Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, November 29, 2015

JE HILI NI DONGO LA JANUARY MAKAMBA KWA RAIS MAGHUFULI AU WATU WANAPOTOSHA? INGIA HAPA MWANAWANE UONE ALICHOPOST MAKAMBA WATU WALIVYOTAFSIRI NA MAJIBU YA MAKAMBA





πŸ‘‡πŸΏπŸ‘‡πŸΏπŸ‘‡πŸΏπŸ‘‡πŸΏ MAANA YA IZO PICHA ALIZOPOST JANUARY MAKAMBA

Nyani wawili ni Makamba na JK (kumbuka kwa Makamba kupata ujasiri wa kupost hayo lazima kuna uzito nyuma yake)...binadamu mwenye mkia ni Makufuli...Tafsiri sasa..
Nyani wawili wako pembeni wakimuangalia/shangaa binadamu kujidai nyani na kucheza mchezo wa Nyani bila kuomba ushauri, alafu kwenye makazi/mjini wakati wenye mchezo wapo na ni mchezo wa kuchezwa porini.

Ya pili, hilo ni tusi...anasema walimfanyia kila kitu yeye alitakiwa kuja na kuenjoy the ride, little do they know wanamtandikia nguruwe red carpet...na unajua nguruwe wanavyojua kujigalagaza kwenye matope na hawajui thamani ya chochote..😜😜

! Hizo chain zina wakilisha chama na huyo mtu ni Makufuli.
Anachojaribu kusema chochote atakacho fanya/jaribu kufanya, rangi yoyote atakayo paka...bado amefungwa na minyororo hawezi kutoroka, sana sana ataing'arisha minyororo iliomfunga wakati yeye akiendelea kua mtumwa...😎

Ni kweli kwani hata choice ya Kikwete baada ya Membe kuangukia pua ilikua ni Makamba..lakini Edo akaharibu mchezo wote wakaishia kwa Makufuli wakitwgemea Kikwete ataendelea kua mwenyekiti na atamcontrol...

Ile ya ngazi ina maanisha,
 Mchezo wa porini....mfano wake ni pale unapopewa majina ya wauza madawa na kuwaita chemba hakuna anaejua ulichofanya ukirudi mjini unashusha mkwala mbuzi...😎😎

Ila pia hiyo ngazi inaonyesha mpandaji hatofika anakotaka kufikia nafikiri anamaanisha hiyo ngazi ni system huwezi jitengenezea ngazi bila kuwashirikisha wanasystemπŸ˜ƒ

Ukiangalia post zake zote maana yake ni karibia ile ile..!! Kwani anafeel kua alifanya kazi kubwa sana kwenye kampaini na anahisi kama kwa asilimia kubwa amewezesha Makufuli kua katika nafasi hio. So anaona kama Mheshimiwa kishapata sasa anamuona hafai..ana muignore, as they say alitegemea kua
aziri mkuu.


Mwenyewe Makamba ajibu


Saturday, September 12, 2015

LOWASSA AITEKA MANYONI KWA MUDA: AVUNJA REKODI YA MAGHUFULI.

WATU WENGI WAJITOKEZA KUMSIKILIZA. 

ASEMA ATAMALIZA KERO YA MAJI MANYONI.

Na Furaha Venance (Baba D): Manyoni

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Ngoyai Lowassa leo ameuteka mji wa Manyoni kufuati mapokezi makubwa aliyoyapata wilayani. Msafara wa mgombea huyo uliwasili katika viwanja vya shule ya Msingi Tambukareli kwa usafiri wa chopa akiambatana na viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fedrick Sumaye, aliyekuwa Naibu Waziri wa Ajira na vijana, Mh. Makongoro Mahanga, Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu na viongozi wengine. watu wengi waliojitokeza walikuwa wakisukumana kwa lengo la kumshuhudia kwa macho yao mgombea huyo huku wengine wakipigania ili kumshika wengine wakiwabeba watoto wao juu ili wamshuhudie mgombea huyo ambaye anaonekana ni mgombea mwenye mvuto na ushawishi kuliko wagombea wote katika uchaguzi huu. Aidha mara Chopa ilipowasili katika viunga vya Manyoni, ikiwa angani, wakazi wa Manyoni, walianza kukimbilia na wengine wakifunga maduka yao ili tu kumshuhudia mgombea huyo kat.

