TAARIFA KWA UMMA
OR-TAMISEMI
inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na
Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za
Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana
29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya
Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na
wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na
Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa
na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi
759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa
kujiunga na vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11
Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote
wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi
atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti,
nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2016 pamoja
na fomu za kujiunga (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya
OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu
Mkuu,
OR-TAMISEMI
No comments:
Post a Comment