H
|
AWA NI KATI YA WATU WALIONISUKUMA MIMI KUINGIA KWENYE MUZIKI WA HIP HOP
KAMA MSANII.MIMI SIKUWA NAJUA KAMA NINA KIPAJI MPAKA NILIPOANZA KUUPENDA MZIKI
WA HIP HOP.NILIANZA KUUPENDA MUZIKI WA HIP HOP MIAKA YA 90 MWISHONI.
NIKAENDELEA KUWA SHABIKI MZURI SANA MPAKA MWAKA 2004 AMBAPO NILIZIDI KUUPENDA
ZAIDI NA KUAMUA KUANDIKA UBETI WANGU WA KWANZA MWISHONI MWA MWAKA 2004. WAKATI
NAANDIKA UBETI HUO SIKUWA NA JUA KAMA NINA KIPAJI NILIANDIKA TU KWA KUWA
NAUPENDA MUZIKI HUO. NA LENGO LA KUANDIKA ILIKUWA NI KWA AJILI YA KUJIFURAHISHA
TU.BAADA YA KUANDIKA WIMBO HUO ULIOKUWA UNAITWA DUNIA YA MATANGAZO. NIKAWA SIWEZI
KUANDIKA KIITIKIO CHA WIMBO HUO MPAKA NILIPOMUOMBA RAFIKI YANGU ANIANDIKIE
KIITIKIO NA KUFANYA HIVYO.HUYO RAFIKI YANGU ANAITWA BULLET.MWANZONI MWA MWAKA
2005 NILIINGIA STUDIO ZA UJUMBE RECORDS ZILIZOKUWA JENGO LA CCM MWANZA.WIMBO
HUU NILIURECORD KWA KUTUMIA MDUNDO WA MSANII MWINGINE.YANI NILIFANYA KWA AJILI
YA KUSIKILIZA MIMI MWENYEWE.BAADA YA KUUCHUKUA STUDIO NILIWASIKILIZISHA RAFIKI
ZANGU AMBAO WALINIAMBIA NI MZURI NA KUNISHAWISHI KUINGIA RASMI KWENYE GAME.
K
|
WA KIFUPI MIMI NISINGEKUWA MSANII KAMA NISINGEKUWA NAAUPENDA MZIKI WA HIP
HOP.KWA HIYO HAO JAMAA HAPO KWENYE PICHA WAMECHANGIA SANA LEO HII KUWEPO KALA JEREMIAH.
BY. Kala jeremiah
No comments:
Post a Comment