Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, April 29, 2013

MAJIBU YA UV-CCM ARUSHA MJINI KWA HUSSEIN BASHE

Uvccm Wilaya Arusha Mjini

KWA NDUGU YETU HUSSEN BASHE NA WAPOTOSHAJI WENGINE HASWA WA CHADEMA KUHUSU KUKAMATWA KWA LEMA MBUNGE WA ARUSHA MJINI

 
Tangu yalipo tokea mauaji ya kijana mwana chuo wa uhasibu kitendo kilicho pelekea LEMA kukamatwa kwa uchochezi yamesemwa mengi sana kuhusu hili suala na lawama kupewa MH MKUU WETU WA MKOA WA ARUSHA MAGESA MULONGO hatuna malengo ya kumtetea ... mkuu wetu wa mkoa bali kuweka ukweli wazi hapa na kuondoa upotoshaji ambao unafanywa kwa makusudi na baadhi ya wanzetu.
 
 
Suala la kukamatwa kwa Lema mbunge wa Arusha ni kama wanavyo kamatwa wahalifu wengine Lema alifika uhasibu badala ya kupitia kwa viongozi yeye akaenda moja kwa moja kwa wanachuo na kuanza kuwahutubia kitendo ambacho ni utomvu mkubwa wa nidhamu mbunge alipaswa aende ofisini na kuonana na uongozi wa chuo ili apewe taarifa na uongozi wa chuo wampeleke kuongea na wanachuo lakini Lema hakufanya hivyo badala yake alikwenda bila utaratibu na adabu.
 
 
Baada ya Lema kufika na kumaliza kuongea aliyo yaona kuwa ametosheka RC MULONGO alifika na kwasababu uhasibu wanafunzi ni wengi na sauti tunatofautiana aliomba vi pasa sauti ili aweze kuongea na kusikika vizuri hapo kuna dhambi gani mtu kuomba vipasa sauti na vilikuwepo na akapewa ili aongee lakini kwa vile tayari Lema alishaa mwaga sumu tayari walebaadhi ya wanachuo walifanya kama LEMA alivyokuwa amewaelekeza kuwa wafanye fujo.
 
 
Ndugu HUSSEN BASHE kuhusisha kukamatwa kwa LEMA na suala la uchaguzi wa kata nne za ARUSHA mjini hizi ni propaganda ambazo chadema wanazieneza nashangaa na wewe kuwasaidia chadema kufanya propaganda chafu MKUU WA MKOA YEYE NDIYE KIONGOZI WA ULINZI NA USALAMA WA MKOA WETU amekosea wapi kumkamata mwalifu au kukiwepo uchaguzi basi serikali isiwadhibiti wahalifu Bashe post yako uliyo post jana umesukumwa na chuki na wala siyo mapenzi mema NDUGU HUSENI BASHE nawanachadema ambao mmekuwa mkimlaumu mh mkuu wetu wa mkoa kuwa ametumia ubabe sisi kama CHAMA TAWALA TUNARIDHISHWA SANA NA UCHAPAKAZI WA MKUU WETU WA MKOA MAGESA MULONGO kuhusu suala la wauaji kutafutwa lazima watafutwe lakini pia wachochezi na wenyewe ni lazima watafutwe pia maana wote ni tatizo.
 
 
USHINDI WA KATA ZETU NNE UPO NJE NJE BASHE ARUSHA UNAYO ISEMA WEWE KUWA CCM INASHINDWA UMEISOMA MTANDAONI ILA KWA SISI TUNAOISHI ARUSHA WANANCHI WANASEMA WAMETUELEWA nahawako tayari kurudia makosa tena kwa yaliyo tokea wamejifunza Arusha ni mji wakitalii hauhitaji wahuni mwanzo tuliwambia wananchi hawakutuelewa ila kwasasa baada ya kuionja sumu ya CHADEMA wameelewa MKUU WETU WA MKOA VIJANA WA ARUSHA TUKO NA WEWE KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKO KW AMUJIBU WA SHERIA BILA KUMWONEA YEYOTE KAMA UNAVYO FANYA ONGERA MAGESA S.MULONGO KWA KUTEKELEZA VYEMA ILANI YETU YA UCHAGUZI
 
 
Afisa habari wa UVCCM wilaya ya Arusha mjini ndugu
SAIDI A. SAIDI

HII NDIYO HATI YA MASHTAKA ALIYOSHITAKIWA NAYO LEMA BAADA YA MENGINE KUFUTWA

 
Kumbuka baadhi ya Mashtaka kabla ya Lema kifikishwa mahakami leo asubuhi, yalikuwa:
 
1. “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni woga” na hivyo kuwataka wanachuo wasiwe waoga.
 
