Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

BONGO MOVIE


DEVOTHA ALFRED, ACTRESS WA TANZANIA ANAYEISHI UJERUMANI, AJICHANGA KUINGIA HOLLYWOOD.
 
 
Devotha

Devetha Alfred ni muigizaji wa kitanzania anayeishi nchini Ujerumani ambako anasoma huko kwa sasa. Muigizaji huyu wa kike mwenye mvuto wa asili alisomea sanaa chuo kikuu cha Dar es salaam na kucheza baadhi ya filamu nchini Tanzania kabla ya kwenda ujerumani ambako analiendeleza libeneke la uigizaji na wasanii wa scandinavia hususani VAD Productions kutoka nchini Denmark. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuchonga mawili matatu na actress huyu hivyo tiririka nayo hapo chini.................

SWP: mzima Devotha? wewe ni mtanzania au? and unakaa germany au Denmark?

DEVOTHA: Mzima sijui we we.mi ni mtanzania naishi Germany ila Denmark naenda kufanya film tu

SWP: Ulianza lini sanaa ya filamu and huko Germany unasoma au umeolewa?

DEVOTHA: Sanaa nilianza mwaka .2011 nilicheza kwenye movie ya Misukosuko, Ndoa Ya Utata na Daktari Wa Giza .Tanzania nimesomea films chuo kikuu Mlimani(University of Dar es salaam), Germany nasoma. Jina langu kamili ni Rosemary Alfred Mahali ila natumia Devotha sana ni jina langu la utotoni.

SWP: Now unasoma huko una mpango wa kurudi Tanzania au ndiyo wataka kufanya mishe za kwenda Hollywood kabisa?

DEVOTHA: Mipango ya kwenda Hollywood ipo na hata sasa kuna kampuni ndogo ndogo za marekani zinanitaka kufanya nao Kazi .sehemu mbalimali ila shule inabana kusafiri mbali .Na Tanzania ni nyumbani ntarudi tu hakukwepeki pia Nina mipango ya kufanya fillm na mastaa wa Tanzania na nchi mbalimbali za kiafrika .ila kwa sasa bado nipo shule, pia nataka nifanye films nyinyi za kuwaonyesha waafrika maisha ya huku ulaya maaana tunajua mambo mengi ya Africa kupitia movies za kiafrika.sasa ni muda wa kuwaonyesha waaafrica maisha ya ulaya huku tukitangaza lugha ya kiswahili.

SWP: Umefanya filamu ngapi huko Ulaya mpaka sasa?

DEVOTHA:
Huku Europe nimefanya movie mbili ya kwanza short film passport love ambayo Mimi ndio mwandishi Na ya pili ndio hio bado jina halijawekwa wazi Vad Production tuliofanya Na Mr nice.

Picha chini inamuonyesha Devotha akiwa behind the scenes ya filamu ya Passport Love
 
Habari kwa msaada wa Swahiliworldplanet



Filamu ya Shaymaa ya Wastara kuanza kutikisa soko mwezi ujao, mwenyewe asema hamna mfano wake bongo!
Filamu ya Shaymaa ya Wastara kuanza kutikisa soko mwezi ujao, mwenyewe asema hamna mfano wake bongo!
Bongo Movie, imefanya mahojiano na mwanadada Wastara Sajuki  pamoja na mambo mengi waliyoongea naye moja lilikuwa ni kuhusu Filamu yake mpya ya Shaymaa inayotarajiwa kuingia sokoni kwa kasi hapo mapema mwezi ujao.
Katika interview hiyo fupi ya kutaka kujua ni nini mwanadada huyu anafanya kwa sasa Wastara amesema kwa sasa moyo wake, macho yake na akili yake ipo kwenye Filamu hii mpya anayotarajiwa kuitoa hapo mwezi wa kumi moja.
“Kwakweli kwa sasa siwazi ktu chochote, mawazo yangu yoote, akili, na nguvu zangu yapo juu ya SHAYAMAA, hii Filamu ni nzuri sana, kila nikiitazama nazidi kuipenda, sizani kama kuna Filamu kama hii kwa sasa” Alisema Wastara.
Filamu hii  amemshirikisha Yusuph Mlela na Nisha na amewataka fans wote wanaotaka kujua nini kimafanyika humo ndani kujipatia nakala zao mapema kwani copy zitakuwa chache sana.
Via: Bongo Movies

No comments:

Post a Comment