Kufuatia kukamatwa kwa Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki [Chadema] kupitia ukurasa wake wa facebook Mh. Godbless Lema ameandika hivi;
"Jana Jumamosi, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari aliitwa na Jeshi la Polisi Makao Makuu Arusha.
Mh Mbunge aliitikia wito na kufika kituoni hao na kuwekwa chini ya ulinzi akituhumiwa kushambulia na kujeruhi huko Makuyuni wakati wa Uchaguzi mdogo wa udiwani mwezi jana.
Polisi walijaribu kumuweka ndani, Mh Nassari akaridhia na kuanza kuvua saa yake, mkanda na kukabidhi bastola yake ili zoezi la kumuweka mahabusu kama walivyokuwa wamepanga litimia. Kumbuka angewekwa mahabusu jana wangemtoa Jumatatu. Mbunge wetu alifahamu hilo na aliridhia yote!
Kichekesho sasa kikawa na Polisi hao kuanza kuhaha wenyewe wasijue cha kufanya. ...Waligundua wamechemsha kumuweka mahabusu Arusha kwasababu kosa ni la Makuyuni kama ni kweli, wakajaribu kutafuta wenzao wa Makuyuni waje wamchukue wakaambiwa gari haina mafuta. Wakajishauri sana na wasijue cha kufanya.

Nje waandishi wakawa wanzidi kuongezeka na baadhi wakihoji sababu hasa za kumkamata Mbunge huyo na kumuweka mahabusu. Mchecheto ukawazidi, mwishowe wakaamua kumuachia tu arudi nyumbani na kumtaka akaripoti siku nyingine..
Huu ndio weledi wa Jeshi letu mpaka leo!"

No comments:
Post a Comment