Kabla mgombea huyo hajapanda jukwani, viongozi mbalimbali wa chama hicho walihutubia. Sumaye akiwahutubia wananchi wa Manyoni, alishangaa ndani ya miaka 50 ya utawala wa CCM Hospital ya Manyoni haina dawa, wagonjwa kulala chini huku akina mama wajawazito wakiagizwa kuleta vifaa vya kujifungilia ili hali huduma hiyo inatolewa bure. Akihutubia kwa njia ya kuuliza maswali, sumaye aliuliza, “tuliweka misingi kwamba watoto chini ya miaka 5 watibiwe bure. Je wanatibiwa bure?” alijibiwa na umati wa watu, “Hapana!”. “Hospitali yetu kuna dawa?” alijibiwa “hakuna.” Aidha aliendelea kuwaeleza wananchi kwamba, chama cha mapinduzi kimeshindwa kuwaletea maendelea ndani ya miaka 50 kitaweza ndani ya miaka 5? “Sasa tumewaletea rais anayeweza kuwaletea maendelea naye si mwengine ni Edward Lowassa.”

“Huko kote tulikopita tumepokelewa na watu wengi sana, wananchi wanataka mabadiliko. Sasa CCM wanaomba huruma ya wananchi. Si mmemsikia Maghufuli, anasema hakuna haja ya kuchoma kitanda kama kina kunguni! Eti unamuua kunguni kitandanda unakiacha. Kwa lugha ya Maghufuli kitanda ni CCM na kama kitanda kina kunguni dawa yake ni kukitoa nje na kukianika kipigwe jua huko nje miaka 50.” Alisema Sumaye na kushangiliwa na umati wa watu waliofurika katika viwanja hivyo.

Mapema kabla ya kuzungumza Sumaye, aliyekuwa naibu waziri wa Ajira na Vijana, Mh. Makongoro Mahanga, alisema, “Ndugu zangu nimekuwa naibu waziri wa Ajira na Vijana kwa muda mrefu, CCM wasiwadanganye hakuna ajira huko, ajira zitakuwepo chini ya serikali ya UKAWA.” Aidha Tundu Lissu akiwazungumzia Mawaziri hao wastaafu, aklisema kwamba, mawaziri hawa hawana shida ya maisha, wangeamua kukaa kimya kama alivyokaa kimya Msuya (Waziri Mkuu Mstaafu), ama wangeamua kutumika na CCM kama anavyotumika Warioba licha ya madhambi waliyomfanyia. “Ndugu zangu, Lowassa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa sasa wa Mizengo Pinda...Sumaye naye analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, hawana shida ya maisha wameamua kuungana na sisi ili kuwaletea maendeleo...” Alisema Lissu.

Lowassa apanda jukwaani

Ukawadia sasa wasaa wa mgombea huyo kupanda jukwaani saa 6:09. Umati wa watu ulilipuka kwa kelele wakiimba Rais! Rais!, rais! Rais! Huku wakinyajua mabango yao yaliyobeba ujumbe mbalimbali. “Kwanza ni washukuru kwa mapokezi makubwa haya, mmejitokeza kwa wingi asanteni sana.” Alisema lowassa akionekana kushangazwa na umati wa watu waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo. Ndugu zangu nimekuja hapa kuwaomba kura, wangapi watanipa kura siku hiyo?” aliuliza na kujibiwa kwa watu kunyoosha mikono juu. Aidha aliwaambia Wanamanyoni kuwa wamchague alimalize tatizo la maji. “Haiwezekani zaidi ya miaka 50 wilaya ya Manyoni ina matatizo ya maji! Haiwezekani kabisa! Nichagueni tufanye mchakamcha wa maendeleo. Mbunge wa hapa namjua vizuri sana, Chiligati amekimbia matatizo.” Alisema.

