Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, July 29, 2013

MJINI MANYONI, JAMAA AFIA GUEST

Manyoni.
Kijana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake amekutwa amefariki katika Nyumba ya kulala wageni hapa mjini Manyoni, mtu huyo ambaye chanzo cha kifo chaka mpaka sasa hakijajulikana, amefia katika nyumba ya kula wageni inayojulikana kwa jina la Luxury Pub ambayo inapakana na Stetionary maarufu ya Calo.
 
Taarifa zaidi zinasema kuwa, wahudumu wa 'guest' hiyo waligundua tukio hilo majira ya saa kumi jioni na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Manyoni ambacho kipo jirani na 'guest' hiyo.
 
Wakati nafika eneo la tukio na polisi ndiyo walikuwa wanatoka na mwili wa marehemu huyo, hadi tunaingia mitamboni haijajulikana kama mtu huyo alikuwa ni mkazi wa Manyoni au alikuwa msafiri na haijajulikana mpaka mauti yanamkuta alikuwa peke yake au na mtu mwingine.

Chanzo: Mimi mwenyewe

Sunday, July 28, 2013

KUKAMATWA KWA NASSARI HII NDO KAULI YA LEMA

Godbless Lema - Arusha, TanzaniaKufuatia kukamatwa kwa Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki [Chadema] kupitia ukurasa wake wa facebook Mh. Godbless Lema ameandika hivi;

"Jana Jumamosi, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari aliitwa na Jeshi la Polisi Makao Makuu Arusha.


Mh Mbunge aliitikia wito na kufika kituoni hao na kuwekwa chini ya ulinzi akituhumiwa kushambulia na kujeruhi huko Makuyuni wakati wa Uchaguzi mdogo wa udiwani mwezi jana.

Polisi walijaribu kumuweka ndani, Mh Nassari akaridhia na kuanza kuvua saa yake, mkanda na kukabidhi bastola yake ili zoezi la kumuweka mahabusu kama walivyokuwa wamepanga litimia. Kumbuka angewekwa mahabusu jana wangemtoa Jumatatu. Mbunge wetu alifahamu hilo na aliridhia yote!


Kichekesho sasa kikawa na Polisi hao kuanza kuhaha wenyewe wasijue cha kufanya. ...Waligundua wamechemsha kumuweka mahabusu Arusha kwasababu kosa ni la Makuyuni kama ni kweli, wakajaribu kutafuta wenzao wa Makuyuni waje wamchukue wakaambiwa gari haina mafuta. Wakajishauri sana na wasijue cha kufanya.


Nje waandishi wakawa wanzidi kuongezeka na baadhi wakihoji sababu hasa za kumkamata Mbunge huyo na kumuweka mahabusu. Mchecheto ukawazidi, mwishowe wakaamua kumuachia tu arudi nyumbani na kumtaka akaripoti siku nyingine..
Huu ndio weledi wa Jeshi letu mpaka leo!"

Friday, July 26, 2013

KALA JEREMIAH AJISALIMISHA KWA EDWARD LOWASA

Huku ikisemekana kuwa Mh. Edward Lowasa akiendelea kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya maandalizi ya kugombea urais uchaguzi mkuu ujao 2015. Msanii wa Kizazi kipya Kala Jeremiah ambaye hapo awali katika wimbo wake ujulikanao kwa jina la Wimbo wa Taifa hatimaye aamua kujikabidhi kwa Edward Lowasa, kupitia ukurasa wake wa facebook hivi ndivyo Kala alivyoamua kujikabidhi kwa kada huyo wa CCM Mh. Edward Lowasa;




 MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.

KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.

BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.

MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.

NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI

NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.

MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.

MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.

KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.

tafakari chukua hatua






 
 


Thursday, July 25, 2013

MADAI YA MAMA SHAROMILIONEA KUDHULUMIWA MALI ZA MWANAE, HAYA NDIYO MAJIBU YA KITALE

Kitale Rais Wa Matejah
Kufuatia Mama mzazi wa marehemu Sharomilionea, kulalamika katika vyombo vya habari kuwa amedhulumiwa mali za mwanawe likiwemo gari, haya ndiyo majibu ya Kitale aliyekuwa swahiba mkubwa wa Sharo kwa watanzania na mama Sharo kupitia ukurasa wake wa facebook.

"Hii Ni Kwa Ajili Ya WATANZANIA WOTE: MaREHeMu sHaRo Milionea aliacha GARi aina ya OPA Naomba kuwambia Watanzania ILE gari aipo chini yangu mm Gari ipo Chini ya MUDY SUMA Ambaye ni mwenye Gari ambayo marehemu alipata nayo ajari Na MAMA Yake SHARO kulalamika kwenye vyombo vywa HABARI pia ni sawa na ni Haki yake kwa sababu mwenye gari ALIAHAIDI kusamehe gari yake ambayo marehemu alipata nayo ajari ila aliomba kukaa na gari ya marehemu kwa muda mfupi ili aweze kununua gari nyngne sasa kinachomshangaza mama MWaKa sasa UNakwenda gari aijauzwa wala nini kwa hiyo mama anaisi mm na mudy letu ni moja hapana mzazi wng mm nipo pamoja na wewe na WATANZANIA wote Naomba MUELEWe Hvyo gari sinayo mm..MAANa Kila MUaNdishi Wa Habari ANaniama MIMI"

Tuesday, July 23, 2013

JINA LAKO LINAANZIA NA HERUFI GANI? TAZAMA HAPA TABIA NA SIFA ZA WATU WENYE JINA LINALOANZIA NA HERUFI KAMA LAKO


HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.

HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anap
otaka kulinda vilivyo katika himaya yake.

HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.

HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.

HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.

HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.

HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.

HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.

HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.

HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.

HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.

HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.

HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.

HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.

HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.

Kwa msaada wa:
                               http://mc-garab.blogspot.com



 

Thursday, July 18, 2013

KAMA ULIKOSA TUKIO! TAZAMA PICHA ZA NDOA/HARUSI NILIYOFUNGA NA REGINA S. MAFFA

 
Hizi ni baadhi ya picha siku nilipofunga ndoa na Regina katika Kanisa Katoliki la Kurasini, siku ya Jumamosi tarehe 15/06/2013 kama ulikosa kuhudhuria na ulipenda uwepo, usijali, nimekuletea baadhi ya picha za tukio Zima nadhani utafurahia, twende kazi.....
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Nawashukuru wote mliotuunga mkono katika jambo hili, Mungu awabariki sana, kama unataka kuona Send off ilikuwaje! bofya hapa  http://fvenance.blogspot.com/2013/05/sherehe-ya-send-off-ya-regina-s-maffa.html

 
 



Friday, July 12, 2013

TAFSIRI NA UKALIMANI

TAFSIRI NA UKALIMANI

 
Tafsiri [Translation]

Imeandaliwa na Mwl. Venance. F
Anapatikana kwa simu: 0715 33 55 58,
 barua pepe: furahavenance@gmail.com 
 

Dhana  ya Tafsiri.

