1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Kufuatia
marekebisho kadhaa ya kanuni hususan zinazolenga kwa sasa Utaratibu wa Kutunga
Sheria kuhusiana na mambo ya fedha, nasi kama
Kambi Rasmi ya Upinzani tutafanya marekebisho katika utaratibu tutakaotumia
katika kutoa maoni yetu kwa Serikali.
Kwa
muda mrefu, kufuatia utaratibu wa mfumo wa bajeti ulivyokuwa huko nyuma,
tulitumia muda mwingi kuishauri serikali
namna bora ya kuboresha bajeti na utendaji wake wa kazi. Hata hivyo, kwa bahati
mbaya sana , serikali hii imekuwa siyo sikivu vya
kutosha hata kama pale ambapo ushauri unaotolewa
uko wazi kwa masilahi na mustakabali mwema wa Taifa letu.
Aidha,
pale ambapo Serikali imechukua maoni yetu, mara nyingi imekuwa haina ustaarabu
wa kutambua, kukiri na kushukuru mchango wa Kambi ya Upinzani, bali mbele ya
macho ya umma imeendelea kutoa kebehi kujaribu kuuaminisha umma kuwa vyama vya
upinzani havina ufumbuzi mbadala kwa matatizo yanayolikabili Taifa.
Mheshimiwa Spika,
Tatizo
kubwa la Serikali inayoongozwa na CCM ni kukosa weledi wa kutekeleza kikamilifu
vipaumbele vyake pamoja na kuviainisha kupitia Mpango wake wa miaka 5, bajeti
na programu mbalimbali. Hali hii inaweza kutafsiriwa kama
uwezo duni wa kusoma alama za nyakati ikiwemo kubuni na kusimamia
inachokiamini. Ni dhahiri vilevile unapolazimika kufanya jambo usiloliamini au
lisilo kipaumbele chako, bali cha kulazimishwa na mazingira unatekeleza bila
kujua undani wake na hatma yake ni kuharibu zaidi.
Mheshimiwa Spika,
Kwa
kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mtambuka, Mwaka huu tutajielekeza kuzungumzia
mambo makuu machache ambayo sisi tunaamini ni vipaumbele muhimu ambavyo Waziri
Mkuu na wasaidizi wake wanapashwa kuja na majibu ya kueleweka kwa Watanzania.
Aidha, mengine yatawasilishwa kupitia hotuba zetu mbalimbali katika Wizara
husika.
2. TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA MSTAKABALI WA
TAIFA
Mheshimiwa Spika,
Tarehe 18
Novemba, 2011 Bunge lako tukufu lilipitisha Muswada
wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Kufuatana malalamiko mengi
kuhusu utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria hiyo na kufuatia vikao kati ya
Mheshimiwa Rais na Kamati Maalum ya CHADEMA pamoja na wadau wengine, Sheria
hiyo ilifanyiwa marekebisho wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge hili uliofanyika
mwezi Februari mwaka 2012.
Marekebisho hayo yalikuwa ni awamu ya kwanza
ya awamu tatu za marekebisho ya Sheria hiyo kwa mujibu wa makubaliano yetu na
Mheshimiwa Rais. Awamu nyingine mbili za marekebisho zilitarajiwa kukamilika
kabla ya mwisho wa mwaka jana, yaani 2012. Hata hivyo, hadi nasoma maoni haya
leo hii, Sheria ya Marekebisho ya Katiba haijafanyiwa marekebisho mengine
yoyote.
Mheshimiwa Spika,
Mara
baada ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa mwaka jana,
Mheshimiwa Rais alifanya uteuzi wa wajumbe na watendaji wakuu wa Tume na Tume
yenyewe ilianza kazi mwezi Mei, 2012. Kwa maana hiyo, hadi kufikia leo Tume ya
Mabadiliko ya Katiba imeshafanya kazi kwa karibu mwaka mmoja.
Kwa
masikitiko makubwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kulijulisha Bunge
lako tukufu kwamba katika kipindi hiki mtiririko wa matukio kadhaa ndani na nje
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha kwamba haina weledi, dhamira au
nia ya kusimamia mchakato huru usiofungamana na upande wowote.
Katika
mwaka wa kwanza wa mchakato wa upatikanaji Katiba mpya, Tume ya Mabadiliko ya
Katiba imethibitisha hofu tuliyokuwa nayo toka mwanzo kwamba lengo la mchakato
wa Katiba Mpya uliowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni
kuhakikisha kwamba mabadiliko pekee yakayokuwepo ni yale yenye kulinda matakwa
ya CCM na Serikali yake au yale pekee yatakayokuwa na Baraka za “Status Quo”.
Mheshimiwa Spika,
Kwanza,
Tume haikuweka utaratibu wowote madhubuti wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya
masuala yote yanayohusu Katiba Mpya ili kuwaandaa wananchi kuchangia maoni yao kwa Tume wakiwa na
uelewa wa kutosha. Badala yake, wakati wa mikutano ya Tume ya kupokea maoni ya
wananchi, wajumbe wa Tume walipewa jukumu la kuwaeleza wananchi juu ya Katiba
Mpya kwa muda usiozidi nusu saa!
Kwa
kulinganisha, Tume ya Katiba ya Kenya
ilifanya kazi ya kutoa elimu kwa umma kwa nchi nzima kwa muda wa miezi sita
kabla ya kuanza kukusanya maoni ya wananchi wa Kenya juu ya Katiba Mpya. Matokeo
yake ni kwamba mchakato wa Katiba Mpya wa Kenya umeiletea nchi hiyo Katiba
Mpya ya mwaka 2010 ambayo imeanza kudhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo
mambo yatokanayo na Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo wa hivi karibuni
yalivyotatuliwa.
Mheshimiwa Spika,
Pili,
muda uliowekwa na Tume wa kukusanya maoni ya wananchi ulikuwa mdogo sana ukilinganisha na
ukubwa wa nchi yetu na wingi wa Watanzania. Katika Majimbo karibu yote ya
uchaguzi Tanzania Bara, Tume iliendesha wastani wa mikutano saba kwa kila jimbo
kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi.
Katika
mikutano hiyo wananchi walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya kwa muda
wa dakika tano kila mmoja na
mikutano yenyewe ilichukua muda wa masaa matatu ikiwa ni pamoja na muda wa
kutambulishana wajumbe wa Tume na mambo mengine yaliyo nje ya kuchukua maoni ya
wananchi.
Mheshimiwa Spika, matokeo
yake ni kwamba kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Sinde
Warioba kwa waandishi habari tarehe 5 Januari mwaka huu, hadi awamu nne za
kukusanya maoni ya wananchi zinakamilika tarehe 19 Desemba, 2012, Tume
ilikwisha kufanya mikutano 1,776 kwa nchi nzima. Aidha, kwa mujibu wa maelezo
ya Mwenyekiti Warioba, hadi kufikia kipindi hicho wananchi wapatao 64,737
walikwishatoa maoni yao
kwa kuzungumza wakati wananchi 253,486 walitoa maoni kwa njia ya maandishi, na
wengine 16,261 walitumia njia ya “posta, tovuti ya Tume, mitandao ya kijamii na
ujumbe mfupi wa simu za mkononi....” Kwa hiyo, kwa mujibu wa taarifa hizi za
Mwenyekiti wa Tume, kati ya Watanzania takriban milioni 45, ni Watanzania
334,484 ndio waliotoa maoni juu ya Katiba Mpya hadi kufikia tarehe 4 Januari,
2013. Idadi hii ni sawa na asilimia 0.7
ya Watanzania wote! Na hao ndio waliotoa maoni yao kwa muda wa dakika tano kila mmoja,
wakiwamo waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili tukufu.
Mheshimiwa Spika, ni
wazi, kwa takwimu hizi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa vyovyote vile,
Katiba Mpya itakayotokana na maoni haya haiwezi kuwa Katiba Mpya ya Watanzania
wote. Utaratibu wa hovyo namna hii utazaa Katiba Mpya ya hovyo!!! Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba utaratibu huu wa hovyo hauwezi kutupatia
Katiba Mpya yenye maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya kutatua migogoro mingi ya
kisiasa, kijamii na kidini ambayo inaikabili nchi yetu kwa sasa.
Mheshimiwa Spika,
Tatu,
licha ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kutangaza kuwa Tume itakuwa huru katika
utekelezaji wa majukumu yake, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kila
dalili za Tume kutokuwa huru au kuutafsiri uhuru vibaya. Kwa mfano, kuna
ushahidi kwamba Tume imekuwa na mawasiliano ya karibu na Serikali na Ofisi ya
Rais kwa namna ambayo inaashiria Tume kutokuwa huru. Ndio maana katika hotuba
yake ya kumaliza mwaka uliopita na kufungua Mwaka Mpya, Rais Jakaya Kikwete
alilitangazia taifa ratiba ya kazi za Tume ambayo Tume yenyewe ilikuwa
haijawahi kuitoa hadharani.
Katika
hotuba yake hiyo, Rais Kikwete alitangaza sio tu kumalizika kwa awamu za kukusanya
maoni ya wananchi, bali pia alitangaza ratiba ya Tume kuanza kuchukua maoni ya
vyama vya siasa, taasisi nyingine na ‘makundi maalum’, tarehe ya kutolewa kwa
Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya, Mikutano ya Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalum
la Katiba na hata tarehe ya kura ya maoni na upitishwaji wa kura ya maoni
kuihalalisha Katiba Mpya.
Mheshimiwa Spika, Rais
asingeweza kufahamu ratiba hii yote bila kupatiwa taarifa ama na Tume yenyewe
ama na watendaji au watumishi wake au na wajumbe wa Tume. Mbali na taarifa ya
kwisha kwa awamu ya tatu ya zoezi la kukusanya maoni ya wananchi, taarifa hizi
hazikuwa zimetolewa hadharani na Tume kabla ya hotuba ya Mwaka Mpya ya Rais
Kikwete!
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni imetambua siku zote kwamba msemaji rasmi wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ni Mwenyekiti wa Tume Joseph Warioba. Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni haijawahi kusikia wala kuona mahali popote ambapo Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba imempa Rais Kikwete jukumu la kuwa msemaji wa Tume. Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji kama Rais
anaweza kupatiwa taarifa za kina namna hiyo kuhusiana na shughuli za Tume, kuna
uhakika gani kwamba yeye au Serikali yake hawatoi kwa Tume maelekezo ya
kichinichini juu ya nini cha kufanya, kwa namna gani na kwa wakati gani.
Mheshimiwa Spika,
Nne,
wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikitoa taarifa za kina juu ya shughuli zake
kwa Rais Kikwete na Serikali yake, Tume hiyo hiyo imetangaza wazi wazi kwamba
haiwajibiki kwa Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
Zaidi ya kumtuma Naibu Katibu wa Tume, viongozi wa Tume kama vile Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume wamekataa kuhudhuria vikao vya Kamati ya
Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili kuieleza Kamati juu ya utekelezaji wa
majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi.
Katika
hili, Tume imeungwa mkono na Serikali hiyo hiyo inayoelekea kupata taarifa za
kina juu ya utekelezaji wa kazi zake! Hii ni licha ya kupatiwa jumla ya
shilingi bilioni 33.944 za walipa kodi wa Tanzania zilizoidhinishwa na Bunge katika mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya
kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo, wakati Tume inaharibu mchakato wa Katiba
Mpya kama tulivyoonyesha hapa, Bunge – kwa
kupitia kwa Kamati yake – limezuiliwa kuhoji shughuli za Tume kwa hoja kwamba
Tume iko huru.
Mheshimiwa Spika, hii
inaweza kuwa mara ya kwanza kwa chombo cha umma kinachotumia mabilioni ya fedha
za umma kilichopewa majukumu ya umma na Sheria iliyotungwa na Bunge hili tukufu
kukataa kuwa chini ya usimamizi wa kikatiba wa Bunge (parliamentary oversight)!
Aidha,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imesikitishwa sana na kushindwa kwa Kamati husika ya Bunge
kudai madaraka yake ya usimamizi yasipuuzwe na Tume na/au Serikali. Udhaifu huu
wa Bunge na Kamati unaweza kuligharimu Taifa endapo mchakato wa Katiba Mpya
utachakachuliwa na kuliingiza Taifa katika machafuko ya kisiasa, kidini au
kijamii.
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili
tukufu juu ya uwajibikaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa matumizi ya mabilioni
ya fedha za umma iliyoyaidhinishiwa mwaka jana na inayoyaomba mwaka huu wa
fedha.
Mheshimiwa Spika,
Tano,
Tume imetengeneza utaratibu wa mabaraza ya kikatiba ambao kwa ushahidi wa
mwanzo tu unaonyesha kwamba hayo ni mabaraza ya CCM na sio mabaraza ya katiba
ya Watanzania wote. Hili limefanyika kwa kupitia Mwongozo Kuhusu Muundo, Utaratibu wa Kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya
Katiba ya Wilaya (Mamlaka za Serikali za Mitaa) na Uendeshaji Wake,
uliotolewa na Tume mwezi Februari mwaka huu. Kwa mujibu wa Muundo huu, wajumbe
wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya watachaguliwa na Kamati za Maendeleo za Kata
(maarufu kama ‘WDC’) baada ya kuwa wamechaguliwa moja kwa moja na wananchi
katika vijiji na mitaa. Wajumbe wa WDC ni Madiwani wa Kata ambao ni Wenyeviti
wake, Watendaji wa Kata ambao ni Makatibu na Wenyeviti wa Vijiji au Mitaa.
Mheshimiwa Spika, kwa
kufuatana na chaguzi za vijiji na mitaa za mwaka 2009, zaidi ya asilimia 90 ya
vijiji na mitaa inaongozwa na wenyeviti ambao ni wanaCCM. Aidha, kutokana na
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, zaidi ya asilimia 80 ya Kata zote nchini
zinaongozwa na madiwani wa CCM. Hawa ndio waliochagua wajumbe wa Mabaraza ya
Wilaya ya Katiba tangu mwanzoni mwa wiki iliyopita. Matokeo yake, kwa taarifa
ilizo nazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutoka sehemu mbali mbali za nchi
yetu, kila mahali wagombea ambao hawakuwa wanaCCM walienguliwa katika ngazi ya
uchaguzi wa vijiji au mitaa au wameenguliwa na WDC baada ya kushinda katika
ngazi hizo.
