UHAKIKI WA RIWAYA
JINA LA
KITABU: ,MFADHILI.
MWANDISHI: HUSSEIN TUWA
MHAKIKI: MWL. FURAHA VENANCE
Mwaka 2012
Mwaka 2012
Utangulizi kuhusu Riwaya.
Mfadhili ni riwaya iliyoandikwa
na Hussein Tuwa, ni riwaya inayoongelea juu ya penzi zito baina ya watu wawili,
Gaddi Bullah na Dania Theobald na jinsi ambavyo penzi hilo linavyoingiliwa na
mitihani,majaribu na misukosuko mikubwa na namna ambavyo kila mmoja
anavyojaribu kukabiliana na hiyo misukosuko. Ni riwaya inayogusa moyo na
isiyochosha kusomwa na wasomaji wa kila aina.
Mwandishi Hussein Tuwa pamoja na
kuandika riwaya hii, pia ameandika riwaya nyingine inayoitwa, Mkimbizi.
Utangulizi kuhusu uhakiki wa
riwaya hii.
Tunapofanya uhakiki wa kazi za
fasihi huwa tunachambua vipengele mbalimbali
vya fasihi, vipengele hivyo ambavyo huchambuliwa ni fani na maudhui,
katika fani huwa tunajishughulisha na Vipengele kama, wahusika, mandhari,
mtindo, muundo, matumizi ya lugha, jina la kitabu na jalada, wakati katika
maudhui huwa tunashughulika na vipengele kama vile dhamira, migogoro, ujumbe,
falsafa ya mwandishi, mtazamo wa mwandishi.
Hivyo basi katika kazi hii,
nimeanza uhakiki kwa kuanza na kipengele cha wahusika ambacho ni kipengele cha
fani, nimeamua kuanza hivi ili kukupa fulsa msomaji na mtumiaji wa tahakiki
hii, uweze kuwajua wahusika katika riwaya hii, na pindi tutakapoanza kuangalia
dhamira basi utakuwa unajua ni nani anayehusika na dhamira hiyo. Hivyo basi
tuanze kwa kuwaangalia wahusika maana ndio wanaobeba dhamira:
WAHUSIKA
Wahusika ni wakala wa vitendo
katika kazi ya fasihi. Wahusika ni watu au viumbe waliokusudiwa na mwandishi
wawakilishe tabia za watu katika kazi ya fasihi. Na wahusika katika kazi ya
fasihi ni Muhusika/wahusika wakuu na wahusika wasaidizi.
Wahusika
wakuu.
Hawa ni wahusika wanaojitokeza
mara kwa mara katika kazi ya fasihi na mara nyingi ndio wanaobeba dhamira kuu
ya mwandishi lakini pia husaidia kujenga dhamira ndogondogo. Riwaya hii ya
Mfadhiri ina wahusika wakuu wawili, Gaddi Bullah na Dania.
1. Gaddi Majid Bullah
Ø
Ni mtu mcheshi na mchangamfu, kama mwandishi
anavyothibitisha anaposema, “ Na hii
ilitokana na jinsi Gaddi alivyobadilika mara baada ya kukutana na Dania na
kurudia ucheshi na uchangamfu wake wa zamani” [Uk 97]
Ø
Ni msomi aliyeajiliwa katika kampuni ya
mawasiliano, mwandishi anathibitisha hili anaposema, “….kampuni ile kubwa ya
mawasiliano nchini ambayo ilimwajiri mara baada ya kumaliza masomo yake ya
elimu ya juu miaka mitano iliyopita.” [Uk 57]
Ø
Anashushwa cheo kutoka Meneja wa mkoa katika
tawi la Arusha hadi kuwa Afisa wa kawaida wa kukusanya madeni. Rejea Ukurasa wa
57.
Ø
Kaka pekee wa Bi Hanuna.
Ø
Mume wa Nyambuja ambaye wanakuja kuvunja ndoa
yao kutoka na kusalitiwa, kama mwandishi anavyothibitisha anaposema, “Wiki
moja baadaye Gaddi na Nyambuja waliachana kisheria….” [Uk 68]
Ø
Anasalitiwa na Mke wake kwa kuanzisha uhusiano
na mwanaume mwingine, mwandishi anathibitisha hili kupitia muhusika Nyambuja
anaposema katika barua aliyomwandikia Gaddi, “Gaddi nimependana na mtu
mwingine, na nimekuwa nikisaliti ndoa yetu kwa muda mrefu.” [Uk. 65]
Ø
Hakufanikiwa kupata mtoto katika uhai wa ndoa
yake na nyambuja, kama mwandishi anavyothibitisha hili anaposema, “Gaddi aliguna kwa mshangao, akilini mwake
akikumbuka jinsi yeye alivyokuwa akisononeka kwa kutopata mtoto wakati wa ndoa
yake...” [Uk. 83]
Ø
Anaanzisha uhusiono wa mapenzi na mwanamke
mwingine aitwatae Dania
Anafaa
kuigwa
2.
Dania Theobald.
Ø
Ni binti wa miaka kama ishirini na nne.
Ø
Ni binti mrembo na wakuvutia.
Ø
Ni binti anayetoka katika familia ya kitajiri,
kama mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika Mama Mlole anaposema, “ Akiwa ni mtoto aliyetoka katika familia ya
Kitajiri.” [Uk. 81]
Ø
Ni msichana asiyedanganyika kwa fedha. Mwandishi
anathibitisha hili akimtumia muhusika Mama Mlole anaposema, “Sio hivyo tu, bali Dania alikuwa ni binti
mwenye uwezo kifedha; kwa hiyo hakuwa msichana aliyeweza kudanganyika kwa fedha
kama wengine.” [Uk. 82]
Ø
Ni mwanamke anayehitaji penzi la kweli, rejea
mwandishi anaposema “…hakuwa msichana
aliyeweza kudanganyika kwa fedha kama wengine. Kwake kilichohitajika ni penzi
tu.” [Uk. 82]
Ø
Mpenzi wa Jerry ambaye baadaaye anakuja
kusalitiwa na Jerry kwa kuanza uhusiano na mwanamke wa Kizungu huko Marekani,
kama mwandishi anavyosema akimtumia muhusika Mama Mallo, “ Mwaka wa pili ulipoisha Jerry alileta barua kuwa alikuwa amepata
mwanamke wa kizungu aliyepanga kufunga nae ndoa hukohuko Marekani.” [Uk.
87]
Ø
Alijaribu kujiua baada ya kusalitiwa na Jerry
kama mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika Mama Mallo anaposema, “ …Sasa hili lilkuwa ni pigo la mwisho na
Dania alivurugikiwa kabisa….alijaribu kujiua…” [Uk.87]
Ø
Ni mama wa Junior aliyezaa na Jerry.
