Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Tuesday, September 30, 2014

FACEBOOK YAPATA MPINZANI, WADAU WAUBATIZA ANTI-FACEBOOK

Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.

Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.

Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.

Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.

Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.

Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.
CHANZO BBC

Tuesday, September 23, 2014

HIVI NDIVYO TULIVYOSHEREHEKEA KATIKA BIRTHDAY YA MTOTO WETU DAVID

My son, David alizaliwa tarehe 22/09/2013, mwezi huu wa 9, tarehe 22 alikuwa ndo anafunga mwaka, hivyo kama wazazi tuliamua kuandaa chakula cha jioni ili kujumuika na ndugu, marafiki na jamaa zetu ili kwa pamoja tuweze kuadhimisha siku hii muhimu katika familia yetu. Kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao hawakuweza kufika kutoka na umbali au matatizo ya hapa na pale ambao walipenda wajumuike nasi lakini haikuwezekana, tumuona tuwaletee tukio zima katika picha, basi jumuika nasi kwa kuangalia picha hizi


 David na mama yake

                Baba D.


 Mwabeza akisoma neno la Mungu




 Baba David akiwakaribisha wageni


 Mama David akiwapungia mkono wageni 


 Mr. Prosper, ndiye alikuwa Dj. wa shughuli yenyewe


                                                                                       








 David akimlisha keki yake wa baba wa ubatizo, John Kimolo
         David akimlisha keki mama yake

   Akimmlisha keki baba yake

 Akimlisha keki bibi yake

 Akimlisha keki baba Enosh, (Mwl. Mwabeza)

















  Hii ndo familia, mama, dady, son












Tunakuombea kwa Mungu mtoto wetu David,uendelee kukua vizuri, akupe maisha mazuri na marefu, wazazi wako tunakupenda sana. Mungu akulinde.

Tunapenda kuwashukuru wote waliohudhuria katika shughuli ya kumpongeza mtoto wetu kwa kutimiza mwaka mmoja. Janeth Lubasi, Boniface Manyasa, Steven Mandia, familia ya Mwabeza, familia ya Madata, Moris Nyamwale, familia ya John Kimoro, familia ya Gwamaka, Sarah Mgulula, Maria Ntandu, Edward Mbuya, John Maghway, Mama Schola, Sylvery Hussein, Stewart Prosper, Elizabeth, Agnes, n.k. Tunawashukuru hawa wote kwa kuweza kutupa kampani ya kutosha katika siku hii muhimu ya mtoto wetu kutimiza mwaka mmoja. Mungu awabariki sana na awazidishie pale walipopungukiwa.

Familia ya Mr. & Mrs Furaha Venance Kaguo