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni ina ushahidi kwamba viongozi wa kiserikali kama vile
Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa waliwahamasisha wenyeviti wa vijiji, mitaa na
madiwani kuhakikisha kwamba wagombea wote wasiokuwa wa CCM, hasa wa CHADEMA,
wanaenguliwa katika chaguzi za vijiji, mitaa au kata. Mfano mzuri ni wa Mkuu wa
Wilaya ya Musoma Jackson Msome aliyeitisha mkutano wa wenyeviti wote wa mitaa
ya Musoma Mjini na kuwapa maelekezo ya kuhakikisha kwamba watu wasiokuwa wanachama wa CCM
hawapati nafasi katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya au Manispaa hiyo.
Mheshimiwa Spika, licha
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupatiwa maoni ya wadau kwamba utaratibu huo
utaharibu mchakato wa Katiba Mpya, Tume ilikataa kata kata kuubadilisha Muundo
wa Mabaraza haya. Ni wazi kwamba Tume inafahamu inachokifanya.
Ni
wazi vile vile kwamba Tume inafahamu matokeo ya hicho inachokifanya, yaani
kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ambayo ni ya wanaCCM. Na wala
haihitaji shahada ya uzamivu kufahamu kwamba Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yenye
kutawaliwa kwa kiasi hicho na wanaCCM yatatoa maoni ya aina gani juu ya Rasimu
ya Katiba Mpya yatakayoijadili. Itakuwa ni Katiba Mpya kwa jina tu, mambo
mengine ya msingi yatabaki vile vile. Kwa maneno mengine, itakuwa ni Katiba ile
ile, ya watu wale wale, wa chama kile kile.
Mheshimiwa Spika,
Uchakachuaji wa mchakato wa Katiba Mpya wa aina hii ndio ulioiingiza Zimbabwe katika machafuko makubwa ya kisiasa
toka mwaka 1998 na Kenya
mwaka 2007/2008. Kwa utaratibu huu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inaelekea
Serikali ya CCM inaelekea kutotaka kujifunza kutokana na yaliyowakuta jirani
zetu wa Kenya na marafiki
zetu wa Zimbabwe .
Mheshimiwa Spika,
Sita,
Serikali imekataa ama imeshindwa kuheshimu makubaliano iliyofikia na wadau
mbali mbali ikiwemo CHADEMA, kufanya marekebisho zaidi ya Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba. Kwa sababu hiyo, bado haijulikani wajumbe mia moja na sitini na sita
watakaotokana na taasisi mbali mbali zilizotajwa na Sheria hiyo watateuliwa kwa
utaratibu gani na nani atakayefanya uteuzi huo.
Vile
vile, bado hakuna muafaka juu ya uhalali wa idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge
Maalum la Katiba kutoka Zanzibar kushiriki
katika mjadala wa Katiba Mpya kwenye masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania
Bara wakati hakuna mjumbe hata mmoja wa Tanzania Bara anayeweza kushiriki
katika mijadala ya kikatiba inayohusu masuala ya Zanzibar yasiyokuwa Mambo ya Muungano.
Zaidi
ya hayo, bado hakuna majibu yanayotosheleza yanayompa Rais mamlaka ya
kuliitisha upya Bunge Maalum la Katiba na kulielekeza ‘kuboresha’ masharti ya
Katiba Mpya mara baada ya Bunge hilo
kuipitisha. Aidha, haijulikani ni uhalali upi wa kisheria na kikatiba
utakaoiruhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuendesha kura ya maoni ya
kuhalalisha Katiba Mpya kwa sababu Katiba na Sheria za Uchaguzi za sasa
hazitambui wala kuweka utaratibu wa kuendesha kura ya maoni.
Mheshimiwa Spika, kushindwa
kwa Serikali kuleta Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
ili kufanya marekebisho katika maeneo tajwa ni ushahidi wa wazi kwamba Serikali
ya CCM haina nia ya dhati na dhamira safi ya kuhakikisha
Tanzania
inapata Katiba Mpya inayoistahili.
Aidha,
si nia ya CHADEMA kuendelea kushiriki na kubariki mchakato huu kama ulivyo sasa
kwani ishara zote ziko wazi kuwa Katiba inayokusudiwa ni ile tu itakayokidhi
matakwa ya Wana- CCM na Washirika wake na hivyo kutokutimiza azma ya kuwa na
Katiba itakayoponya majeraha mbalimbali na kurejesha uzalendo, mshikamano na
upendo wa dhati miongoni mwa Watanzania na kisha mfumo wa Utawala utakaokidhi
mahitaji ya wakati.
Kwa
sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inatangaza
rasmi kwamba: CHADEMA itajitoa ushiriki
wake katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo yafuatayo hayatapatiwa
ufumbuzi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu, yaani tarehe 30 Aprili, 2013:
1.
Kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa
mabaraza ya wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata, na
badala yake wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya wachaguliwe moja kwa moja
na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na WDC;
2.
Serikali ilete mbele ya Bunge hili tukufu Muswada
wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yatayofanyia maeneo
yafuatayo marekebisho:
(a)
Vifungu vyote vinavyohusu uwakilishi katika Bunge
Maalum la Katiba wa taasisi zilizoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba;
(b)
Vifungu vyote vinavyohusu ushirikishi wa wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar
katika mijadala inayohusu mambo yasiyokuwa ya muungano ya Tanzania Bara;
(c)
Vifungu vyote vinavyohusu mamlaka ya Rais
kuitisha tena Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kuwa limeshapitisha Rasimu ya Katiba
Mpya kwa lengo la kufanya marekebisho katika Rasimu kabla haijapelekwa kwenye
kura ya maoni;
(d)
Vifungu vyote vinavyohusu mamlaka ya kikatiba nay
a kisheria yatakayoiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendesha na kusimamia
kura ya maoni;
3. ANGUKO LA ELIMU TANZANIA :
ANGAMIZO LA KIZAZI NA JANGA LA TAIFA.
Mheshimiwa Spika,
Nianze
kuzungumzia umuhimu wa elimu kwa kumnukuu Rais wa 55 wa Marekani, John
F.Kennedy (1917 – 1963);
“Our progress as a nation can be no swifter
than our progress in education. The human mind is our fundamental resource”
Mheshimiwa Spika,
Siku
za karibuni kumekuwepo mjadala mzito sana
kuhusiana na hali ya elimu nchini. Pamekuwepo na malalamiko mengi sana yakiwemo yaliyomtaka
Waziri wa Elimu Mhe. Shukuru Kawambwa na Naibu wake Mhe Phillip Mulugo
wajiuzulu kama ishara ya uwajibikaji wa
kisiasa. Ni dhahiri kuwa elimu yetu kama Taifa imeporomoka kwa kiasi kikubwa
cha sasa kuhatarisha mustakabali wetu kama
Taifa.
Mheshimiwa
Spika, ni mwaka mmoja tu umepita tangu Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni inayoongozwa na CHADEMA itoe angalizo kali kwa Serikali juu ya kasi
kubwa ya kuporokoka kwa Elimu ya Tanzania na hivyo kuitaka
Serikali kuchukua hatua madhubuti ili kuliepusha Taifa na balaa hilo. Hata hivyo, Serikali hii ya CCM imeendelea
kupuuza ushauri mzuri inayopewa bure na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na
matokeo yake ni kwamba anguko la mwaka huu ni kubwa kuliko maanguko yote
yaliyowahi kutokea katika Historia ya Tanzania ambapo asilimia 60.6 (240,903) ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha
nne wamepata daraja sifuri na wengine asilimia 26.02 (103,327) daraja la nne.
Jumla ya kufeli huku ni zaidi ya asilimia 86.62 au sawa na
Mheshimiwa
Spika, kufuatia kufeli huku kwa kutisha kwa wahitimu wa kidato cha nne
mwaka 2012, wadau wengi walitaka baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu akiwemo
waziri kuwajibika. Ni bahati mbaya sana
kuwa Waziri Mkuu ni mmoja wapo wa viongozi Wakuu aliyestahili kuchukua hatua za
kuwawajibisha wahusika lakini hakufanya hivyo. Badala yake, akakimbilia kuunda
tume ya uchunguzi, ilhali yeye mwenyewe Waziri Mkuu, Waziri wake wa elimu na
serikali yake yote ikijua fika nini kinasababisha kuporomoka kwa elimu yetu.
Yumkini, kama kweli serikali hadi leo haijui
sababu ya kuporomoka kwa elimu yetu, basi haina tena sifa wala weledi wa
kusimamia siyo tu elimu, bali maisha ya kila siku ya Watanzania.
Mheshimiwa
Spika, ni dhahiri kuwa kufeli huku hakuwezi kuchukuliwa kama bahati mbaya hasa ikiwekwa maanani kuwa mserereko wa
watoto wetu kufeli umeshika kasi chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne
hasa kuanzia mwaka 2007.
Mheshimiwa
Spika, mwaka 2007, ufaulu wa vijana wetu wa kidato cha nne ilikuwa
(90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na 2010 (50.4%). Kufuatia mserereko huu wa
kufeli, serikali iliunda timu iliyoshirikisha wataalam kadhaa kubaini chanzo
chake na tiba ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Timu hii iliyokuwa
chini ya Uenyekiti wa Bw. Francis M. Liboy wa TAMISEMI ilikamilisha ripoti yake mwaka 2011 na kutoa mapendekezo kadhaa
kwa serikali. Waziri wa Elimu Mhe. Shukuru Kawambwa anaijua ripoti hii kwani
ndiye aliyeandika dibaji yake. (Angalia
kiambatanisho A)
Mheshimiwa
Spika, mbali na ushauri wetu wa mara kwa mara, serikali hii imebeza
kwa nguvu zote juhudi mbalimbali zinazofanywa na wadau wengine wenye kuumizwa
na kusikitishwa na kuporomoka huku kwa elimu. Watanzania ni mashahidi namna katika
Mkutano wa Kumi wa Bunge, hoja binafsi ya Mheshimiwa James Mbatia (Mb) kuhusu
udhaifu ulioko katika sekta ya elimu ilivyochukuliwa kimzaha na kutolewa majibu
mepesi na Serikali kinyume na kanuni za bunge na hatimaye kuyazima maazimio ya
bunge ya kuinusuru elimu ya Tanzania yaliyokuwa yamependekezwa katika hoja
hiyo. Ni katika mkutano huohuo wa Bunge
ambapo hoja binafsi ya Mheshimiwa Joshua Nassari (Mb) kuhusu Baraza la Mitihani
linavyoathiri elimu ya Tanzania
iliondolewa katika orodha ya shughuli za mkutano wa kumi wa Bunge bila ridhaa
ya mtoa hoja kinyume na kanuni ya 58(5).
Mheshimiwa
Spika, kitendo cha Serikali ya CCM chini ya mwavuli wa wingi wa
wabunge wake bungeni, cha kuzivuruga
hoja hizi na hivyo kusababisha maazimio ya bunge juu ya hoja hizi kutotekelezwa
ni udhaifu mkubwa sana kwa chama kinacho tawala cha CCM na Serikali yake na ni
ushahidi uliokamilika kwamba Elimu kwao sio kipaumbele cha taifa.
Mheshimiwa
Spika, Serikali ambayo Elimu sio kipaumbele chake, haiwafai Watanzania
kwa karne hii. Kuendelea kuukumbatia utawala na aina hii ni kukaribisha maafa
yasiyoepukika kwa Taifa. Mbali na kulisababishia Taifa hili aibu kubwa mbele ya
majirani zetu na jamii ya kimataifa kwa vijana walio wengi wa Kitanzania
kuonekana kuwa na elimu ya mashaka na isiyoweza kuhimili ushindani wa soko la
ajira, ubovu wetu wa elimu umedumaza uwezo wetu wa ndani wa kusimamia
rasilimali za Taifa, Aidha kambi Rasmi
ya Upinzani inawapa angalizo wananchi wote wa Tanzania kwamba haya yote
yanatokea kwa kuwa Serikali ya CCM haijaiweka Elimu kuwa kipaumbele cha taifa
na kwamba umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala kwa
kuchagua chama chenye nia ya dhati ya kuleta mabadilko kitakachounda Serikali
inayojali elimu ya watoto wao na bila shaka chama hicho hakiwezi kuwa CCM tena.
Mheshimiwa
Spika, Taifa kupitia hotuba hii linataka kujua Serikali ina nini
cha kusema kuhusiana na utafiti huu iliofanya mwaka 2011, imetekeleza mangapi
kati ya mapendekezo 27 yaliyotolewa. Aidha ni kwa nini imeunda tume nyingine
kwa kutumia fedha za walipa kodi wa nchi hii ingali ripoti nyingine inayohusu
somo hilo hilo
ikiwa mkononi.
3.1
UNYANYAPAA WA FIKRA
VYUO VIKUU
Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema ya katiba ya nchi yetu kuheshimu
haki ya uhuru wa mawazo kama ilivyowekwa bayana katika Ibara ya 18(a) na Ibara
ya 20(1) kwa kutoa uhuru wa mtu kushirikiana na wengine, kumekuwepo na
propaganda mbalimbali hasa kwenye taasisi za elimu ya juu, zenye kuminya nafasi
na uhuru wa vyama vya upinzani kuendesha shughuli zake kwa usawa, uwazi na kwa
haki katika ngazi ya elimu ya juu kama ambavyo chama tawala kimejiwekea na
kujitengenezea mazingira hayo.
Mheshimiwa Spika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema hivi: "Lakini kutoa uongozi maana yake siyo
kuwanyang'anya watu wenyewe mamlaka yao .
Watu lazima wafanye uamuzi wao wenyewe kuhusu maisha yao ya baadae kwa kufuata njia za demokrasia.
Uongozi hauwezi kuchukua nafasi ya demokrasi; uongozi lazima uwe sehemu ya
demokrasi"
Mheshimiwa Spika, tafakuri ya nukuu hii imekuja wakati ambao ushiriki
wa wanafunzi wa elimu ya juu katika siasa unaonekana kulemea upande moja tu wa
kukipendelea na kukipa uwezo chama tawala katika shughuli zake kwenye taasisi
hizo. CCM wamefikiri na kuamua
kuanzisha mkoa maalumu kwa sasa wakitambua kuwa vyuo (hasa vyuo vikuu)
haviruhusiwi kuendesha shughuli za siasa vyuoni, kama ilivyo majeshi, makanisa
au misikiti na ili kuthibitisha hilo
wameelekeza pia shughuli za mkoa maalumu ulioanzishwa zifanyike nje ya chuo.
Lakini tujiulize na kutafakari zaidi kuhusu mshindo (impact) wa
shughuli za mkoa maalumu wa kisiasa ndani ya himaya za vyuo vikuu na elimu ya
juu nchini.