Ø
Anaanza tabia ya ulevi wa kupindukia. Rejea
mwandishi anaposema, “Alianza kunywa
pombe kali tena kwa wingi.” [Uk. 87] Pia katika Ukurasa wa 88 mwandishi
anaendelea kuthibitisha hili anaposema, ”Akawa
mlevi wa kupindukia. Hakuna kilichomzuia kunywa pombe kali…”
Ø
Anaanza uhusiano wa mapenzi na mwanaume mwingine
aitwaye Gaddi Bullah baada ya kusalitiwa na Jerry.
Ø
Anapata ugonjwa wa ini kutokana na athari ya
pombe kali alizokuwa akinywa kama mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika
Dokta Virani anaposema, “Ini lake la
kulia limeathirika kutokana na pombe kali alizokuwa akinywa, wakati wa
mfadhaiko wake uliotokana na madhila aliyofanyiwa na Jerry.” [Uk. 105]
Ø
Anafadhiliwa sehemu/kipande cha ini na Gaddi
Bullah ili lipandikizwe katika ini lake, mwandishi analithibitisha hili
anaposema; "Gaddi Bullah ndiye mfadhiri wako Dania..." [Uk
140]
Ø
Mapenzi yanaathiri utendaji wake kazini kwani
hapo awali alikuwa ni mfanyakazi bora, mwenye nidhamu na ushirikiano kazini
kama mwandishi anavyosema kupitia mhuhusika Mama Mlole; "Miaka minne
iliyopita Dania Theobald alikuwa mmoja kati ya wafanyakazi wenye nidhamu, bidii
na ushirikiano mkubwa hapa makao makuu." [Uk 81]
Baadhi ya tabia
zake zinafaa kuigwa na jamii.
Ø Wahusika
wadogowadogo.
è
Bi.
Hanuna Bint Majid
è
Ni dada
pekee wa Gaddi Bullah.
è
Ni mjane, Kama mwandishi anavyosema; “Hanuna Bint Majid Bullah, maarufu kama Bi.
Hanuna, ambaye ni mjane.”
è
Anafukuzwa kwenye nyumba
è
Ana mapenzi ya dhati kwa kaka yake Gaddi Bullah.
è Anawekwa rumande kwa kosa la kumshambulia
Dania, kama mwandishi anavyosema, " Hapo Jerry alikuja juu. Alipiga
simu polisi na muda si mrefu Bi. Hanuna alikamatwa na kuwekwa rumande kwa kosa
la shambulizi." [Uk. 127]
Nunu.
è
Rafiki yake Dania
è
Mpenzi wa Boaz
è
Ni msichana mrembo.
è
MSichana jasiri.
Boaz
è
Mpenzi wa Nunu.
è
Anashirikiana na Nunu kumtafuta Gaddi Bullah
Anafaa
kuigwa.
Jerry
è
Msomi na mtaalamu wa kompyuta
è
Alikuwa mpenzi wa Dania kabla ya kumsaliti.
è
Anapata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani.
è
Hana mapenzi ya dhati kwa Dania.
è
Anatoweka baada ya kutakiwa kumtolea ini Dania.
è
Baba ya Junior.
Hafai
kuigwa
Nyambuja
è
Mke wa kwanza wa Gaddi Bullah
è
Anamsaliti mumewe kwa kuanzisha uhusiano wa
mapenzi na mwanaume mwingine.
Hafai
kuigwa.
Wahusika wengine ni;
è
Dokta Virani
è
Mama Mlole [Fausta]
è
Junior
DHAMIRA.
Dhamira ni wazo au mawazo
yaliyomo katika kazi ya fasihi na kwa kawaida katika kazi ya fasihi huwa tuna
dhamira kuu na dhamira ndogondogo, tukianza na dhamira kuu.
Ø
Dhamira kuu.
Dhamira kuu ni wazo kuu
linalojitokeza katika kazi ya fasihi, dhamira kuu katika riwaya hii ni mapenzi
na ndoa, sasa tuangalie ni kwa jinsi gani mwandishi ameijadili dhamira hii;
1. Mapenzi na Ndoa.
Mwandishi Hussein Tuwa amejadili suala la
mapenzi na ndoa katika pande mbili tofauti, kwanza ameonesha mapenzi ya dhati
na mapenzi ya ulaghai lakini pia ameonesha ndoa za dhati na ndoa za ulaghai.
tukianza na mapenzi ya dhati, mapenzi ya dhati yanajitokeza kwa:
[a] Gaddi Bullah kwa mke wake wa kwanza
anayeitwa Nyambuja,
Mwandishi ameonesha mapenzi ya
dhati aliyokuwa nayo Gaddi Bullah kwa mke wake, Mwandishi anathibisha hili
anaposema; "...na mke mzuri aliyempenda sana na aliyeamini kuwa naye alikuwa
akimpenda kawa dhati." [Uk 60]
mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo
kwa mke wake pia yanajidhihirisha pindi mke wake huyo alivyoanza kubadirika
kitabia, Gaddi alipewa ushauri na rafiki yake, lakini kwa kuwa alikuwa
akimpenda mke wake hakuukubali ushauri aliopewa. Mwandishi anathibitisha hili
anaposema; " ...Lakini kwa maoni yangu naona bora na wewe ujitafutie nyumba ndogo
ujiliwaze..." mwandishi anaendelea
kwa kusema; " ..Lakini hilo Gaddi hakuliafiki." [Uk 64]
[b] Gaddi Bullah kwa Dania.
Mapenzi ya dhati pia yanajitokeza kwa muhusika
Gddi Bullah kwa Dania, mwandishi anaonesha mapenzi haya ya dhati tangu kuanza
kwa uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili hawa na hata mara baada ya Dania
kumsaliti Gaddi Bullah, bado Gaddi alionesha mapenzi ya dhati kwa Dania na hata
Dania alipoanza kuumwa ini Gaddi alijitolea ini lake moja kumsadia Dania ili
apone yote haya aliyafanya kwa kuwa Bullah alikwa na mapenzi ya dhati kwa
Dania, kama mwansihi anavyothibitisha akiwatumia wahusika ha wote wawili,
mathalani Dania anapomuuliza Gaddi; " Umeokoa maisha yangu
Gaddi...baada ya yote niliyokufanyia...na hukutaka nijue kuwa ni wewe...kwa
nini mpenzi? Gaddi anamjibu kwa kumwambia; " Kwa sababu nakupenda
Dania!" [Uk. 144]
[c] Mapenzi ya dhati kati ya
Nunu na Boaz
Nunu na Boaz walipendana sana
kuonesha mapenzi ya dhati kati, walishirikiana wakati wa shida na raha, na hata
wakati Nunu anapewa kazi na Dania ya kumtafuta Daddi Bullah walishirikiana
pamoja kumtafuta na wakati mwingine hata kuhatarisha maisha yao. Rejea Uk 1-56 Nunu na Boaz wanavyoshirikiana
kumtafuta Bullah na hadi kuwalazimu kumteka nyara Bi Hanuna ambaye ni dada yake
Gaddi.
