwa kuwa waliletwa na Makonda ambaye ilibidi akimbilie katika kibanda kimojawapo kilichomo ukumbini hapo ili kunusuru maisha yake, "kama siyo jitihada za Humphrey Polepole na Said Kubenea kuwatulia raia waliokuwa na hasira kali leo hii kwa Makonda tungekuwa tunasimulia habari nyingine, kwani alichofanyiwa Makonda na baadhi ya vijana hapo ukumbini kama atarudia tena kufanya tukio kama hilo basi jamaa ni sikio la kufa," Alisikika kijana mmoja ambaye anadai alimbana Makonda kisawasawa.

Kijana huyo mwenye siasa tata huku ndani ya CCM akipambana kumchafua Lowasa na nje ya CCM anapambana kumchafua Warioba aliokolewa na Jeshi la Polisi ambao kabla ya kumtoa ndani ya kibanda alichojificha iliwabidi wawasogeze watu mbali na eneo ili wasije wakamgeuza nyama Kijana huyo aliyekuwa ameongazana Amon ambaye naye alikuwa Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka katika Kundi la watu wenye ulemavu.

Watu kama wawili watatu hivi  walijeruhiwa katika tukio hilo, huku mmoja wa vijana waliokuja na Makonda ukumbini akiponea chupuchupu baada ya kuokolewa na jesshi la Polisi nje ya ukumbi.



GODBLESS LEMA (Kupitia ukurasa wake ameandika hivi kuhusiana na vurugu hizo)

Tokea nizaliwe sijawai kukasirishwahivi kama nilivyokasirika leo na jambo la huyu muhuni Makonda kumpiga na chupa mzee warioba ni kukosa heshima kukosa akili na ustaarabu ni upumbavu .ushenzi na uhuni wa hali ya juu

kitendo cha ccm kuwatuma wahuni wa chuo cha diplomasia kumshambulia mzee warioba ni dalili tosha ya kushindwa kwa utawala kama judge ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu na vilevile ni kada mkubwa ndani ya ccm anatendewa uhuni huu wewe mtanzania wa kawaida watakufanya nini??? mti mbichi unatendwa hivi mti mkavu je...
.ni wakati sasa wa watanzania kujiuliza hii katiba PENDEKEZWA inayo siri gani ambayo ccm hawataki wananchi tuijue???? kwanini wanatumia nguvu nyingi kutunyamazisha??? kwanini hawataki tuijadili????? kwanini hawataki wananchi waelimishwe???hii ni karne ya 21 ni karne ya kubishana kwa hoja sio karne ya matusi na vurugu mjibuni warioba na tume yake kwa hoja simlisema mnauhakika na katiba "pendekezwa"imezingatia matakwa ya wananchi sasa wanaogopa nini???mbona nyie mkifanya makongamano yenu hakuna mtu anayewaingilia???

tuacheni tupate elimu juu ya katiba tunayoitakaninatoa rai kwa kila mzalendo wa taifa hili kukilaani kitendo cha muhuni makonda kumpiga mzee warioba na laana ya mungu ishuke juu yakeShame on you makonda‪#‎ALAANIWE_MAKONDA




PETER MSIGWA (Katika ukurasa wake wa facebook naye ameandika hivi)
"Nilikuwa ndani ya ubungo plaza ,niliwaona vijana wengi waliobeba mabango hawakufika hata hamsini . Wengi wao ni chini ya miaka 18,' walikuwa na Amon Yule mlemavu wa macho na Paul makonda. Nilichokiona ni ni upuuzi ujinga,mkubwa , vijana wale hata hawajui wanachokifanya,
Akili ndogo ndio imetamalaki ....shame on you CCM".


Hapo Makonda mwenye shati jeupe katikati aking'ang'ania mkono wa Mzee Warioba ili kujinusuru na kipigo cha wananchi maana kabla ya hapo alikichezea haswaaaa
 
                                         Mzee Warioba akitolewa ukumbini na wanausalama 



Baadhi ya vijana wanaodaiwa kutumika na CCM wakiwa na mabango yao huku wakizomea

ZITTO KABWE (Kupitia ukurasa wake wa facebook amaendika hivi.
"Nalaani vikali kabisa vurugu zilizotokea katika mdahalo wa Katiba. Tabia mbaya kabisa kuendekeza vurugu badala ya hoja. Mambo ya kihayawani. Shindana kwa hoja"

Usalama wa Mzee Warioba ukulindwa

Baadhi ya wahudhuriaji wakiwazua wenzao kutojibu mapigo jambo ambalo baadaye lilishindikana baada ya kuona wenzao wa upende wa pili hawataki kutulia ilibidi wawatoe mkuku ukumbini

Friday, October 31, 2014

NI SHIIIIIIIIIIIIIIDA!!! MASOGANGE AZIDI KUJIANIKA MITANDAONI


Katika ukurasa wake wa facebook, Masogange ametupia picha hii hapa huku ikiambana na ujumbe wa , sijui lengo lake lilikuwa nini?