Mheshimiwa
Spika, ni ngumu kuamini kuwa
shughuli za siasa vyuoni, ambazo Tanzania Commission of University Act imeweka
bayana kuwa ni kosa, zitaweza kudhibitiwa ikiwa vyama vingine vinajiwekea
uhalali na mazingira ya kuingiza wanavyuo kwenye siasa, jambo ambalo udhibiti
wake ni mgumu kwa mamlaka husika hasa vyuoni kwa kuwa wanavyuo hufanya vikao
vya siasa kwa siri, na kwa nyakati ambazo uongozi wa vyuo hauna taarifa.
Mheshimiwa
Spika, kwa uangalifu mkubwa,
ningependa kutoa angalizo kuwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitokubali
unyanyapaa wa fikra wa aina yoyote utakaoendana na kujenga matabaka kutokana na
utofauti wa mitazamo baina ya jamii ya wasomi kwa kuwa, kutoka taasisi
mbalimbali za elimu ya juu , chimbuko la viongozi mahiri wa nchi hii pamoja na
nchi nyingine mbalimbali duniani limechipukia. Kambi Rasmi ya Upinzani,
itaendelea na juhudi zake za kuhakikisha kuwa taifa kwa kupitia wanafunzi wa
elimu ya juu, wanapata fursa mbalimbali za kuikomboa jamii ya kitanzania ambayo
inadumazwa kwa unyanyapaa wa fikra.
Mheshimiwa
Spika, njia pekee ya kufuta
unyanyapaa wa fikra kwa vijana waliopo kwenye elimu ya juu ni kwa Serikali
kurejesha rasmi na kuruhusu uwepo wa siasa katika elimu ya juu na vyuo vikuu
vyote nchini kama shughuli ambazo ni nje ya masomo ili kusaidia kujenga uwanja
wa demokrasia katika serikali za vyuo na vile vile itasaidia katika kuweka
mazingira ambapo wasomi wetu wanaanza kujifunza mbinu na utendaji wa kisiasa
katika mazingira ya elimu ili waweze kujifunza kuishi pamoja, kupingana kwa
hoja na kujua jinsi ya kuvumiliana katika mazingira ya tofauti mbalimbali za
kiitikadi, imani, na mtazamo kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya
CHADEMA ya mwaka 2010. Hapa nikisisitiza maneno ya baba wa Taifa, Mwalimu
Nyerere juu ya kuboresha maisha ya Watanzania:
"Tukiwasaidia watu wa
Tanzania kuendelea, ndiyo tunaiendeleza Tanzania . Maana Tanzania Ni ya
Watanzania Na Watanzania Ni wote, Hakuna mtu mwenye haki ya kusema "Mimi
ndiyo watu". Wala hakuna Mtanzania
mwenye haki ya kusema " Najua linalowafaa watanzania
na wengine lazima wafuate".
3.2 BODI YA
MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Mheshimiwa Spika,lengo la kuanzishwa kwa bodi ya mikopo ya wanafunzi
wa elimu wa juu ni katika kusaidiakupunguza maumivu ya wazazi na walezi wa
kitanzania katika kuhakikishsa vijana wetu wanapata elimu ya juu kwa kusaidiana
na taasisi hii ya Serikali (HELSB), kwa kugawa mikopo kwa waombaji wenye vigezo
sahihi na kuwapa mikopo kwa viwango vya madaraja ,balimbali ya uhitaji.
Mheshimiwa
Spika, Vigezo ambavyo vimekua
vikitumika katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, vimekua
vikilalamikiwa. Baadhi ya wanufaika wa mikopo hii, wamejikuta wakipewa asilimia
chache huku wakiwa wametoka katika familia za kifukara ambazo hazina uwezo wa
kuendesha maisha yao .
Familia nyingi hazina uwezo hata wa kuhimili mlo mmoja kwa siku, je mzigo wa
kuwasomesha watoto na vijana wao ngazi ya elimu ya juu nani ataubeba? Kutokana
na udhaifu huu, vijana wameanza kujigawa katika matabaka ya 'wao'(matajiri na
wenye nazo) na 'sisi'(masikini, wasionacho) na wamefikia mahali wananukuu
maandiko ya dini kuwa "mwenye nacho huongezewa, asiye nacho hupokonywa
hata kile kidogo walicho nacho".
Mheshimiwa
Spika, Malalamiko juu ya bodi
ya mikopo ya elimu ya juu yameendelea kuwa mengi, huku waombaji wakilalamikia
mlolongo wa taratibu zilizowekwa ili muombaji aweze kufanikisha usajili wake
katika bodi. Malalamiko haya yameendana sambamba na utaratibu mbovu wa utunzaji
wa kumbukumbu za watu katika mfumo mzima wa elimu Tanzania ambao unajenga urasimu
mgumu katika kupata taarifa za mwombaji na hivyo waombaji kulazimika kujaza
taarifa upya kila mwaka mpya wa masomo unapoanza.
Mheshimiwa
Spika, Bodi ya mikopo iliingia
gharama ya kununua mfumo utakaotumika katika kuchambua viwango vya ukopeshaji
kwa wanafunzi , kutoka kwa kampuni ya nchini Afrika Kusini ya ADBSC kwa gharama
za dola za kimarekani shilingi 188,000 na marekebisho ya mtambo huu
yaliigharimu bodi kiasi cha dola za kimarekani 42,000. Mfumo huu ulitarajiwa
kupunguza malalamiko ya waombaji na badala yake malalamiko yanaongezeka kila
kukicha.
Mheshimiwa
Spika, Ongezeko la malalamiko
mbalimbali juu ya ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi waliopo vyuoni hali
ambayo imekua ikisababisha migomo ya mara kwa mara katika taasisi hizo nalo
limekua tatizo lisiloisha. Na tumeshuhudia migomo hiyo ikiambatana na kusimamishwa
ama kufukuzwa kwa wanavyuo, hali ambayo inajenga kizazi chenye hofu hasa
inapokuja katika kutetea haki zao za msingi.
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa kifungu
cha 19 (1) cha sheria No. 9 iliyoanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu, ni wajibu wa kila mtu aliyenufaika na mikopo ya elimu ya juu kurejesha
mkopo serikalini kupitia Bodi ya mikopo. Pamoja na changamoto ya urejeshwaji wa
mikopo kwa walionufaika, bodi haijafanya kazi ya kutosha katika kufuatilia na
kujua kuhusu wanufaika wa mikopo hiyo (tracking system).
Mheshimiwa
Spika,ni dhahiri kuwa bodi ya
mikopo haijaweka utaratibu na mfumo sahihi wa kuwafuatilia wadeni wake, na
hivyo kuna asilimia kubwa ya wanufaika wa mikopo hiyo ambao wako makazini na
wana ajira, lakini mpaka leo hawajawahi kukatwa marejesho ya mikopo wala
kufuatiliwa na bodi kwa ajili ya taratibu za kuwaingiza katika mfumo wa
marejesho.
Mheshimiwa
Spika, ni wazi kuwa kumekuwa na
ubabaishaji mkubwa si katika marejesho tu, hata katika utoaji wa mikopo kwa
wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu. Pamoja na ushauri ambao Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni ulitoa kwa Serikali katika uwasilishaji wa hotuba ya mwaka
2012/2013 kuanzisha na kutumia mfumo wa urejeshaji mikopo kwa kutumia
technolojia ya kibenki kupitia mitandao ya simu kama M-PESA,TIGO PESA, Airtel
Money, Z-Pesa, n.k, Serikali na bodi ya mikopo inaonekana kutofuata ushauri huu
na hivyo kuendelea kuwanyima fursa wahitaji wa mikopo.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani
bungeni inaitaka wizara husika pamoja na bodi ya mikopo kutoa maelezo juu ya
utekelezaji wa mapendekezo haya, kama wamefanya tathmini juu ya uanzishwaji wa
mfumo huu, faida na hasara zake na kama la!
hawajafanya tathmini, wizara husika itoe kauli katika mkutano huu wa bunge, juu
ya njia mbadala na mfumo utakaohakikisha wanufaika wanapata uraisi katika
urejeshaji wa makato ya mikopo yao .
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani, inaendelea kusisitiza juu ya utekelezaji wa mapendekezo yake,
yaliyopo katika ilani ya CHADEMA ya kuivunja Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
kutokana na uendeshaji mbovu, mfumo wake mbovu wa kisheria, na uongozi ambao
umeshindwa kufanya elimu ya juu ipatikane kwa kila kijana na ambayo kutokana na
uongozi usiofaa imeshindwa kukusanya madeni toka kwa wakopaji.
3.2
HATIMA YA WATOTO WANAOSHINDWA KUENDELEA NA
MASOMO YA SEKONDARI BAADA YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI
Mheshimiwa
Spika, kwa mujibu wa tafiti
mbalimbali, watoto na vijana wa Kitanzania walio chini ya umri wa miaka 18
ambao wamefeli darasa la saba na au kidato cha nne, kwa sasa ni wastani wa
watoto 800,000 kwa sasa. Kwa wengi wa watoto hawa ambao wengi hutoka familia
masikini, hawana uwezo wa kujiendeleza na hawana sifa za kuajiriwa ikiwa ni
pamoja na umri mdogo. Kundi hili ni kubwa na linakuwa kwa kasi.
Mheshimiwa
Spika, kwa kipindi cha miaka
51 ya Uhuru, Serikali haijatengeneza sera yoyote au sheria ya kusaidia kundi
hili kubwa ili liweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ili
waweze kujikimu wao wenyewe na kuchangia katika pato la taifa. Kundi hili
lililo hazina kubwa ya nguvukazi ya Taifa letu siku za usoni limeachwa solemba
huku likipewa majina ya kebehi ya kila aina ikiwemo wazururaji, vibaka,
machinga nk.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kueleza mbele ya Bunge hili, kwamba inampango gani
wa kupunguza idadi hii ya watoto wanaobaki mitaani bila shughuli rasmi ya
kufanya? Pili kwa wale ambao imeshindikana kabisa kuendelea na masomo, kuna
mpango gani wa kisera wa kuweza kuwasaidia ili waweze kushiriki katika shughuli
rasmi za kiuchumi ili kulinusuru
taifa kuondokana na umasikini
uliokithiri?
4. DEMOKRASIA, UTAWALA BORA NA HAKI
ZA BINADAMU
4.1.
DAFTARI
LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA CHAGUZI ZA
KIDEMOKRASIA NCHINI.
Mheshimiwa Spika, chaguzi
huru na za haki ni kipimo muhimu cha demokrasia ya kweli. Kwa kutambua umuhimu
huu katika chaguzi na hatimaye katika kuongoza nchi, ibara ya 5(1) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inatoa haki ya kupiga kura kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka
kumi na minane.
Mheshimiwa Spika,
ili kuweka utaratibu mzuri wa kila raia wa Tanzania mwenye sifa ya kupiga kura
aweze kupiga kura, ibara ya 5(3) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imetoa fursa kwa Bunge kutunga sheria ya Uchaguzi ambayo pamoja na
mambo mengine, itaanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuweka utaratibu
wa kurekebisha yaliyomo katika daftari hili.
Mheshimiwa Spika, Ni
vyema kwamba Daftari la Kudumu la Wapiga kura lipo, lakini ni bahati mbaya sana
pia kwamba utaratibu wa kurekebisha au kuboresha yaliyomo katika daftari hilo hauendi
sawia na haki ya raia kupiga kura na
mahitaji makubwa ya kukuza demokrasia katika chaguzi hapa nchini.
Mheshimiwa Spika,
mara kadhaa nimemuuliza Waziri Mkuu mbele ya Bunge hili juu ya mkakati wa
Serikali kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura .
Wakati wote majibu yamekuwa ni mepesi na yasiyokidhi hitaji hili muhimu la
Kikatiba. (Tazama Taarifa Rasmi za Bunge (Hansard) za tarehe 19 Aprili, 2012 na
8 Novemba, 2012).
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu akijibu swali langu la papo kwa papo juu ya Maboresho
ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, katika Mkutano wa Tisa wa Bunge, tarehe 8
Novemba, 2012, alisema kwamba mfumo uliopo wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni mzuri. Jambo hili linaibua mashaka makubwa juu ya
utayari wa Serikali kulinda haki ya mwananchi ya kupiga kura kama ilivyotolewa
na Katiba ya Nchi, kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na wanachi
kukosa haki ya kupiga kura kutokana na Daftari hilo kutofanyiwa marekebisho.
Aidha mtazamo huo wa Waziri Mkuu, hautoi fursa ya kulifanyia maboresho Daftari
la Kudumu la Wapiga kura kwa wakati; na kwa maana hiyo haki ya kupiga kura na
demokrasia ya uchaguzi katika Taifa hili vipo katika hatari ya kupotezwa au
kupatikana kwa hisani ya watawala na siyo haki ya kikatiba.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tangu uchaguzi mkuu wa 2010,
kumefanyika chaguzi ndogo mbili za Ubunge katika Majimbo ya Igunga Tabora na
Arumeru Mashariki mkoani Arusha. Aidha, kata kadhaa zimerudia chaguzi nchini
kwa sababu mbalimbali. Katika chaguzi hizi, daftari la Kudumu la Wapigakura
halikufanyiwa marekebisho na hivyo kuwanyima wananchi wengi waliokuwa na sifa
ya kuandikishwa na kupiga kura haki ya kushiriki katika chaguzi hizo.
Mheshimiwa Spika, Ni kilio cha muda mrefu ndani ya nchi hii kuwa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haiko huru na inafanyakazi zake kwa shinikizo la
viongozi waliopo madarakani. Kilio hiki kimethibitishwa na Tume yenyewe pale
walipokutana na Tume ya marekebisho ya Katiba wakati walipotoa maoni yao .
Mheshimiwa
Spika, kuna mchakato wa
maandalizi ya siri unaoendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kuandaa
utambuzi wa wapiga kura kwa kutumia mfumo wa “biometric” kwa maana ya kumtambua
mpiga kura kwa alama za mwili kama alama za vidole na au mboni ya jicho kama
sehemu ya maandalizi ya Uchagizi Mkuu ujao wa 2015. Kwa mujibu wa taarifa
tulizo nazo, tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshaanza maandalizi mengi ya
msingi bila hata vyama vya siasa kujua
Aidha, mchakato huu unaofanywa kwa siri kubwa na
unaokisiwa kutumia zaidi ya dola za kimarekani million 200 tayari umeanza
kutafutiwa fedha.
Mheshimiwa Spika, teknologia hii kwa siku za
karibuni imetumika katika chaguzi nchini Ghana
na Kenya .
Kote huko, ilifeli na chupuchupu ingeyaingiza mataifa hayo katika vurugu kubwa
za uchaguzi. Mataifa haya yalilazimika kurudia mfumo wa upigaji na uhesabuji
kura “manually” hali iliyosababisha hofu kubwa.