Tukigeukia katika uhalisia wake,
katika jamii yetu wapo watu ambao hupendana sana na wakawa na mapenzi ya dhati
na kusaidiana na kushirikiana kwa kila hali na mali kama tulivyoona kwa Nunu na
Boaz katika riwaya hii.
[d] Mapenzi ya dhati ya Dania
kwa Jerry.
Vilevile tunaona mapenzi ya dhati
ya Dania kwa Jerry, pamoja na Jerry kumfanyia Dania kila aina ya vituko, kama
vile kuk=mkimbia katikati ya maandalizi ya arusi yao, na kumtumia barua kuwa
amepata mchumba mwingine huko Marekani na aliporejea kutoka Marekani na kutaka
kurudiana na Dania, Dania anakubali ingawa alikuwa na mwanaume mwingine na hii
yote ni kwasababu Dania alimpenda Jerry, kama mwandishi anavyothibitisha
akitumia muhusika Dania anaposema; “Nilimuona Jerry ni bora kuliko
Gaddi..." [Uk 135]
Tukigeukia katika uhalisia wake,
ni wazi kuwa katika jamii zetu, wapo watu wanaoangukia katika mapenzi na watu
ambao kiukweli hawawapendi ila kwa kuwa yeye anampenda basi hujikuta
anajiingiza katika uhusiano naye matokeo yake ndiyo hayp sasa, usaliti, visa,
vitimbi na kuona kuwa ndoa chungu.
[e] Mapenzi ya dhati kati ya
Gaddi Bullah na Bi. Hanuna.
Hawa ni ndugu waliopendana sana,
na hata katika matatizo yaliyomkuta Gaddi Bullah, Bi. Hanuna alikuwa bega kwa
bega na kaka yake, na hakuwa tayari kumsaliti kaka yake kwa kiapo walichopeana
pindi akitafutwa na watu ambao hakutaka kuwaona tena katika maisha yake
kutokana na unyama aliofanyiwa, kwa mfano Mwandishi anamwonyesha Bi. Hanuna
akikataa kata kata kumweleza Nunu mahali alipo Gadii Bullah, kama Mwandishi
anvyosema akimtumia Bi. Hanuna mwenyewe; "Na kaniapiza kuwa nisithubutu
hata siku moja kuwapeleka au kuwatajia mahala alipo...kwa sababu siwezi kuvunja
kiapo changu na kumsaliti mdogo wangu pekee kwa ajili ya mahayawani kama
nyinyi!" [Uk. 31-32]
Haya yote bi Hanuna aliyafanya
kawa sababu walipendana sana na Gaddi, furaha ya Gaddi ilikuwa furaha ya Bi.
Hanuna na kuumia kwa Gaddi kulikuwa ni kuumia kwa Bi. Hanuna na ndio maana kila
aliyemuudhi mdogo wake kwake alikuwa adui yake.
Tukigeukia katika uhalisia,
katika jamii yetu wapo ndugu ambao wanapendana na kushirikiana kwa kila hali
kama wanavyoonekana Gaddi na Bi. Hanuna katika riwaya hii.
[f] Mapenzi ya dhati ya Gaddi
Bullah kwa Junior.
Gaddi Bullah alimpenda sana
Junior kama mtoto wa kumzaa mwenyewe, na hata Junior alipopata ajali ya
kuanguka kutoka kwenye mti ni Gaddi ndiye aliagizwa apelekwe hospitali nae
akafuata na alipomrudisha nyumbani hakuweza kumuacha peke yake, kama mwandishi
anavyosema; "Gaddi alilazimika kusubiri pale nyumbani hadi atakaporudi,
kwanza kwa kuhofia hali atakayokuwa nayo Junior pindi akiamka na kukuta si mama
yake wala Gaddi aliyekuwepo pale nyumbani..." [Uk 119]
Na hata wakati anaumwa Gaddi
alimwachia husia Dania amtunze vizuri Junior, Mwandishi anathibitisha
anapomtumia Gaddi kusema; "Junior Dania... Junior! Mtunze vizuri
Junior! Umepewa bahati ya kuu...ndelea kuishi ili umtunze mwan...na...o!"
[Uk 146]
Haya yote Gaddi Bullah aliyanya
kwa kuwa alimpenda sana Junior. Na tukigeukia katika uhalisia wake katika jamii
zetu, wapo watu au familia ambazo utamkuta baba si mzazi wa mtoto au mama
lakini wakaonesha mapenzi ya dhati kwa watoto hao kana kwamba wao ndiyo
wamewazaa, upendo ambao hata mzazi husika hawezi kutoa kama tunavyoona kwa
Jerry.
[g] Mapenzi ya dhati ya Mama
Mlole kwa wafanyakazi walio chini yake.
Mwandishi amemtumia muhusika Mama
Mlole [Fausta] kama kiongozi anayewajali na kuwapenda wafanyakazi wake na
kuwasaidia pindi wanapopatwa na matatizo, kwa mfano Mama Mlole anaonesha
mapenzi ya dhati kwa kumsaidia Dania kurudi kazini licha ya kuwa na matatizo,
lakini pia Mama Mlole alimsaidia na Gaddi Bullah ili asifukuzwe kazi kutokana
na kutuhumiwa kuhusika na malipo hewa. Mwandishi anathibitisha hili anapomtumia
muhusika Mama Mlole anapoongea na Gaddi Bullah; "Ndio... na kwa hatua
aliyofikia, ilibidi aachishwe kazi, lakini kwa kumsaidia, nikiwa kama Afisa
Utumishi wa kampuni, nilipendekeza apewe likizo.... nilifanya kazi ya ziada
kuushawishi uongo wa kampuni juu ya hili, jinsi nilivyofanya kazi ya ziada
kulishawishi lile jopo la wakaguzi kule Arusha kukupa wewe nafasi
nyingine...badala ya kukufaukuza kazi..." [Uk 88]
Mama Mlole pia alikuwa
akimtembelea Dania wakati alipokuwa anaumwa ili kujua maendeleo yake kama
anavyosema; "Mimi nilikuwa nikimtembelea mara kwa mara kuona maendeleo
yake na kuleta ripoti kwenye uongozi wa kampuni.