Akiendelea kujinadi alisema kwamba, atashughulikia matatizo yote ya afya, maji, elimu, na miundo mbinu. Anachohitaji wamchagulie wabunge na madiwani kutoka vyama vya ukawa ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Manyoni. Ukafika muda akampandisha mgombea Ubunge wa Jimbo hilo bwana Emmanuel Mpandagoya kueleza matatizo yanayowakabiliwa Wanamanyoni. Akizungumzia kero za Wanamanyoni, Mgombea huyo alisema, Manyoni inakabiliwa na tatizo la maji, walimu wa hususani walimu wa masomo ya Sayansi, umeme, “Kuna vijiji hapa manyoni havina huduma ya maji wala umeme, tunaomba Mh. Rais utakapochaguliwa tu tunaomba utusaidie kuondoa kero hii.” Alisema mgombea huyo. Aidha aliongeza kuwa kumekuwa na kero za michango  na kodi nyingi kwa wananchi wa Manyoni.

Mgombea huyo wa urais mara baada ya kupokea kipaza sauti kwa mgombea ubunge, aliwauliza wananchi kama mbunge huyo anaweza kuwa mbunge na kuitikiwa na umati wa watu kuwa anaweza huku wengine wakiimba Imma! imma! Imma. “Ndugu zangu Wanamanyoni tuchagueni tumalize kero hizi.” Alisema Lowassa ambaye alitumia dakika 12 kuongea na Wanamanyoni.

Wanamanyoni wanasemaje?

Wakiongea na mwandishi wa Baba D Blogy, wakazi wa Manyoni walikuwa na maoni tofautitofuati kuhusiana na ujio huo wa Lowassa. “Ndugu yangu nilikuwa nasikia kuwa wanaojitokeza katika mikutano yake wanabebwa na malori ili kujaza mikutano yake, leo nimeshuhudia mwenyewe hawa watu wamekuja kwa mapenzi yao tu.” Alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shaban. Mkazi mwingine wa Manyoni ambaye hakupenda kujitambulisha alisema kuwa wakati wa ujio wa Maghufuli hapa Manyoni alivyokuja kujitambulisha watu hawakujitokeza kama hivi leo, tena wengine tulibebwa kutoka vijijini kuja kumshuhudia lakini leo licha ya kuchelewa kupata taarifa za ujio huu nimekuja kwa mapenzi yangu kutoka Kintiku.”
Dereva bodaboda aliyejitambulisha kwa jna la Rama, “alienda mbali zaidi na kusema kuwa haijawahi kutokea chama cha upinzani kwa historia ya Manyoni kukusanya watu wengi kiasi hiki. Huyu jamaa CCM wakicheza anapita.”

Kwenye vijiwe vya madereva tax na boda boda stori za leo ni Lowassa tu, wengine walisikika wakisema huu ni wakati wa mabadiliko, wengine ambao walionekana kuwa wachahce walionekana bado wana imani na CCM na mgombea wake Maghufuli. “Maghufuli ndiyo kila kitu hamuoni barabara?” alisikika dereva mmoja wa tax na kushambuliwa na wenzake ambao wanaonekana kumzidi nguvu. “CCM imeshindwa kwa miaka 50 ni wakati wa kuwapima wengine.” Alijibiwa na mwenzake na kushangiliwa na wenzake.

Wengine waponda
Wakazi wengine waponda, wadai umati uliojitokeza si kwamba wanampenda Lowassa ila walikuja kumuona tu anafananaje. “Wala hakuna jipya alilolizumza leo.” Alisema mkazi mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Mgombea huyo anaendelea na mikutano mingine katika majimbo mengine ya Mkoa wa Singida.

Simu: 0715 33 55 58


Wednesday, September 9, 2015

KAMA HUKUFANIKIWA KUITAZAMA HOTUBA FULL YA GWAJIMA AKIMJIBU DR. SLAA INGIA HAPA



Askofu Gwajima akijibu tuhuma dhidi yake na dhidi ya maaskofu wa Kanisa Katoliki zilizotolewa na mwanasiasa Dr Slaa. 08/09/2015. 


Wednesday, August 19, 2015

BAADA YA WASANII WENGI KUONESHA MSIMAMO WAO KUHUSU WAGOMBEA WANAOWAUNGA MKONO, MKALI WA BONGO MOVIE, RAY KIGOSI AMEANDIKA HAYA


Baada ya baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie kuonesha msimamo wao katika kuwaunga mkono wagombea flani wa Urais. Msanii mwenzao Ray Kigosi ameonesha msimamo wake na kwa maneno haya.