 2. Wakati anaongea na wanachuo kuhusu ujio wa mkuu wa mkoa mhe mulongo ambaye alionekana kuchelewa, inadaiwa mhe Lema aliwaambia wanachuo, “NImepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 mkuu wa mkuu atafika, asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya msingi ya kupatiwa ulinzi.
 
3. Baada ya mkuu wa mkoa kufika aligoma kuongea na wanachuo bila kuwa na kipaza sauti akataka PA system ifungwe ndio aweze kuongea, alipose,a maneno hayo wanafunzi wakaanza kuguna kuwa anaringa, mkuu wa mkoa akasema, kwa hali hii hataweza kuongea na wanafunzi wasio na adabu. Baada ya hapo mhe Lema akasema mbele ya wanachuo, “Hawa ndio viongozi wetu tunaowategemea wanakuja wanajivuta utafikiri wanakwenda kwenye send-off”?.


Hati hiyo ya mashtaka hapo juu, kwa msaada wa Jamii Forums, tembelea hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/442480-hati-ya-mashitaka-ya-mhe-lema-baada-ya-mengine-kutupiliwa.html kusoma maoni ya watu mbalimbali kuhusiana na hati hiyo Jamii Forums

LEMA AACHIWA KWA DHAMANA

Tazama picha baada ya lema kufikishwa mahakamani

Lema akiwa kizimbani

Dogo janja Joshua Nasari alikuwepo




Mabango pia hayakuwa nyuma kwa wafuasi na mashabiki wake

MBOWE AMTWISHA MZIGO ZITTO KABWE

 
Tabora. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuhakikisha chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mbowe alisema chama chake kitahakikisha kinachukua majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki), Ismail Aden Rage (Tabora mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma Kapuya, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alimwagiza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo hayo yanachukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Alimtaka kufanya kampeni za mtaa kwa mtaa, nyumba kwa hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Town School mjini Tabora, pamoja na mambo mengine alisema anazindua kampeni hiyo kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi ambapo Zito Kbwe alikabidhiwa jukumu la kuisimamia kanda hiyo.
Aliwageukia polisi na kuwataka kukiunga mkono chama hicho ili kikifanikiwa kuingia madarakani kiweze kuwaboreshea mishahara yao kuliko ilivyo sasa akidai wanalipwa mishahara kiduchu ikilinganishwa na ugumu wa kazi yao.
“Nyie makamanda nanyi mmepigika kama sisi, sasa ninachowaomba tuungeni mkono kupambana na hawa CCM ili tuwakomboe wanyonge,” alisema Mbowe.

 
 
Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alisema Kanda ya Magharibi ina historia katika nchi kwa Mkoa wa Tabora kuwa kitovu cha mapambano ya uhuru wa nchi na Kigoma kuwa kitovu cha mapambano ya mageuzi.
 
Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Sunday, April 28, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAR. 29-04-2013

.

.

.

.

.



.
.
 
.
 
 
.
 
HABARI ZA MICHEZO
 
.
 
.
 
.
 
.
 
.
 
.
 
 
.
 
 
.
 
.

ALIYEZIKWA AKIWA HAI HUKO CHUNYA MBEYA AFUKULIWA NA KUKUTWA AMEKUFA

 

        SOMA HABARI YA TUKIO ZIMA NA TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO BAADA YA HABARI HII

 

Vijana wakifua kaburi

 KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.

 

Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.

Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.

 

Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu.

 

Baada ya Mzee huyo kupoteza fahamu Vijana hao walianza kutandika fito ndani ya kaburi kisha kufukia kwa udongo kiasi kwa lengo la kutenganisha na Mwili wa Marehemu Pita uliokuwa kwenye jeneza baada ya kuwazika kwenye kaburi moja.

 

Baada ya kukamilika kwa zoezi la mazishi kundi la vijana lilielekea hadi nyumbani kwa Mzee aliyezikwa akiwa hai na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kutotoa siri wakidai Siri ya Jeshi.

Hata hivyo baadhi ya wananchi walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Credo Kayanza ambaye pia alitoa taarifa kwa Diwani wa Kata hiyo Chesco Ngairo ambao kwa pamoja walitoa taarifa Jeshi la Polisi ambao baada ya taarifa hiyo walifika eneo la tukio huku wakidhani lililotokea ni kuchomwa kwa nyumba pekee.

Jeshi la Polisi baada ya kufanya upelelezi na kubaini kitendo hicho waliwaamuru baadhi ya Vijana kufukua kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya Vijana hao kulipwa.

Baada ya kufukuliwa kwa kaburi hilo Mwili wa Marehemu Mzee Mwachirui ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya Uchunguzi huku Mwili wa Pita ukizikwa upya palepale.