Mama Mlole anayafanya yote haya
kwakuwa anawapenda wafanyakazi wake, na tukiaangalia katika uhalisia wake, wako
mabosi au wakuu ambao huwapenda wafanayakazi waliochini yao na hata
wanapokabiliwa na matatizo huwasaidia kama tulivyoona kwa Mama Mlole.
[h] Mapenzi ya dhati kati ya
Nunu na Dania.
Nunu alikuwa ni rafiki wa kweli
wa Dania, walishirikiana bega kwa bega, wakati wa maadalizi ya arusi ya Dania
na Jerry, Nunu alikuwa ndiye mwenyekiti wa kamati, na hata Dania aliposalitiwa
na Jerry na Dania kuanza tabia ya ulevi ni Nunu ndiye alikuwa akimsaidia Dania
kumlelea mtoto wake na hata Dania alipoanza kuumwa Nunu alikuwa tayari kumtolea
ini lake kama mwandishi anavyothibitisha hili anaposema, “Nunu naye
alijitolea. Vipimo vilionesha kuwa maini yake yote yalikuwa safi na aliweza
kabisa kumtolea Dania ini moja, lakini damu yake ilikuwa haioni kabisa na ile
ya Dania." [Uk 132]
Na hata Dania alipompa Nunu kazi
ya kumtafuta Gaddi Bullah aliifanya kwa moyo wote kwakuwa alimpenda rafiki
yake.
Tukiaangalia uhalisia wake na
jamii yetu, wapo marafiki aina ya Dania na Nunu ambao hupendana, husaidiana
katika shida na raha, kupeana ushari unaojenga. n.k huu ndio urafiki unaofaa.
[i] Mapenzi ya dhati ya Dania
kwa Mtoto wake {Junior]
Vilevile mapenzi ya dhati
yanajidhihirisha kwa Dania kwa mtoto wake, Dania alimpenda sana mtoto wake
[Junior] mpaka kuamua kurudiana na Jerry ambaye ndiye baba wa wmtoto wake ili
mwanae apate malezi ya baba na mama kama mwandishi anavyothibitisha hili
akimtumia muhusika Dania anaposema; "Siwezi Nunu, siwezi...nimeshaanza
naye uhusiano nadhani Junior anastahili zaidi kulelewa na baba yake mzazi
kuliko baba wa kambo." [Uk.115]
Tukigeukia katika uhalisia wake,
katika jamii yetu wapo wazazi ambao huwapenda watoto na hata kutopenda kuona
watoto wao wanapatwa na matatizo katika makuzi yao.
{j] Mapenzi ya dhati kwa
wazazi wa Dania kwa mtoto wao Dania.
Pia mapenzi ya dhati yanajitokeza
kwa wazazi wa Dania, kwa mfano baba yake Dania [Mzee Theobald] anamjengea Dania
nyumba na hata Dania anapoanza kuumwa ini wazazi wake wanakuwa tayari kujitolea
ini moja kwa ajili ya mtoto wao lakini kutokana na uzee na kuumwa kisukari kwa
Mzee Theobald inashindikana kama mwandishi anavyosema akimtumia muhusika Mzee
Theobald; "Dokta, mimi niko tayari kujitolea ini laangu kwa ajili ya
mwanagu!" pia mwandishi anaendelea kusema, "Na wakati huo huo
mama naye alijitolea." [ Uk
132]
Tukiigeukia jamii yetu, wapo
wazazi aina ya Mzee Theobald na mkewe, ambao huwapenda watoto wao na kujitoa
kwa kila hali ili mradi tu kuona kuwa watoto wao wanaishi maisha mazuri na
salama.
[k] Mapenzi ya dhati kati ya
Dokta Virani na Gaddi Bullah
Vilevile katika riwaya hii ya Mfadhili
mwandishi ameonesha mapenzi ya dhati aliyonayo Dokta Virani kwa Gaddi
Bullah, Dania pamoja na Bi. Hanuna. kwa mfano tunamwona Dokta Virani akipigana
kufa na kupona kuokoa maisha ya Dania na hata kumuangaikia kumtafutia mfadhili
wa kumfadhili ini katika vyombo mbalimbali vya habari, vilevile anamsaidia
Dania kumjua mfadhili aliyemfadhili ini jambo ambalo lilikuwa likimsumbua sana
Dania, Mwandishi analithibitisha hili akimtumia muhusika Dokta Virani
akimw.ambia Dania; "Gaddi Bullah ndiye mfadhili wako Dania..." [Uk
140]
Lakini pia mwandishi ameonesha
mapenzi ya dhati ya Dokta Virani kwa Gaddi Bullah na jinsi alivyojitahidi
kuokoa uhai wa Gaddi, lakini Mungu
alimpenda zaidi Gaddi, akamtwaa. [Uk 144-148]
Pia mapenzi ya dhati ya Dokta
Virani kwa Bi. Hanuna. katika riwaya hii tunaona baada ya Bi. Hanuna kukamatwa
na kuwekwa rumande ni Dokta Virani anahangaika na kumtoa kwa dhamana kama
mwandishi anavyosema; "Dokta Virani alipopata taarifa alihangaika huku
na huko kumpatia dhamana, lakini ilishindikana." Mwandishi anaendelea
kusema; "Siku iliyofuata, Dokta Vilani alifanikiwa kumtoa kwa
dhamana." [Uk 127]
Hata katika jamii yetu watu jamii
ya Dokta Virani wapo, huwajali wateja wao, huwapenda na wakati mwingine kuwa
sehemu ya familia hizo kama tunavyomuona Dokta Virani na akina Gaddi Bullah.