Photo: ITS FURAHIDAY

Kutazama picha zaidi za Masogange bofya HAPA

Friday, October 24, 2014

MAELFU WAMZIKA FR. MAKWANDA, ATHIBITISHA KUWA ALIKUWA KIPENZI CHA WATU, MKUU WA MKOA SINGIDA AMPA TANO.


Na.Venance Furaha-Manyoni

Wakazi wa Manyoni na vitongoji vyake na wageni mbalimbali kutoka Mkoa wa Singida na mikoa mingine nchini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Ndugu Parseko Kone, wamejitkeza kwa wingi leo kumzika Fr. Makwanda aliyefariki kwa ajali ya gari wakati akitokea Itigi kwenda Manyoni. ajali hiyo iliyotoa uhai wa Fr. Makwanda ilitokea eneo la Mabondeni usiku wa jumatatu, tarehe 20/10/2014. ajali hiyo huenda ilitokea kati ya Saa nne au tano usiku hivi. Mji mzima wa Manyoni ni kama ulikumbwa na simanzi baada ya taarifa za kifo cha Padri huyo kuanza kusambaa. Baadhi ya wakazi wa Manyoni wakiongea na BabaD Blog.wakimuelezea Padri huyo, walisema kuwa   alikuwa mtu mcheshi, mkarimu, na aliyependa kujichanganya na kila mtu bila kujali dini ya mtu.
"Kusema kweli ndugu yangu huu msiba ni pigo kubwa sana si kwa Wakatoliki pekee bali kila mtu aliyekuwa akimfahamu huyu jamaa atakuwa ameguswa na tukio hili" Alisema Mzee Juma aliyejitambulisha kuwa anatokea maeneo ya Majengo. 

Mkazi mwingine wa Manyoni ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake, alidai kuwa Padri Makwanda ni kama alijitabiria kifo, "Ujue padri wetu ni kama alikuwa anajua kuwa hivi karibuni hatakuwa nasi, ni juzi juzi tu alikuwa anatuonesha  eneo ambalo kama akitangulia kufa mwili wake utapumzishwa na hapo na ndipo alipopumzishwa siku ya leo (Jana) kweli huyu  padri alikuwa kipenzi cha watu ona umati wote huu!"

Akimzungumzia marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Parseko Kone, alisema kuwa Fr. Makwanda alikuwa mtu wa watu, mara nyingi nikiwa hapa manyoni Fr. Padri Makwanda alinipa sehemu ya kulala, alinihudumia chakula hakika nilikuwa nahudumiwa kama mtoto...katika hali ya kibanadamu Fr. Makwanda alikuwa kama kijana wangu, lakini kiroho alikuwa ni baba yangu." Alisema Mkuu wa Mkoa.

Wageni wengine waliohudhuria ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi. Fatuma Tawafiq, vingozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu na dini mbalimbali, wawakilishi mbalimbali kutoka Parokia na majimbo mbalimbali.

Mwili wa marehemu kabla ya kupumzishwa katika nyumba yake ya milele, misa ya kumuombea marehemu  ilifanyika katika kanisa la RC Manyoni, Parokia ya Kupaa Bwana na baada ya shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu yalifuatiwa na maandamano kuelekea makazi ya Mapadri ambako ndiko Mwili wa Fr. Makwanda ulipolazwa.

Mpaka mauti inamkuta Padri Makwanda alikuwa ni Msaidizi wa Paroko parokia ya Kupaa Bwana Manyoni.

BWANA AMETOA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Fr. Makwanda enzi za uhai wake


Fr. Makwanda enzi za uhai wake

Jinsi ilivyokuwa maeneo ya makaburini
















Hii ndiyo gari aliyopata nayo ajali

Baba D. blog inaungana na Wanamanyoni wote kuipa pole familia ya Fr. Makwanda, Paroko wa Parokia ya Kupaa Bwana na waumini wote wa parokia hiyo. R.I.P Fr. Makwanda.

Picha kwa hisani ya Sylvery Hussein, Edga Madeje na wadau wengine.

