Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Wednesday, January 1, 2025

WAKAZI KATA YA MAKANDA WAUPOKEA MWAKA MPYA KWA NAMNA YAKE: MATUKIO NA PICHA

Sherehe za kufungua mwaka 2025 limesindikizwa Bonanza lililowakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi na wadau wengine huku likisindikizwa na mechi kali ya kirafiki kati ya timu ya COMBINE FC kutoka Makanda na CENTRE BOY (pichani kushoto) kutoka Kintinku. Mchezo ambao umemalizika kwa CENTRE BOY kuibuka wababe kwa ushindi wa  1:0 dhidi ya COMBINE FC  na mshindi kujinyakulia zawadi ya Tsh. 100,000/= huku mshindi wa pili akiondoka na TSH. 50,000/=

Bonanza hilo ambalo limefanyika leo Tarehe 01:01:2026 katika Kata ya Makanda liliendeshwa kwa udhamini wa  mmoja ya wadau wa maendeleo kata ya Makanda, ndugu Ernest Zacharia (Chimbaha) akitumia siku siku hii kama sikukuu ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya mafanikio yake ndani ya miaka 10.

Mgeni Rasmi wa Bonanza hilo, Mh. Jumanne Mlagaza Diwani wa Kata ya Makanda akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika Bonanza hilo alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuumaliza mwaka 2024 salama  na kuuanza mwaka 2025.

Pia ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kuboresha uongozi ulio thabiti na kulifanya taifa kuwa katika mikono salama kupitia 4R. Aidha aliwashukuru Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji pamoja na viongozi wote wanaosimamia maendeleo ndani ya jimbo,  wilaya na halmashauri ya manyoni.

Amesisitiza zaidi kwa wananchi kujitokeza katika shughuli za maendeleo, kutoa ushirikiano utii na nidhamu kwa  viongozi wapya wa serikali za mitaa waliochaguliwa hivi karibuni, kuimarisha ushirikiano wa kata kupitia michezo na sekta mbalimbali.

Mh. Mlagaza amewasisitiza vijana kuchangamkia fursa za maendeleo zinazotolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Bonanza hilo lilihitimishwa na sherehe za kusherehekea ubingwa wa timu ya Ipumbuza FC kwa kuchukua ubingwa kombe la POLISI JAMII CUP KATA YA MAKANDA.

Aidha Bonanza hili lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Mh Diwani wa Kata ya Makanda mh Jumanne S Mlagaza, Mtendaji wa Kata ndg Joseph E Waziri, diwani kata jirani ya Mpendo mh Bernard Antony Kapaya, Afisa Mawndeleo kata ya Makanda, Mwenyekiti wa kijiji cha Makanda ndugu Chenda Licas Masigazwa, watendaji wa vijiji, kijiji cha Makanda na Magasai, wenyeviti wa  vitongoji vya kijiji cha Makanda, viongozi wa chama cha mapinduzi ngazi tofauti, wadau wa maendeleo na michezo na wananchi wa kata ya Makanda na Kintinku

Tazama picha za tukio zima hapa chini.


Kikosi cha Timu ya Centre Boy kutoka Kintinku

Baadhi ya Viongozi wa Kata wakiongozwa na Mh. Jumanne Mlagaza, Diwani wa Kata ya Makanda wakifuatilia Bonanza la Kuukaribisha mwaka Mpya






Viongozi wa Kata wakiwa katika picha ya pamoja
 na wachezaji wa Timu ya Centre Boy kutoka Kintinku.

Viongozi wa Kata wakizungumza na Waamuzi na Wachezaji
Mh. Jumanne Mlagaza, Diwani Kata ya Makanda akitoa zawadi, pembeni yake kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Makanda, Bw. Waziri Joseph.

            Viongozi wakizungumza na wachezaji wa timu zote


   Viongozi Mbalimbali akiwemo Mh. Diwani Kata Mwenyeji ya                 Makanda (mwenye kanzu) pamoja na Waamuzi                 waliotoka Dodoma 
Kikosi cha timu ya Combine FC kutoka Makanda