TZ na Afghanistan haziwatunzi wazee vyema
Sweden ndio nchi nzuri zaidi duniani kuishi maisha ya uzeeni
wakati Afghanistan ndio kubaya zaidi kwa wazee kwa mujibu wa utafiti uliofanywa
na Umoja wa Mataifa.
Utafiti huo unaotizama hali ya watu wazee na mazingira wanamoishi, ulifanywa
katika mataifa 91. Norway na Ujerumani, zilikuwa katika nafasi za juu huku
Ingereza ikiwa katika nafasi ya 13.
Utafiti huo unaonya kuwa nchi nyingi duniani, hazina mifumo mizuri ya kutunza
wazee.
Ifikapo mwaka 2050, wazee watakuwa wengi kuliko vijana walio chini ya miaka
15, wengi wakiwa ktika nchi zinazostawi.
Utafiti huo ulikusanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukadiria idadi ya
watu, UNPF na shirika la kimataifa la kutetea maslahi ya wazee HelpAge.
Nchi zenye mifumo mizuri ya kuwatunza wazee
- Sweden, Norway na Ujerumani zilikuwa juu kwenye orodha.
- Uingereza ilikuwa ya 13 nyuma ya Ireland
- Nchi zengine ambazo ziko katika fasi za kwanza kumi ni Uholanzi, Canada, Switzerland, New Zealand, Marekani, Iceland na Japan
- Afghanistan, Tanzania na Pakistan ni za mwisho kwenye orodha hiyo.
Watafiti wanasema walitumia vigezo 13 ikiwemo mapato, ajira, huduma za afya,
Elimu, na mazingira....katika kile wanachosema ni utafiti wa kwanza wa aina yake
duniani.
Aidha , watafiti wanasema kuwa nchi nyingi kote duniani zinakabiliwa na
changamoto kubwa kutokana na idadi kubwa na inayoendelea kukuwa ya wazee
72katika mataifa hayo.
"kutokana na ongezeko la mahitaji ya nchi mbali mbali duniani, nchi hizi nazo
zinaendelea kukabiliwa na matatizo ya kukidhi mahitaji ya wazee,'' alisema
Silvia Stefanoni, kaimu afisaa mkuu mtendaji wa shirika la HelpAge
International.
Sweden ilikuwa ya kwanza katika nchi bora zaidi kwa kukidhi mahijati ya
wazee, Afghanistan ilikuwa ya mwisho. Mataifa ya ulaya ndio yalifanya vyema
katika kuwatunza wazee.
Sio kwa kuwa nchi hizo ni tajiri ndiposa zinawatunza wazee vyema kwa sababu
hata nchi ambazo uchumi wao sio mzuri, bado huwatunza vyema wazee, ikiwemo Sri
Lanka, Bolivia na Mauritius.
Urusi ilikuwa nambari, (78), India (73) na Uturuki (70) wakati Brazil
ilishikilia nambari (31) huku China ikiwa nambari (35)
Via: bbc swahili
No comments:
Post a Comment