"Usiku wa jana nimetafakari vi2 vingi sana kuhusu Nchi yangu iliyobarikiwa kila aina ya utajiri wa madini mbuga za wanyama wakiwemo aina mbalimbali za wanyama wa kuvutia na hekta kubwa za misitu Ila ninaona vipofu wengi sana wasiolewa nini 2lichobarikiwa ndani ya Tanzania ye2. 2meingiz
wa mikenge mingi sana katika mikataba tena mibovu bajeti kandamizi Kwa wa2 wa hali ya chini mifumuko ya bei kila kukicha hali ngumu kwa wasanii wa Tanzania kila siku ahadi zisizotekelekeza why nasema hivyo wasanii wenzangu? 2meumia kwa kipindi kirefu sana bila msaada wowote ha2na haki miliki wa kazi ze2, zinaibiwa kama njugu sokoni kariakoo yani 2li2pwa kama taka taka kwenye dampo lakini sasa hivi kipindi cha uchaguzi ndio 2naonekana umuhimu we2 tuamke kuwaambia wananchi wachague viongozi makini watakaoweza ku2vusha Watanzania kwenda ha2a nyingine. 


Tuna wa2 wengi sana nyuma ye2 wanaotuamini sisi wasanii kama kioo cha jamii tusiwapoteze Watanzania kuwaambia Viongozi wa chama flani ndio wanafaa kwa vijisenti vidogo 2navyopewa. Watanzania huu ni wakati sahihi waku2lia na kuwachagua viongozi makini wanaofaa Ni katika kukumbushana 2 waswahili wanasemaje utakaokatanao kuni ndio utakaota nao moto.”

Via: EATV

Tuesday, August 18, 2015

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ORODHA YA MAJINA YA WANACHAMA WA CHADEMA WALIOTEULIWA KUGOMBEA UBUNGE

Kurugenzi Ya Habari Chadema

Mkoa Jimbo CHAMA MGOMBEA ALIYETEULIWA
Mara
1. Rorya CDM STEVEN J OWAWA
2. Tarime Mjini CDM ESTHER N MATIKO
3. Tarime Vijijini CDM JOHN HECHE
4. Musoma Vijijini CDM ZAKARIA MBULA CHIRAGWILE
5. Butiama CDM YUSUPH R KAZI
6. Bunda Mjini CDM ESTHER BULAYA
7. Mwibara CDM HARUN D CHIRIKO
8. Musoma Mjini CDM VINCENT J NYERERE
9. Bunda Vijijini CDM SULEIMAN DAUDI

Simiyu
1. Bariadi CDM GODWIN SIMBA
2. Maswa Magharibi CDM ABDALA PATEL
3. Maswa Mashariki CDM SYLVESTER KASULUMBAYI
4. Kisesa CDM MASANJA MANANI
5. Meatu CDM MESHACK OPULUKWA
6. Itilima CDM MARTINE MAGILE

Shinyanga
1. Msalala CDM PAULO MALAIKA
2. Kahama Mjini CDM JAMES LEMBELI
3. Kahama Vijijini (Ushetu) CDM SIMON BUKAKIYE ISAYA
4. Shinyanga Mjini CDM PATROAS PASCHAL K
5. Kishapu CDM FRED T MPENDAZOE

Mwanza
1. Ukerewe CDM JOSEPH MKUNDI
2. Magu CDM KALWINZI NGONGOSEKE
3. Nyamagana CDM EZEKIA D. WENJE
4. Buchosa CDM MARTINE KASWAHILI
5. Sengerema CDM HAMIS TABASAMU
6. Ilemela CDM HIGHNESS KIWIA
7. Misungwi CDM LEONIDAS KONDELA

Geita
1. Bukombe CDM PROF. KULIKOYELA KAHIGI
2. Busanda CDM ALPHONCE C MAWAZO
3. Nyang'wale CDM GEORGE MABULA
4. Chato CDM DR. BENEDICT LUKANIMA
5. Mbogwe CDM NICODEMUS H MAGANGA
Kagera
1 Karagwe CDM PRINCE RWAZO
2 Kyerwa CDM BENEDICT MTUNGIREHI
3 Bukoba Mjini CDM WILFRED LWAKATARE
4 Muleba Kaskazini CDM ANSBERT NGURUMO
5 Muleba Kusini CDM ALISTIDES KASHASILA
6 Biharamulo CDM DR. ANTHONY MBASSA