Mapenzi ya Ulaghai / Uongo
Pamoja na kuwa mwandishi ameweza
kuonesha ni kwa jinsi kuna watu wenye mapenzi ya dhati kwa wenzi wao, ndugu,
jamaa na marafiki, mwandishi kwa upande mwingine ameonesha nai kwa jinsi gani
katika jamii yake kuna watu wasio na
mapenzi ya dhati kwa watu wanaohusiana nao, kama vile wanandoa, wapenzi,
marafiki, ndugu, jamaa na marafiki. Ebu tuangalie sasa jinsi mapenzi ya ulaghai
yanavyojitokeza katika riwaya hii;
[a] Dania kwa Gaddi Bullah
Dania hakuwa na mapenzi ya dhati
kwa Gaddi Bullah, na ndio maana mara aliporejea mpenzi wake wa zamani aitwaye
Jerry ilikuwa ni rahisi kwa Dania kukubali kurudiana nae ingawa alikuwa na
mahusiano na Gaddi Bullah mpaka kufikia hatua ya kumfukuza Gaddi nyumbani
kwake, kama mwandishi anavyoonesha akimtumia muhusika Dania anapomwambia Gaddi
Bullah; "Gaddi samahani sana kwa hili, lakini naomba ujue sitakuwa
tayari kumyima mwanangu nafasi ya kuishi na baba yake mzazi kwa ajili ya mtu
yoyote! Nakuomba uondoke Gaddi..." [Uk 122]
Hata katika jamii yetu, mapenzi
ya aina hii yapo, wapa watu kama Dania ambao hujikuta wakijiingiza katika
mahusiano na watu wengine ili kutafuta faraja kutokana na kuachwa au kusalitiwa
na wenza wao lakini si kwamba wana mapenzi ya dhati na pindi inapotokea
kurubuniwa tena na wenza wao wa zamani inakuwa rahisi kwao kukubali na kuwa
chungu kwa yule anayeachwa kama tulivyoona kwa Gaddi Bullah.
[b] Jerry kwa Dania
Jerry hakuwa na mapenzi ya dhati
kwa Dania, kwa mfano katika riwaya hii tunamwona Jerry akimkimbia Dania katika
hatua za mwisho za maandalizi ya arusi yao na kwenda Marekani kwa ajili ya
masomo, na anapofika huko anamwandikia Dania barua kuwa amepata mwanamke mwingi
wa kizungu anataka kumuoa kama mwandishi anavyosema; " Mwaka wa pili ulipoisha Jerry alileta barua kuwa alikuwa amepata
mwanamke wa kizungu aliyepanga kufunga nae ndoa hukohuko Marekani.” [Uk 87]
Na hata Jerry aliporejea na
kuomba msamaha kwa Dania, Dania anamsamehe lakini pindi Dania anapoanza kuumwa
na yeye kuombwa ajitolee ini anatoweka kabisa kama mwandishi anavyoonesha;
"Baada ya hapo Jerry Gwandume alitoweka. Alitoweka kabisa siku ya operesheni hakuonekana na kwenye simu
akawa hapatikani. Nyumbani kwake hakupatikana..." [Uk 133]
Mwandishi anaendelea kusema;
"...na hapo ndipo ilipoeleweka dhahiri kuwa Jerry amekimbia kumtolea ini
lake Dania." [Uk 133]
Katika jamii yetu watu aina ya
Jerry wapo, ambao huwaraghai wasichana kwa maneno mazuri lakini inapofika
wakati wa shida huwakimbia na kutoweka kama tulivyoona kwa Jerry.
[c] Nyambuja kwa Gaddi
Nyambuja hakuwa na mapenzi ya
dhati kwa Gaddi Bullah, pamoja na kuwa Nyambuja alikuwa ameolewa lakini bado
akawa anaisaliti ndoa yake kwa kuanzisha uhusiano na mwanaume mwingine, na hata
barua aliyomwandikia Gaddi Bullah inaonyesha dhahiri kuwa Nyambuja hakuwa na
mapenzi ya dhati kwa mumewe. Rejea barua aliyoandika Nyambuja anaposema; “Gaddi
nimependana na mtu mwingine, na nimekuwa nikisaliti ndoa yetu kwa muda mrefu.”
[Uk 65]
Tukigeukia katika uharia wake,
watu kama Nyambuja wapo, zipo ndoa nyingi katika jamii zetu ambazo zimekuwa
zikijaa usaliti, dharau. n.k. Katika ndoa mume anaweza kumsaliti mke na mke pia
anaweza kumsaliti mume kama tulivyoona kwa Nyambuja.
[d] Rafiki wa Bullah kwa Bullah.
Rafiki wa Gaddi Bullah pia hakuwa
na mapenzi ya kweli na Gaddi Bullah, kwa mfano rafiki huyo anamshauri Gaddi
Bullah kutafuta nyumba ndogo wakati akijua kuwa ulimwengu wa sasa umejaa
magonjwa ya hatari hususani UKIMWI. Rafiki wa kweli hawezi akatoa ushari kama
huo. Rejea Ukurasa wa 67 rafiki huyo anapomshauri Gaddi, anasema; “Gaddi unajua mimi sijaoa. Nitawezaje kutoa
ushauri juu ya suala kama hilo?.....Lakini kwa maoni yangu naona bora na wewe
ujitafutie nyumba ndogo ujiliwaze…” [Uk 67]
Pia mwandishi anaonesha urafiki
huu wa mashaka anaofanyiwa Gaddi na huyo rafiki yake kwa kuamua kumsaliti na
kuanzisha uhusiano wa mapenzi na mke wa Gaddi Bullah, Mwandishi anaonesha hili
akimtumia Gaddi Bullah anaposema; "Na
wewe! Nilidhani kuwa u rafiki yangu! Nilikuwa nakuletea matatizo yangu kumbe
ulikuwa ukinilamba kisogo?” [Uk 67]
Hata katika jamii zetu urafiki wa
aina hii upo, utakuta mtu anajifanya kuwa ni rafiki wa kweli lakini kumbe ndiye
anaekuzunguka na kukuharibia mambao yake kama tulivyoona kwa Gaddi na rafiki yake.
Ø
Dhamira ndogo ndogo.
Haya ni mawazo yanayojitokeza ili
kujenga dhamira kuu. Dhamira ndogondogo zinazojitokeza katika riwaya hii ni;
1. Usaliti.
Hii ni dhamira nyingine
inayojitokeza katika riwaya hii, sasa tuangalie jinsi usaliti huo unavyojitokeza
katika riwaya hii;
[a] Nyambuja anamsaliti Gaddi
Bullah.