Mheshimiwa
Spika, Si kwamba Kambi Rasmi
ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA haiafiki matumizi ya teknologia mpya
kurahisisha na kuboresha mfumo mzima wa uchaguzi katika nchi yetu, bali
inatambua athari kubwa zinazowezekana siku za usoni kama zoezi hili lililo
“sensitive” halitafanywa katika misingi ya uwazi na ushirikishwaji wadau muhimu
kama vyama vya siasa katika hatua zote la
tangu awali kabisa. Ni kwa sababu hizi basi, tunaitaka Serikali kutoa maelezo
ya kina kuwa ni sheria gani iliyotungwa na bunge inayoruhusu uboreshaji wa
daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo huu na ni bajeti ipi inatumika kutekeleza mpango huo?
Na ni kwa nini mpango huo unafanyiaka kwa siri?
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali haioneshi dhamira ya
dhati ya kusukuma mchakato wa kuleta marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi ili kuondoa ukomo wa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura
(wa mara mbili kwa kipindi cha miaka
mitano) na badala yake daftari hilo liwe huru wakati wote kuandikisha
wapigakura wapya wanaotimiza masharti ya kupigakura na kuingiza marekebisho ya taarifa za wapigakura wengine, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa kusikiliza na kuzingatia sauti na utashi wa watu
na uzingativu wa kutosha wa dalili za nyakati na mazingira ya nchi pamoja na
kuheshimu maono na falsafa za waasisi wa taifa letu,
inakusudia kuleta Hoja Binafsi kuhusu marekebisho ya sheria zote za uchaguzi
nchini ili kuinusuru haki ya kikatiba ya raia wa Tanzania kushiriki kikamilifu
katika chaguzi tena zilizo huru na za haki.
4.2 MFUMO WA KUKABIDHIANA MADARAKA KATIKA OFISI
ZA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI.
Mheshimiwa Spika,
Pamoja
na Taifa kuwa katika mchakato wa kuandika upya Katiba ya nchi yetu, hakuna
“guarantee” kuwa katika hiyo itakuwa tayari kwa ukamilifu wake kabla ya
uchaguzi mkuu wa 2015. Hivyo basi ni bora hatua zote za urekebishaji wa
viashiria vya mvurugano kuendelea kushughulikiwa sambamba na mchakato wa Katiba
Mpya.
Mheshimiwa Spika,
Ni jambo la kiungwana kwa viongozi wanaoondoka madarakani kukabidhi madaraka na
ofisi kwa wale watakaoingia madarakani na katika ofisi hizo.
Mheshimiwa Spika,
pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa muda wa siku saba, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano Ibara ya 42(1) kuwa “Rais
Mteule atashika madaraka ya Rais mapema
iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa kuwa Rais, lakini kwa hali
yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba”. Lakini
utaratibu huo haujatungiwa sheria na ni utaratibu ambao ulikuwepo tangu enzi za
chama kimoja na kwa misingi hiyo haukidhi mahitaji ya kipindi hiki cha vyama
vingi endapo itatokea kwamba mgombea urais kutoka chama cha upinzani atashinda
uchaguzi na kuapishwa kushika madaraka ya Urais.
Mheshimiwa Spika,
kwa kuwa nchi mbalimbali duniani zimeanzisha sheria ya kipindi maalumu cha
mpito cha kukabidhiana madaraka ya Urais baada ya uchaguzi mkuu wa Rais na
wabunge,
Na
kwa kuwa sheria kama hii huelekeza mtu
atakayesimamia rasilimali za nchi ili kudhibiti ubadhirifu mkubwa ambao
hufanyika katika kipindi hiki cha mpito;
Na
kwa kuwa nchi yetu imeridhia kipindi cha uongozi wa u-rais wenye ukomo wa miaka
kumi;
Na
kwa kuwa mfumo wetu wa Siasa ya vyama vingi sasa umekomaa na hivyo kutoa nafasi
ya uwezekano wa chama cha upinzani kutwaa madaraka ya Dola;
Hivyo
basi ni jambo la busara sana
kutunga sheria ya Kipindi cha mpito chenye kutoa muda wa kutosha na utaratibu
utakaotumika kuruhusu kukabidhiana madaraka ya urais na serikali (Presidential
Transition Act) kutoka utawala mmoja kwenda mwingine ili kuepusha migongano au
hofu ya kutojua kitakachotokea.
Mheshimiwa Spika,
ni azma ya Kambi Rasmi ya Upinzani, CHADEMA
kuleta hoja binafsi Bungeni ili Bunge liazimie kutungwa kwa sheria hii
muhimu sana kwa
Taifa letu siku za usoni.
4.3
UCHOCHEZI
WA KISIASA: UDINI, UKABILA NA “UGAIDI”
Mheshimiwa Spika, nchi
yetu kwa miaka mingi imesifika sana
duniani kutokana na tunu yake ya “Amani na Utulivu.” Hata hivyo, tunu hii ya
amani na utulivu iko mashakani baada ya kuibuka kwa matukio kadhaa ya uvunjifu
wa amani yenye sura ya udini.
Mheshimiwa Spika,
matukio hayo ni pamoja na mgogoro kati ya waislamu na wakristo huko Geita,
Tunduma na kwingineko juu ya uhalali wa kuchinja ambapo watu kadhaa
walijeruhiwa na wengine kuuwawa. Matukio mengine ni kushambuliwa kwa viongozi
wa dini akiwemo Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga ambaye
alimwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana, Padre Ambrose Mkenda ambaye
alinusurika kifo baada ya kupigwa risasa
na kuvunjwa taya na Padre Evaristi Mushi ambaye aliuwawa kwa kupigwa risasi
tarehe 17Februari, 2013.
Mheshimiwa
Spika, matukio haya ya kihalifu yenye sura ya kidini
yalijumuisha pia kuchomwa moto nyumba za ibada hususan makanisa huko Zanzibar na Dar es Salaam
na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali . Aidha matukio haya yalizua
hofu kubwa miongoni mwa wananchi kwa kuwa hawakuwa na uhakika wa usalama wao.
Mheshimiwa
Spika, mengi
yamesemwa, mengi yameandikwa, mengi yamehubiriwa kwenye nyumba za ibada na
vyombo vya habari. Lakini jambo moja ambalo halijasemwa wazi na ambalo tumekuwa
na kigugumizi kulisemea, ni hili: Kwamba
kwa kiasi kikubwa mgogoro huu wa kidini nchini, hasa mgogoro wa uchinjaji wa kitoweo, umechochewa
na baadhi ya wanasiasa wa kutoka chama tawala.
Mheshimiwa
Spika, Madhehebu ya dini yamekuwapo kwa muda mrefu
nchini na katika kipindi chote hicho, hakujawahi kutokea mgogoro wa uchinjaji
wa nyama kwa minajili ya kitoweo. Pamoja na kwamba Kambi Rasmi ya upinzani
Bungeni, haina nia ya kutoa hukumu juu ya matukio haya, lakini ni vema Watanzania
wakaelewa kwamba kwa vyovyote iwavyo, serikali ya CCM haiwezi kukwepa lawama
katika kulikuza tatizo hili; na kwamba
imeshindwa kujua wajibu wake wa msingi wa kuilinda nchi na raia wake na
kuhakikisha jamii yote inaishi kwa upendo na kuvumiliana. Uhalifu wowote
unaotokea dhidi ya nchi na raia ni dalili ya wazi kabisa ya udhaifu wa Serikali
iliyoko madarakani katika kutimiza wajibu wake. Utawala unaotumia dini kuwagawa
wananchi wake na kutafuta ushindi
Mheshimiwa
Spika, uchochezi na propaganda za kidini na kikabila
vilichagizwa kasi na CCM mara baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi vya siasa kama mojawapo ya turufu yake ya kukabiliana na vyama vya
upinzani. Uchochezi huu ulishika kasi katika uchaguzi wa mwaka 2005 na mwaka
2010. Vikundi kadhaa vya kidini vilifadhiliwa kuhubiri chuki dhidi ya dini
nyingine waziwazi na kwa muda mrefu katika maeneo kadhaa ya nchi. Mihadhara,
mahubiri na hata matamko ya hatari na uchochezi yalitolewa waziwazi hata
kupitia vyombo kadhaa vya habari vya kidini na mitandao ya kijamii. Malalamiko
mengi yalitolewa lakini Serikali ilifumbia macho tatizi hili kwani ilionekana
kuwa mpasuko na hofu iliyo matokeo ya propaganda hizo ulikinufaisha zaidi chama
tawala na baadhi ya viongozi wake.
Mheshimiwa
Spika, chuki na hofu hii iliyopaliliwa kisiasa sasa
ndiyo inayoitesa nchi yetu na hakika linastahili kuwa somo kwa wanasiasa wote
walioasisi uhalifu huu dhidi ya mstakabali mwema wa Taifa letu.
Mheshimiwa
Spika, kama vile hili
halitoshi, sasa tunashuhudia kuibuka kwa uchochezi mpya wa kisiasa tena wenye
ubia kati ya chama Tawala na vyombo vya dola na kinachoitwa “Ugaidi”.
Mheshimiwa
Spika, vitendo viongozi wa dini kujeruhiwa na kuuwawa
kwa kupigwa risasi, kuchoma moto nyumba za ibada huko Zanzibar
na Dar es Salaam ni Ugaidi kwa mujibu wa tafsiri ya Sheria ya Ugaidi ya Tanzania . Kambi
Rasmi ya Upinzani inashangazwa sana kuona kwamba
Serikali haikuyachukulia matukio haya ya wazi ya kigaidi kama ni ugaidi ila
imekuwa hodari sana
kuchukua suala la mtu aliyebambikiwa kesi ya ugaidi kwa ushahidi wa kughushi
kuwa yeye ndiye gaidi. Pili, Kwa mujibu wa Sheria ya ugaidi mtu yeyote
anayefanya mawasiliano na gaidi au magaidi, yeye pia anahamasisha ugaidi na
hivyo naye anastahili kuunganishwa katika tuhuma hizo za mashtaka ya ugaidi.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitika sana kuona wale wote
waliokuwa wakiwasiliana na hao wanaoitwa magaidi ambao pia ni viongozi wa CCM
na washirika wao hawajachukuliwa hatua
yoyote. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaulaani mkakati huu wenye nia ovu ya
kufifisha demokrasia hapa nchini. Aidha Kambi ya Upinzani inaamini kwamba, kamwe mpango huu haramu hautafanikiwa na naomba kuchukua nafasi hii
kuonya kuwa vyama vya siasa vifanye siasa zake kwa ushindani wa sera na isiwe
kwa mikakati ya kiharamia ya kudhuru, kubambikiza na kisha kutengeneza ushahidi
kwa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama. Hili nalo likiachiwa likakomaa
litaliingiza Taifa letu katika hatari nyingine ya machafuko.
4.4
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa Spika,
ni dhahiri kwamba uhuru wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) ni
kichocheo muhimu sana
katika kujenga na kukuza demokrasia katika Taifa lolote linaloamini katika
haki. Hali kadhalika, uhuru wa kujieleza na kupata habari ni miongoni mwa haki za
msingi za raia. Ibara ya 18 ya Katiba yetu inaweka msisitizo kwamba, kila raia wa Tanzania anao uhuru wa maoni na
kueleza fikra zake, uhuru wa kutafuta na kupokea habari na haki ya kufanya
mawasiliano bila kuingiliwa katika mawasiliano yake.
Mheshimiwa Spika,
matukio yaliyotokea mwaka jana peke yake katika tasnia ya habari ni kinyume cha
katiba ya nchi lakini pia yanapingana na dhana ya Utawala Bora na kaulimbiu ya
Serikali ya Uwazi na Uwajibikaji (Transparency and Accountability).
Mheshimiwa
Spika, gazeti la MwanaHALISI limefungiwa kwa muda
usiojulikana na serikali. Muda usiojulikana maana yake, ni hadi mtawala
atakapotaka na au hadi waliolifungia gazeti watakapojisikia kutaka
kulifungulia.
Mheshimiwa
Spika, kwa taarifa zilizopo, gazeti hili limefungiwa
bila wamiliki wa kampuni inayochapisha gazeti hilo kupewa haki ya kusikilizwa. Mbali na
kitendo hiki kuwataabisha wafanyakazi kadhaa walioajiriwa na kampuni
inayochapisha gazeti hili, kitendo hiki kimewanyima mamilioni ya Watanzania
haki yao ya
kupata habari kwa mujibu wa katiba. Kutokana na hali hiyo, ninaisihi serikali
itafakari upya uamuzi wake wa kulifungia gazeti hili ili kuondoa kiza na
malalamiko kuwa gazeti la MwanaHALISI limefungiwa kwa sababu ya kulinda uhalifu
dhidi ya waliomteka na kumtesa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dr.
Steven Ulimboka.
Mheshimiwa
Spika, katika
kadhia hiyo hiyo ya kuminywa kwa vyombo vya habari na uhuru wa habari,
mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa kwa kupigwa kitu kilichohisiwa kuwa
bomu na polisi. Utata mkubwa umezunguka tukio hili na polisi walewale ambao kwa
mtazamo wa jumla ni watuhumiwa, wameachiwa mamlaka ya kuchunguza na kushtaki
kuhusiana na kifo hiki.
Mheshimiwa
Spika, kifo hiki kimelitia doa kubwa Taifa letu na
zaidi kutokana na kitendo cha Serikali kuonekana kulinda wahalifu. Sina hakika kama watu walioshiriki katika kumpiga na kumuua Mwangosi
wamekamatwa, ila nina hakika kuwa kifo chake kimepunguza wigo wa upatikanaji
habari.
Mheshimiwa
Spika, kilio hiki cha kuundwa kwa Judicial Commission
of Enquiry kimekuwa cha muda mrefu na kila mwaka nazungumzia jambo hili katika
hotuba zangu bila hatua zozote kuchukuliwa. Mara kadhaa, nimezungumza na wewe
ndani na nje ya Bunge. Rais Jakaya Kikwete naye nimemwandikia na hata
kuzungumza naye kuhusiana na haki hii ya msingi ya raia. Pamoja na wote kuahidi
kuchukua hatua, hadi sasa hakuna hatua iliyochokuliwa hali inayoashiria
serikali kujua ukweli na pengine kuhusika na hivyo kulindana katika mauaji.
Mheshimiwa Spika,
napenda kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani kutoa pole kwa Ndg. Absalom
Kibanda, Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa
Gazeti la Mtanzania kwa maumivu na mateso makali aliyoyapata kutoka kwa watu
wasiotaka kusikia uhuru wa kujieleza. Na kama ilivyo kwa matukio mengine kadhaa
ya kuongezeka kwa utesaji wa aina hii, tunaitaka serikali itoe tamko rasmi la
ni nani waasisi na watekelezaji wa mkakati huu wa kuzima uhuru wa wanahabari na
vyombo vyao.