Mbeya
1. Lupa CDM NJELU KASAKA
2. Songwe CDM MPOKI MWANKUSYE
3. Mbeya Mjini CDM JOSEPH MBILINYI
4. Kyela CDM ABRAHAM H MWANYAMAKI
5. Rungwe CDM JOHN D MWAMBIGIJA
6. Busokelo CDM BONIPHACE A MWAMUKUSI
7. Mbozi CDM PASCHAL HAONGA
8. Momba CDM DAVID E SILINDE
9. MBARALI UKAWA MODEST KILUFI
10. Mbeya Vijijini CDM ADAM NZELA
11. Tunduma CDM FRANK MWAKAJOKA
12. Vwawa CDM FANUEL MKISI

Iringa
1 Ismani CDM PATRICK OLE SOSOPI
2 Kalenga CDM MUSSA L MDEDE
3 Mufindi Kaskazini CDM JUMANNE K MASONDA
4 Iringa Mjini CDM PETER MSIGWA
5 Kilolo CDM BRIAN KIKOTI
6 Mafinga Mjini CDM WILLE MUNGAI

Njombe
1 Njombe Kusini CDM EMMANUEL MASONGA
2 Lupembe (Njombe Kask) CDM EDWIN E SWALE
3 Wanging’ombe CDM DISMAS A LUHWAGO
4 Makete CDM JACKSON T MOGELA
5 Ludewa CDM ATHROMEO MKINGA
6 Makambako CDM ORAPH MHEMA
Rukwa
1 Nkasi Kusini CDM ALFRED DANIEL SOTOKA
2 Kwela CDM DANIEL NAFTAL NGOGO
3 Nkasi Kaskazini CDM KESSY SOUD
4 Sumbawanga Mjini CDM SADRICK MALILA
5 Kalambo CDM VICTOR MATENI

Tanga
1 Kilindi CDM JERADI K MREMA
2 Muheza CDM ERNEST MSINGWA
4 Korogwe CDM AMANI H KIMEA
5 Korogwe Vijijini CDM EMMANUEL KIMEA

Kilimanjaro
1. Rombo CDM JOSEPH SELASIN
2. Same Magharibi CDM CHRISTOPHER S MBAJO
3. Same Mashariki CDM NAGENJWA KABOYOKA
4. Moshi Mjini CDM JAFARY P MICHAEL
5. Hai CDM FREEMAN A MBOWE
6. Siha CDM DR. GODWIN MOLLEL

Arusha
1 Arumeru Mashariki CDM JOSHUA NASSARI
2 Arumeru Magharibi CDM GIBSON MESIYEKI
3 Arusha Mjini CDM GODBLESS LEMA
4 Longido CDM ONESMO OLE NANGOLE
5 Monduli CDM JULIUS KALANGA
6 Karatu CDM WILLE QAMBALO
7 Ngorongoro CDM ELIAS NGORISA

Manyara
1 Simanjiro CDM JAMES KINYASI OLE MILLYA
2 Mbulu Vijijini CDM MIKEL PETRO AWEDA
3 Hanang CDM MAGOMA RASHID DERICK
4 Babati Mjini CDM PAULINE P GEKUL
5 Babati Vijijini CDM LAURENT SURUMBU TARRA
6 Kiteto CDM KIDAWA ATHUMANI IYAVU
7 Mbulu Mjini CDM PAULO HERMAN SULLE

Dar es Salaam
1. Ubungo CDM SAED KUBENEA
2. Kawe CDM HALIMA JAMES MDEE
3. Ukonga CDM MWITA MWIKWABE WAITARA
4. Ilala CDM MUSLIM HASSANALI HEIDERALI
5. Kibamba CDM JOHN JOHN MNYIKA

Pwani
1 Chalinze CDM MATHAYO TM. TORONGEY
2 Kibaha Mjini CDM MICHAEL PAUL MTALY
3 Kibaha Vijijini CDM EDITHA BABBEIYA
Morogoro
1. Mikumi CDM JOSEPH HAULE
2. Morogoro Kusini CDM DAVID LUKAGINGIRA
3. Kilombero CDM PETER E LIJUALIKALI
4. Mlimba CDM SUZAN L. KIWANGA
5. Mvomero CDM OSWALD MLAY
6. Ulanga Magharibi CDM ALPHONCE MBASSA
7. Ulanga Mashariki CDM PANCRAS KONGOLI
8. Morogoro Mjini CDM MARCOSSY ALBANIE