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo Marehemu alizikwa katika eneo tofauti na alipokuwa amefukiwa awali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo pia ametoa wito na kuwaasa wananchi na jamii kuacha tabia ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi kwa madai kuwa hauna faida kwao bali huchochea migogoro katika jamii zao.

 

Aidha ameongeza kuwa wakumbuke kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria ambapo pia amewaomba wenye taarifa za walipo waliohusika na mauaji hayo kuzifikisha polisi haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao ingawa hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

TAZAMA TUKIO HILO KATIKA PICHA

 
 
VIJANA WAKICHIMBUA KABURI ALIMOZIKWA ALIYEKUWA HAI
 
 
 
JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA TAYARI LIMETOLEWA HILO PEMBENI SASA ANAFUKULIWAALIEZIKWA HAI
 
MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI SASA UNATOLEWA KABURINI
 
 
PICHA YA JUU NA CHINI, MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUTOLEWA KABURINI
 
MWILI WA ALIEKUFA KWA UGONJWA ULIZIKWA TENA NA WANAUSALAMA KUONDOKA NA MWILI ALIEZIKWA AKIWA HAI
 

BASHE AMPINGA MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUHUSU SUALA LA LEMA NA KITENDO CHA MADIWANI WA NZEGA KUJITENGEA MIL. 82 KWA AJILI YA SAFARI TU

 
Kufuatia kitendo cha madiwani wa Nzega mkoani Tabora kujitengea tsh 82 mil. kwa ajili ya safari tu ya kutembelea Arusha na Dodoma, na lile tukio la Mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Husein Bashe aamua kufunguka na haya ndo maelezo yake aliyoyaandika katika ukurasa wake wa facebook.
 
 
Ndg zangu,Awali ya yote niwatakie Juma Pili Njema na Kwa Ndg zetu wanoenda kanisani siku ya Leo waendelee kuombea Taifa letu na Viongozi wetu kufanya maamuzi ya Busara juu ya Hatima ya Maisha ya Watanzania na Taifa kwa Ujumla.


Nimeanza na maneno hiyo hapa juu kufatia matukio miwili,Moja ni Tukio la Arusha na Pili ni Tukio la Maamuzi ya Baraza la Madiwani la wilaya ya nzega.
 

 Nzega
Halmashauri ya wilaya nzega imepitisha Bajeti na mipango ya Mendeleo ya mwaka wa fedha 2013/4 kilichonisikitisha ni Madiwani kujitengea milioni 82 kwa ajili ya ziara Kwenda mkoa ya Arusha ,Dodoma Kama ziara ya kujifunza,Wakati wilaya inakabiliwa na Changamoto za uharibifu aw miundo mbinu kufatia muda Nyingi,makazi ya wananchi wengine yameharibika,shule za msingi na secondaries hazina Madawati,waalimu hawana nyumba ,vituo vya Afya having dawa za kutosha,tunakabiliwa na tatiizo la Maji Mijini na vijijini.


Wakati Hali ikiwa hivi fedha hizo ni Intrest(RIBA) iliyotokana na fedha zilizowekwa benki Baada ya mgodi kutulipa 2bn,Wabunge wakiwa wajumbe wa kamati ya fedha wamepitisha hili,mbali hapo wameunda tume ya Watu 15 Kwenda Dar kukutana na Katibu mkuu aw Nishati kufatilia madai Kila mjumbe atapewa posho ya siku 80,000 kwa siku 10 mbali na posho za madereva kwani wataondoka na gari za halmashauri,mbali na mafuta,kuna tume ya kufatilia mji mdogo nayo inawajumbe 10 imetengewa mamilioni ya pesa.


Mbali na Hilo wakubwa wameamua kumchukua fedha 2bn kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Nzega ikiwa na dhamira ya kutoa mikopo kwa Wananchi aw Nzega,wanafanya maamuzi haya huku wakifahamu Halmshauri ya wilaya ya Nzega Ina Fedha za Mfuko aw Maendeleo ya Vijana ,Mfuko aw Maendeleo ya Kina Mama ,Mabilioni ya Jk vyote hivi vimeshindwa kusimamiwa na Fedha zake kwa Miaka yote hazijawahi kuwa na Mrejesho chanya Leo tena wanatenga fedha ili kuanzisha Benki itakayoendeshwa na Watu wale wale,kwa Mfumo ule ule,kuwakopesha Watu wale wale ambao Mara zote wanaposhindwa kurejesha hutumika sasa zile zile kuwasamehe.
 