Tafsiri imefasiliwa kuwa, ni Kutoa mawazo kutoka katika lugha moja kwenda lugha nyingine bila ya kubadilisha maana. [TUKI 2002: 271]

Catford [1965:20] anasema tafsiri ni, “Kuchukua mawazo yaliyo katika maandishi kutoka lugha moja {lugha chanzi} na kuweka badala yake mawazo yanayolingana katika lugha nyingine {lugha lengwa}.

Vilevile imefasiliwa kuwa ni “Mawazo yaliyotolewa kutoka lugha moja hadi lugha nyingine.”

 TUKI [2002: 271] Tafsiri ni kueleza maana ya maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.



Maana zote hizo tulizoziangalia, utaona kuwa, kuna mambo matatu muhimu yanayojitokeza, mambo hayo ni:   


(i)                 Mawazo yanayotakiwa kutafsiriwa sharti yawe katika maandishi.

(ii)               Mawazo au ujumbe kati ya lugha chanzi na lugha lengwa sharti yalingane.

(iii)             Tafsiri inaweza kuwa kutoa maana ya maneno au mawazo.

Baada ya kuangalia maana ya tafsiri, sasa tuangalie maana ya mfasiri na sifa anazotakiwa kuwa nazo mfasiri:

Mfasiri

Mfasiri ni mtu anayefanya tafsiri kutoka lugha moja hadi lugha nyinge.[TUKI:2000:165]

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, mfasiri ni mtu anayehamisha mawazo kutoka lugha moja (lugha chanzi) kwa kutumia lugha nyingine ili mawazo hayo yaeleweke na watu wasiojua au kuielewa lugha chanzi, na mawazo hayo sharti yawe katika maandishi.



                                                      Sifa za mfasiri bora

Mfasiri bora anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

    Ã˜      Awe na ujuzi wa lugha fasaha, hii ina maana kuwa awe anajua kwa ufasaha lugha zote mbili, yaani lugha chanzi na lugha lengwa.

      Ø      Awe na ufahamu mkamilifu wa ujumbe au mada iliyoandikwa katika matini chanzi na uwezo au jinsi ya kuelezea ujumbe au mada hiyo kwa ufasaha katika lugha lengwa.

Ø      Awe amesoma maandishi ya matini chanzi hadi ayafahamu kinaga ubaga halafu aweze kuyafikiria katika lugha lengwa.


                                              Historia ya Tafsiri Afrika mashariki

Taaluma hii ya tafsiri ina historia ndefu hapa dunia tangu kale, lakini kwa hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla historia hii ya tafsiri haina historia ndefu kwani inaanzia karne ya 19 ambapo wamisionari walitafsiri vitabu mbalimbali vya kikristo ikiwemo biblia kutoka lugha ya kiingereza kwenda Kiswahili na lugha nyingine za makabila makubwa nchini Tanzania.

Na hata wakati wa utawala wa kikoloni hasa waingereza walitafsiri maandiko mbalimbali ya taaluma na fasihi ya Ulaya kwa lugha ya Kiswahili Na hata baada ya uhuru wapo wazalendo waliofanya juhudi za kutafsiri vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili mfano mzuri ni Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius K. Nyerere ambaye alitafsiri vitabu viwili vya mwandishi mashuhuri wa tamthiliya wa Uingereza William Shakespeare ambavyo ni: Juliasi Kaizari [1963] na Mabepari wa Venisi[1969] {Tazama pia Mwansoko na wenzake 2006 : 5}

Mfano wa tafsiri ambazo zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ni pamoja na ya,Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa ambayo imetafsiriwa na Abdilatif Abdalla, House boy ya Ferdinand Oyono iliyotafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele. Juliasi Kaizari na Mabepari wa Venisiza zaWilliam Shakespeare zilizotafsiriwa na Julius K. Nyerere, Hekaya za Abunuwasi, Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa, Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton na Mashimo ya Mfalme Suleiman kilichotafsiriwa na Sir Rider Haggard, Takadini,kimetafsiriwa na Mathews Bookstore and Stationers, Nitaolewa Nikipenda ambacho kimetafsiriwa na Crement M. Kabugi. vitabu vingine vilivyotafsiriwa ni kama vile; Orodha, Barua Ndefu Kama Hii n.k.

Mpaka sasa wataalamu mbalimbali wamekuwa wakiendelea kutafsiri maandiko mbalimbali kama vile mikataba na ripoti mbalimbali za kimataifa, sheria ambazo mwanzo zilikuwa zikiandikwa kwa lugha ya kiingereza, vitabu vya kiada na ziada, kazi za kifasihi, n.k



Mambo ya kuzingatia katika tafsiri

Katika sehemu hii tutaangalia mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa katika tafsiri, hivyo basi, tutagawa mambo hayo ya kuzingatia katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza mchakato wa kutafsiri na sehemu ya pili, tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa mchakato wa kutafsiri. Tukianza na:


[a]  Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza mchakato  wa kutafsiri.


1.     Kwanza unatakiwa kusoma matini nzima.

Mtu anayetaka kutafsiri matini yoyote ile jambo la msingi la kuzingatia ni kuisoma matini nzima tena kwa umakini ili kuelewa maudhui ya matini chanzi, kuweka alama sehemu za matini zenye utata au zisizoeleweka vizuri,  hii itamsaidia kubaini ni aina gani ya marejeo muhimu yatakayomsaidia kutafsiri mfano wa marejeo hayo ni kama kamusi, ensiklopedia, orodha ya msamiati na istilahi mpya.

2.    Unatakiwa kubaini lengo la matini chanzi

Baada ya kuisoma matini chanzi, je! Umeweza kubaini lengo la matini chanzi ni nini? Kubaini lengo la matini kutakusaidia kuweza kutafsiri bila kutofautiana/kukinzana na lengo la matini chanzi, mathalani, matini mbili tofauti zinaweza kueleza jambo lilelile na kutumia data zilezile lakini mtindo wa lugha uliotumika unaweza ukaonesha mitazamo miwili tofauti.

Hebu angalia tamthilia ya Mercant of Venice, iliyoandikwa na William Shakespeare na kutafsiriwa na Mwalimu J.K. Nyerere kwa lugha ya Kiswahili na kuitwa Mabepari wa Venisi, kumbuka kuwa tamthiliya hiyo ingeweza kuitwa pia Wafanyabiashara wa Venisi lakini ukiangalia tafsiri ya kwanza [Ya Mwalimu Nyerere] inatupa hisia hasi wakati ya pili huwezi kupata hisia yoyote.{Mwansoko na wenzake 2006:15}

3.     Unatakiwa kubaini hadhira/ wasomaji lengwa.

Kabla ya mfasiri hajabaini wasomaji au hadhira ya wasomaji wa matini yake ya tafsiri ni vema kwanza akaibaini hadhira ya matini chanzi na ndipo abaini hadhira/ wasomaji mahususi wa matini yake ya tafsiri, maswali anayotakiwa kujiuliza mfasiri ili aweze kuibaini hadhira ya matini yake ya tafsiri ni: je msomaji wa tafsiri yake ni nani? Ana kiwango gani cha elimu, ni msomi wa kawaida au msomi aliyebobea? Wana umri gani na ni jinsia gani? Je hadhira yake imo katika tabaka gani katika jamii? Baada ya kupata majibu ya maswali hayo, mfasiri atakuwa ameibaini hadhira yake,na hii itamsaidia mfasiri kuamua umbo la matini yake, kama ataamua iwe katika umbo la gazeti, jarida, kijarida, n.k. jambo la kuzingatia umbo la matini ya tafsiri ishabihiane na hadhi ya umbo la matini chanzi. Kwa kuibaini hadhira ya matini lengwa itamsaidia mfasiri kuamua kuirahisisha tafsiri yake au kuifanya iwe ngumu kutegemeana na uwezo wa hadhira ya tafsiri lengwa.