Mwandishi ameonesha katika ndoa
kwa kuwatumia wahusika Gaddi Bullah na Nyambuja, kwa mfano nyambuja anaamua
kuisaliti ndoa yako kwa kuanza uhusiano wa mapenzi nje ya ndoa na mwanaume
mwingine, hili Mwandishi analithibitisha akimtumia Nyambuja mwenyewe anaposema
katika barua aliyomwandikia Gaddi Bullah, “Gaddi nimependana na mtu
mwingine, na nimekuwa nikisaliti ndoa yetu kwa muda mrefu.” [Uk 65]
[b] Jerry anamsaliti Dania
Usaliti mwingine unaojitokeza
katika riwaya hii, ni usaliti unaofanywa na Jerry kwa Dania, kwa mfano
Mwandishi anamuonesha Jerry akienda masomoni Marekani kaatika hatua za mwisho
za maandalizi ya ndoa yake na Dania, na anapofika huko anamwandikia Dania kuwa
amepata mwanamke mwingine wa kizungu anaetaka kumuoa, hili linathibitishwa na
Mwandishi anaposema; " Mwaka wa pili
ulipoisha Jerry alileta barua kuwa alikuwa amepata mwanamke wa kizungu
aliyepanga kufunga nae ndoa hukohuko Marekani.” [Uk 87]
[c] Dania anamsaliti Gaddi
Bullah
Mwandishi pia ameonesha usaliti
katika mapenzi akimtumia muhusika Dania, kwa mfano Mwandishi anamwonesha Dania
akimsaliti mpenzi wake [Gaddi Bullah] kwa kuamua kurudiana na mpenzi wake wa
zamani aliyezaa naye mtoto na kuamua kuachana na Gaddi, Mwandishi unaonesha
usaliti huu akimtumia Dania anapomwambia Gaddi Bullah;"Gaddi samahani
sana kwa hili, lakini naomba ujue sitakuwa tayari kumyima mwanangu nafasi ya
kuishi na baba yake mzazi kwa ajili ya mtu yoyote! Nakuomba uondoke
Gaddi..." [Uk 122]
[d] Gaddi Bullah anasalitiwa
na Rafiki yake.
Mwandishi pia ameonesha usaliti
katika urafiki, amemtumia muhusika rafiki yake Gaddi
ambaye anaamua kumsaliti rafiki
yake [Gaddi Bullah] wakati akiwa ni rafiki wa karibu wa Gaddi na alimtegemea
sana kwa ushauri pindi anapoptwa na matatizo, Mwandishi analionesha hili
anaposema; "Baadaye aliamua kwenda kwa rafiki yake kumpasha habari
habari juu ya masahibu yake. na huko alipata mshituko mkubwa. Mke wake mwenyewe
ndiye aliyemfungulia mlango, tena akiwa khanga moja tu...ilhali rafiki yake
akiwa amejitawanya kwenye sofa akiwa kidari wazi na kaptura tu!" [Uk
66]
Tukigeukia katika uhalisia wake,
usaliti katika ndoa, mapenzi na hata marafiki wa kawaida tu limekuwa ni tatizo
katika jamii na ni suala ambalo linatakiwa kupigwa vita sana katika dunia hii
yenye magonjwa ya kila aina.
2. Ulevi.
Mwandishi Hussein Tuwa hakuwa
nyuma kujadili suala la ulevi na athari zake kwa afya ya binadamu, katika
riwaya yake hii amemtumia muhusika Dania
pamoja na Gaddi Bullah kuelezea dhamira hii. Tukianza na Dania, mwandishi
anamwonesha Dania akianza tabia ya ulevi wa pombe kali baada ya kusalitiwa na
Jerry ambaye alikwa ni mpenzi wake, kama mwandishi anavyosema akimtumia
muhusika Mama Mlole, “Alianza kunywa
pombe kali tena kwa wingi.” [Uk 87] mwandishi hakuishia hapo tu bali
ameonesha na athari za tabia hiyo ya ulevi kama vile kupata ugonjwa wa ini kama
mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika Dokta Virani anaposema," “Ini lake la kulia limeathirika kutokana na
pombe kali alizokuwa akinywa, wakati wa mfadhaiko wake uliotokana na madhila
aliyofanyiwa na Jerry.” [Uk 105]
Lakini pia athari nyingine
anazozipata Dania kutokana na ulevi wa kupindukia ni kupoteza ufanisi wa kazi,
hili pia linathibitishwa na mandishi anaposema; "Na hapo ndipo utendaji
wake kazini ulipoathirika vibaya sana. kazi zikawa haziendi kabisa. Alipofikia
hatua ya kuja ofisini akiwa amelewa zaidi ilikuwa ni zaidi ya kuvumilika."
[Uk 88]
Mwandishi pia amemtumia muhusika
Gaddi Bullah kuelezea dhamira hii ya ulevi, tofauti na Dania ambaye yeye
ametumiwa kuonesha dhamira ya ulevi wa pombe, Gaddi Bullah ametumika kuelezea
dhamira ya Ulevi wa uvutaji wa sigara uliokithiri kama mwandishi
anavyothibitisha anaposema, "Alikuwa akivuta sigara mfululizo huku
kichwa chake kikiwa kimetawaliwa na mawazo mazito..." [Uk 57]
Mwandishi hakuishia hapo kuonesha
tataizo la uvutaji sigara, ameonesha pia athari zake ambapo katika riwaya hii
anamtumia muhusika Gaddi Bullah kutokana na uvutaji wa sigara uliokitiri Gaddi
anapata matatizo ya mapafu na hatimaye kuaga dunia kutokana na matatizo hayo.
Hivyo basi suala la ulevi jamii inatakiwa kuachana nalo kwa ni hatari kwa afya
na uhai wa binadamu.
3. Malezi kwa watoto.
Hii ni dhamira nyingine
inayojitokeza katika riwaya hii, Mwandishi amemtumia muhusika Dania kuilezea
dhamira hii, tunamwona Dania akitaka kurudiana na Jerry ambaye ni baba wa mtoto
wake ili kwa pamoja waweze kumlea mtoto wao akiamni kuwa malezi ya mtoto ni ya
wazazi wote wawili kama mwandishi anavyothibitisha hili akimtumia muhusika
Dania mwenyewe, "Ni kweli kuwa Jerry alinikosea, na nikweli kuwa wewe
nilikupenda! Lakini Jerry ni baba wa mtoto wangu! Na naomba uelewe kuwa uamuzi
huu ni kwa ajili ya mwanetu..." [Uk 122]
4. Unafiki.
Hii ni dhamira pia inayojitokeza
katika riwaya hii, katika kuijadili dhamira hii Mwandishi amemtumia rafiki yake Gaddi Bullah, anamwonesha Gaddi Bullah akiomba ushauri kwa
rafiki yake huyo kuhusiana na matatizo yake na mkewe, rafiki huyo anamshauri
Gaddi atafute nyumba ndogo. Rejea ukurasa wa 64 Mwandishi anaposema, “Gaddi unajua mimi sijaoa. Nitawezaje kutoa
ushauri juu ya suala kama hilo?.....Lakini kwa maoni yangu naona bora na wewe
ujitafutie nyumba ndogo ujiliwaze…”
Rafiki huyo anashauri hivyo huku
kumbe yeye ndiye chamzo anayemsaliti mwenzake kwa kumzunguka kwa mke wake, kama
mwandishi anavyothibitisha hili anaposema;
“ Na wewe! Nilidhani kuwa u rafiki yangu! Nilikuwa nakuletea matatizo yangu
kumbe ulikuwa ukinilamba kisogo?” [Uk 67]
Tukigeukia katika uharisia, tabia
hii ya unafiki imeshamiri katika jamii zetu, unaweza ukawa na rafiki au ndugu
ambaye akawa mnafiki kwako. Jamii inatakiwa kuondokana na tabia hii kwa haifai
kabisa.