4.5
UWAJIBIKAJI WA KISIASA
(POLITICAL ACCOUNTABILITY)
Mheshimiwa
Spika, uwajibikaji wa kisiasa
ni moja kati ya misingi ya utawala bora katika uendeshaji wa shughuli za
Serikali. Serikali inayofuata misingi ya utawala bora huwa inawajibika kwa mema
na mabaya yanayotokea chini ya utawala wake. Ni vyema ikaeleweka kuwa hitaji la
kumtaka kiongozi wa kisiasa kuchukua hatua za uwajibikaji wa kisiasa, pale
jambo linalosababishwa na uzembe wa ama yeye binafsi, walio chini ya mamlaka
yake na hata mfumo anaousimamia, siyo jambo la chuki binafsi; bali ni kielelezo
cha uongozi unaojali, unaojutia madhila yaliyosababishwa na ulio tayari
kujirekebisha ili yaliyotokea yasijirudie tene siku za usoni.
Mheshimiwa
Spika, Serikali ya Tanzania siku zote hujikweza kama
Serikali inayofuata misingi ya utawala bora. Lakini jambo la kushangaza ni
kwamba kila mara viongozi wake wanakwepa kuwajibika kwa mambo mengi ya aibu
yanayotokea chini ya utawala wake.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni imekuwa ikipiga kelele ikiwataka mawaziri wa Serikali hii
kuwajibika kwa kujiuzulu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kusimamia vyema
kazi za Serikali lakini hakuna chochote kinachofanyika jambo ambalo
limesababisha maovu kuendelea kufanyika na hivyo kuathiri ustawi wa Taifa.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani ilimtaka waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
kujiuzulu kwa kushindwa kuzuia mauaji holela ya raia wasio na hatia
yaliyofanywa na polisi maeneo kadhaa hapa nchini lakini hakufanya hivyo.
Tulimtaka Waziri wa Elimu na Naibu wake kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia mfumo
wa Elimu hapa nchini jambo ambalo limepelekea kiwango cha wanafunzi wanaopata
alama sifuri katika mitihani kuongezeka
kila mwaka na hivyo kuweka hatarini mustakabali wa maisha ya wanafunzi hao na Taifa kwa jumla lakini bado
wameng’ang’ania madaraka. Tuliitaka Serikali kuwawajibisha Makamanda wa Polisi
wa Mikoa ya Morogoro na Iringa kwa kusimamia mauaji ya raia wasio na hatia
lakini mpaka leo wanafurahia maisha kana kwamba hakuna kilichotokea.
Mheshimiwa Spika,
Waziri Mkuu ndiye Kiongozi Mkuu wa shughuli zote za Serikali. Ofisi ya Waziri
Mkuu ndiyo daraja kati ya Serikali Kuu na wananchi. Ni dhahiri kuwa Waziri Mkuu ndiye mtunza
nidhamu na uwajibikaji mkuu katika Taifa hili. Ni nafasi ya uongozi
inayostahili kuwa tayari kupokea lawama katika kufanya maamuzi magumu. Ni
nafasi inayohitaji uwezo wa kufanya maamuzi hayo mazito na kwa wakati kwa
maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, kwa
idadi ya makosa ya kizembe yanayotokea katika nchi hii, na jinsi viongozi
kadhaa wa serikali hii wasivyowajibika tena kwa kubeza na kukejeli malalamiko
ya mara kwa mara ya wananchi; kitendo cha Waziri Mkuu kukaa kimya wakati mwingi bila
kutumia rungu lake la madaraka kulitetea au kuliokoa Taifa ni kigezo tosha cha
kutafakari kama upole nauungwana wa Waziri Mkuu leo ni tija au fedheha kwa
Taifa?
Mheshimiwa Spika,
napenda nimkumbushe Waziri Mkuu kwamba, Ofisi yake inategemewa sana kwa mustakabali wa maisha ya Watanzania.
Kwa misingi hiyo, Waziri Mkuu hana budi kuwa mstari wa mbele katika kujibu kero
na matatizo ya wananchi kwa haraka kuliko ilivyo sasa.
Mheshimiwa Spika,
bado taifa liko katika msiba mzito uliosababishwa na kuporomoka kwa ghorofa
katikati ya Jiji la Dar Es Salaam .
Ofisi ya Waziri Mkuu imekalia kwa muda mrefu bila kuchukua hatua stahiki ripoti
kadhaa zilizotahadharisha kuhusu ujenzi holela wa maghorofa katika nchi yetu.
Mbali na waliopelekwa mahakamani, hakuna waliochukua hatua ya kuwajibika
kisiasa / kiutendaji. Hili ni janga kuu na ishara ya watendaji na viongozi
wengi wa Serikali kutokutambua kuwa nafasi zao za kazi ni dhamana waliyonayo
kwa niaba ya Umma.
Mheshimiwa
Spika, si nia yangu
kutangaza mgogoro na Serikali kwa tabia hii ya kutowajibika, lakini napenda
kuiasa Serikali kwamba kwa tabia hii inajitangazia mgogoro yenyewe na
wananchi. Hili si jambo zuri kwani
uvumilivu wa wananchi utakapofikia ukomo, Serikali isishangae kuona nguvu ya
umma ikitumika kuwawajibisha viongozi wanaong’ang’ania madaraka huku wakiwa
hawana sifa na weledi wa kufanya kazi za umma. Aidha, naomba kuwataka wananchi
wasiendelee kutegemea “muujiza wa uwajibikaji” hivyo watafakari wenyewe uwezo
walio nao kuchukua hatua muda muafaka ukifika.
5.0 DENI LA TAIFA
Mheshimiwa Spika,
Mwaka 2012
takwimu zinaonyesha kuwa deni la taifa limeongezeka kwa asilimia 15.2. Ndani ya
mwaka mmoja wa fedha kutoka shilingi bilioni 18,258.62 Desemba 2011 na kuwa
shilingi bilioni 21,028.61 Desemba 2012 . Kati ya hizo deni la nje lilikuwa ni
asilimia 75.97 na sababu inayotolewa kuwa ndiyo chanzo cha kuongezeka kwa deni hili kwa kasi namna hiyo
ni pamoja na mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu
hususani ya Barabara na Umeme na malimbikizo ya riba .
Mheshimiwa Spika,
Kambi
Rasmi ya Upinzani inamtaka Waziri Mkuu
ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali
alieleze Bunge hili ni utaratibu gani
uliotumika nje ya Bunge kuchambua na kuithinisha matumizi hayo kwani bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa ajili ya
miradi ya barabara ilikuwa ni shilingi trilioni 1, na bajeti nzima ya nishati
ilikuwa shilingi bilioni 502 ( bajeti
2012/2013) ilhali mkopo huu ulio katika deni la Taifa ni zaidi ya shilling
trilioni 3? Ni miradi gani mikubwa hivyo ya barabara na umeme ambayo
iligharimiwa na fedha hizo kama kweli
zilikopwa kwa ajili ya kuhudumia miradi hiyo.
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Taarifa
ya tume ya mipango iliyowasilishwa kwenye kamati ya Bunge zima na Waziri
Stephen Wassira inaonyesha kuwa barabara zilizojengwa kwa kipindi hicho ni
kilomita 170.6 ikilinganishwa na lengo na bajeti iliyopitishwa na Bunge ya
kujenga kilomita 414 kwa mwaka 2012/2013 kwa barabara kuu kwa kiwango cha lami,
hii ikiwa ni sawa na asilimia 41.2 tu ya lengo lililokuwa limepangwa .
Aidha
ukarabati uliofanyika kwa barabara kuu ulikuwa kilomita 64.57, ikilinganishwa
na lengo la kukarabati kilomita 135 kwa mwaka 2012/2013 na kwa upande wa ujenzi
na ukarabati wa barabara zinazounganisha Mikoa na Wilaya ni ujenzi wa kilomita
8.2 tu ndio umekamilika ukilinganisha na lengo la kujenga kilomita 31.9 kwa
mwaka kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa ukarabati ni kilomita 99.45 tu
zilikarabatiwa ikilinganishwa na lengo la kilomita 573.6 zilizokuwa zimepangwa
kufanyiwa ukarabati ( chanzo: taarifa ya ofisi ya rais tume ya mipango).
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Aidha
kwa upande wa miradi ya umeme ambayo ilitekelezwa ni pamoja na maandalizi kwa
ajili ya ujenzi wa bomba la gesi ambayo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kulipa
fidia wanakijiji wapatao 3,092 na kwa upande wa mradi wa mgodi wa makaa ya mawe
Kiwira kwa ajili ya kuzalisha MW 200 ni stahiki za wafanyakazi kulipwa pamoja
na sehemu tu ya madeni ya CRDB, NSSF na PSPF ndio viliweza kulipwa.
Ni wazi kuwa taarifa hizi mbili yaani ya Waziri wa fedha na ile ya Tume ya mipango inaonyesha wazi kuwa kuna tatizo kubwa kuhusiana na suala la deni la Taifa, kwani upande mmoja unasema fedha hizo zilikopwa kwa ajili ya miradi ya umeme na barabara wakati upande wa tume ya mipango unaonyesha wazi kuwa hakuna miradi kama hiyo iliyoweza kutekelezwa kwa kipindi hicho.
Mheshimiwa Spika,
Ni wazi kuwa taarifa hizi mbili yaani ya Waziri wa fedha na ile ya Tume ya mipango inaonyesha wazi kuwa kuna tatizo kubwa kuhusiana na suala la deni la Taifa, kwani upande mmoja unasema fedha hizo zilikopwa kwa ajili ya miradi ya umeme na barabara wakati upande wa tume ya mipango unaonyesha wazi kuwa hakuna miradi kama hiyo iliyoweza kutekelezwa kwa kipindi hicho.
Mheshimiwa Spika,
Taarifa
ya serikali inaonyesha kuwa hakuna kitengo / idara ya madeni na sasa ndiyo
serikali ipo kwenye mchakato wa kuanzisha idara ya madeni ambayo pamoja na mambo
mengine itakuwa na jukumu la kujenga uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu na
kuhakikisha usimamizi madhubuti wa deni la Taifa. (Chanzo: Taarifa ya Waziri wa
fedha juu ya mwongozo, matazamio na upeo wa bajeti ya serikali kwa Bunge
2013/2014, tarehe 25 machi 2013)
Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Spika,
Kambi
Rasmi ya Upinzani inamtaka Mhe Waziri Mkuu alieleze Bunge kwa kuwa haikuwepo
idara kwa ajili ya uchambuzi juu ya mikopo hii, nani alikuwa anahusika na kusimamia
ukopaji huu na hasa kuhusiana na riba kwani katika taarifa hiyo takwimu
zinaonyesha kuwa fedha iliyolipwa kwa ajili ya deni la nje kama riba tu
ilikuwa kiasi cha shilingi bilioni 66.1 wakati deni halisi tulilipa kiasi cha
shilingi bilioni 35.5 na hivyo tulilipa jumla
ya shilingi bilioni 101.56 kwa deni hilo.
Aidha
kwa upande wa deni la ndani tulilipa kiasi cha shilingi bilioni 1,044.85 na
kati ya fedha hizo tulilipia riba ya kiasi cha shilingi bilioni 210.7 tu.
Je, riba halisi kwa ajili ya mikopo hiyo tuliyochukua ilikuwa ni kiasi gani kwa mwaka? Na je madeni mapya riba yake iko kiasi gani kwa mwaka? Na ni kitengo gani kilihalalisha uchukuaji huu wa mikopo hiyo. Ni vyema sasa taarifa rasmi ya madeni ya Taifa yawe yanawekwa hadharani kwani kuna hisia ya kuwepo ufisadi wa kutisha kupitia akaunti ya madeni ya njekama
ilivyokuwa EPA.
Je, riba halisi kwa ajili ya mikopo hiyo tuliyochukua ilikuwa ni kiasi gani kwa mwaka? Na je madeni mapya riba yake iko kiasi gani kwa mwaka? Na ni kitengo gani kilihalalisha uchukuaji huu wa mikopo hiyo. Ni vyema sasa taarifa rasmi ya madeni ya Taifa yawe yanawekwa hadharani kwani kuna hisia ya kuwepo ufisadi wa kutisha kupitia akaunti ya madeni ya nje
6.0 GESI ASILIA
Mheshimiwa Spika;
Waziri
Mkuu akiwa ndiye msimamizi na mdhibiti wa shughuli za kila siku za Serikali
ndani na nje ya Bunge, anapaswa kutoa maelezo kuhusu hali inayoendelea hivi
sasa katika sekta ndogo (sub sector) muhimu kwa nchi yetu ya gesi asili kuhusu
mazungumzo yanayoendelea na makampuni mbalimbali ya kimataifa na mikataba
inayozidi kusainiwa huku kukiwa na ombwe la kisera na udhaifu wa kiuongozi
katika sekta hizo nyeti hali ambayo itakuwa na athari za muda mrefu sana kwa
taifa.
Mheshimiwa Spika;
Mpaka
sasa kwa mfano nchi haina sera ya gesi asili huku sera ya nishati ikiwa
imepitwa na wakati, lakini mazungumzo yanaendelea na mikataba inazidi kusainiwa
bila kuwa na mfumo thabiti wa kuhakikisha kwamba rasilimali za nchi
zinanufaisha wananchi wa maeneo husika kwa ridhaa yao .
Aidha,
kumekuwepo na ufisadi kama ambavyo ulielezwa pia katika taarifa iliyowasilishwa
bungeni Novemba 2011 ambayo msingi wake ulikuwa pia madai ya Kambi ya Upinzani
ya Julai 2011; hata hivyo mpaka sasa
sehemu kubwa ya maazimio ya Bunge toka wakati huo mpaka sasa hayajatekelezwa
kwa ukamilifu.
Wakati
ufisadi huo ukiwa haujashughulikiwa, yameibuka madai mengine ya kasoro katika
mkopo wa ujenzi wa Bomba la gesi, huku kukiwa pia na tuhuma za usiri katika
mkataba huo ikiwemo kuhusu dhamana na masharti mengine yaliyoko kwenye mikataba
ya ujenzi wa bomba husika.