Dodoma
1. Kongwa CDM ESAU NGOMBEI
2. Dodoma Mjini CDM SINGO BENSON KIGAILA
3. Bahi CDM MATHIAS LYAMUNDA
4. Chilonwa CDM JOHN CHOGONGO

Singida
1 Iramba Magharibi CDM JESCA KISHOA
2 Iramba Mash(Mkalama) CDM OSCAR KAPALALE
3 Singida kaskazini CDM DAVID DJUMBE
4 Singida Mashariki CDM TUNDU A LISSU
5 Singida Magharibi CDM MARCO ALLUTE
6 Manyoni Magharibi CDM LUPAA DONALD
7 Manyoni Mashariki CDM ALLUTE EMMANUEL
Tabora
1 Nzega Mjini CDM CHARLES MABULA
2 Igunga CDM NG’WIGULU KUBE
3 Urambo CDM SAMWELI NTAKAMLENGA
4 Ulyankulu CDM DEUS KITAPANDYA NGERERE
5 SIKONGE CDM SAID NKUMBA
6 Manonga CDM ALLY KHALFANI NGUZO

Katavi
1 Mpanda Mjini CDM JONAS KALINDE
2 Mpanda Vijijini CDM MUSSA MASANJA
4 Katavi CDM GEORGE SAMBWE
5 Nsimbo CDM GERALD KITABU
6 Kavuu CDM LAURENT SENGA MANGWESHI

Kigoma
1 Kigoma Kaskazini CDM DR. YARED FUBUSA
2 Kigoma Mjini CDM DANIEL LUMENYELA

Ruvuma
1 Peramiho CDM ELASMO MWINGIRA
2 Mbinga Magharibi/Nyasa CDM CUTHBERT S. NGWATA
3 Mbinga/Mbinga Vijijini CDM EDWIN B AKITANDA
4 Songea Mjini CDM JOSEPH FUIME
5 Madaba CDM EDSON MBOGORO

Orodha ya Majimbo yaliyobaki itatolewa baada ya kukamilika kwa mashauriano katika UKAWA.
Mhe. John Mnyika
Kny. Katibu Mkuu – CHADEMA
18.08.2015