 Huu ni mchezo kwenye maisha ya wananchi aw wilaya ya nzega ambao hawana High school ,hawana barabara za uhakika,waalimu hawana makazi,wanafunzi hawana maabara,hawana Madawati,zahanati hazina Madawa,mikopo ya Mabilioni ya Jk haikufanikiwa,mikopo ya Mfuko aw Maendeleo wa Vijana haikufanikiwa,mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Kina mama haikufanikiwa Leo zinatengwa fedha za kuanzisha Benki ya kukopesha wana nzega,kuna Mabenki mawili nzega,kuna taasisi za mikopo zaidi 5 kwa matatizo yanayokabili wilaya lie huu ni Kupoteza fedha za wananchi wa nzg kwa posho na kuandaa maradi ambayo haina Tija.


TUKIO LA ARUSHA.
Tukio la kuuwawa Kijana aw Chou cha uhasibu na matokeo Yake badala ya kutafuta wauwaji kunatengenezwa mazingira ya kuleta Instabillity kwa kumkamata LEMA, Kaka yangu Mulongo katika hili alivolisimamia na kulitekeleza ameonyesha Udhaifu aw Hali ya Juu na matokeo Yake inavunjia heshima Serekali ya Chama chetu na Kuongeza chuki dhidi ya CCM Hakukua na sababu ya Kubahave the way he did pale chuoni,alionyesha kiburi hakua humble,hakutumia Busara katika jambo hili.

 Wakati kuna Kijana ameuwawa,na yeye ndie Rais wa eneo lile attitude alionyesha Hakukua na leadership pale,tunakabiliwa na uchaguzi kuna mtu ameuwawa na si Tukio la kwanza,Nguvu iliyotumika kumkamata lema Leo CCM mkoa aw Arusha wanakabiliana na maswali mengi kuliko Majibu,inasikitisha viongozi wanaotuwakilisha kuongoza ndio hao tunawaona Bungeni,ndio hao Kina Mulongo na maamuzi na attitude ya kaka Mulongo,ndio hao Kama Baraza la Madiwani aw Nzega ambao kwao semina safari,posho,maradi isiyotekelezeka,kuunda tume ya kuchunguza madai ya wafanyakazi ni kuitengea fungu Wakati kk Bajeti wameisha tenga fedha za kulipa madeni halafu unaunda tume ya kuchunguza madeni ambayo umeisha lipa.


Ndg zangu wana CCM chuki za Watanzania dhidi ya chama chetu zinaongezeka Kila siku na hii ni kutokana na Tabia zetu wenyewe Wakati hospitalini hakuna Vifaa vya Kina mama kujifungulia sisi tunajitengea fedha za ziara 82m,posho za 80,000 kwa siku,tunaanzisha miradi ambayo haitawasaidia wananchi kk kero zao za Kila siku,Wakati mwanafunzi ameuwawa na kibaka tunatumia mabomu,Rundo la Askari kumkamata mtu Moja kwakua si mwana CCM,wananchi nyumba zimebomolewa na mvua,hakuna Bajeti ya kuwasaidia hawa Watu,hakuna Madawati,dawa hospitali,tunaelekeza fedha ktk mambo yasiyogusa maisha Yao.

 Unless tubadilike na kuanza kutambua Watanzania hawajatupa madaraka ilituchezee maisha Yao,unless tutambue uongozi ni dhamana tutendelea kuchukiwa na Leo sitashangaa Arusha tukipoteza kata 4 zilizowazi,tunawalazimisha Watanzania kutafuta matumaini kwa wapinzani kwa sisi wenyewe kuamua kujipa Utawala badala ya Uongozi.Binafsi swala la nzega nimekiandikia Barua chama changu wilayan kukiomba kutazama upya maamuzi ya Full Council na kutambua upya vipaumbele halmashauri ya nzg inakabiliwa na Changamoto Nyingi hawatakiwi kuchezea fedha za walipa kodi.Hili la Arusha CCM inatakiwa kutolishabikia RC amemishandle the whole thing.

TAARIFA YA CHADEMA - KASKAZINI KWA UMMA KUKAMATWA KWA LEMA

 

CHADEMA

TAARIFA KWA UMMA
KUKAMATWA KWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI MHE GODBLESS LEMA NA MASHTAKA YA UCHOCHEZI WA VURUGU ZILIZOTOKEA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.

 
Ndugu wanahabari na wakazi wote wa mkoa wa Arusha.

Juzi usiku wa kuamkia tarehe 26 Aprili 2013, jeshi la polisi walifika nyumbani kwa Mhe Lema kwa lengo la kumkamata. Awali kufika kwao muda huo wa usiku wa manane kulileta mashaka kwenye familia ya mbunge mpaka ilipojiridhihirisha kuwa waliofika ni polisi kweli na sio wavamizi au majambazi. Katika kufika kwao polisi walikuwa wameweka tishio la kutaka kutumia nguvu usiku huo wa manane kwa kupiga mabomu na kuvunja nyumba iwapo mhe Lema asingefungua mlango na kujisalimisha kwa polisi. Walileta mbwa zaidi ya 15 na vikosi vya askari ambao waliizunguka nyumba wakiwa na mabomu na silaha nzito. Hata hivyo umati mkubwa sana wa watu yaani wapiga kura ulijitokeza, jambo ambalo liliashiria kuwa hatua zozote za nguvu ya polisi ingeweza kuzaa balaa ambalo lisingeweza kubebeka. Nguvu kubwa hii ya polisi yenye sura ya kuonyesha ubabe na uonevu imetufedhehesha sana na inatupa wasiwasi kuwa itakuja kusababisha hali ambayo sio nzuri siku si nyingi.
 

Mimi mwenyewe nilifika eneo la tukio muda huo, nilifanya mazungumzo ya kirefu sana na RPC kamanda Sabas pamoja na RCO kamanda Wambura. NIlizungumza pia na Mhe Lema na mawakili wetu juu ya jambo hili ndipo mida ya saa tisa usiku mhe Lema alifungua mlango na moja kwa moja tulielekea kituo cha polisi. Kwa mazingira ya muda wenyewe OCD aliagiza maelezo ya Mhe Lema yachukuliwe asubuhi ya siku ya terehe 26 Aprili.
 

Kuanzia saa nane mchana siku ya jana, ndipo jeshi la polisi walipoanza kumhoji Mhe Lema na chama tulimwomba wakili Humphrey kuwepo kwa ajili ya kumsaidia mhe Lema katika mahojiano hayo.
 

Mpaka sasa mhe Lema yupo mahabusu baada ya kunyimwa dhamana. Shitaka la msingi ambalo amefunguliwa ni la uchochezi (Shitaka namba 390) katika chuo cha uhasibu na kupelekea mkuu wa mkoa wa Arusha kuzomewa na wanachuo na hatimaye polisi kuanza kupiga mabomu hali iliyopelekea kufika hapo ilipofika.
 

Sasa vigezo vya shauri hili la uchochezi kwa mujibu wa mashtaka rasmi yaliyopo polisi limesababishwa na maneno yafuatayo ambayo inadaiwa mhe Lema aliyasema siku ya tukio hapo chuo cha uhasibu;
 
  1. “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni woga” na hivyo kuwataka wanachuo wasiwe waoga.

  2. Wakati anaongea na wanachuo kuhusu ujio wa mkuu wa mkoa mhe mulongo ambaye alionekana kuchelewa, inadaiwa mhe Lema aliwaambia wanachuo, “NImepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 mkuu wa mkuu atafika, asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya msingi ya kupatiwa ulinzi.

  3. Baada ya mkuu wa mkoa kufika aligoma kuongea na wanachuo bila kuwa na kipaza sauti akataka PA system ifungwe ndio aweze kuongea, alipose,a maneno hayo wanafunzi wakaanza kuguna kuwa anaringa, mkuu wa mkoa akasema, kwa hali hii hataweza kuongea na wanafunzi wasio na adabu. Baada ya hapo mhe Lema akasema mbele ya wanachuo, “Hawa ndio viongozi wetu tunaowategemea wanakuja wanajivuta utafikiri wanakwenda kwenye send-off”?.

  4.  


Katika kuchukuliwa maelezo yake mhe Lema amesisitiza kauli yake hiyo na kuwa hata mazingira ya namna ilivyotumika ni kauli njema kabisa.


Propaganda na upotoshwaji unaonezwa na mkuu wa mkoa kuwa mhe Lema alikimbia na kujificha na kwamba kwa nini alilitelekeza gari lake hapo chuoni na kwa nini hakuja polisi kulichukua gari lake ni kauli ya kufilisika sana kifikra na la kukosa mambo ya msingi ya kuongea. Baada ya vurugu hizi kutokea hata yeye mkuu wa mkoa alikimbia na kuondoka na gari yake, Mhe Lema alishindwa kulifikia gari lake kutokana na mabomu hayo, Mhe Lema alijikuta mwenyewe baada ya msaidizi wake kuzidiwa na moshi wa bomu liloanguka karibu yake akiwa katika jitihada za kumuokoa mhe Lema ambaye bomu lilikuwa limeelekea usawa wake, ndipo wanausalama watatu asiowafahamu walimficha na kisha walimtoa chuoni kwenye gari kwa utaratibu ambao haukuwa rasmi.
 

Ukweli, mkuu wa mkoa amelikoroga vibaya, hakuna mahali katika jambo hili lote Mhe Lema amewaambia wanachuo mzomeeni mkuu wa mkoa, hakuna mahali mhe Lema amewaambia wanachuo mtupieni chupa mkuu wa mkoa. Wote waliokuwep kwenye eneo la tukio wanashangaa na kujiuliza maswali mengi sana. Inashangaza kwa nini ajenda ya mauaji ya kutisha na kuhuzunisha na kilio cha wanachuo cha kudai kupatiwa ulinzi kimeyeyeyuka na sasa kila kitu ni Lema Lema!!