Mheshimiwa Spika:
Kutokana
na hali hiyo mwezi Februari 2013 katika maswali ya papo k wa papo bungeni,
niliuliza swali kwa Waziri Mkuu iwapo
mikataba hiyo sasa inaweza kutolewa kwa bunge na kwa wabunge na kuahidi kwamba
wabunge wanaweza kupata nakala hiyo kwa kufuata masharti ya Sheria naomba
ninukuu kauli yake “ serikali imekwisha kubali kwamba, Bunge hili
linayo fursa ya kupata mkataba wowote, kubwa ni kufuata utaratibu kupitia ofisi
ya spika”
Kambi
Rasmi ya Upinzani kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini alitumia
sheria ya kinga, haki na madaraka ya Bunge kuomba kuona nakala ya mkataba wa
ujenzi wa bomba husika ili kutekeleza wajibu wa kibunge wa kuishauri na
kuisimamia Serikali lakini toka wakati huo mpaka sasa mikataba hiyo imeendeelea
kufanywa kuwa ni siri hata kwa wabunge.
Hata
baada ya mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania na Rais wa China masuala hayo
yameendelea kufanywa kuwa siri; hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani kupitia Bunge
hili inaitaka Serikali kuweka wazi masharti ya mikopo na dhamana zinazohusika
kwa kuzingatia kwamba mwelekeo unaonyesha kuwa miradi ya chuma na makaa ya mawe
ya Mchuchuma na Liganga imetumika kama sehemu ya mpango wenye kuacha maswali
mengi kuhusu unyonyaji wa rasilimali za taifa katika sekta hizo muhimu.
Mheshimiwa Spika:
Udhaifu
huo unapaswa kurekebishwa kwa kuongeza jitihada za kutekeleza ahadi za
kuhakikisha kwamba matumizi ya gesi
katika viwanda vya mbolea, viwanda vya bidhaa za kemikali zinazotokana na
mafuta (petrochemicals), saruji na uzalishaji wa umeme katika mikoa ya Mtwara,
Iringa, Ruvuma, Dar es Salaam
na maeneo mengine yanayohusika.
Pamoja
na Serikali kuingia makubiliano ya awali (MOU) na Kampuni ya kutoka nchini
Marekani ya Symbion kuhusu uzalishaji wa umeme mkoani Mtwara, ieleze pia hatua
ilizochukua katika kurekebisha kasoro zilizopo kwenye miradi ya Mchuchuma na
Liganga na Mnazi Bay kwa kuzingatia ahadi ilizotoa mwaka
2004.
Mheshimiwa Spika;
Kambi
Rasmi ya Upinzani pamoja na kutaka maelezo zaidi na vielelezo vya ziada kuhusu
utekelezaji wa ujenzi wa bomba la gesi na matumizi ya gesi; inatoa mwito kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania kwa ujumla kufungua
mjadala mpana zaidi wa kitaifa kuhusu gesi kwa kujikita katika suala la ubovu
wa sera ya gesi na mchakato unaoendelea hivi sasa kuhusu rasimu ya sera hiyo na
uozo wa mikataba kwenye utafutaji, uvunaji na usafirishaji wa gesi.
Serikali
badala ya kuendelea kukimbilia kusaini mikataba mipya kuhusu utafutaji wa gesi
asili na mafuta ishughulikie kwanza ubovu wa mikataba ya utafutaji wa mafuta na
gesi kuweka hadharani ripoti ya uchunguzi kuhusu mikataba 26 ambayo ilikamilika
tangu mwaka 2012 na kueleza hatua ambazo zimechukuliwa toka wakati huo.
Hatua
hii ni muhimu kwa kuwa toka kusomwa kwa orodha ya mafisadi (list of shame )
tarehe 15 Septemba 2007 mpaka sasa yamekuwa yakitolewa madai mbalimbali kuhusu
baadhi ya viongozi na watendaji kutuhumiwa kufanya ufisadi kupitia mikataba ya
utafutaji na uvunaji wa gesi asili, utafutaji wa mafuta na uchimbaji wa madini
na kufichwa kwa fedha katika akaunti za nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika:
Ziara
ya Rais wa China
ambayo ilihusisha usiri katika kusainiwa kwa mikataba 17 ya Sekta mbalimbali
imedhihirisha kwa vitendo kwamba Serikali inayoongozwa na CCM isivyo na dhamira
ya kutekeleza maazimio ya Bunge kuhusu usimamizi wa kibunge kwenye michakato ya
mikataba.
Wabunge
na wananchi wakumbuke kwamba mwaka 2008 kufuatia kashfa ya Richmond , Bunge lilipitisha azimio kwamba
kamati za kisekta za Bunge zihusishwe kwa niaba ya wananchi kwenye maandalizi
ya mipango na mikataba kuanzia hatua za awali ili kuishauri na kuisimamia
Serikali; azimio ambalo halitekelezwi na hivyo kuibua migogoro kati ya wananchi
na wawekezaji na maeneo mengine kufanya nchi kuingia mikataba mibovu.
Mathalani,
wakati Tanzania imekopa
mkopo mkubwa kutoka China
kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la gesi; miaka michache iliyopita kutokana na udhaifu
wa mipango na mikataba ulifanyika ujenzi wa Bomba lingine kutoka Songosongo
chini ya kampuni ya Songas kwa mkopo. Hata hivyo, katika mradi huo kulijengwa
bomba lenye kipenyo kidogo na matokeo yake ni kwamba miaka michache baadaye
taifa linaingia gharama kubwa ya mkopo mwingine kutokana na upungufu wa
miundombinu ya gesi asili huku kukiwa na mzigo wa madeni makubwa ya mikopo ya
awali. Serikali inapaswa kutoa maelezo kuhusu hatua ilizochukua kurekebisha
hali hiyo toka wakati huo na kuhakikisha uwajibikaji wa viongozi na watendaji
waliohusika ambapo wengine mpaka sasa bado wako katika ofisi za umma.
7.0 BUNGE KAMA
MUHIMILI WA KUISIMAMIA NA KUISHAURI SERIKALI
Mheshimiwa
Spika, mamlaka ya Bunge yameainishwa
katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara za 62 hadi 64. Ibara hizi zote
zinaeleza majukumu ya Bunge juu ya kusimamia utendaji mzima wa Serikali katika
mchakato wa kuwapatia huduma za msingi wananchi.
Mheshimiwa
Spika, jukumu hili kwa hali ilivyo sasa
linashindwa kutekelezeka kutokana na ukweli kwamba Bunge linakosa taarifa au
uelewa wa kutosha kuhusu sekta mbalimbali za kiutendaji. Kwa hali ya kawaida ni
vigumu kumshauri au kumsimamia mtu bila ya kuwa na uelewa wa ziada kumzidi yule
unaye mshauri au kumsimamia.
Mheshimiwa
Spika, ili kukidhi matakwa ya Ibara ya
64 ni lazima Kurugenzi husika ndani ya Bunge kuwezeshwa kuwa na watendaji
wanaoweza kuwasaidia waheshimiwa wabunge kutimiza matakwa ya Ibara hiyo.
Mheshimiwa
Spika, sambamba na hilo, Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka kuelewa toka kwa Mhe Waziri Mkuu, Miswada binafsi ya
waheshimiwa wabunge Zitto Kabwe uliohusu mabadiliko ya sheria ya maadili ya
viongozi na John Mnyika uliohusu uanzishwaji wa baraza la vijana la Taifa
ambayo tayari imekwishawasilishwa Ofisini kwa Katibu wa Bunge ni lini italetwa
rasmi Bungeni kwa utaratibu wa kuzifanya ziwe sheria za nchi?
Mheshimiwa
Spika, Katika hotuba yangu ya mwaka
jana nilieleza kuhusu Watendaji wa Serikali kushindwa kutimiza masharti ya
kifungu cha 10 cha sheria ya Haki na Madaraka ya Bunge mwaka 1988 na marejeo
yake ya mwaka 2002. Hali ya kutokuheshimu sheria hii bado inaendelea,
Waheshimiwa wabunge wameomba kupatiwa nyaraka mbalimbali toka Serikalini
kupitia kwa Katibu wa Bunge, lakini kwa bahati mbaya hadi sasa nyaraka hizo
bado hazijatolewa.
Mheshimiwa Spika, katika hali kama
hii, je Bunge linaweza kukidhi matakwa ya Ibara za 63? Utaishauri vipi na
kuisimamia Serikali ukiwa huna taarifa za kutosha? Je, ni mara ngapi
waheshimiwa Mawaziri wametoa majibu ya kudanganya na kupelekea waheshimiwa
wabunge kukiambia kiti kuwa Waziri hajajibu swali lake? Mapungufu haya yote
yanasababishwa na kutokuwepo kwa taarifa sahihi na za ziada kuwawezesha
waheshimiwa wabunge kufanyakazi ili kukidhi matakwa ya Kikatiba.
Mheshimiwa
Spika, Katika moja ya
taarifa za asasi za kiraia zinazofuatilia mwenendo wa Bunge, pamoja na mambo
mengine zimeonesha kuwa Bunge letu ni dhaifu na kuwa halitekelezi majukumu
yake. Taarifa za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
na The Citizens’ Parliament Watch (CPW) za Februari 13, 2013 zimeonesha kuwa
“…kumeendelea kuwa na mivutano yenye upendeleo wa vyama
katika kujadili na kuchangia hoja na kuonekana Mh Spika, Naibu Spika na
Wenyeviti wa vikao kutumia vibaya kanuni za Bunge kuwadhibiti Wabunge kulingana
na vyama vyao. Ukiukwaji wa Kanuni za Bunge, matumizi mabaya ya muda na kukosa
tija kumeendelea kuliathiri Bunge letu. Aidha baadhi
ya Wabunge wamekuwa na matumizi ya lugha zisizostahili Bungeni na hata
kushambuliana katika ubinafsi wao. Wakati wabunge wengine wakitumia muda wao nje ya Bunge
kukutana na wananchi na kueleza ufanisi wao ndani ya Bunge, wengine wametumia
nafasi hizo kupingana na wananchi na kulidhalilisha Bunge mbele ya jamii”.
Mheshimiwa Spika, Asasi hizi zinatukumbusha mambo muhimu sana kwa jamii yetu. Tuna
kila wajibu wa kuwatendea haki watu wetu na kutafakari taarifa zinazotupima
utendaji wetu na kuchukua hatua kurekebisha udhaifu huu.
8.0 MAMBO
MUHIMU YA KUKUMBUSHA
Mheshimiwa
Spika, mara kadhaa, Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA imekuwa ikiitaka Serikali kutekeleza
mambo ya msingi katika usitawi na maenedeleo ya Taifa hili lakini kwa
masikitiko makubwa ni kwamba Serikali hii ya CCM inayojiita sikivu imeendelea
kuziba masikio yake juu ya mahitaji muhimu kwa Taifa.
Kwa mfano, Kambi Rasmi ya Upinzani ilitoa pendekezo
zuri la kuwapatia wazee wote pensheni (Universal Pension) sambamba na kuwa na
mpango maalum wa kuwawezesha wazee wetu hawa kuishi maisha ya amani katika siku
zao za uzeeni.
Licha ya Kambi ya Upinzani kuonesha njia ya kupata
fedha za kuwalipa wazee hawa, lakini mpaka leo Serikali imekuwa na kigugumizi
cha kutekeleza nia hii njema. Jambo hili linapelekea Kambi ya Upinani iamini
kwamba Kauli aliyoitoa Waziri Mkuu, tarehe 01 Oktoba, 2009 wakati akiwahutubia
wazee kwamba: “Wazee ni rasilimali na
hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu na kuleta mabadiliko ya
kiuchumi” ilikuwa ni kuwakejeli na kuwahadaa wazee waliovuja jasho kuijenga
nchi hii hadi hapa ilipo. Kambi ya
Upinzani inaitaka Serikali ieleze ukweli ili wazee hawa wajue kama
Serikali imeamua kuwatupa wajitafutie utaratibu mwingine wa maisha.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni imekuwa ikipiga kelele sana
juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma unaofanywa na Serikali kwa kisingizio
cha uendeshaji wa shughuli za Serikali.
Limekuwa ni jambo la kawaida kwamba katika bajeti ya Waziri Mkuu, na
wizara nyingine, fedha za matumizi ya kawaida ni takribani asilimia 80 wakati
fedha za maendeleo ni ni takriban asilimia 20 tu. Jambo la kushangaza hapa ni
kwamba hata hii asilimia 20 ya fedha za maendeleo, zaidi ya nusu zinatoka kwa
wahisani. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali iueleze umma wa watanzania:
Kipi ni kipaumbele; kutumia fedha za walipa kodi wa Tanzania kwa matumizi ya ofisi, au
kuwaletea wananchi maendeleo?
Aidha ni vyema Serikali ikaeleza Taifa ni njia gani
inatumia kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwani kila siku tunaona kukua kwa
kutisha kwa matumizi ya kawaida ya Serikali. Ni dhahiri hakuna uchungu na fedha
za walipa koda kwa Serikali hii ya CCM.
Mheshimiwa
Spika, Jambo jingine ambalo
Kambi Rasmi ya Upinzani ingependa kuikumbusha Serikali ni kuhusu Sherehe za
Kitaifa. Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukihoji matumizi yasiyofanyiwa ukaguzi
ya sherehe za kitaifa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuweka bayana
matumizi ya fedha katika Sherehe za kitaifa kuwa kuwa fedha inayotumika ni
fedha ya wananchi.
Mheshimiwa
Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni inaikumbusha tena Serikali kusema ukweli kuhusu dhamira ya
kuhamia Dodoma .
Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri tena Serikali kufuta mpango huu kwani ni
upotezaji wa fedha za wananchi na fedha zinazopotezwa zielekezwe kwenye mipango
mingine ya maendeleo na Dodoma iendelee kuwa mji wa Kibunge na Elimu
kama ambavyo Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwa ikishauri kila wakati.
9.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI 2012/2013 NA UCHAMBUZI WA
BAJETI YA 2013/2014
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka wa fedha 2012/2013, Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake
iliidhinishiwa kiasi cha shilingi bilioni 35.2 ikiwa ni matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 3.4
ilikuwa ni mishahara ya watumishi, shilingi bilioni 10.6 ikiwa ni ruzuku kwa
taasisi, na shilingi bilioni 21.1 matumizi mengineyo. Hadi kufikia Februari
2013, shilingi bilioni 20.7 sawa na asilimia 59 zilikuwa zimepokelewa kutoka
hazina.
Mheshimiwa Spika,
kwa upande wa Miradi ya Maendeleo, Ofisi ya Waziri Mkuu ilitengewa shilingi
bilioni 91.7 lakini hadi kufikia Februari, 2013 ni kiasi cha shilingi bilioni
10.7 sawa na asilimia 11.7zilizokuwa
zimetumika katika miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Spika,
kwa mchanganuo huo ni kwamba fedha za matumizi ya kawaida zinatumika zaidi
kuliko fedha za maendeleo. Aidha, karibu
asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo, Ofisi ya Waziri Mkuu haikutekelezwa hadi
kufikia Februari 2013.