5. Ufisadi / Wizi kazini.
Mwandishi pia amejadili suala la
ufisadi sehemu ya kazi, amemtumia muhusika Afisa Usafirishaji ambaye anapeleka
orodha malipo ya magari saba yaliyofanyiwa matengenezo huku magari matano
yakiwa magari hewa kama mwandishi anavyosema,
“ Kwani ilionekana kuwa katika magari saba yaliyofanyiwa malipo kwa
matengenezo, ni mawili tu ndio hasa yaliyopelekwa matengenezo. Ni wapi pesa za
malipo ya yale magari matano mengine zilikwenda?” [Uk 68]
Tukigeukia katika uhalisia wake,
suala la ufisadi au wizi sehemu za kazi ni suala ambalo linasumbua sana jamii
yetu, si serikalini au katika makampuni binafsi ufisadi kama vile kuandaa vocha
za malipo hewa, rushwa tena zile kubwa kubwa, matumizi mabaya ya mali za ofisi.
n.k ni tatizo sugu na jamii inatakiwa kuondoka nalo.
6. Elimu.
Mwandishi hakuwa nyuma kujadili
suala la elimu na umuhimu wake kwa jamii. Katika kujadili dhamira hii mwandishi
anaonesha kuwa elimu ni ufunguo unaoweza kumfunguliwa mtu milango mipya ya
maendeleo kielimu na kiuchumi, kama Mwandishi anavyothibitisha hili anaposema
akimtumia muhusika Mama Mlole, “ Mke anamtaka, lakini na masomo pia
anayataka. Masomo ambayo yangemfungulia milango mipya ya maendeleo kielimu na
kiuchumi.” [Uk 84]
Hata katika jamii zetu, jamii
imekuwa ikisisitiza sana suala la elimu, watu wengi waliosoma wamepata kazi
nzuri na wana maisha mazuri kama tulivyoona kwa Gaddi Bullah, lakini pia wapo
vijana waliopata elimu zao nje ya nchi kama tulivyoona kwa Jerry.
7. Uongozi bora
Vilevile suala la uongozi bora
limejitokeza katika riwaya hii, kwa mfano mwandishi anamtumia muhusika Mama
Mlole [Fausta] kujadili dhamira hii, tunamwona Mama Mlole jinsi alivyokuwa na
upendo kwa wafanayakazi waliochini yake, anawasaidia pindi wanapopatwa na
matatizo, mathalani anamsaidia Dania na Gaddi Bullah wasifukuzwe kazi kama
mwandishi anavyothibitisha hili akimtumia Mama Mlole mwenyewe; "Ndio...
na kwa hatua aliyofikia, ilibidi aachishwe kazi, lakini kwa kumsaidia, nikiwa
kama Afisa Utumishi wa kampuni, nilipendekeza apewe likizo.... nilifanya kazi
ya ziada kuushawishi uongo wa kampuni juu ya hili, jinsi nilivyofanya kazi ya
ziada kulishawishi lile jopo la wakaguzi kule Arusha kukupa wewe nafasi
nyingine...badala ya kukufaukuza kazi..." [Uk 88]
Mwandishi pia anasisitiza suala
la uongozi, akiwataka viongozi wabadilike wawe viongozi wa kuwajenga watu
waliochini yao kitabia na kimaadili kama Mwandishi anavyosema akimtumia Mama
Mlole; "Utawala wa kusubiri mfanyakzi akosee ili umuadhibu siku
hizi umepitwa na wakati, Gaddi! Utawala wa sasa ni wa kumjenga mfanyakazi
kitabia na kimaadili ili asiingie kwenye makosa yatakayosababisha kuchukuliwa
hatua za kinidhamu. Viongozi tunatakiwa tubadilike sasa, Gaddi!" [Uk
93]
Tukigeukia katika uhalisia wake,
katika jamii yetu viongo bora kama Mama Mlole wapo lakini pia wapo viongozi
ambao wao husubiri wafanyakazi wao wakosee ili wawachukulie hatua kama
kuwafukuza kazi au kuwapa onyo kali. Hivyo viongozi wanatakiwa kubadilika na
kwenda na wakati.
8. Nafasi ya mwanamke.
Katika riwaya hii mwanamke
amechorwa katika pande mbili, amechorwa katika upande hasi lakini pia mwanamke
amechorwa katika upande chanya, upande hasi mwanamke amechorwa kama kiumbe duni
na dhaifu wakati katika upande chanya amechorwa kama mtu jasiri, mchapa kazi,
mwenye upendo. n.k. Ssasa hebu tuangalie nafasi ya mwanamke katika jamii kama
alivyochorwa katika riwaya hii tukianza na upande hasi;
Katika riwaya hii mwanamke amechorwa
kama kiumbe duni, dhaifu, katika nafasi mwanamke amechorwa kama;
[A] Chombo cha starehe.
Mwandishi amemchora mwanamke kama
chombo cha starehe anayeweza kutumiwa kuwastarehesha wanaume na wakapokeza
jinsi wanavyotoka ili mradi kufurahisha nafsi zao, hili linathibitishwa na
Mwandishi katika riwaya hii akimtumia muhusika Jerry anapomwambia Gaddi Bullah;
"Hakuna haja ya kupoteza muda. Tumeamua kufunga ndoa kwa kuzingatia
maslahi ya mwanetu, kwahiyo bwana we kaa pembeni sasa. Muda wako kwa Dania
umekwisha." [Uk. 121]
Mwandishi pia amemtumia rafiki
yake Gaddi Bullah kumchora mwanamke kama chombo cha starehe kwa kuwa mwanaume
anaweza kumtumia kujilawa na kuburudisha nafsi, kama anavyosema; “...Lakini kwa maoni yangu naona bora na
wewe ujitafutie nyumba ndogo ujiliwaze…”[Uk 64]
Hata katika jamii yetu
inayotuzunguka wanawake kwa kujijua au kutojua wamekuwa wakifanywa kama chombo
cha starehe kuwastarehesha wanaume, jamii inatakiwa kubadilika na kuondokana na
dhana hii kwani mwanamke pia anastahiri heshima katika jamii.