Mhe Lema amenyimwa dhamana na hivyo shauri hili litapelekwa mahakamani siku ya jumatatu ambako ndiko atakapopata dhamana.
 

Mpaka sasa, hatujui aliyeleta malalamiko haya polisi ni nani ili kufungua mashataka dhidi ya Lema. Hata hivyo shitaka la uchochezi lina dhamana. Wakili wetu alipohoji na kuuliza kwa nini mhe Lema asipate dhamana maana ipo wazi kabisa kuwa ni shitaka lenye kuweza kupata dhamana alijibiwa hivi, “Ndio hivyo hatapata dhamana, ataipata jumatatu mahakamani”. Kauli hii aliisema Kamanda RCO Wambura akiwa na Kamanda RPC Sabas. Aidha wakili wetu alifedheheshwa na kauli hii ya kibabe kuwa, “unaliona kosa hili kuwa ni dogo lakini Lema ametufanya tumeshinda usiku kucha nyimbani kwake na mpaka sasa tupo hapa tumeacha familia zetu, atakaa ndani”. Nasi pia tumesikitishwa sana na kauli hii.
 
 
Makosa ambayo hayana dhamana (Capital offence) ni pamoja na kosa mauaji (Murder), Uhaini (Traeason), Ugaidi (Terrorism), Ubakaji, uhalifu kwa kutumia silaha na makosa mengine kama yalivyotajwa katika sheria zetu. Kosa hili lina dhamana lakini kuna mamlaka zimeamua kufanya ubabe ili kuonyesha umwamba. Hatuna ugomvi na jeshi la polisi, tunafahamu na tumetambua kiini cha tatizo kiko wapi. SISI TUTASHUGHULIKA NA KIINI.
 

Kama chama, tunaendelea na tafakari juu ya mambo yote haya. Tumeshawasiliana na mawakili wetu ambao kwenye kesi hii watakuwa mawakili wa kutosha kabisa kumtetea mhe Lema. Sambamba na hilo mawakili wetu wanaendelea na utaratibu wa kufungua kesi ya kumshtaki mkuu wa mkoa wa Arusha mhe Magesa mulongo kwa kosa la kumtishia kwa maneno makali mhe Lema na pia kutoa maneno ya uzushi, upotoshaji na uongo kwa jamii kuwa mauaji ya mwanachuo Henry Kago yalikuwa yamepangwa na wanasiasa ili kujipatia umaarufu.
 
 
Kwa ujumla jambo hili mpaka lilipofika hatua hii ya mashtaka kwa mhe Lema, limegubikwa na hila, ubabe na nia mbaya katika kulishughulikia. Hii inatupa mashaka makubwa kwamba, tutavumiliana kwa hali hii mpaka lini? Tutafumba macho na kuacha mambo yapite hivi hivi mpaka lini?
 

Tunaliomba jeshi la polisi lisikie kilio cha vijana hawa wa chuo cha uhasibu na waimarishe ulinzi kwenye maeneo ya makazi yao. Tuwaombe pia na uongozi wa chuo cha uhasibu kuharakisha mchakato wa kuwarudisha wanachuo hawa kuendelea na kumalizia masomo yao kwa mwaka wao huu wa masomo. Walikuwa na madai ya msingi sana, walihitaji kusikilizwa na sio kupigwa vimaneno ya vijembe na kufyatuliwa mabomu. Tunawaomba walimu wa chuo cha uhasibu wawe wakweli na waungwana sana kwa kueleza kile kilichotokea siku ya tukio na wasifanye kwa shinikizo lolote kupindisha ukweli.
 
 
Mwisho tunawaomba wakazi wa Arusha waendelee kuwa wapole na watulivu, wajue wazi kabisa hakuna hila itakayoshinda haki na ukweli. CHADEMA ni chama kikubwa na majaribu yetu ni makubwa sio ya kitoto, hata na hili tutashinda tu.
 

Nimalizie kwa kusema, “Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni woga”. Vitabu vya dini vinasema hivyo na sisi tunasema hivyo hivyo. Wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla, tusiogope kuitaja dhambi kuwa ni dhambi. Pasipo kuvunja sheria za nchi na pia bila kuathiri misingi ya kudumisha heshima kwa mamlaka zilizopo bado tunaweka wazi na kuwaambia na kusisitiza kuwa Watanzania tusiwe waoga.



Imetolewa leo tarehe 27 Aprili 2013
Amani Golugwa
KATIBU WA CHADEMA – KANDA YA KASKAZINI.

