Haya ndiyo mambo
yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jana
jioni:
i)Kosa la kwanza
ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi
kubwa kuliko zote ni woga ".Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo
unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting
for)"
ii)Kosa la pili
ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na
mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye
send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’ Kwa hiyo
huo ni uchochezi
iii) Kosa la Tatu
ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba
nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na
haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa
mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa
kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’ Huu
nao umeitwa kwamba ni uchochezi.
Hayo ndo makosa matatu ya Mbunge Lema yaliyomfanya avamiwe na jeshi la polisi nyumbani kwake kama jambaza sugu hatimae kukamatwa na kunyimwa dhamana hivyo atasota rumande hadi jumatatu.
No comments:
Post a Comment