4.    Unatakiwa kubaini mtindo wa matini chanzi.

Vilevile, mfasiri anatakiwa kujua, matini chanzi imetumia mtindo gani katika kuwasilisha maudhui yake, imetumia mtindo wa kirasimu? Au imetumia mtindo wa kitaaluma? Je imetumia mtindo wa kiuandishi wa habari au mtindo wa kimawasiliano yasiyo rasmi? Je ametumia lugha rasmi au ya mtaani? Na inatakiwa mtindo wa matini chanzi ilingane na ile ya matini lengwa. Tazama mifano ifuatayo:


Kingereza: Please, Sir do no mind it! If I arrive earlier I’ll wait for you

Kiswahili: Mkubwa! Kausha tu! Na kama nitatia maguu mapema,

                   nitakusikilizia  Palepale


Ukiangalia mfano huo, utaona kuwa, mitindo iliyotumika katika sentensi hizo ni mitindo miwili tofauti, katika mfano tuliouangalia katika lugha chanzi, mtindo wa lugha uliotumika ni mtindo rasmi, wakati katika tafsiri [lugha lengwa] mtindo uliotumika ni mtindo wa lugha ya mtaani, jambo ambalo si zuri katika tafsiri. Mtindo wa lugha lengwa sharti ulingane na mtindo wa lugha chanzi.

hivyo katika mfano huo, mtindo sahihi ungetakiwa kuwa;


    Tafadhari! usijali! kama nitafika mapema, nitakusubiri.

5.     Kusoma matini kwa mara ya mwisho

Jambo lingine la kuzingatia ni kuisoma upya matini chanzi. Katika kipengele hiki, mfasiri anashauriwa aisome matini chanzi kwa mara ya mwisho huku akipigia mstari au kuandika katika kidaftari kidogo msamiati, istilahi na misemo muhimu ya matini chanzi kama vile, methali, nahau maneno ya kitamaduni yasiyotafsirika, majina maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au kuyaandika katika kidaftari kidogo ili iwe rahisi kwa mfasiri kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza kutafsiri  lakini pia kumsaidia mfasiri asiyasahau wakati wa kutafsiri.


Hayo ndiyo mambo ambayo, mfasiri anatakiwa kuyazingatia kabla hajaanza mchakato wa kutafsiri. Hivyo basi, sasa tugeukie upande wa pili ambao ni:


     [b]   Mambo ya kuzingatia wakati wa mchakato  wa kutafsiri.


1.     Maandalizi ya kutafsiri

Katika hatua hii, mfasiri anatakiwa kufahamu vizuri maudhui ya matini chanzi, ujumbe wake, mtindo wa matini na kuwekea alama sehemu zenye utata au zisizoeleweka vizuri, anashauriwa kupigia mstari au kuandika katika kidaftari kidogo msamiati, istilahi na misemo muhimu ya matini chanzi kama vile, methali, nahau maneno ya kitamaduni yasiyotafsirika, majina maalumu, n.k. kwa kupigia mstari au kuyaandika katika kidaftari kidogo ili iwe rahisi kwa mfasiri kuyatafutia visawe vyake kabla hata ya kuanza kutafsiri  lakini pia kumsaidia mfasiri asiyasahau wakati wa kutafsiri au kuyatolea ufafanuzi zaidi katika tafsiri yake.

2.     Uchambuzi wa matini chanzi

Katika hatua hii, mfasiri anatakiwa kuchunguza kwa makini maneno, methali, nahau, misemo pamoja na maelezo mengine ya matini chanzi aliyoyaandika au kuyapigia mstari katika hatua ya maandalizi na kuyatafutia visawe vyake katika lugha lengwa, hapa mfasiri anashauriwa kutumia marejeo mbalimbali kama vile, kamusi, ensiklopedia, orodha ya msamiati na istilahi mpya.


Mfasiri anatakiwa kuwa na shajara au daftari dogo kwa ajili ya kuandika na kuhifadhi maneno na maelezo muhimu ya matini chanzi na visawe vyake, visawe vinavyoonekana kufaa viorodheshwe vizuri ili iwe rahisi kuvirejelea wakati wa kutafsiri, vilevile mfasiri kama ataona kuwa matini chanzi ni ndefu sana, anashauriwa kuigawa matini hiyo katika sehemu ndogondogo kama vile, sura, aya au sentensi na kuanza kushughulikia sehemu moja baada ya nyingine.

3.     Uhawilishaji

Uhawilishaji ni uhamishaji wa mawazo kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa, au uhamishaji wa mawazo au ujumbe kutoka matini asilia kwenda matini ya tafsiri. Hii ina maana kuwa katika hatua hii, visawe vya kisemantiki [kimaana] vya matini chanzi vilivyobainishwa katika hatua ya uchambuzi huamishwa katika matini lengwa [kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa] na kupangwa vizuri kisarufi na kimantiki ili fasiri hiyo iwe na maana kwa wasomaji wake.

4.    Kusawidi /Kuandaa rasimu ya kwanza ya tafsiri.

Katika hatua hii, mfasiri huandika rasimu yake ya kwanza ili kupata picha fulani ya matini aliyoikusudia, katika uandaaji wa rasimu ya kwanza, kwa kufanya hivi, mfasiri anaweza kugundua kuwa anahitaji taarifa zaidi tofauti na alizozipata katika hatua ya uchambuzi, na hivyo kulazimika kuchunguza zaidi matini chanzi na hata kupekua zaidi na zaidi marejeo yake aliyoyaandaa kwa kuyatumia katika tafsiri. Jambo la kuzingatia, mfasiri anatakiwa wakati akihamisha mawazo au ujumbe azingatie umbo na lengo la matini chanzi ili kutoathiri tafsiri yake.


5.     Kudurusu / kuipitia rasimu ya kwanza

Baada ya kusawidi rasimu ya kwanza, mfasiri anatakiwa kuivundika rasimu yake ya tafsiri kati ya juma moja hadi mawili baada ya kukamilika kwake na kuanza kuidurusu/ kuipitia rasimu hiyo kwa jicho la kihakiki zaidi na kuangalia kama kuna makosa ambayo yamejitokeza katika rasimu yake au la na kuyafanyia marekebisho pale inapobidi.

6.     Kusomwa kwa rasimu ya tafsiri na mtu/watu wengine

Baada ya mfasiri kuipitia rasimu yake ya kwanza, na kuifanyia masahihisho kwa makosa yaliyojitokeza, anatakiwa kuwapa watu wengine waidurusu rasimu hiyo iliyofanyiwa marekebisho ili waipitie tena na kuirekebisha, hivyo basi wasomaji hao wanaweza  wakahakiki,wakashauri, n.k. Wasomaji hawa husaidia kuona kama tafsiri iko sahihi, inaeleweka na ina mtiririko mzuri wenye mantiki.