MBOWE, ZITO WALIPUKA

Wasema hawatapokea tena makapi ya CCM
Mkakati wa kuidhoofisha Chadema waanikwa
 
 
 
WAKATI Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akisema kuwa chama chake sasa hakitawapokea na kuwapa nafasi za uongozi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaofukuzwa, mkakati wa kukivuruga chama chake umebainika, MTANZANIA Jumapili linaripoti.

Mbowe, wakati akitoa kauli hiyo jana mkoani Tabora, taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa mkakati unaodaiwa kuandaliwa na chama dola kukidhoofisha Chadema unaendelea kuratibiwa kwa karibu na ‘virusi’ (mashushu) waliopenyezwa ndani ya chama hicho na huenda yakaibuliwa mambo mengi zaidi yanayodaiwa kufanywa na chama hicho.
 

Aidha matukio yanayotokea bungeni, nguvu za dola kutumika kupita kiasi, uwepo wa ‘virusi’ ndani ya chama hicho ni miongoni mwa mambo yanayotajwa na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwamba chama hicho kinaandaliwa anguko.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa mkakati wa kukidhoofisha Chadema ulianza tangu siku nyingi na unaratibiwa kwa ukaribu na ‘virusi’ wanaodaiwa kupenyezwa ndani ya chama hicho, ambacho katika siku za hivi karibuni kimepata uungwaji mkono mkubwa.


Inaelezwa kuwa kumekuwa na juhudi kubwa zinazofanywa na mahasimu wa Chadema kutaka kukidhoofisha chama hicho kupitia harakati zake za kisiasa, ambazo imekuwa ikizifanya kwenye mwanga na gizani.

Kwamba matukio ya sasa yanayotokea bungeni, wanachama wake kuundiwa kesi na hata kukamatwa kwa Mbunge wake wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ni matokeo ya mkakati huo.


Inadaiwa kuwa mahasimu wa Chadema wamekuwa wakifanya juu chini kuhakikisha wanakibana chama hicho kuanzia bungeni, ambako imeonekana wazi kuwa umaarufu wa chama hicho kwa kiasi kikubwa umechangiwa na wabunge wake kuibana vilivyo serikali pindi wanapowasilisha hoja mbalimbali ndani ya vikao vya Bunge.


Tayari hali kama hiyo imeshuhudiwa Bungeni hivi karibuni, baada ya wabunge wake watano kusimamishwa kwa kukaidi kiti cha spika, wakati kiti hicho kikishindwa kuwachukulia hatua wabunge wa CCM wanaokwenda kinyume na kanuni zake.

Inaelezwa kuwa hatua hiyo ni mkakati wa kukifanya Chadema kishindwe kutekeleza majukumu yake sawa sawa.

Kuibuka kwa matukio ya wana Chadema wawili, mmoja akidaiwa kumrekodi mwingine wakidaiwa kupanga mikakati ya kutisha, nako kunaelezwa wazi kwamba chama hicho hakipo salama kama kinavyofikiri.

Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azaveli Lwaitama, kwa upande wake anasema mizengwe inayofanywa dhidi ya Chadema si ya kukidhoofisha kama wanavyofikiri, bali ni kukipandisha juu chama hicho.

Akitolea mfano tukio la kukamatwa kwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema kwa tuhuma za kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu, Dk. Lwaitama alihoji mamlaka ya Mkuu wa Mkoa kumkamata mbunge aliyechaguliwa kwa kura za wananchi, akidai kuwa ni ya kipuuzi.

“Wenzetu wa Kenya wameshaondoka katika mfumo huu wa kipuuzi, eti mkuu wa mkoa ambaye hakuchaguliwa na wananchi anajipa mamlaka ya kumkamata mbunge aliyewekwa madarakani na wananchi..huu mimi nasema ni upuuzi,” alisema Dk Lwaitama.


Wakati hayo yakitokea, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesema chama chake hakitawapokea na kuwapa nafasi za uongozi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaofukuzwa.

Amesema utaratibu wa awali wa kuwapokea na kuwapa nafasi za uongozi wanaCCM wanaofukuzwa au kujiondoa wenyewe kwenye chama hicho na kukimbilia Chadema, sasa umesitishwa.


Mbowe aliyasema hayo jana, katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu, Tabora na kuhudhuriwa na makada wake wa Kanda ya Magharibi, inayojumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora.


Katika hotuba yake hiyo, alisema dhamira ya Chadema kwa sasa ni kukiimarisha na kukipatia viongozi walioandaliwa tofauti na vyama vingine vya kisiasa nchini.

Alitoa mfano wa viongozi wa CCM aliodai kuwa idadi kubwa ya viongozi wake wanapatikana kutokana na uwezo wao wa fedha badala ya ule wa kiuongozi.


