Na.Venance Furaha-Manyoni

"Kusema kweli ndugu yangu huu msiba ni pigo kubwa sana si kwa Wakatoliki pekee bali kila mtu aliyekuwa akimfahamu huyu jamaa atakuwa ameguswa na tukio hili" Alisema Mzee Juma aliyejitambulisha kuwa anatokea maeneo ya Majengo.
Mkazi mwingine wa Manyoni ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake, alidai kuwa Padri Makwanda ni kama alijitabiria kifo, "Ujue padri wetu ni kama alikuwa anajua kuwa hivi karibuni hatakuwa nasi, ni juzi juzi tu alikuwa anatuonesha eneo ambalo kama akitangulia kufa mwili wake utapumzishwa na hapo na ndipo alipopumzishwa siku ya leo (Jana) kweli huyu padri alikuwa kipenzi cha watu ona umati wote huu!"
Akimzungumzia marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Parseko Kone, alisema kuwa Fr. Makwanda alikuwa mtu wa watu, mara nyingi nikiwa hapa manyoni Fr. Padri Makwanda alinipa sehemu ya kulala, alinihudumia chakula hakika nilikuwa nahudumiwa kama mtoto...katika hali ya kibanadamu Fr. Makwanda alikuwa kama kijana wangu, lakini kiroho alikuwa ni baba yangu." Alisema Mkuu wa Mkoa.
Wageni wengine waliohudhuria ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi. Fatuma Tawafiq, vingozi mbalimbali wa dini kutoka madhehebu na dini mbalimbali, wawakilishi mbalimbali kutoka Parokia na majimbo mbalimbali.
Mwili wa marehemu kabla ya kupumzishwa katika nyumba yake ya milele, misa ya kumuombea marehemu ilifanyika katika kanisa la RC Manyoni, Parokia ya Kupaa Bwana na baada ya shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu yalifuatiwa na maandamano kuelekea makazi ya Mapadri ambako ndiko Mwili wa Fr. Makwanda ulipolazwa.
Mpaka mauti inamkuta Padri Makwanda alikuwa ni Msaidizi wa Paroko parokia ya Kupaa Bwana Manyoni.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
Fr. Makwanda enzi za uhai wake
Fr. Makwanda enzi za uhai wake
Jinsi ilivyokuwa maeneo ya makaburini
Hii ndiyo gari aliyopata nayo ajali
Baba D. blog inaungana na Wanamanyoni wote kuipa pole familia ya Fr. Makwanda, Paroko wa Parokia ya Kupaa Bwana na waumini wote wa parokia hiyo. R.I.P Fr. Makwanda.
Picha kwa hisani ya Sylvery Hussein, Edga Madeje na wadau wengine.
No comments:
Post a Comment