Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, July 1, 2013

JULIUS MTATIRO: JWTZ WANATUMIKA VIBAYA NA CCM

 
Haya ni maelezo aliyoyatoa ndugu Julius Mtatiro Naibu Katibu Mkuu TZ Bara-CUF [Pichani  kulia] kupitia ukurasa wake wa facebook, Mtatiro anaelezea namna alivyokuwa akifuatiliwa na maofisa anaodhani kuwa ni wa JWTZ
 
"Eti jana wamekuja na magari yao kwenye hoteli niliyofikia mara tatu. Mara ya kwanza wamefika wanamuuliza muuza duka aliye karibu na hoteli kuwa ati kama nipo hotelini, akawaambia wawaulize wenye hoteli, wakasepa. Baadaye saa 1 jioni wamerudi na magari mawili, moja likapitiliza na lingine likamshusha ofisa aliyevaa kiraia, wakati anashushwa mita 100 kutoka hotelini kwa kificho, bahati nzuri nyuma yake palikuwa na BG wetu, akanipigia simu. Nikaona hawa washenzi lazima tuwaeleze ukweli. Nikafungua mlango ili nisikie ikiwa mgeni atagonga kengele ya mlango wa reception, kweli ikalia, mimi nikatoka chumba...ni moja kwa moja, nikasema liwalo na liwe. Nikamkabili akiwa mapokezi, nikamuuliza.....bila shaka unamtafuta Mtatiro, akashtuka sana, nikavua kofia, nikamwambia ndo mimi.
 
 
Ni kama nilimpa pigo zito, akaniuliza za siku, nikamjibu za siku kwani mara ya mwisho tulionana lini? Akasema tulisoma wote chuo kikuu, nikahamisha mazungumzo, nikamwambia Mbona mmepaki gari mbali hivyo....akachekacheka. Nikamwambia usicheke, karibu chumbani kwangu upaone ili mtakapokuja kunifuata msipate shida. Akakaa kimya na kuguna.
Nikamwambia....sitahama hoteli hii ili kuwakimbia, nyinyi wauaji, nyinyi siyo mungu, mnaweza kudhuru miili tu lakini si roho na siku zenu zinahesabika, mnatumika vibaya, mnatesa raia badala ya kuwalinda......
 
 
Nikakasirika nikarudi chumbani. Nasikia alibaki pale kwa dakika 3, akaomba kiberiti kwa mhudumu ili avute sigara, mhudumu akamwambia pale aliposimama sigara haziruhusiwi.
Walinzi wetu walishafika, akawapigia simu wenzake, gari yao ya jeshi ikasogea hotelini. Akatoka, wakaondoka.
 
 
Dawa ya hawa washenzi si kuwakimbia, ni kula nao sahani moja tu. Kama wao wameshapewa kibali cha "piga tu" nasi lazima tujichunge. Na jana niliapa, wangeniletea ushenzi, kabla hawajaniua, ningemwaga ubongo wa mmoja wao ili niache kumbukumbu. Hatuwezi kuishi katika nchi yetu kama wakimbizi.
 
 
Hatuwezi kuacha raia wateswe na kunyanyaswa eti viongozi tunaogopa kufa. KIFO kipo tu, hata Mahita alistaafu na siku moja atakufa."
 

No comments:

Post a Comment