Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Saturday, April 27, 2013

NAAKAYA AJUTIA KURUDISHA KADI YA CHADEMA NA KUCHUKUA YA CCM

Nakaaya Sumari
 
MSANII, Nakaaya Sumari, amesema kuwa anajuta kurudisha kadi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Akizungumza na Clouds FM, Nakaaya ambaye anatarajia kujifungua muda si mrefu, alisema kuwa anajutia uamuzi wake huo, japo watu wanafikiri kuwa alipewa pesa ili ahame CHADEMA.
 
“Moja ya vitu ninavyojutia ni kurudisha kadi yangu ya CHADEMA na kuingia CCM, najua ‘nimebugi’, lakini si kama watu wanavyoongea kuwa nilipewa hela, kama nilipewa hela si saa hii ningekuwa nakula bata, lakini wapi! Mi sijapewa hela,” alisema.
 
Msanii huyo aliongeza kuwa aliingia kwenye siasa kutokana na ushawishi wa watu, hasa kwa sababu ya kibao chake cha ‘Mr. Politician’.
 
“Watu wasiongee sana, maana hawajui kwanini nilihama CHADEMA, wanajuaje, je, kama nilitishiwa au vitu vingine kama hivyo...najua hapo nilibugi sana kuhama,” alisema.
 
Aidha, alisema kuwa, baada ya kujikita katika siasa, aliona inamchanganya na kuona hiyo si sehemu yake kutokana na siasa kuwa mchezo mchafu.
 
 
Chanzo: Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment