Tarehe 04/05/2013 nilikuwa safarini Babati mkoa wa Manyara, huko nilienda kulipa mahari, maana nimechoka kuwa 'bado nipo nipo kwanza' zifuatazo ni baadhi ya picha za safari hiyo;
Huyu ndo Mzee wangu, Mzee Venance Kaguo
akiwa ukweni akiangalia mandhari
Mama Mkwe [Mama Regina] akimtembeza mzee wangu
kumuonesha mazingira ya ukweni
Baba akifurahia jambo, huku mdogo wangu
anayenifuata, Waziri akiwa pembeni
Tukipata chai nzito kabla ya kikao cha kupangiwa mahari hakijakaa
Nikiwa na Mshenga wangu Mzee Gobret (Baba Kalay)
Nikiwa na Mshenga na Mzee wangu kulia
Huyo wa kulia ndo alikuwa Mkalimani maana Mshenga alikuwa full Kiiraq
Mshenga, Mkalimani, Mzee na Bwana harusi mtarajiwa
tukijadili kabla hatujaingia ndani
Hapa mi na Mzee wangu tukijadili jambo baada ya kupata maelezo na taratibu
tunazotakiwa kuzizingati, si unajua ukikosea kidogo mafaini
Mshenga akikazia jambo fulani
Hapa wameingia ndani, Mkalimani akimfafanulia Mzee jambo
Hapa Mzee akionekana kufurahia jambo
Mshenga akiwa kazini
Huyo mwenye koti na kofia rangi damu ya mzee ndiyo Baba mkwe mwenyewe,
anayefuatia ni baba mkubwa wa wife, na aliyevaa kofia nyeusi na mgorori wenye miraba miekundu ni uncle wa wife
Hapa Baba mkubwa wa wife akiandika koo tatu akishirikiana na uncle
maana hayo majina ya Kiiraq yalitushinda kuandika wakati wakizitaja
Mahari imeshapangwa, wamemalizana Mzee ananipa kilichojili ndani
maana mi sikutakiwa kuingia ndani kwa mujibu wa mila na desturi za Kiiraq
Mjomba mtu naye akatokea, hapo ananiambia
"Si unaona nilikwambia mjomba ndo kila kitu, tumemaliza bwana
kuwa na amani mjomba wangu"
Huyo ndo aliyenipeleka Manyara, mtoto wa Kiiraq ndo Bibi Harusi Mtarajiwa
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, naishukuru sana familia yangu Baba na Mama kwa kufunga safari ndefu toka Dar. mpaka Babati Manyara kwa ajili ya kwenda kulipa mahari ya kijana wao, pia namshukuru Mdogo wangu Waziri Venance naye kufunga safari na kuacha kazi zake kuja kunipa 'suport' kaka yake kutoka Mwanga Kilimanjaro hadi Manyara.
Pia namshukuru sana Kipenzi changu Regina S. Maffa kwa kunikubali kuwa mimi kuwa wake, kunikubali mimi kijana ninayetoka familia ya kawaida kabisa, hakuwa kama wale wengine. Namshukuru pia Mshenga wangu kwa ngumu na nzito aliyoifanya, namshukuru pia Denis Chirimi pamoja na Mr. Kalay kwa kuniunganisha na Mshenga Mzee Gobret maana bila wao sijui kama ningepata mshenga mzuri, na ukizingatia huko sikuwa mwenyeji wala mtu ninayefahamiaana naye huko ambaye angeweza kufanya kazi hiyo.
Mwisho naishukuru familia yake Regina kwa kunikubali nami kuwa kijana wao wa kiume, wasiwe na hofu binti yao atatunzwa vizuri sanaaaaa.
Ndoa itafungwa Tarehe 15/06/2013 DSM, kwa wale ambao nimewapa kadi za michango na wengine nilishindwa kuwafikia wapo nilio wa in-box nawakumbusha bado napokea michango, michango yenu muhimu kufanikisha jambo hili jema. unaweza tuma kwa M-pesa: 0755 44 06 99 na Tigo Pesa 0715 33 55 58 na Airtel money: 0787 33 55 53
No comments:
Post a Comment