Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, November 2, 2014

MAKONDA ATUMIA VIJANA KUVURUGA MDAHALO WA KATIBA, WENZAKE WAMFANYIA MBAYA KAMA ATARUDIA TENA BASI NI SIKIO LA KUFA


Katika tukio hilo PAUL MAKONDA chuchupu kuangukia katika mikono ya watu wenye hasira mara baada kukimbilia kujisalimisha kwa Jaji Warioba ili asidhurike na watu hao waliokuwa na hasira kama watu kama mbogo mbogo aliejeruhiwa.

Mara baada ya kutokea vurugu hizo, Prof. Kabudi alimfuata Makonda na kumuambia kuwa anachokifanya siyo atakuja kuumia, katika hali ya kujitetea Makonda alidai kuwa amekoja mwenyewe wala hakuja na kundi hilo la watu.

Vijana hao walionekana kuwa wamelewa kutokana na harufu walizokuwa wanazitoa midomoni mwao wakati wakipiga kelele wanadaiwa kuwa waliletwa na Makonda ambaye ilibidi akimbilie katika kibanda kimojawapo kilichomo ukumbini hapo ili kunusuru maisha yake, "kama siyo jitihada za Humphrey Polepole na Said Kubenea kuwatulia raia waliokuwa na hasira kali leo hii kwa Makonda tungekuwa tunasimulia habari nyingine, kwani alichofanyiwa Makonda na baadhi ya vijana hapo ukumbini kama atarudia tena kufanya tukio kama hilo basi jamaa ni sikio la kufa," Alisikika kijana mmoja ambaye anadai alimbana Makonda kisawasawa.

Kijana huyo mwenye siasa tata huku ndani ya CCM akipambana kumchafua Lowasa na nje ya CCM anapambana kumchafua Warioba aliokolewa na Jeshi la Polisi ambao kabla ya kumtoa ndani ya kibanda alichojificha iliwabidi wawasogeze watu mbali na eneo ili wasije wakamgeuza nyama Kijana huyo aliyekuwa ameongazana Amon ambaye naye alikuwa Mbunge wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka katika Kundi la watu wenye ulemavu.

Watu kama wawili watatu hivi  walijeruhiwa katika tukio hilo, huku mmoja wa vijana waliokuja na Makonda ukumbini akiponea chupuchupu baada ya kuokolewa na jesshi la Polisi nje ya ukumbi.



GODBLESS LEMA (Kupitia ukurasa wake ameandika hivi kuhusiana na vurugu hizo)

Tokea nizaliwe sijawai kukasirishwahivi kama nilivyokasirika leo na jambo la huyu muhuni Makonda kumpiga na chupa mzee warioba ni kukosa heshima kukosa akili na ustaarabu ni upumbavu .ushenzi na uhuni wa hali ya juu

kitendo cha ccm kuwatuma wahuni wa chuo cha diplomasia kumshambulia mzee warioba ni dalili tosha ya kushindwa kwa utawala kama judge ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu na vilevile ni kada mkubwa ndani ya ccm anatendewa uhuni huu wewe mtanzania wa kawaida watakufanya nini??? mti mbichi unatendwa hivi mti mkavu je...
.ni wakati sasa wa watanzania kujiuliza hii katiba PENDEKEZWA inayo siri gani ambayo ccm hawataki wananchi tuijue???? kwanini wanatumia nguvu nyingi kutunyamazisha??? kwanini hawataki tuijadili????? kwanini hawataki wananchi waelimishwe???hii ni karne ya 21 ni karne ya kubishana kwa hoja sio karne ya matusi na vurugu mjibuni warioba na tume yake kwa hoja simlisema mnauhakika na katiba "pendekezwa"imezingatia matakwa ya wananchi sasa wanaogopa nini???mbona nyie mkifanya makongamano yenu hakuna mtu anayewaingilia???

tuacheni tupate elimu juu ya katiba tunayoitakaninatoa rai kwa kila mzalendo wa taifa hili kukilaani kitendo cha muhuni makonda kumpiga mzee warioba na laana ya mungu ishuke juu yakeShame on you makonda‪#‎ALAANIWE_MAKONDA




PETER MSIGWA (Katika ukurasa wake wa facebook naye ameandika hivi)
"Nilikuwa ndani ya ubungo plaza ,niliwaona vijana wengi waliobeba mabango hawakufika hata hamsini . Wengi wao ni chini ya miaka 18,' walikuwa na Amon Yule mlemavu wa macho na Paul makonda. Nilichokiona ni ni upuuzi ujinga,mkubwa , vijana wale hata hawajui wanachokifanya,
Akili ndogo ndio imetamalaki ....shame on you CCM".


Hapo Makonda mwenye shati jeupe katikati aking'ang'ania mkono wa Mzee Warioba ili kujinusuru na kipigo cha wananchi maana kabla ya hapo alikichezea haswaaaa
 
                                         Mzee Warioba akitolewa ukumbini na wanausalama 



Baadhi ya vijana wanaodaiwa kutumika na CCM wakiwa na mabango yao huku wakizomea

ZITTO KABWE (Kupitia ukurasa wake wa facebook amaendika hivi.
"Nalaani vikali kabisa vurugu zilizotokea katika mdahalo wa Katiba. Tabia mbaya kabisa kuendekeza vurugu badala ya hoja. Mambo ya kihayawani. Shindana kwa hoja"

Usalama wa Mzee Warioba ukulindwa

Baadhi ya wahudhuriaji wakiwazua wenzao kutojibu mapigo jambo ambalo baadaye lilishindikana baada ya kuona wenzao wa upende wa pili hawataki kutulia ilibidi wawatoe mkuku ukumbini

No comments:

Post a Comment