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Waziri Mkuu atoe majibu kuwa inawezekanaje
hadi kufikia “quota” ya 3 ya mzunguko wa bajeti, asilimia 90 ya bajeti ya maendeleo
haijatekelezwa?
Mheshimiwa Spika,
Kwa mwaka huu 2013/2014 Ofisi ya Waziri Mkuu inaomba kuidhinishiwa shilingi
bilioni 35.08 kwa matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 43.87 kwa bajeti ya
maendeleo. Wakati matumizi ya kawaida yamepungua kwa asilimia 0.34
ukilinganisha na mwaka 2012/2013, bajeti ya maendeleo imepungua kwa asilimia 52.2
ukilinganisha na mwaka 2012/2013.
Mheshimiwa Spika,
licha ya bajeti ya maendeleo kupungua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na mwaka
jana bado imeendelea kuwa tegemezi kwa wahisani. Katika shilingi bilioni
43.87 za maendeleo, shilingi bilioni
37.87 sawa na asilimia 86.3 ni fedha za nje na shilingi bilioni 6 sawa na
asilimia 13.7 ni fedha za ndani.
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani haiamini kama tunaweza
kupata maendeleo ya kweli kwa kutegemea fedha za wahisani katika bajeti za
maendeleo.
Mheshimiwa Spika, katika
miradi ya meaendeleo imetengwa shilingi
bilioni moja kwa ajili ya uendelezaji wa kuzikia viongozi wa Kitaifa. Kambi
ya Upinzani inataka kujua kama ni ombi la
viongozi wa kitaifa kuandaliwa eneo maalumu la kuzikwa au ni utashi wa Serikali
kufikiri kwamba viongozi wa kitaifa wanahitaji eneo maalumu la kuzikwa!
Kwa
uzoefu ni kwamba waasisi wa Taifa hili walizikwa kwenye makazi yao . Kwa nini viongozi wa kitaifa walio hai
sasa wasifuate mfano huo? Hivi kweli kuna mantiki yoyote ya kutumia shilingi
bilioni moja ya kuandaa sehemu ya kuzikia watu ambao hawajafariki wakati kuna
watu wenye njaa, wagonjwa, wamama wajawazito wanaojifungulia sakafuni ambao wanahitaji
huduma ya matibabu na dawa ili wapone?
Mheshimiwa Spika,
katika bajeti ya maendeleo, Kitengo cha Maafa kimetengewa shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kujenga uwezo wa kukabiliana na
maafa. Mheshimiwa Spika, Watanzania wameshuhudia maafa makubwa katika nchi yetu
hasa ya kuzama kwa Meli kwa mfano Meli ya MV Bukoba, Meli ya MV Skagit na Meli
ya MV Spice Islanders huko Zanzibar
na pia wameshuhudia kuporomoka kwa maghorofa na mengine kuungua moto. Katika
ajali na maafa haya Watanzania wengi walipoteza maisha yao na daima waokoaji wa
ndani wamekuwa na uwezo mdogo sana wa kuokoa watu na hivyo kutegemea zaidi
waokoaji na vifaa toka nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kuwa fedha hizi ni ndogo na hivyo ni vyema
Serikali ieleze uwezo huo unaokusudiwa kujengwa ni upi!
Mheshimiwa
Spika, katika kupunguza
gharama za uendesha wa shughuli za Serikali,
Kambi ya Upinzani imekuwa ikipinga matumizi mabaya ya fedha za umma na hasa
posho za vikao (sitting allowances) kwa kuwa vikao ni sehemu ya majukumu yao ambayo wanalipwa
mshahara. Kambi Rasmi ya Upinzani inazidi kusisitiza kuwa posho za vikao zifutwe
kwani zinaongeza gharama za uendeshaji wa Serikali ambazo si za lazima.
Jedwali lifuatalo linaonesha tofauti ya posho za
vikao katika kasma 210314 kwenye Fungu 37 kwa idara zilizo Ofisi ya Waziri Mkuu kati ya
mwaka wa bajeti 2012/2013 na 2013/2014.
Chanzo:
Randama Ofisi ya Waziri Mkuu, Fungu 37
KASMA
|
IDARA
|
POSHO YA VIKAO-
2012/2013
|
2013/2014
|
210314
|
Utawala
|
95,000,000
|
92,000,000
|
Fedha
na Uhasibu
|
20,250,000
|
8,850,000
|
|
Sera
na Mipango
|
31,500,000
|
19,950,000
|
|
Ukaguzi
wa Ndani
|
17,400,000
|
17,400,000
|
|
Habari,
Elimu na Mawasiliano
|
3,000,000
|
3,000,000
|
|
Ugavi
|
20,000,000
|
42,000,000
|
|
Sheria
|
1,500,000
|
1,200,000
|
|
Menejimenti
ya Mifumo ya Habari
|
800,000
|
600,000
|
|
Uratibu
wa Maafa
|
39,000,000
|
39,000,000
|
|
Maadhimisho
ya Sherehe za Kitaifa
|
47,000,000
|
47,000,000
|
|
Bunge
na Siasa
|
15,000,000
|
16,000,000
|
|
Maendeleo
ya Sekta Binafsi
|
24,000,000
|
43,500,000
|
|
Uratibu
wa Shughuli za Serikali
|
100,500,000
|
61,500,000
|
|
Mpiga
Chapa wa Serikali
|
55,100,000
|
53,000,000
|
|
470,050,000
|
445,000,000
|
||
Tofauti
kati ya matumizi ya mwaka wa fedha 2012/13 na 2013/14 ni shilingi 25,050,000/-
Mheshimiwa Spika,
Baada ya maelezo haya naomba
kuwasilisha.
......................................................................
FREEMAN
AIKAELI MBOWE (MB)
KIONGOZI
WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI
MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU
11.04.2013
KIAMBATANISHO A
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA
WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA YA UTAFITI
KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA
UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO
CHA 4 MWAKA 2010
Juni, 2011
Rasimu 2
i
SHUKRANI
Utafiti
huu umehusisha wataalamu mbalimbali katika hatua za kubuni, kutayarisha,
kukusanya,
kuchambua takwimu na kuandika ripoti. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi
kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kwa
pamoja zinawashukuru wataalamu wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine
katika
hatua mbalimbali za utafiti huu. Pia tunawashukuru wadau wote wa elimu
waliohusika
katika kutoa taarifa za utafiti. Aidha shukrani za pekee ziiendee Wizara ya
Fedha
kwa kufanikisha mchakato mzima wa utafiti.
Shukrani
pia zimwendee Bwana Jumanne Abdallah Sagini, Naibu Katibu Mkuu -
TAMISEMI
kwa kuwa msimamizi mkuu wa kazi hii. Aidha, shukrani za dhati ziwaendee
wajumbe
wa kikundi kazi kilichohusika katika utafiti huu kuanzia hatua za awali hadi
mwisho.
Wajumbe hao ni:
JINA
TAASISI WADHIFA
1.
Francis M. Liboy OWM-TAMISEMI - Mwenyekiti
2. Lawrence John Sanga WEMU
- Katibu
3. Fred
Davidson Sichizya WEMU - Mjumbe
4.
Abdallah Shaban Ngodu WEMU - Mjumbe
5.
Hadija Mchatta Maggid WEMU - Mjumbe
6.
Paulina Jackson Mkoma WEMU - Mjumbe
7. Elia
Kalonzo Kibga WEMU - Mjumbe
8.
Paulina Mbena Nkwama OWM-TAMISEMI - Mjumbe
9.
Makoye J.N. Wangeleja TET - Mjumbe
10.Edward
Simon Haule NECTA - Mjumbe
Aidha
shukrani zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa TET kwa kugharamia vikao vya kikundi
kazi
kupitia huduma ya ukumbi na chakula wakati kikiwa Dar-es-salaam.
Prof.
Hamisi O. Dihenga
Katibu
Mkuu
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Rasimu 2
ii
DIBAJI
Ripoti
hii ya utafiti inahusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa
Kidato
cha 4
mwaka 2010. Utafiti huu umefanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu-
Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya
Ufundi (WEMU) ikihusisha Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani la
Utafiti
huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa
Taifa
wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri kwa
wadau
wa elimu Serikali iliamua kufanya utafiti ili kuweza kubaini chanzo na ukubwa
wa
tatizo.
Utafiti huu unatoa mapendekezo kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu na ubora wa
elimu
ya sekondari.
Ripoti
hii inaonesha kwamba yapo masuala ya kimfumo, mfano mapungufu katika
usimamizi
na uendeshaji wa elimu nchini ambayo yanaweza kutatuliwa na serikali moja
kwa
moja. Aidha, yapo masuala yanayohusu kujenga uwezo kwa wasimamizi na
watekelezaji
wa mitaala, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora na vya kutosha vya
kufundishia
na kujifunzia na uboreshaji wa majengo na miundombinu ambayo
yanahitaji
nguvu ya pamoja kati ya serikali na wabia wake.
Matokeo
ya utafiti huu ni muhimu kwa serikali, washirika wa maendeleo na wadau
mbalimbali
wa elimu kwani inaonesha chanzo na ukubwa wa matatizo na changamoto
zinazojitokeza
na inatoa mapendekezo ya namna ya kuyatatua na kukabiliana na
changamoto
za kielimu. Hivyo sote kwa pamoja yatupasa tujipange na kuelekeza nguvu
zetu
kupitia mipango yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili tuweze
kuyamaliza
matatizo haya na kuinua ubora wa elimu nchini.
Ninawaomba
wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza
kupiga
hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo
nia ya
dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa
elimu
ya
sekondari nchini.
Mh.
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Rasimu 2
iii
YALIYOMO
SHUKRANI............................................................................................................................................
i
DIBAJI...................................................................................................................................................
ii
VIFUPISHO...........................................................................................................................................
v
MUHTASARI
PEMBUZI.....................................................................................................................
vi
SURA
YA KWANZA :
UTANGULIZI................................................................................................
15
1.1.
Usuli ......................................................................................................................................
15
1.2.
Hoja ya Kufanya Utafiti .......................................................................................................
18
1.3.
Malengo ya Utafiti................................................................................................................
19
1.4.
Maswali ya Utafiti.................................................................................................................
19
1.5.
Muundo wa Ripoti................................................................................................................
20
SURA
YA PILI: MAPITIO YA
MAANDIKO....................................................................................
21
2.1
Sera na Mipango ya Elimu..................................................................................................
21
2.2
Mipango na Mikakati ya Elimu ...........................................................................................
22
2.3
Uongozi katika Elimu ...........................................................................................................
23
2.4
Usimamizi na Uendeshaji....................................................................................................
24
2.5
Ugharamiaji wa Elimu .........................................................................................................
25
2.6
Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu........................................................................................
27
SURA
YA TATU: MWONGOZO WA
UTAFITI...............................................................................
55
3.1.
Utangulizi ..............................................................................................................................
55
3.2.
Mbinu ya Utafiti ....................................................................................................................
55
3.3.
Eneo la Utafiti .......................................................................................................................
56
3.4.
Uchaguzi wa Sampuli ..........................................................................................................
56
3.5.
Zana za Utafiti ......................................................................................................................
57
3.6.
Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti ................................................................................
58
3.6.1.
Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya Taifa ................................................................
58
3.6.2.
Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na Halmashauri ..........................
58
3.6.3.
Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika Jamii.................................................
59
3.7.
Uchambuzi wa Data.............................................................................................................
59
3.8.
Maadili ya Kufanya Utafiti...................................................................................................
59
SURA
YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA
DATA................................... 61
4.1.
Utangulizi ..............................................................................................................................
61
4.2. Usimamizi
na Uendeshaji wa Elimu ..................................................................................
63
4.2.1.
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali.................................
63
4.2.2.
Mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii......................................................................
68
4.2.3.
Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu........................................................................
69
4.2.4.
Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya Kielimu.......................................................
69
4.2.5.
Ufinyu wa Bajeti ya Elimu ...........................................................................................
70
4.2.6.
Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu .................................................
71
4.2.7.
Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka
2010 75
4.3.
Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala .............................................................................
76
4.3.1.
Utayarishaji wa Mitaala................................................................................................
76
Rasimu 2
iv
4.3.2.
Uwepo wa Mihtasari Shuleni na Vyuoni....................................................................
77
4.3.3.
Utekelezaji wa Mtaala ..................................................................................................
78
4.3.4.
Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala Ulioboreshwa ...............................................
79
4.3.5.
Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala ........................................................................
79
4.4.
Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa...........................................................................
80
4.4.1.
Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 .......................................................
80
4.4.2.
Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4..........................
82
4.4.3.
Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4 ..................................................
83
4.4.4.
Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-CA)
Katika
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4................................................................................
85
4.4.5.
Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTA .......................................................
86
4.4.6.
Matumizi ya Miongozo na Nyaraka Mitihani .............................................................
88
4.4.7.
Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2............................................................
88
4.4.8.
Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa .........................................
90
4.5.
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ...................................................
93
4.6.
Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu...............................................................
97
4.6.1.
Mfumo wa Utayarishaji wa
Walimu...............................................................................
97
4.6.2.
Ajira na Upangaji wa Walimu .....................................................................................
98
4.6.3.
Uwepo wa Walimu katika Shule
..................................................................................
100
4.6.4.
Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa Walimu ..............................................
106
4.7.
Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia ........................................................
108
SURA
YA TANO: HITIMISHO NA
MAPENDEKEZO..................................................................
115
5.1.
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................................................
115
5.2.
Utekelezaji wa mitaala ......................................................................................................
118
5.3.
Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa.........................................................................
119
5.4.
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu .................................................
121
5.5.
Mfumo wa utayarishaji wa walimu..................................................................................
121
5.6.
Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia..........................................................................
124
REJEA
...............................................................................................................................................
126
VIAMBATISHO
...............................................................................................................................
130
Kiambatisho
Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti ......................................................
130
Kiambatisho
3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa...........................................
132
Kiambatisho
4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika Halmashauri
zilizofanyiwa
utafiti.......................................................................................................................