7.     Usawidi /Kuandika rasimu ya mwisho

Baada ya kupata maoni kutoka kwa wasomaji wa pili, mfasiri anaweza kuyatumia maoni, mapendekezo na maelekezo yao kusahihisha tena tafsiri yake na hatimaye kuandaa na kutoa rasimu ya mwisho ambayo itakuwa tayari kwa kusomwa na wasomaji.


                                               Njia / mbinu za Tafsiri

Zipo njia mbalimbali ambazo hutumika katika kutafsiri, baadhi ya njia hizo ni kama vile:

(i)                  Tafsiri ya neno kwa neno. [Word to word translation]

(ii)                Tafsiri sisisi.[ Literal translation]

(iii)               Tafsiri ya kimaana/uwazi.[ Semantic translation]

(iv)               Tafsiri ya kimawasiliano.[Communicative translation]


(i)                 Tafsiri ya neno kwa neno  [Word to word translation]

Hii ni aina ya tafsiri ambayo mofimu na maneno hufasiriwa yakiwa pweke pweke kwa kuzingatia maana zake za msingi bila kujali muktadha. Katika aina hii ya tafsiri mpangilio wa mofimu na maneno wa lugha chanzi hubakia vilevile bila kubadilika. Na kwa kawaida matini inayotafsiriwa huandikwa chini ya matini ya lugha chanzi. Tazama mifano ifuatayo ya tafsiri ya neno kwa neno:


Kiswahili: Alisoma hadi asubuhi

Kingereza: He/past/study/until/morning



Kiswahili: Alikimbia mpaka ofisini kwake

Kingereza: He/past/run/until/office/his



Kiswahili: Anasoma kitabu changu

Kingereza: He/present/book/my



Kiswahili: Walikula chakula chote

Kingereza: They/past/eat/food/all



Umuhimu wa njia hii, humsaidia mtu kuelewa muundo wa lugha chanzi na jinsi lugha chanzi inavyofanya kazi, kaina hii ya tafsiri hutumiwa na wataalamu wa lugha kuonesha namna  maumbo au muundo wa lugha chanzi ulivyo, lakini mapungufu yake ni kuwa, aina hii ya tafsiri huwa haitoi maana inayokusudiwa kwa uwazi zaidi.



(ii)               Tafsiri sisisi [ Literal translation]

Hii ni aina ya tafsiri ambayo maneno hufasiriwa yakiwa pweke pweke kwa kuzingatia maana za msingi katika lugha chanzi bila kujali sana muktadha lakini ni tafsiri inayofuata mfumo wa kisarufi hasa kipengele cha kisintaksia ya lugha lengwa. Ebu tuangalie mifano ifuatayo:

Kingereza: He was taken at the Central Police Station

Kiswahili: Alipelekwa kwenye kituo cha kati cha police.

Badala ya kuwa: Alipelekwa kituo kikuu cha polisi



(iii)             Tafsiri ya kisemantiki/maana au uwazi [Semantic Translation]

Hii ni aina ya tafsiri ambayo mfasiri huegemea zaidi kwenye lugha chanzi. Katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hufasiri kila neno katika sentensi jinsi lilivyo lakini kwa kufuata sarufi hususani vipengele vya kisemantiki na kisintaksia ya lugha chanzi. Inaitwa tafsiri ya kisemantiki kwa sababu, mfasiri anapofasiri hutakiwa kuweka mkazo kwenye maana ya matini kama ilivyokusudiwa na mwandishi wa matini chanzi.



Katika aina hii ya tafsiri, masahihisho au urekebishaji wa neno au jambo lolote unalodhani limekosewa haliruhusiwi isipokuwa unaweza kuweka hayo marekebisho au ufafanuzi katika tanbihi. Sasa tuangalie baadhi ya mifano ya aina hii ya tafsiri:



Kiswahili: Alikwenda mpaka hospitali

Kingereza: He went up to hospital


Kingereza: Jane married John

Kiswahili: Jane alimwoa John



Aina hii ya tafsiri, ina faida kubwa katika ukuaji wa lugha lengwa kwa kuingiza miundo ya misemo kutoka lugha chanzi, mathalani, lugha ya Kiswahili imepokea miundo mipya ya misemo kutoka lugha ya Kingereza, baadhi ya miundo hiyo ni kama vile:



Kiswahili: Usiku mwema          à    kutoka Kingereza: Good night

Kiswhili: Mabibi na mabwana   à   kutoka Kingereza: ladies and gentlemen

Kiswahili: Wako mtiifu               Ã    Kutoka Kiingereza: Yours Sincerel

Kiswahili: Naomba nichukue nafasi hii.. à Kutoka Kiingereza: May I take this opportunity…

                     [Tazama pia Mwansoko na wenzake: 2006]



(iv)              Tafsiri ya kimawasiliano/ huru [Communicative Translation]

Hii ni aina ya tafsiri inayomlenga msomaji [hadhira] wa matini lengwa, ambaye katika aina hii ya tafsiri hatarajii kukutana na ugumu wowote katika matini atakayoisoma, bali hutarajia kukutana na tafsiri nyepesi ya dhana za kigeni katika utamaduni na lugha yake kwa kadiri itakavyoonekana. Hivyo basi, mfasiri wa aina hii ya tafsiri yuko huru kutafuta maneno na mafungu ya maneno yanayolingana na maneno, methali, nahau, utamaduni na mazingira ya lugha lengwa, pamoja na kuwa tafsiri ya kimawasiliano kufuata sarufi ya lugha lengwa ni lazima pia ifuate utamaduni, mazingira na historia ya jamii ya lugha lengwa. Tuangalie mifano ifuatayo:



Kingereza: Jane married John

Kiswahili: John alimwoa Jane



Kingereza: No need to cry over spilt milk

Kiswahili: Maji yakimwagika hayazoleki



Kiingereza: What comes around goes arround

Kiswahili: Mla vya watu, naye vyake huliwa.


 
Kiswahili: Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli

Kiingereza: A friend in need is a friend in need
 

 
Kiswahili: Bahati haiji mara mbili

Kiingereza: Golden chance never comes twice



Aina hii ya tafsiri hulenga kutoa athari ile ile au inayokaribiana kwa hadhira ya matini lengwa kama ilivyo kwa hadhira ya matini chanzi[ matini asilia], hii ni aina ya tafsiri ambayo hutumika sana kufasiri mawazo ya kigeni katika lugha na mazingira mapya, mawazo ambayo huelezwa katika misingi ya lugha, utamaduni na mazingira yanayoeleweka kwa hadhira ya matini lengwa. 