Monday, August 17, 2015

HAYA SASA! MGAWANYO WA MAJIMBO KWA VYAMA VYA UKAWA HUU HAPA, MAJIMBO 12 YAMEBAKI WANAENDELEA NA MAJADILIANO

Ufuatao ni mgawanyo wa majimbo katika kila mkoa Tanzania Bara;-
Mkoa wa Mara
Kwenye mkoa huu majimbo yote tisa wamekabidhiwa Chadema. Majimbo hayo ni Rorya, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Musoma Vijijini, Butiama, Bunda Mjini, Mwibara, Musoma Mjini na Bunda Vijijini.
Mkoa wa Simiyu
Chadema wamegawiwa Jimbo la Bariadi, Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Kisesa, Meatu, Itilima ambapo Busega limekwenda kwa CUF.
Mkoa wa Shinyanga
Majimbo ya Mkoa wa Shinyanga ambayo ni Msalala, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Shinyanga Mjini, Kishapu na Ushetu yamekwenda Chadema.
Mkoa wa Mwanza
Jimbo la Ukerewe, Magu, Nyamagana, Buchosa, Sengerema, , Ilemela, Misungwi yamekabidhiwa Chadema kuhu Jimbo la Kwimba na Sumve wakikabidhiwa CUF.
Mkoa wa Geita
Bukombe, Busanda, Nyang’wale, Chato na Mbogwe yamekwenda Chadema.
Mkoa wa Kagera
Jimbo la Karagwe, Kyerwa, Bukoba Mjini, Muleba Kaskazini, Muleba Kusini, Biharamulo yamekwenda Chadema ambapo Jimbo la Ngara na Nkenge yamekwenda NCCR-Mageuzi na Bukoba Vijijini limechukuliwa na CUF.
Mkoa wa Mbeya
Katika Mkoa wa Mbeya Jimbo la Lupa, Songwe, Mbeya Mjini, Kyela, Rungwe, Busekelo, Mbozi Mashariki, Momba, Mbeya Vijijini, Tunduma na Viwawa yamekwenda Chadema huku Ileje likikabidhiwa kwa NCCR.
Mkoa wa Iringa
Jimbo la Ismani, Kalenga, Mufindi Kaskazini, Iringa Mjini, Kilolo na Mafinga Mjini yamekabidhiwa kwa Chadema ambapo Jimbo la Mufindi Kusini linapiganiwa na NCCR-Mageuzi.
Mkoa wa Dar es Salaam
Jimbo la Ubungo, Kawe, Ukonga, Ilala na Kibamba ni Chadema huku Kinondoni, Temeke, na Mbagala ikielekezwa kwa CUF.
Mkoa wa Njombe
Njombe Kaskazini, Lupembe, Wanging’ombe, Makete, Ludewa na Makambako yamekwenda Chadema.
Mkoa wa Rukwa
Jimbo la Mkasi Kusini, Kwela, Mkasi Kaskazini, Sumbawanga Mjini na Kalambo ni Chadema.
Mkoa wa Tanga
Handeni Mjini, Handeni Vijijini, Pangani, Tanga Mjini, Bumbuli, Mlalo, Lushoto na Mkinga ambapo Korogwe, Muheza, Kilindi na Korogwe Vijijini ni Chadema.
Mkoa wa Kilimanjaro
Jimbo la Rombo, Same Magharibi, Same Mashariki, Moshi Vijijini, Siha, Moshi Mjini na Hai ni Chadema huku Vunjo ikienda kwa NCCR.
Mkoa wa Arusha
Jimbo la Arumeru Mashariki, Arumeru Magharibi, Arusha Mjini, Longido, Monduli, Karatu na Ngorongoro ni Chadema.
Mkoa wa Manyara
Jimbo la Simanjiro, Mbulu Vijijini, Hanang, Babati Mjini, Babati Vijijini, Kiteto na Mbulu Mjini ni Chadema.
Mkoa wa Pwani
Jimbo la Bagamoyo, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji Utete, Mafia, Rufiji na Kibiti ambapo Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Chalinze ni Chadema.
Mkoa wa Morogoro
Jimbo la Kilosa na Morogoro Kusini Mashariki (CUF) ambapo Mikumi, Morogoro Kusini, Kilombero, Mlimba, Mvomero, Ulanga Magharibi, Ulanga Mashariki na Morogoro Mjini ni Chadema.
Mkoa wa Dodoma
Jimbo la Kondoa Mjini, Kondoa Vijijini na Chema ni CUF; Jimbo la Kibakwe na Mtera ni NCCR-Mgeuzi huku Jimbo la Kogwa, Dodoma Mjini, Bahi na Chilonwa yakiwa ni ya Chadema.
Mkoa wa Singida
Jimbo la Iramba Magharibi, Iramba Mashariki, Singida Kaskazini, Singida Mashariki, Singida Magharibi, Manyoni Magharibi na Manyoni Mashariki ni Chadema.
Mkoa wa Tabora
Jimbo la Bukene, Nzega Vijijini, Igalula, Tabora Kaskazini, Kaliua na Tabora Mjini ni CUF ambapo Jimbo la Nzega Mjini, Igunga, Urambo, Ulyankulu, Sikonge na Manonga ni Chadema.
Mkoa wa Katavi
Jimbo la Mpanda Mjini, Mpanda Vijijini, Katavi, Nsimbo na Kavuu ni ya Chadema.
Mkoa wa Kigoma
Buyungu, Mhambwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Kigoma Kusini, Manyovu (NCCR-Mageuzi) na Kigoma Kaskazini pia Kigoma Mjini ni Chadema.
Mkoa wa Ruvuma
Jimbo la Tunduru Kaskazini, Namtumbo na Tunduru Kusini ni CUF ambapo Mbiga Mjini ni NCCR-Mageuzi. Jimbo la Madaba, Songea Mjini, Mbinga Mashariki/Mbinga, Mbinga Maghribi/Nyasa na Peramilo ni Chadema.
Mkoa wa Mtwara
Jimbo la Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba, Mtwara Vijijini, Nanyamba na Nanyumbu ni CUF ambapo Jimbo la Lulindi, Masasi na Ndanda ni NLD.
Mkoa wa Lindi
Jimbo la Mtama, Kilwa Kaskazini, Kilwa Kusini, Lindi Mjini, Ruangwa, Nachingwea, Liwale na Mchinga ni CUF.

