SAFARI YANGU YA KWENDA TABORA.
S
|
afari yangu kuelekea mkoani
tabora ilikuwa na changamoto nyingi, Ila kubwa namshukuru Mungu nilifika salama
na kurudi salama. Najua kuna FANS wangu wengi wananipa support haswa katika
maombi ya familia yangu. So najua itakuwa vizuri kama
nitashare na nyie jinsi safari yangu nzima ilivyokuwa.
Nimetumia siku tano so
nitakuwa naielezea kwa day after day ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka
naenda mpaka narudi.
I
|
la wakati naipanga hii safari
ili kwenda kumuona mume wangu, iliniweka katika wakati na maamuzi magumu sana
kama fans zangu mnavyofahamu nina watoto wadogo akiwepo mdogo wa miezi mine
4, Tabora ni mbali sana ni mwendo wa karibia masaa 14 kutokea Dar Es Salaam
watoto ni wadogo nikisafiri nao nikaona nitakuwa nawatesa, Nikafanya
maamuzi magumu mno ya kuwaacha wanangu kwa wadada wasaidizi wangu wa nyumbani.
Hizi ni changamoto za maisha inapofika wakati mgumu kama
huu ulionifikia mimi inabidi ufanye maamuzi mazito, so nikawaacha wanagu Lincon
na Linstone.
Lincon na Mdogo Wake Linston.
DAY1. IJUMAA
28/06/2013
S
|
iku ya Ijumaa tarehe 28/June
Tulikutana Ubungo, Tukitumia usafiri binafsi na tulikuwa watu 5. Tukaanza
safari yetu na tunamshukuru mungu tulifika salama Mkoani Morogoro, Tukaendelea
na safari Ila tukiwa kati ya Morogoro na Dodoma gari yetu kidogo ikaleta tabu,
hapa ni kati ya Moro na
Dom
Baridi ya hapa ilikuwa ni
balaa.
hapa baba mkwe akicheki
tatizo la gari.
Baada ya dk kadhaa gari
ikawa iko poa.
Baada ya gari kuwa poa
tukaendelea kwa safari tukaingia Dodoma, Tukapata chai kidogo
Tukisubiria Chai hapa ni
Dodoma.
Baada ya chai tukirudi
garini kuendelea na safari.
na gari nayo ikapata
lishe/mafuta. then tukaendelea na
safari.
Tulipofika Ikungi
Kabla hatujafika Singida mjini gari ikaharibika tena , dereva akasema ni
tatizo dogo linarekebishika fasta then tutaendelea na safari,
Tukapata Fundi pale pale
Ikungi, hapa akitazama tatizo.
dah ikawa vise versa tatizo
likawa kubwa, it was around saa tisa hivi alasiri tupo Ikungi, mpaka saa 6 usiku
gari haikufaa ikabidi tutafute hotel kulala hapo.
Mida ya saa sita hivi gari
ikawa bado haijatengamaa.
DAY2.JUMAMOSI 29/06/2013
S
|
iku ya pili tukaamka na
kujiandaa, ila mpaka tunamalizia kujiandaa gari ilikuwa bado haijatengamaa, ili
wote tusiwe tumestuck sehemu moja tukaamua kugawana wengine wabaki na gari na
wengine tutangulie. Kutokea hapo Ikungi tukapata usafiri wa NOAH mpaka Singida
Mjini si Mbali sana ilikuwa mwendo kama wa dk 20 ama 30 hivi, Tulipofika Singida Mjini
tukapata HIACE ambayo tulianza safari kuelekea Igunga.
hapa ilibidi tufanye safari
za kuunga unga mana usafiri pia ulikuwa wa tabu,
mwendo wa masaa kama mawili
na nusu ama matatu tukawa tumefika Igunga, tukakata tiketi za kuelekea Tabora
mjini..
Hapa ni stendi Igunga
tukisubiria basi.
Usafiri ni wa Tabu mno
tukapata basi ila tulikosa siti takasimama ,
it was a very rough road
kutokea hapo Igunga mpaka Tabora mjini na ni mwendo karibu wa masaa 3 na nusu
hivi, Ila Mungu alisadia tukafika salama Tabora mjini mida ya saa 11 kama na dk
20
Mwenyeji wetu akitusaidia
kutuonyesha hoteli.
Kutoka stendi ya mabasi
mpaka ilipo hoteli ni mwendo wa dk 2 tu kwa miguu.
na kuanza tafuta hotel. By
the way nilitamani sana nikiingia Tabora nielekee Gerezani Ila nilikuwa
nilishachelewa kwa uliza uliza niliambiwa Kutembelea gerezani mwisho ni saa 9
alasiri.
Uchovu wa
safari.
K
|
atika kuulizia ulizia hoteli
tukapelekwa Hotel inaitwa Mwafrika Hotel, Pale Tulikosa nafasi ila meneja wa
pale akachukua jukumu la kututafutia sehemu nyingine , tukapata sehemu nyingine
lakini tukapanga next day wakitoka watu tutarudi pale.
Aliyevaa Jezi ni Meneja Wa
Mwafrika Hoteli, Anayenielekeza ni Mmiliki wa Mwafrika Hotel.
Huyu ni shemeji yangu kabisa
kabisa, ni mume wa dada yangu"post ya changamoto na Opportunity" mtamfahamu
vyema. Hapa ndo alituchukua na kutupeleka hotel nyingine kwa usiku
huu.
DAY3. JUMAPILI
Tuliamka asubuhi tukajiandaa
kuelekea gereza Kuu Uyui, ila tulipitia Mwafrika hotel kuacha mizigo yetu mana
kwa siku hiyo tutakuwa pale.
Then safari ya kuelekea
Gereza Kuu la Uyui,
S
|
i mabali
kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5 hivi kwa Gari, tukawa tumefika
gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata kujiandikisha na kila kitu
halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana pia tulikuta watu wengine ambao
nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na
sie tukaitwa katika listi tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria
zao za kuzima simu na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko
kijichumba kidogo tu.
K |
iukweli it was a very SAD
moment, nilipomuana mume wangu, akiwa kwa upande wa pili na sikuwa namuona
vizuri mana hiyo nyavu iliyotenganisha hapo ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa
Kujizui MACHOZI yalianza kunitoka, Ila mume wangu alikuwa MORE THAN STRONG
akinisihi nisilie ye yuko poa, Kiukweli Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na
mie Napata nguvu. Swali la Kwanza aliniuliza
Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako wako salama , Kutokana na umbali
wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia Naendelea Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko
Upande Wetu, Misukosuko niliyoipata njiani nawaza ningekuwa na watoto
ingekuwaje”?? .Tukaongea mawili matatu kama
dakika tano hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka. Kuna nguo
nilibeba tukaambiwa zikakaguliwe kwanza then ndo atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka then tukaondoka.
K
|
iukweli
after kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia kuwa
yuko mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache sana na
nilikuwa na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale wakatuambia kwa
waliotoka mbali huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at least hata dk kumi, so
nikipanga kurudi tena siku ya Jumatatu.
Jioni Baada ya Kutoka
Gerezani, Nilikutana na Sister Wangu ambaye hatujaonana zaidi ya miaka 20.
Kwenye post ya changamoto na opportunity nae mtamfahamu.
DAY4.JUMATATU
N
|
iliamka
asubuhi na kujiandaa, Baada ya kumaliza nikatoka kwenda kutafuta baadhi ya vitu
alivyoniagiza, So nilipokamilisha vyote nikaanza safari ya kwenda Gereza Kuu
Uyui kwa siku nyingine tena, Leo nikiwa nimeongozana na mwanasheria
ambaye yeye anafanya shughuli zake kule kule kwa ajili ya mambo mawili matatu.
T
|
Nikiwa na
mwanasheria.
T
|
Hapa Nikiagana na
Mwanasheria.
DAY5.JUMANNE
B
|
aada ya kukosa usafiri wa
kurudi Dar Siku ya Jumanne, nikitazama Tabora ni mbali nikasema ngoja niende
Gerezani kuomba hata dakika moja ya kumuaga mume wangu, nikaelekea gerezani
Uyui, Ila dah nikaomba sana
wanilikatalia, nikaamua kurudi zangu kiunyonge hotelini, kuja kusubiria
Jumatano kusafiri kurudi zangu Dar.
DAY6.JUMATANO
N
|
ikaanza safari ya kurudi dar,
Tuliondoka Tabora saa 12 asubuhi, After Masaa Mengi njiani by saa 2 na nusu
hivi nikafika salama Dar, nilikuwa So excited kuwaona wangu, Thanx God Nilifika
salama na niliwakuta wanangu wako salama.
NYONGEZA
Jumatatu tarehe
8/Julai/2013, mume wangu anapandishwa tena mahakamani huko Tabora, Bado nahitaji
msaada wenu katika kunisaidia maombi.
SHUKRANI.
N
|
apenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote wote ambao mpaka sasa mko pamoja na
familia yangu, Kiukweli ni wengi mno sitaweza kuwataja wote na naomba
msinihukumu kwa hilo ni wengi mno, Ila kwanza kabisa naendelea kumshukuru Mungu
naamini yuko pamoja na familia yangu, naamini hatatuacha , pili kwa wasaidizi
wangu wa kazi nyumbani kwangu niliwaachia wanangu mikononi mwao na nikawakuta
wako salama, Ndugu wote wanaonisupport, marafiki wote wanaonisupport, Ila
Shukrani zangu za dhati pia ziwaendee FANS wangu woteeeeee popote walipo kwa
kunisaidia kwenu katika maombi inatia moyo.
Chanzo: www.joycekiria.com
No comments:
Post a Comment