Ebu tuangalie baadhi ya mifano tuliyoiangalia katika tafsiri ya Kisemantiki [maana] tunavyoweza kutafsiri katika njia ya tafsiri ya kimawasiliano:

Kiingereza                                                  Kiswahili

Good night                                                Lala salama

Ladies and Gentlemen                              Ndugu zangu

Yours Sincerely                                        Ni mimi

May I take this opportunity to…             Naomba mnisikilize



Hivyo basi, katika aina hii ya tafsiri, mfasiri hutafuta methali au misemo inayopatikana katika lugha lengwa inayohusiana au kukaribiana na ile ya lugha chanzi. Ebu jaribu kutafsiri misemo/methali zifuatayo ya lugha ya Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza:



Adhabu ya kaburi aijuaye maiti

Asiyekubali kushindwa si mshindani

Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa

Chema chajiuza kibaya chajitembeza

Dua la kuku halimpati mwewe

Bandubandu humaliza gogo

Jogoo wa shamba hawiki mjini

La kuvunda halina ubani

Mtegemea cha nduguye  hufa masikini


Faida ya aina hii ya tafsiri, humfanya mfasiri kuwa huru kutumia maneno au mafungu ya maneno ambayo huweza kutoa athari ile ile au inayokaribiana na maneno au mafungu ya maneno katika matini ya lugha chanzi, lakini mapungufu ya aina hii ya tafsiri huweza kutokea iwapo mfasiri ataamua kuegemea mno kwenye mawazo, historia, mazingira au itikadi ya lugha lengwa. Ebu tuangalie mifano ifuatayo:

 
Kingereza: The Merchant of Venice

Kiswahili: Mabepari wa Venisi

 
Ukiangalia mfano huo utaona kuwa, The Merchant of Venice, tamthiliya iliyoandikwa na William Shakespeare, ingefaa pia kufasiriwa kuwa, Wafanyabiashara wa Venisi, lakini Mwalimu J.K Nyerere aliamua kuifasiri kuwa, Mabepari wa Venisi kutokana na kuwa Nyerere ndiye mwasisi wa itikadi ya Ujamaa nchini Tanzania, hivyo aliegemea katika itikadi kufasiri.



Hivyo basi, mtu anapokuwa anafanya kazi ya kufasiri, maandishi yo yote kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine atajikuta akiangukia katika moja wapo ya njia tulizozijadili hapo juu, lakini ikumbukwe tafsiri ya neno kwa neno ni nadra sana kutumiwa na wafasiri wengi, na njia hizo huweza kuingiliana katika matini moja ya tafsiri.

                                        
Ukalimani  [Interpritation]

Ukalimani ni nini?
Ukalimani imefasiliwa kuwa ni, uhusishaji wa kuhamisha maana kutoka lugha moja (lugha chanzi) kwenda lugha nyingine (lugha lengwa) katika mazungumzo. Hivyo basi tunaweza kusema pia, ukalimani ni hali ya mtu kuhamisha mawazo ya kinachozungumzwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine katika mazungumzo. Hii ina maana kuwa ukalimani ni lazima uhusishe pande mbili, upande wa kwanza sharti awepo mtu anayezungumza lugha fulani na upande mwingine kunakuwa na mtu ambaye anasikiliza hicho kinachozungumzwa na kuyarudia hayo yanayozungumzwa kwa kutumia lugha nyingine tofauti na ile iliyotumiwa na mazungumzaji wa kwanza.

Hivyo basi, ukiangalia, maana hiyo tuliyoiangalia utaona kuwa, ukalimani ni taaluma inayohusu mazungumzo wakati tafsiri yenyewe uhusu maanadishi, kwa maana hiyo huwa tunatafsiri maandishi kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine na tunakalimani mazungumzo kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine.

Ukalimani ulianza pale ambapo mataifa mbalimbali yenye kuzungumza lugha tofauti tofauti yalipoanza kuingiliana na kushirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii, kisiasa, kichumi na kiutamaduni, kwa mfano ujio wa wageni Afrika Mashariki kama vile Waarabu, Wajerumani na Waingereza ili waweze kuwasiliana na wenyeji wao waliambatana na watu ambao walikuwa wakiwatumia kama wakilamani wao.

Kwa sasa hivi ukalimani umekuwa kama taaluma muhimu, ukalimani unafanyika katika mahakama, kanisani, katika mikutano ya kimataifa, mahubiri ya kidini, n.k na kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna vifaa maalumu ambayo hutumika kukalimani mazungunzo kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine, ambayo huvaliwa masikioni katika kumbi za mikutano. Na sasa ni taaluma inayofundishwa katika shule za sekondari na elimu ya juu kama ilivyo kwa tafsiri kutokana na umuhimu wake.

Mkalimani ni mtu muhumi sana katika kufanikisha mawasiliano kwa watu wanaotumia lugha mbili tofauti, au lugha inayotumika katika eneo hilo msikilizaji haielewi na haijui na ndiyo maana utakuta wakalimani wakihitajika mahakamni, mikutano ya kimataifa, katika mahubiri ya kidini au mahali popote pale ambapo wazungumzaji hawawezi kuelewana kwa kuwa wanatumia lugha tofauti.

Sifa za mkalimani bora

Ø      Awe mtu anayezielewa lugha chanzi na lugha lengwa vizuri

Ø      Awe ni mtu ambaye ameishi pande zote za lugha anazozikalimani ili kuelewa mila na desturi za watumiaji wa lugha hizo.

Ø      Awe stadi wa ukalimani, hapa inatakiwa awe na uhodari wa kukalimani, kuzungumza vizuri, maneno kusikika, awe na uwezo wa kukalimani neno kwa neno au sentensi na sentensi, kutumia ishara zinazoambatana na ishara za mzungumzaji wa lugha chanzi na hata kutumia mtindo anaodhani unaweza kuwavutia wasikilizaji wake.

Ø      Muadirifu, ambaye hawezi kupotosha au kubadili ukweli wa kinachozungumzwa, nah ii ni muhimu kwa sababu wakalimani hutumika hadi mahakami hivyo kama si mwadirifu huweza kuufanya upande mmoja ukakosa haki inayostahiri.

Ø      Asiwe mbaguzi, hapa ina maana mkalimani asiamue kupotosha ukweli wa kile kinachozungumzwa kwa kuwa tu kinaendana kinyume na itikadi yake ya kisiasa, kidini, kiutamaduni, n.k. wala asiangalie jinsia ya mtu umri au hali ya mtu anayemfanyia ukalimani.

Kielelezo: 1


  Namna mkalimani anavyotakiwa kuwa
   sambamba na mzungumzaji
 
Mambo ya kuzingatia katika Ukalimani

Kwa ujumla yapo mambo kadha wa kadha, ambayo mkalimani anatakiwa kuyazingatia anapotaka kufanya ukalimani, mambo hayo tunaweza kuyagawa katika makundi mawili, ambayo ni:

  1. Kabla ya kuanza ukalimani

Katika hatua hii, mkalimani anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

(a)   Awe na uelewa mzuri wa lugha zote anazotaka kukalimani, hapa tuna maana kuwa awe na uwezo wa kuzungumza na kuelewa lugha chanzi na lugha lengw, hii itasaidia mkalimani kutopotosha kile kinachozungumzwa na mzungumzaji wa lugha chanzi.

(b)   Awe anaijua historia na utamaduni wa jamii zote mbili, yaani ile ya lugha chanzi na ile ya lugha lengwa.

(c)    Kama ni ukalimani rasmi, ni vizuri kwa mkalimani akamjua mzungumzaji wa lugha chanzi, ni vema pia ukafanya naye mazungumzo kidogo ili kumzoea, na kutambua vionjo vyake ili iwe rahisi kwa mkalimani pindi atakapokuwa anafanya ukalimani asionekane kama mgeni.

(d)   Vilevile ni muhimu kwa mtu anayekalimani, akawa na uelewa mzuri wa mada inayozungumzwa, hii itamrahisishia mkalimani katika ukalimani wake.

  1. Katika ukalimani wenyewe

Mkalamani anapokuwa amesimama mbele ya hadhira [wasikilizaji] pamoja na mzungumzaji wa lugha chanzi kwa ajili ya kuanza ukalimani, anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:

(a)   Kuwa makini katika kusikiliza kile kinachozungumzwa na mzungumzaji wa lugha chanzi ili kuepuka kuachwa mahali na kuepuka kumuomba mzungumzaji kurudia mara kwa mara.

(b)   Itambue hadhira ya lugha lengwa, ni watu wa namna gani, wana kiwango gani cha elimu, ni wasomi wa kawaida au waliobobea, ni watu wa jinsia na umri gani,? Hii itakusaidi kujua aina ya msamiati na miundo ya tungo utakayoitumia, kama iwe rahisi au migumu kutokana na hadhira yako ilivyo.

(c)    Tumia mitindo unayodhani itaeleweka vema na hadhira/ wasikilizaji wa lugha lengwa, kwa mfano kama hadhira yako ni vijana, jaribu kutumia mitindo inayopendwa na vijana, kama wasikilizaji wako ni watu rasmi na we huna budi kuwa rasmi.

(d)   Weka mkazo sehemu ambazo mzungumzaji wa lugha chanzi anaweka mkazo ili kuepuka utofauti yako na mzungumzaji wa lugha chanzi, na hata kuepuka kuathiri lengo la mzungumzaji wa lugha chanzi.

(e)    Unatakiwa pia kutumia ishara zinazotumiwa na mzungumzaji wa lugha chanzi, hii itawafanya wasikilizaji waamini kile kinachozungumzwa na mzungumzaji wa lugha chanzi ndiyo kilekile kinachozungumzwa na mkalimani.

Kielelezo: 2

Mkalimani anatakiwa kutumia ishara zinazotumiwa na mzungumzaji.

na si kama inavyoonekana katika mchoro huu. Tazama kielelezo na. 2

(f)     Usiwe muda mwingi unamtazama mzungumzaji wa lugha chanzi na kusahahu kuitazama hadhira yako, hivyo unatakiwa kuitazama hadhira yako ili kugundua kama wako pamoja na wewe au kuna sehemu hawajakuelewa ili uweze kuwafafanulia zaidi.

(g)   Muombe mzungumzaji wa lugha chanzi kurudia sehemu unayodhani hujaisikia au hujaielewa vizuri, kwani ni makosa kwa mkalimani kukalimani sehemu au jambo ambalo hukulisikia vizuri au kulielewa.

Hivyo basi hayo ndiyo mambo muhimu ambayo mkalimani anatakiwa kuyazingatia anapokuwa anafanya ukalimani. Jambo la kuzingatia, mkalimani hutakiwa kuingiza hisia zako unapokuwa anafanya ukalimani. na ukalimani mzuri unawezekana kwa kiwango ambacho mila na desturi zote yaani za lugha chanzi na lugha lengwa zinalingana ama kushabihiana.

                                                    Dhima za Tafsiri na Ukalimani

Tafsiri na Ukalimani ina dhima zifuatazo:



F     Hutuwezesha kujifunza lugha tofauti.

Kati ya mazoezi mazuri anayoweza kutumia mtu katika kujifunza lugha nyingine, basi zoezi la kutafsiri au kukalimani mara kwa mara humsaidia mtu kujifunza lugha kwa urahisi zaidi, kwani kwa kufanya tafsiri ya mara kwa mara kutamsaidia mtu kugundua miundo na vipengele mbalimbali vya lugha na jinsi vinavyofanya kazi katika lugha anayojifunza.





F     Hutumika kama njia ya mawasiliano.

Kutokana na maingiliano ya mataifa mbalimbali yanayotumia lugha tofauti tofauti, tafsiri hutumika kurahisisha mawasiliano baina ya makundi ya watu wanaotumia lugha tofauti tofauti, hutumika kutolea maelezo ya kibiashara kama vile maelekezo ya jinsi ya kutumia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nje au zinazouzwa nje ya nchi, katika matangazo ya kitalii ili kuwavutia watalii kutoka mataifa mbalimbali, vilevile hutumika katika vyombo vya habari, tafsiri pia inatumika katika nyaraka rasmi, mikataba, vitabu vya ziada na kiada, lakini pia ukalimani hulahisisha mawasiliano miongoni mwa watu wanaozungumza lugha tofauti.



F     Tafsiri na Ukalimani hutumika kueneza utamaduni.

Tafsiri imekutanisha lugha na tamaduni mbalimbali duniani na kusababisha tamaduni na lugha hizo kuathiriana, kwa mfano mara baada ya waarabu kuingia Afrika Mashariki na vitabu mbalimbali vya Kiarabu na Kiislamu kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ilisababisha utamaduni wa Kiswahili kuathiriwa na utamaduni wa Kiarabu na Kiislamu kutoka na kuiga kwa mambo mengi kutoka huko, lakini pia hata walipokuja wazungu na kutafsiri vitabu vyao vya kifasihi, kutafsiriwa kwa Biblia, n.k. ilisababisha pia utamaduni wa Mswahili kuathiriwa na utamaduni wa Ulaya.



F     Tafsiri na Ukalimani ina dhima ya kuwasilisha ujumbe wa manufaa kwa watu ambao hawafahamu lugha chanzi [lugha asilia]



                      Changamoto/ mapungufu katika tafsiri na Ukalimani

Mfasiri katika kazi yake ya kufasiri hukumbana na changamoto mbalimbali, ambazo huweza kusababisha tafsiri kuwa na mapungufu ya hapa na pale. Baadhi ya changamoto au mapungufu hayo ni kama vile:



(i)                 Tofauti za kiisimu kati ya lugha chanzi na lugha lengwa.

Tofautui za maumbo, miundo na maana kati ya lugha ya Kiswahili na lugha ya Kingereza wakati mwingine husababisha matatizo au upungufu katika tafsiri na ukalimani. Kwa mfano maumbo ya vitenzi vya Kiingereza huruhusu kauli nyingi elekezi kutoonesha umoja au wingi wa wahusika wala majina ya vitu mahususi vinavyoambatana na maelekezo yanayotolewa tofauti maumbo ya vitenzi vya Kiswahili ambavyo huonesha umoja na wingi wa wahusika na hata kuwa na majina ya vitu husika, tazama mifano ifuatayo kama ilivyotolewa na, Mwansoko [2006]



Kingereza                           Kiswahili

No parking       à           Usiegeshe gari hapa [je kisichoruhusiwa kuegeshwa ni gari tu?]

No Smoking     à            Usivute sigara[ Je ni sigara tundiyo hairuhusiwi kuvutwa?]

Arrivals           à             Wanaowasili

Departures      à            Wanaosafiri



Vilevile tofauti za maana kati ya lugha ya Kingereza na Kiswahili huweza kuathiri tafsiri au ukalimani, mathalani:





Kiswahili                     Kingereza

Wasiojiweza         à     Disabled [Siyo wote wasiojiweza ni walemavu]

                                                    [na siyo walimavu wote hawajiwezi]

Wezi wa mifukonià     Pickpockets [Hawaibi kwenye mifuko, wanaiba kutoka mifukoni]

 
(ii)               Tofauti za mitindo kati lugha chanzi na lugha lengwa

Tofauti za mitindo ya uzungumzaji pia, huweza kuathiri tafsiri na ukalimani na hii ni kwa sababu unaweza kukuta kuna mitindo fulani inaweza kutumika katika muktadha fulani lakini ikishindwa kupata tafsiri katika lugha nyingine katika muktadha ule ule.mathalani:



                    Kingereza:                                                   Kiswahili                                                    

(i)                 Thou shalt not steal  [mtindo wa kidini]   à     Usiibe 

                  Do not steal [mtindo wa kawaida]             à     Usiibe

(ii)               Lend me your ears [mtindo wa kishairi]   à  Naomba mnisikilize

May I have your attention [kawaida]        à  Naomba mnisikilize

Tafsiri zote tulizoziangalia katika mfano wa (i) na (ii) zimetoa maana au taarifa ili ile iliyomo katika matini chanzi lakini tafsiri hizo hazikuzingatia mtindo wa lugha iliyotumika katika matini chanzi.



(iii)             Tofauti za kitamaduni kati ya lugha chanzi na lugha lengwa

Tofauti za kiutamaduni, yaani taofauti za kimila, desturi na mazingira ya watumiaji wa lugha chanzi na lugha lengwa huweza kufanya tafsiri au ukalimani kuwa mgumu, kwa mfano, katika utamaduni wa Waingereza wana milo minne wakati Waswahili wana milo mitatu na hii hupelekea kuwa vigumu kupata dhana za milo ya hiyo ya Waingereza katika dhana ya Kiswahili. Mfano:



Waingereza wana:             Waswahili wana:

  Breakfast  ------------------ Kifungua kinywa

  Lunch …………………... Chakula cha mchana

  High tea ……………………?

  Dinner ……………………Chakula cha jioni

  Supper …………………….?

 
Kwa hiyo ukiangalia mifano hiyo, utaona kuwa, high tea na supper kuzipata dhana zake katika lugha ya Kiswahili ni ngumu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuwa na milo kama hiyo kwa siku. Lakini pia inakuwa vigumu kupata tafsiri ya vyakula kama vile ugali, makande katika lugha ya Kiingereza kutokana na kutokuwa na vyakula vya aina hiyo.


(iv)              Tofauti za kiitikadi kati ya lugha chanzi na lugha lengwa

Tofauti za kiitikadi pia huweza kuathiri tafsiri na ukalimani, na hii ni kwa sababu, utakuta wafasiri wengi hususani waandishi wa habari kuegemea katika itikadi zaidi, kwa mfano:

 

Kingereza                            Kiswahili

Bussnessman      Ã        mlanguzi  [tafsiri hii inatokana mfasiri kuathiriwa na itikadi

                                                          ya ujamaa]

                                      mfanyabiashara [tafsiri hii inatokana mfasiri kuathiriwa na  

                                                                   itikadi ya ubepari]
 

Freedom fighter   à      wapigania uhuru [Tafsiri ya vyombo vya habari vya 

                                                                        Tanzania wakati wa kupigania uhuru]

                                          Magaidi [Tafsiri ya idhaa ya BBC na Radio za Afrika

                                                          Kusini wakati huo]

Hivyo basi kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, ukalimani mzuri unawezekana kwa kiwango ambacho mila na desturi zote yaana za lugha chanzi na lugha lengwa zinalingana ama kushabihiana.

Na kutokana na umuhimu wa taaluma hii ya tafsiri na ukalimani, serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa Bakita [BAKITA] imeanzisha idara maalumu ya Tafsiri na Ukalimani, na idara hiyo ina majukumu yafuatayo:

Ø      Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha mbalimbali kwa masharika, idara, wizara, balozi na watu binafsi.

Ø      Kuratibu na kutoa huduma za ukalimani kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa na katika shughuli za masharika, makampuni na watu binafsi.

Ø      Kupitia na kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na asasi mbalimbali au wafasiri wa nje.

Ø      Kutoa ushauri kuhusu masula ya tafsiri na ukalimani.     

                                              MAZOEZI
& Zoezi la kwanza

(a) Tafsiri matini ifuatayo ya Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza.



                                                                    MTO

(Siku ifuatayo, asubuhi. Ngoswe na Mitomingi wako kazini. Wanafika nyumba moja).

MITOMINGI:     Hodi! Hodi! Wenyewe! (Kimya, hakuna sauti itokayo). Hodi wenyewe

                             (Kimya) Labda hawajaamka.

NGOSWE:         Kama bado wamelala tuwaache kwanza tuwarudie baadaye.

MITOMINGI:    Mimi naona itakuwa shida shida kwani nyumba za hapa zimesambaa

                            mno.hebu nibishe tena.hodi! hodi! Wenyewe mpo?(Akinyamaza na

                            kunapita kimya. Punde mlango wafunguka na kipande cha

                            mwanamke chatokeza). Habari za asubuhi mama?

MAMA:           Salama, mwaonaje?

MITOMINGI} Hatujambo

NGOSWE    

MAMA:             Sijui niwasaidie nini akina baba?

MITOMINGI:    Mwenyewe yupo sijui?

MAMA:             (Akitazama chini mwenye huzuni anatingisha kichwa). Hayupo

MITOMINGI:    Katoka kitambo?

MAMA:            (Akimtazama Mitomingi kwa jicho kali). Ni marehemu.

MITOMINGI:   (Amtazama  Ngoswe ambaye kainamisha kichwa na wote wanamtazama

                           kwa jicho la huruma). Pole mama.

NGOSWE:        Pole mama.

MAMA:            Nimekwisha poa.

MITOMINGI:   Samahani mama , hata sikufahamu.

MAMA:            Sio neno baba sio kosa lako.

MITOMINGI:   Mungu mkubwa.

MAMA:             Nifanyeje; kazi ya Mungu haina dosari. (Ananyamaza kwa kitambo). Je

                           niwasaidie nini?

MITOMINGI:  Jambo moja dogo tu. Samahani kama nitakusumbua maana kwanza ni

                          asubuhi tena yenyewe ni msiba,

MAMA:            Sio kitu baba.

MITOMINGI:   Nadhani umepata kumsikia Balozi Mitomingi.

MAMA:             Nimemsikia lakini kumwona bado.

MITOMINGI:   Basi mama, huyo Mitomingi, Ngengemkeni Mitomingi ndiye mimi.

MAMA:            (Kwa mshangao): Karibuni ndani mpumzike

MITOMINGI:   Hatukai sana mama.

MAMA:            Basi ngoja niwatolee viti make. (Aingia ndani na kutoka na viti viwili

                          kuwapatia wageni. Yeye aketi chini).

MITOMINGI:   Mama!

MAMA:            Baba!

MITOMINGI:    Nadhani una habari juu ya kuhesabu watu.

MAMA:             (Kwa mshangao): Kuhesabu watu?

MITOMINGI:    Ndiyo kuhesabu watu.

MAMA:             Kuhesabu watu! (Akitingisha kichwa) Hapana.

MITOMINGI:    Balozi wenu hakuwajulisha?

MAMA:             Hata kidogo.

MITOMINGI:    Kweli?

MAMA:             Kwani Tambitambi naye mtu yule!

                           Pombe na yeye ni pete na chanda!

                          Hajali Balozi wake wala nyumba yake.

MITOMINGI:   Ni sawa usemayo mama. Tambitambi yule akili hazimtoshi. Tumefika

                          kwake wala hajulikani aliko!

MAMA:             Kama kuna wanaume mabwege yule ametia for a.

MITOMINGI:   Usizidi kunambia mama, Tambitambi mambo yake hakuna

                           asiyeyafahamu…. Sasa mama!....

MAMA:            Ndiyo baba.

MTOMINGI:    Sisi kama utuonavyo tuko shughulini, shughuli hiyo si nyingine bali hiyo

                          niliyoisema sasa hivi kuhesabu watu. Na huyu kijana ndiye karani

                          mwenyewe ahusikaye. Ingekuwa bora kama  wewe na wanao wote

                          mngetoka nje ili tufanye kazi yetu.

MAMA:            Sasa baba mbona itakuwa vigumu.

MITOMINGI:   Kwa vipi?

MAMA:            Sasa baba utahesabu vipi?

MITOMINGI:    Kwa nini?

MAMA:             Kama utatuhesabu wewe basi u mchawi.

MITOMINGI:    Mbona sikuelewi!

MAMA:             Mchawi ndiye anayehesabu watoto wa wenzake ili awaroge. Sasa wewe

                           umchawi? Hata kama  u mchawi siwezi kukubali utuhesabui maana

                           siwezi kujua nia yako ni mbaya au nzuri.

MITOMINGI:   Mtu akuwaniae uovu haji kweupe.

MAMA:            Sawa usemayo baba.

NGOSWE:        Sasa mama hebu walete wanao na yeyote yule aliye ndani.

MAMA:            Wanangu hawapo wamekwenda shamba kuwania mpunga.

NGOSWE:        Wote?

MAMA:             Ndiyo.

NGOSWE:         Ndio kusema hakuna kiumbe hata kimoja?

MAMA;            Yuko mke mwenzangu.

NGOSWE;       Tuitie.(Mama anasimama kwa unyonge na kuingia ndani. Anarudi peke

                         yake baada ya muda mfupi). Yu wapi?

MAMA:          Aja (Punde mama mwingine atokea. Yu kariby rika moja na mama wa

                        kwanza isipokuwa huyu mbichimbichi).

MITOMINGI:   Habari mama?

NGOSWE:        (Wakati huohuo) Shikamoo.

MAMA WA PILI:   Nzuri (Atazama chini kwa aibu huku akiketi).

NGOSWE:              (Akimtazama mama wa kwanza). Basi; hakuna mtu mwingine ndani?

MAMA WA PILI:  (Akikataa kwa kichwa)

MITOMINGI:       (Kwa mama wa kwanza). Lakini nyie wanawake mbona waoga sana!

                               Hivyo mnataka kuniambia motto wa mgongoni anaweza kwenda

                               kuwania mpunga? (Mama agutuka). Hebu niambie mwanao mchanga

                               yu wapi?

MAMA WA KWANZA:   Sina mtoto mchanga.

MITOMINGI:         Hivyo mama wasema kweli?

MAMA WA KWANZA:    Haki vile.(Mara kwasikika sauti ya mtoto akilia ndani ya 

                                             nyumba).               

MITOMINGI:    Na huyo anayelia kama si mtoto ni nini/ (Mama ainuka wakawaka na

                            kuingia ndani kwa aibu. Muda wapiti na harudi). Mama! Njoo basi

                            tumalize shughuli. Usijali mambo ya motto kulia, ni jambo la kawaida.

                            (Mama atokea amepakata mtoto mchanga. Aketi chini na sasa uso wake

                            umejaa hasira na chuki)…

                      [Imenukuliwa kutoka, Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. Uk 13-15]

2. Jadili hatua za kuzingatia katika mchakato wa kutafsiri.

& Zoezi la pili

1. Linganisha na linganua kati ya taaluma ya tafsiri na ukalimani.

 2. (a) Tafsiri sentensi zifuatazo kwenda lugha ya Kiingereza
(i) Dua la kuku halimpati mwewe
(ii) Bandu bandu humaliza gogo
(iii) La kuvunda halina ubani
(iv) Mla vya watu naye vyake huliwa
(v) Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli

(b) Ni njia gani umetumia katika tafsiri ulizotoa hapo juu, unadhani ni kwa nini?

& Zoezi la tatu    

1. [a] Kwa kutumia mifano, fafanua istilahi zifuatazo:
            [i] Matini chanzi
            [ii] Matini lengwa
           [iii] Lugha chanzi
           [iv] Lugha lengwa 

[b] Tafsiri sentensi zifuatazo kwenda lugha ya Kiswahili
             (i) All that glister is not gold
(ii) Looser casn't be a chooser
(iii) When you make your bed you must lie on it
(iv) There is no incense for something rotting
(v) When in Rome do, do as Romans do

(b) Ni njia gani umetumia katika tafsiri hizo ulizotoa hapo juu, unadhani ni kwanini?

2. "Mfasiri au mkalimani hukabiliana na changamoto mbalimbali katika kufanikisha kazi
      yake." Huku ukitumia mifano thibitisha kauli hiyo.

                                                MAREJEO
Cartford [1995] A linguistic Theory Translation

Mwansoko, H.J.M na wenzake [2006] Kitangulizi cha Tafsiri, Nadharia na

                                                              Mbinu.TUKI.Dar-es-salaam       

Newmark, P [1982] Approaches to Translation, Oxford, Pergamon Press



Newmark, P [1988] A  Text book of Translation, London, Prentice Hall.

                                Oxford University Press Dar-es-salaam



Semzaba, E [2006] Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe. The General Booksellers LTD.

                                 D.S.M

TUKI [2002] Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TUKI, Dar-es-salaam

TUKI [1985] Kiswahili, Jarida la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

www.bakita.org.tz retrieved on Monday 04th July 2011

www.jim-mission.org.uk retrieved on Monday, 04th July 2011

www.ajol.inf retrieved on Monday, 04th July 2011

Vitabu vilivyotafsiriwa ambavyo vimetumika kama marejeo

Ayi Kwei Armah, Wema Hawajazaliwa, kimetafsiriwa na Abdilatif Abdalla

Ferdinand Oyono: House boy, Kimetafsiriwa na Raphael Khasao na Nathan Mwele.

William Shakespeare: Juliasi Kaizari: Kimetafsiria na Julius K. Nyerere

                                     Mabepari wa Venisi: Kimetafsiriwa na Julius K. Nyerere

Hekaya za Abunuwasi: Kimetafsiriwa na Interterritorial Language Committee, East Africa

Alfu Lela Ulela: Kimetafsiriwa na Sir Richard Burton

Sir Rider Haggard: Mashimo ya Mfalme Suleiman

Takadini,kimetafsiriwa na Mathews Bookstore and Stationers,

Nitaolewa Nikipenda ambacho kimetafsiriwa na Crement M. Kabugi. vitabu vingine vilivyotafsiriwa ni kama vile; Orodha, Barua Ndefu Kama Hii n.k.