Kwa upande wa Zanzibar majimbo yote ya uchaguzi wamekabidhiwa Chama cha Wananchi (CUF) isipokuwa Jimbo la Mkwajuni ambalo wamepewa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

KITILA MKUMBO ACHOMOA KUWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA ACT, AWASUKUMIA ZIGO, MWENYEKITI NA KATIBU WAO

Ndugu Wazalendo,
Naomba niwashukuru nyote kwa imani kubwa mliyo nayo juu yangu katika kukiwakilisha chama katika nafasi ya Rais. Naishukuru pia Kamati Kuu kwa imani yake kwangu hata kufikia hatua ya kupitisha azimio la kuniomba nigombee urais kwa chama chetu. Jana Kamati Kuu ilituma ujumbe maalumu nyumbani kwangu kwa ajili ya kuzungumza na familia na jamaa zangu juu ya ombi hili.

Aidha, Nimekuwa nikilitafakari jambo hili tangu Alhamisi nilipoombwa rasmi kutafakari uwezekano wa mimi kugombea baada ya juhudi zetu za kutafuta mgombea kushindikana. Nimefanya mawasiliano mapana katika familia, ndani ya chama, chuoni ninapofanyia kazi, Kanisani kwangu,na kwa watu na taasisi mbalimbali ninazohusiana nazo.

Baada ya tafakari na mawasiliano (consultations) mapana nasikitika kusema kwamba sina utayari na maandalizi ya maana ya kisaikolojia, kifamilia, na kisiasa kuniwezesha kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi huu.

Najua nimewaangusha sana katika uamuzi wangu huu lakini naamini kwamba mtaheshimu uamuzi wangu na kwamba hamtaacha kuthamini mchango wangu katika chama kwa sababu ya kukataa kugombea urais.

Nasikitika kwa tuhuma ambazo baadhi ya wanachama wetu wanarusha katika mitandao ya kijamii na sehemu zingine. Nathamini na kuheshimu haki ya wanachama wetu kuonyesha hasira kwa jambo wasilolipenda. Hata hivyo nawasihi wanachama wetu wajizuie kuzusha mambo yatakayochochea chuki ndani ya chama na kukatishana tamaa.

Nashauri tuwaombe wanachama wetu wengine waandamizi wachukue jukumu hili, wakiwemo mama mwenyekiti na Katibu Mkuu, kuwataja tu kwa uchache.

Tunapotafari haya, tusisahau Malengo Mapana ya chama chetu tuliyojiwekea katika uchaguzi huu. Ni bahati nzuri kwamba tumefanikiwa kuweka wagombea wa ubunge na Udiwani katika kata na katika majimbo mengi. Tusiyumbe.
Ahsanteni.
Kitila Mkumbo 
17 Agosti 2015

Saturday, August 15, 2015

MAKONDA AMLIPUA MAGHUFULI


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bwana Paul Makonda amlipua Maghufuli. Sakata hilo limetokea usiku huu katika mashaindano ya kutafuta vipaji katika Wiliya hiyo. Alichokisema kuhusiana na Maghufuli, tunanukuu; 

"Mh. Rais nisingependa kuzungumzia swala la barabara kwa sababu swala hili limeshaundiwa tume. Lakini wananchi wanafahamu namna magari yao yanavyoharibika kutokana na barabara zinazojengwa chini ya kiwango." Mwisho wa kunukuu.

Ikumbukwe kuwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia ujenzi wa barabara ni Waziri wa Ujenzi Bwana Maghufuli ambaye ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Hili likipokelewa na wapinzani wake laweza kumharibia Maghufuli. We unaonaje kwa hili?


ARUSHA HIZI SASA SIFA!!! YAIFUNIKA DAR NA MBEYA. JIONEE MWENYEWE HII MISIFA





























MUDA HUU KINACHOENDELEA ARUSHA UJIO WA LOWASSA








USHAWAHI KUMUONA LEMBELI KAPIGA GWANDA? INGIA HAPA UMUONE ALIVYOTOKELEZEA

VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO