Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Tuesday, July 9, 2013

ZITTO KABWE AZIDI KUKOMALIA KODI YA SIMUKADI YA TSH 1000 KWA MWEZI

 
Katika ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika:
 
Kodi ya SimKadi ya tshs 1000 kwa mwezi kwa kila mwenye simu ilikuwa kwenye hotuba ya Bajeti (tshs 1470). Waziri wa Fedha akaliambia Bunge kuwa hiyo imefutwa (alikuwa ametoka kwenye Cabinet kabla ya hapo, hivyo Cabinet haikupitisha kodi hii). Katika Mjadala wa Bajeti wa wiki nzima kodi hii haikujadiliwa kabisa maana ilikuwa imeondolewa katika mapendekezo ya Mapato. Kodi hii ikarejeshwa Bungeni kupitia Muswada wa Fedha. Muswada wa Fedha hutafsiri hotuba ya Bajeti kisheria. Kama Kodi hii haikuwa kwenye Hotuba, haikujadiliwa na Bunge, msingi wa muswada wa fedha kuwa na kodi hii haupo. Kodi hii ilirejeshwa kinyemela Bungeni na kupitishwa bila mjadala. Kodi hii ni batili. Kodi hii inakwenda kinyume na msingi wa kodi kwani ni REGRESSIVE in nature. Rafiki yangu Mohamed Mohammed Dewji mmoja wa matajiri wakubwa Afrika, atalipa sawa na dada yangu Salima anaetembea jiji zima kila siku kuuza mihogo mibichi.

Nashawishi wananchi kwa namna wanavyojua waikatae kodi hii mpaka itakapofanyiwa marekebisho makubwa.

Wananchi wanataka kampuni za simu zilipe corporate tax na sio kuwakamua masikini.
 
Na Zitto Kabwe

No comments:

Post a Comment