133
Rasimu 2
v
VIFUPISHO
BEST
Basic Education Statistics in Tanzania
CA
Continuous Assessment (Mazoezi Endelezi)
CG
Capitation Grant
CDTI
Community Development Training Institute
CWT
Chama cha Walimu Tanzania
EFA
Education for All
EMAC
Educational Materials Approval Committee
ETP
Education and Training Policy
FTC
Full Technician Certificate
GBS
General Budget Support
GDP
Gross Domestic Product
GER
Gross Enrolment Rate
MKUKUTA
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania
MMES
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari
MEMK-WSM
Mkakati wa Elimu ya Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za
Msingi
MMEM
Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi
MMEMWA
Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu
MoEVT
Ministry of Education and Vocational Training
MWAKEM
Mafunzo ya Walimu Kazini Elimu ya Msingi
MTEF
Medium Term Expenditure Framework
MDGs
Milemium Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Milenia)
NCDF
National Curriculum Development Framework
NECTA
National Examinations Council of Tanzania
OC
Other Charges
OUT
Open University of Tanzania
OWM-TAMISEMI
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
PETS
Public Expenditure Tracking System
SEDP
Secondary Education Development Programme
TAMONGSCO
Tanzania
Association of Managers of Non Government Schools and
Colleges
TEHAMA
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TET
Taasisi ya Elimu Tanzania
TEN/MET
Tanzania Education
Network/Mtandao wa Elimu Tanzania
TES Tanzania Elimu
Supplies
TIE
Tanzania Institute of Education
TSD
Teachers Service Department (Idara ya Huduma kwa Walimu)
UKIMWI
Ukosefu wa Kinga Mwilini
URT
United Republic
of Tanzania
TRC
Teachers Resource Centre
UPE
Universal Primary Education (Elimu ya Msingi kwa Wote)
WEMU
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Rasimu 2
vi
MUHTASARI
PEMBUZI
Utoaji
wa elimu nchini Tanzania
unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo (ETP) ya
mwaka
1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya
Taifa
2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya
Maendeleo
ya Milenia (MDGs).
Katika
kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu
ilianzishwa.
Aidha, Programu za Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na
Sekondari
(MMES) zilianzishwa kutekeleza program ya sekta. Mafanikio ya MMEM
yameongeza
mahitaji ya upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango wa
Maendeleo
ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu la
kuongeza
uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-
2014) imeweka
kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari.
Kiwango
cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila
mwaka
kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na
2010
(50.4%). Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kufanya utafiti ili kubaini
sababu
za
kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na
tatizo
Utafiti
huu ulifanyika katika mikoa 11, ikiwa ni mmoja kwa kila Kanda ya Elimu. Aidha,
jumla
ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa ikiwa moja iliyofanya
vizuri
na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Kwa kila
Halmashauri
jumla ya shule sita zikiwemo nne za serikali na mbili zisizo za serikali
zilihusika
katika utafiti huu. Jumla ya shule 132 ambapo 88 ni za Serikali na 44 ni
shule
zisizo za Serikali zilihusishwa. Pia, ofisi za elimu na ukaguzi wa shule,
Taasisi ya
Elimu
Tanzania (TET), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), pamoja na baadhi ya
asasi
za serikali na zisizo za serikali zilihusishwa. Jumla ya wajibuji 3,894
walilengwa
katika
utafiti ambapo washiriki 3,037 sawa na asilimia 80.0% walifikiwa.
Taarifa
na takwimu za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Madodoso, Majadiliano ya
Pamoja,
Hojaji, maandiko na makala mbalimbali. Uchambuzi wa takwimu umefanyika
kwa
kuwasilisha hoja za wajibuji katika namba (asilimia), majedwali na chati ili
kuleta
Rasimu 2
vii
taarifa
zenye mantiki kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti kuhusu
kushuka
kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 2010
yamewasilishwa
kama ifuatavyo:-
a)
Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
Utafiti
umedhihirisha kuwa matatizo yanayohusu usimamizi na uendeshaji
yameathiri
ufanisi katika utoaji wa elimu bora nchini. Baadhi ya viongozi wa
elimu
huteuliwa bila kuzingatia utaalamu, taaluma, uwajibikaji, uwezo na
uadilifu.
Aidha, maamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa elimu hufanyika
kisiasa
bila kuzingatia utaalamu na tafiti. Vile vile ufinyu wa bajeti ya Wizara ya
Elimu
na TAMISEMI (Elimu) unafanya usimamizi na uendeshaji wa elimu
kutokuwa
fanisi.
Utekelezaji
wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada na ziada umekuwa na
changamoto
ambazo zimeathiri uchapishaji, usambazaji na upatikanaji wa vitabu
vyenye
ithibati katika shule na vyuo. Aidha, kuna uelewa mdogo kwa wanafunzi
na
walimu katika matumizi ya Kiingereza kama
lugha ya kufundishia na kujifunzia
katika
shule za sekondari na vyuo vya ualimu.
Utafiti
umebaini kuwa, mmomonyoko wa maadili kama vile
matumizi ya lugha
mbaya;
matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
kutozingatia
mafundisho ya dini, matumizi ya dawa za kulevya na kujiingiza
katika
masuala ya mapenzi ni masuala yaliyobainishwa kuchangia kumeathiri
maendeleo
ya taaluma shuleni.
b)
Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala
Utafiti
umeonesha kuwepo kwa changamoto za utayarishaji na utekelezaji wa
mtaala
kwa miaka mitano iliyopita. Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005
umetekelezwa
bila kufanyiwa majaribio (piloting). Aidha, utafiti umebaini kuwa
kwa
miaka mitatu iliyopita (2008 hadi 2010), jumla ya walimu 588 (1.5%)
walipata
mafunzo kabilishi. Taarifa hii inaonesha kuwa walimu wengi hawana
maarifa
na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari uliboreshwa.
Rasimu 2
viii
Ni
muhimu watekelezaji mitaala kupatiwa mafunzo kabilishi ili kuimarisha
utendaji
kazi wao na kuwawezesha kupata fursa ya mabadiliko ya mtaala, dhana
na
nadharia za ufundishaji na ujifunzaji.
Pia,
utafiti umebaini upungufu wa mihtasari ya mtaala ulioboreshwa katika shule
za
sekondari. Katika shule zilizofanyiwa utafiti, takwimu zinaonesha kuwa kuna
upungufu
wa mihtasari kwa wastani wa asilimia 45.4 ambapo masomo ya
Mathematics
na Geography yameongoza kwa kuwa na upungufu wa zaidi ya
asilimia
50. Vilevile, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka
TET
kwenda shuleni.
c)
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
Utafiti
huu ulilenga Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya
utoaji
wa elimu, utekelezaji wa mtaala na ukaguzi wa shule.
Utafiti
ulibaini kuwa asilimia 49 ya wakuu wa shule hawafuatilii kikamilifu utoaji
wa
taaluma shuleni, hali hii inapunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
Hivyo
inapaswa wakuu wa shule wasimamie kikamilifu majukumu yao
kama
ilivyoainishwa
katika Mwongozo wa Usimamizi wa Shule.
Aidha,
ilibainika kuwa hakuna ufuatiliaji wala tathmini iliyofanyika tangu mtaala
wa
elimu ya sekondari ulioboreshwa uanze kutumika mwaka 2005 na kwamba
mitaala
hiyo haikufanyiwa majaribio kabla ya utekelezaji wake. Kutofanya
tathmini
kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa serikali na
wadau
wa elimu kubaini matatizo na changamoto za utoaji elimu na kuyapatia
ufumbuzi
kwa wakati na hivyo kupunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji
Pia
utafiti umebaini kuwa, katika shule 132 zilizotembelewa, shule 18 (13.53%)
zilikaguliwa
mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Hali kadhalika
shule 6
(51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na shule 46 (34.59%)
hazikukaguliwa
kabisa. Aidha, taarifa za ukaguzi wa shule hazifanyiwi kazi
ipasavyo.
Kutokaguliwa kwa shule hizo za sekondari kumepunguza ufanisi wa
usimamizi
na utoaji wa elimu bora.
Rasimu 2
ix
d)
Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu
Ufaulu
wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa huchangiwa na sababu mbalimbali.
Uwepo
wa walimu wenye sifa stahiki shuleni ni moja ya sababu muhimu.
Utafiti
umebaini kuwa, sifa za udahili kwa walimu tarajali wa stashahada ni za
ufaulu
wa kiwango cha chini (1Principal na 1Subsdiary) katika masomo ya
kufundishia
na baadhi yao
hawana wito wa kazi ya ualimu. Aidha utafiti umebaini
kuwa
kuna changamoto katika matayarisho ya walimu tarajali unaosababishwa
na
upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Aidha,
matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu
kimasomo
hususani katika masomo ya sayansi na Mathematics unaosababishwa
pia na
upangaji usiozingatia mahitaji hususan katika sehemu zenye mazingira
magumu.
Katika shule zilizofanyiwa utafiti imebainika kuwa somo la
Mathematics,
lina mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo
kuna
upungufu wa walimu 264 sawa na asilimia 60.6. Tatizo la upungufu wa
walimu
ni changamoto katika utoaji wa elimu.
e)
Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
Matokeo
mbalimbali yahusuyo mfumo wa mitihani yamebainishwa ikiwa ni
pamoja
na muundo wa maswali yatolewayo shuleni kutokidhi viwango
vinavyotumika
na NECTA.
Aidha,
Miundo ya mitihani ya Taifa haiwafikii baadhi ya walimu na wanafunzi na
hivyo
kutoielewa. Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi
hawapati
fursa ya kuiona na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika
shule
za sekondari. Uwepo wa Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani
katika
shule ni muhimu katika kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote
wanapaswa
kupata na kutumia machapisho hayo.
Utafiti
umebaini kuwa, uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule haufanywi
kwa
makini. Aidha, utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’
walizosahihisha
badala ya posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji
Rasimu 2
x
kwa
siku ni baadhi ya masuala yanaweza kuchangia kupungua kwa umakini wa
usahihishaji.
Aidha
utafiti umebaini kuwa, mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45%
majaribio
na mazoezi na 5% projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au
mchakato
wake katika matokeo ya mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu.
Hata
hivyo NECTA wanatumia vigezo vingine vya ulinganifu sanifu ambavyo
mchakato
wake wa kuvitumia haueleweki kwa wadau. Aidha utafiti umebaini
kuwa,
gredi zinazotumika shuleni kwa uzoefu wa miaka mingi ni A (81-100), B
(61-80),
C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa
alama
za gredi zinazotumika kwa Mtihani wa Taifa wa K4 huamuliwa na Kamati
ya
Kutunuku ambapo gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si chini ya alama
70.
Hali hii ya kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu baina ya shule
na
NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama za gredi. Vilevile, kuna
mapungufu
ya kuadhibu watahiniwa kwa kuteremshwa daraja la I au la II kuwa
la III
kutokana na kufeli baadhi ya masomo ya msingi na ya mchepuo.
f) Mazingira
na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
Utafiti
umebaini kuwa katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti, kuna upungufu mkubwa
wa
miundombinu, samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni ikijumuisha
maabara
ya Chemistry (79.6%), Biology (66%) na Physics (65.2%) nyumba za
walimu
(72%), na maktaba (80.6%). Aidha, baadhi ya shule zimepata usajili bila
kutimiza
vigezo na nyingine kujengwa mbali na makazi ya jamii husika. Vilevile
utafiti
umebaini upungufu wa vifaa vya kufundishia ikiwa ni pamoja na vitabu vya
kiada
na ziada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa kwa baadhi ya masomo
kwa
wastani wa 75.5% katika shule zilizofanyiwa utafiti.
Matokeo
ya utafiti pia yamebaini kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa
wanafunzi
katika shule za kutwa, na hivyo kuathiri mahudhurio na umakini wa
wanafunzi
katika ujifunzaji.
Hali
hii ya upungufu wa miundombinu, upatikanaji wa vitabu vinavyoendana na
mihtasari
iliyoboreshwa na kutokuwepo kwa chakula cha mchana ni changamoto
ambazo
zinaathiri utekelezaji wa mitaala shuleni.
Rasimu 2
xi
Mapendekezo
Kutokana
na taarifa za utafiti kuna mapungufu na changamoto mbalimbali zilizoathiri
kiwango
cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 mwaka 2010. Mapendekezo
muhimu
yametolewa ambayo yanaweza kutekelezwa kwa muda mfupi, kati na mrefu.
1. Uteuzi
wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,
uadilifu
na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na
zisikaimishwe
kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;
2.
Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,
tathmini
na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya
utoaji
wa elimu;
3.
Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili
kutatua
changamoto
zilizopo;
4.
Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)
kianzishwe
kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji
na haki
za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa
inakidhi
malengo yaliyokusudiwa; Utaratibu wa motisha kwa walimu
unaoendana
na uzito wa kazi, wadhifa na ugumu wa mazingira anapofanyia kazi
uandaliwe
na utekelezwe ipasavyo;
5.
Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya
mitihani
ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate
sifa za kujiendeleza
kitaaluma
na kitaalamu;
6. Vyuo
vya ufundi stadi kama vile VETA vipanuliwe ili
kuwawezesha wahitimu wa
kidato
cha 4 wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na
stadi
za kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri;
7.
Walimu wenye sifa wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji katika shule
zote.
Pia, Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule
ziandaliwe;
Rasimu 2
xii
8.
Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa
ufundishaji
na ujifunzaji yaimarishwe.
9.
Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo
vinavyotakiwa;
10.Walimu
wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia
pia
alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kama
ilivyoelekezwa
katika mwongozo wa mazoezi endelezi;
11.Utungaji
na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala
inayotekelezwa
12.Adhabu
katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III
baada
ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila
mtahiniwa
apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake;
13.Hadhi
ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja
wanafunzi.
Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada
(Remedial)
14.Mfumo
rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika
kwa
wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki
kwa
watahiniwa;
15.Wasahihishaji
wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu kwa sababu ni
haki ya
mwajiriwa wa serikali;
16.Mafunzo
kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa
kwa walimu na wakaguzi wote. Aidha Mafunzo maalumu kuhusu
dhana
ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na kutekelezwa kwa maafisa
mitaala
na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo;
17.Mihtasari
ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft
copy)
ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo
ya Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi;
Rasimu 2
xiii
18.Jukumu
la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili
kubaini
dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki;
19.Taratibu
za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya
utafiti,
tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake.
20.Fedha
za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia
shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo. Vilevile, Hosteli/mabweni na
nyumba
za walimu zijengwe kwenye shule za sekondari zilizo mbali na makazi
ya
watu, na wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha
mchana;
21.Sifa
za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada
zipandishwe
kuwa Principal mbili za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha
mwalimu
kuwa mahiri kitaaluma;
22.Vifaa
vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa
miundombinu
ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na
ongezo
la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa. Wakufunzi na wahadhiri
wapewe
mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi (Competence Based
Curriculum);
23.Maabara
ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na
kuimarishwa
katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali
watatumia
kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na
kuandika.
Pia Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa
walimu
wa masomo yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za
sekondari;
24.Utaratibu
maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post
Graduate
Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili
kukabiliana
na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi;
25.Ukaguzi
wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa
kupatiwa
nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia;
Rasimu 2
xiv
26.Ufuatialiaji
wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada
pamoja
na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe;
27.Sheria
ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo
na
ithibati katika shule nchini.
No comments:
Post a Comment