Alisema Chadema inajipanga kuhakikisha viongozi wake kuanzia ngazi za chini wanawajibika na kuwatumikia wananchi na kuonya kuwa yeyote atakayebainika kutowajibika katika kutekeleza majukumu yake, chama hakitasita kumchukulia hatua kwa mujibu wa Katiba.

Akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa Kanda za majimbo za chama hicho, alisema ni kuzidi kukijengea uwezo na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, jambo ambalo limekuwa gumu kwa serikali ya CCM.

Aidha, Mbowe aliwaonya wabunge wa chama hicho kwa kueleza kuwa kuanzia sasa watapimwa kwa uwezo wao wa uongozi kutokana na utaratibu mpya wa kanda na namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa kusaidiana kati ya mbunge na mbunge, ambao watakuwa katika kanda moja, licha ya kutofautiana majimbo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, ambaye aliambatana na Mbowe katika mkutano huo, alisema viongozi wa Chadema Kanda ya Magharibi wanapaswa kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya chama chao.

Zitto alisema Chadema kinapita katika kipindi kigumu, hivyo viongozi wake wanapaswa kukiimarisha katika ngazi ya kanda ili kuwaenzi wote waliokipigania kwa muda wa miaka 22 ya uhai wake.


“Ndugu zangu wana kanda ya magharibi, viongozi wa Chadema na wanachama, katu msije kukubali mtu yeyote awagawe kwa misingi na malengo yake binafsi, kwani chama chetu sasa kina maadui wengi wasiokitakia mema,” alisema Zitto.

Aliwataka viongozi wenzake kuwa makini na watu ambao kila wakilala wanawaza kuiangamiza Chadema au kuipoteza kabisa katika siasa kwa kuwagonganisha viongozi wake.


Wakati huo huo, CHADEMA Mkoa wa Arusha kinakusudia kumshtaki mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.


Uamuzi huo umefikiwa siku mbili kabla ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) kupandishwa kizimbani kesho kwa tuhuma za uchochezi katika Chuo cha Uhasibu Arusha.

Hata hivyo, wakati Lema akitarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kesho, taarifa kutoka ndani ya Chadema zimedai kuwepo kwa mpango wa kumbambikizia Mbunge Lema, kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Henry Kago (22), aliyeuawa nje ya Chuo hicho.


Akizungumza jijini hapa jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema uamuzi wa kumfungulia kesi Mulongo umekuja baada ya kujiridhisha dhidi ya mwenendo wake wa kutaka kukidhoofisha chama hicho.


“Tunaendelea kukamilisha taratibu zetu, tayari tumewasiliana na wanasheria wetu juu ya hiki na wametuhakikishia kuwa ni lazima afikishwe mahakamani,” alisema Golugwa.

Alisema uchunguzi wao umebaini kwa kipindi kirefu Mulongo amekuwa akitumia lugha za kejeli, dharau na hata vitisho dhidi ya viongozi wa Chadema, jambo ambalo hawataendelea kulivumilia.

Golugwa alisema Mulongo amekuwa akimtuhumu Lema kwa mambo mbalimbali ya uongo kwa lengo la kumchafua na kumshughulikia.

“Kama tutapuuzia hali hii, ninaamini ipo siku itazidi zaidi ya hapa, kwani mbali na hili, pia tumepata taarifa za kumbambikizia kesi ya mauaji ya kule Uhasibu.”

Kwa upande wake, Wakili wa Lema, Humphrey Mtui, ambaye alizungumza na waandishi wa habari jana, alieleza kushangazwa na Jeshi la Polisi kumvunjia heshima mteja wake.

“Nimeshangaa hatua zilizochukuliwa dhidi ya mteja wangu, amechukuliwa kama mhalifu wa mtaani, wakati ana heshima mbele ya jamii na wapiga kura wa Jimbo la Arusha.

“Nimesikitishwa na hatua iliyochukuliwa kwa mteja wangu ya kunyimwa haki za msingi, kama kunywa chai na kuswaki, huu ndiyo utawala bora katika sheria hata kwa wahalifu?

“Mteja wangu alipaswa kuitwa polisi, kama angeendelea kukataa sheria ingechukua mkondo wake na si kufanya uamuzi wa kuvamia usiku nyumbani kwake,” alisema.

Wakati huo huo, baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha waliozungumza na MTANZANIA Jumapili jana walidai kuwa wanajipanga kufika kwa wingi katika viwanja vya Mahakama kwa ajili ya kumpokea kamanda wao kesho.
 
Chanzo: Gazeti la Mtanzania Jumapili

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 28/04/2013

.
 
.
 
.
 
.
 
.
 
.
 
.
 
HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI
 
.
 
 
.
 
.
 
 
.
 
.
 
.
 
.