Tuesday, October 21, 2014

LUNDENGA AMKIMNGIA KIFUA MISS TZ 2014 ADAI UMRI WAKE NI SAHIHI, CHETI CHA KUZALIWA CHA MISS HUYO CHAZUA UTATA




Kamati ya Miss Tanzania yakata mzizi wa fitna Kwa Sitti Mtemvu? Cheti cha kuzaliwa kilichooneshwa chazua utata

Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga hii leo amezungumza na waandishi wa habari  juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu. Kujua zaidi alichosema Lundenga BOFYA HAPA

Sunday, October 19, 2014

NAMNA YA KUMPIGIA KURA DIAMOND KATIKA TUZO ZA MTV INGIA HAPA

Kumpigia kura DIAMOND ni rahisi saana Bonyeza HAPA  itakupeleka moja kwa moja hadi kwenye picha hii

halafu utabonyeza ilo Neno VOTE chini ya jina la Diamond 

FID Q AJITOKEZA KUMTETEA MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU KUHUSU KUDANGANYA UMRI



Fid Q 1
Fid Q 2
KUHUSIANA NA HABARI ZA MISS HUYO SOMA ZAIDI HAPA

BOFYA HAPA PIA KWA USHAHIDI WA UMRI WA MISS HUYO

HUU NDO USHAHIDI MWINGINE UNAONESHA KUWA MISS TZ 2014 SITTI MTEMVU ALIDANGANYA KUHUSU UMRI

               JUU, LESENI YA UDEREVA INAONESHA KUWA ALIZALIWA TAR. 31/5/1989


HII NI PASSPORT YAKE YA KUSAFIRIA NAYO INAONESHA ALIZALIWA TAR.31/5/1989

Kumbuka kwamba miss huyo alidai kuwa anamiaka 18 na elimu yake ni kiwango cha shahada ya pili yaani Masters SOMA HAPA ZAIDI

Wednesday, October 15, 2014

HUYU NDIYE MISS TZ MWENYE AKILI KULIKO WOTE, AVUNJA RECORD, ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MWAKA 1

MISS TANZANIA 2014 Sitti binti Mtemvu ambaye ni mtoto wa mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu wakati akijinadi alisema kuwa ana miaka 18 na elimu yake ana shahada ya Uzamili (Masters) mfumo wa elimu yetu jinsi ulivyo haiwezekani kijana wa miaka 18 akawa na elimu ya kiwango hicho,
Name:  wpid-mmgm0157.jpg
Views: 133
Size:  89.0 KB

HEBU TUPIGE HESABU;
Masters(Shahada ya uzamili)  miaka  2
Shahada ya kwanza                 miaka  3
Sekondari                                 miaka  6
Shule ya Msingi                       miaka 7
Chekechea  (kama alisoma)     mwaka 1
                                                               
IJUMLISHE HIYO MIAKA, YAANI: 2 + 3 + 6 + 7 + 1 = 19

Maana yake ni kuwa, mrembo huyo alianza shule akiwa na mwaka 0 kama alianzia chekechea, lakini kama alirukia moja kwa moja darasa la kwanza itakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na mwaka mmoja.

Hapa inawezekana, mrembo huyo alidanganya miaka yake ya kuzaliwa au alidanganya kiwango chake cha elimu. lakini kama alichosema kitakuwa na ukweli basi maajabu haya yatakuwa yanapatikana Tanzania tu.

Ila ukitaka kujua kuwa aliudanganya umma BOFYA HAPA UTAJUA MIAKA YAKE HALISI


Julius S. Mtatiro's photo.
Julius S. Mtatiro's photo.

MAELFU YA MAGARI YA TOYOTA YANA HITILAFU, YATAKIWA KURUDISHWA

Kampuni kubwa zaidi ya kuunda magari, Toyota, imeagiza kurejeshwa kwa magari milioni moja nukta saba kote duniani kutokana na hitilafu ya breki za magari hayo.
Kampuni hiyo imesema hitilafu tatu zimetambulika kwenye breki katika miundo mbali mbali za magari ya Toyota ikiwemo muundo wa Lexus.
Magari yaliyo ndani na nje ya Japan yote yameathiriwa na hitilafu hizo.
Hata hivyo kampuni yenyewe imesema haina habari yoyote kuhusu ajali za magari au watu kujeruhiwa kutokana na hitilafu hizo.
Wadadisi wanasema hili ni jambo la kuabisha sana kwa Toyota ambayo imelazimika kuagiza magari yake kurejeshwa kiwandani zaidi ya mara moja kutokana na hitilafu mbali mbali. 
CHANZO: BBC