Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Friday, April 12, 2013

HII NDO RIPOTI ILIYOUNDWA MWAKA 2010 KUCHUNGUZA KUFELI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE -2010

Ripoti inayodaiwa kuundwa na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuchunguza sababu za kufeli wananfunzi wa kidato cha nne mwaka 2010 imewekwa hadharani mitandaoni, kuwekwa kwa ripoti hiyo kunatokana na muweka ripoti hiyo kuguswa na kitendo cha Mh. Tundu Lisu kuigusia bungeni akipinga kitendo cha Waziri Mkuu huyo huyo kuunda ripoti nyingine mwaka huu wakati ile ya kwanza ilitoa sababu za tatizo hilo lakini ripoti hiyo ilifichwa, Mtoa ripoti hiyo katika mtandao wa kijamii wa Jamii Forum anasema,
 
 "Baada ya kumwona Tundu Lissu akiigusia Ripoti hii, nimeonelea ni vema niwashirikishe ripoti yenyewe kwakuwa haikuwahi kuwa kwenye public domain.

Ni Ripoti ya utafiti iliyokuwa commissioned na ofisi ya Waziri Mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne mwaka 2010 ambayo ilitoka mwaka 2011.

Ajabu ni kwamba ripoti hii haikufanyiwa kazi na mwaka huu Ofisi hiyohiyo ya Waziri Mkuu imeunda kamati nyingine kuchunguza tatizo hilohilo! What a waste of resources and our time, all to deviate our attention from discussing pressing matters!

Sijui tunaelekea wapi?

Watanzania, bila kujali tofauti zetu kisiasa tusikubali mambo kama haya. Ni kuchezea raslimali zetu na hatari kwa vizazi vyetu na mustakbali wa Taifa letu."
 
Sasa isome mwenyewe ripoti hiyo! alafu ujiulize je kulikuwa na sababu nyingine za kuunda tume mpya au la! kwa kubofya  link hii hapa : Rasimu ya 2 ya Taarifa ya Utafititi-Ufaulu K4 2010[1].pdf 
 
Pia ukitaka kusoma coments za watu wangine kuhusu ripoti hii bofya hapa: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/432406-ripoti-hii-ilifichwa-chanzo-cha-kuporomoka-elimu-tanzania.html

No comments:

Post a Comment