[B] Mtu asiye na maamuzi
katika jamii
Mwandishi amemchora mwanamke kama
mtu asiye na maamuzi katika jamii yake, kwa mfano anamtumia muhusika Bi. Hanuna
kuthibitisha hili, baada ya Bi. Hanuna kufiwa na mumewe na kwa kuwa hakuzaa nae
anakuwa hana maamuzi na haki yoyote kwa mali aliyochuma na mume wake na ndugu
wa mume wanaamua kumfukuza katika nyumba aliyojenga na mume wake kama mwandishi
anavyosema; " ...ambaye naye hakujaliwa kupata mtoto mpaka mumewe
alipofariki, jambo lililowafanya ndugu wa marehemu mumewe kumfukuza kama mbwa
kutoka kwenye nyumba ya marehemu mumewe." [Uk 60]
Hata katika jamii yetu,
inawachukulia wanawake kama watu wasio na maamuzi katika familia na pindi
inapotokea kufiwa na waume zao huwa wanapata shida na manyanyaso kutoka kwa
ndugu wa mwanaume kama vile kufukuzwa kwenye nyumba, kunyang'anywa watoto na
mali nyingine alizoshirikiana kuzichuma na mumewe. jamii inatakiwa kumpa nafasi
mwanamke na itambue kuwa ana haki sawa kama mwanaume.
[C] Mwanamke amechorwa kama
mtu asiye na msimamo katika maamuzi yake.
Hili Mwandishi amelionesha
kupitia kwa muhusika Dania, ambaye anaonekana kuwa hana msimamo juu ya kila
anachoamua, kwa mfano baada ya Dania kusalitiwa na Jerry na kupata matatizo
mbalimbali kutokana na kusalitiwa huko, baadaye tunamwona akianza uhusiano na
mwanaume mwingine lakini anaporejea yule aliyemsaliti mwanzo na kumrubuni kwa
maneno mazuri anajikuta akirudiana nae kama mwandishi anavyosema; "BIla
kujijua, Dania alijikuta akijiingiza tena katika mapenzi na Jerry." [Uk
113]
Hata katika jamii yetu, wanawake
wengi kwa kutokuwa na misimamo ya kimaisha hujikuta wakijiingiza katika
matatizo mbalimbali kama vile kurubuniwa na wanaume. Hivyo wanawake wenyewe
wanatakiwa kujitambua na kubadilika.
[D] Mwanamke amechorwa kama
msaliti.
Hii ni nafasi nyingine ambayo
mwandishi amemchora mwanamke, kwa mfano tunaona Nyambuja akiisaliti ndoa yake.
Rejea barua aliyoandika Nyambuja kwa Gaddi Bullah anaposema;“Gaddi
nimependana na mtu mwingine, na nimekuwa nikisaliti ndoa yetu kwa muda mrefu.”
[Uk 65]
vilevile nafasi hii ya usaliti
imechorwa kupitia muhusika Dania, ambaye anamsaliti Gaddi Bullah kwa kuamua
kurudiana na Jerry ambaye amezaa naye mtoto na kufikia hatua ya kumfukuza Gaddi
nyumbani kwake baada ya kuwafumania. Rejea Dania anapomwambia Gaddi Bullah; "Gaddi
samahani sana kwa hili, lakini naomba ujue sitakuwa tayari kumyima mwanangu
nafasi ya kuishi na baba yake mzazi kwa ajili ya mtu yoyote! Nakuomba uondoke
Gaddi..." [Uk 122]
Hivyo ndivyo jinsi mwandishi Hussein
Tuwa alivyomchora mwanamke katika upande hasi, yaani kiumbe duni na dhaifu sasa
tugeukie upande wa pili, upande chanya, katika upande huu mwanamke amechorwa
katika nafasi zifuatazo:
[A] Mwanamke amechorwa kama mtu
jasiri.
Mwandishi katika riwaya hii amemtumia
muhusika Nunu Mkwanda, tunaona namna nunu anavyojitoa muhanga na kuamua kumteka
Bi. Hanuna huku akifahamu kuwa kitendo hicho ni cha hatari, alifanya hivyo kwa
kuwa Bi. Hanuna hakuwa tayari kutaja alipo Gaddi Bullah, na allifanya hivyo ili
mradi tu lengo la kumpata Gaddi Bullah
kama alivyomuahidi rafiki Dania limitie, Mwandishi anathibisha hili anapomtumia
Nunu anaposema; Potelea mbali Bi. Hanuna! Alimradi utakuwa umeona ni kwa nini
nimelazimika kufanya hivi baada ya maombi yangu kwako kushindikana, haitakuwa
na neno kabisa kwangu." [Uk. 44]
Hata katika jamii zetu wanawake
jasiri kama Nunu wapo ambao hujitoa kwa kila hali na wakati mwingine hata
kuweza kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya wengine.
[B] Mwanamke amechorwa pia
kama kiongozi bora.
Mwandishi amemtumia muhusika
Fausta Mlole ambaye wanyakazi wake kutokana uongozi wake mzuri na kuwajali
wafanyakazi walikuwa wakimuita kwa jina la Mama Mlole, katika riwaya hii Mama
Mlole anawakilisha wanawake viongozi ambao huwaongoza wafanyakazi waliochini yao
kwa kufauta taratibu, upendo na kuwasaidia, kuwa karibu nao wakati wa shida na
raha kama tunavyomuona Mama Mlole akifanya kwa wafanyakazi wake.
Kwa mfano Mama Mlole kama Afisa
Utumishi anamsaidia Gaddi na Dania wasifukuzwe kazi kama anavyosema; "Ndio...
na kwa hatua aliyofikia, ilibidi aachishwe kazi, lakini kwa kumsaidia, nikiwa
kama Afisa Utumishi wa kampuni, nilipendekeza apewe likizo.... nilifanya kazi
ya ziada kuushawishi uongo wa kampuni juu ya hili, jinsi nilivyofanya kazi ya
ziada kulishawishi lile jopo la wakaguzi kule Arusha kukupa wewe nafasi
nyingine...badala ya kukufaukuza kazi..." [Uk 88]
Hata katika jamii yetu wanawake
viongozi kama Mama Mlole wapo, na wanawaongoza vizuri wafanayakazi pengine
kuwazidi hata baadhi ya wanaume. hivyo wanawake wakiwezeshwa wanaweza.
Hivyo ndivyo jinsi mwandishi
alivyoweza kumchora mwanamke katika nafasi mbalimbali katika jamii yake.
MIGOGORO
Mgogoro wa nafsi.
Gaddi Bullah na nafsi yake
Gaddi Bullah anakuwa na mgogoro
dhidi ya nafsi yake, chanzo cha mgogoro huu ni kuanza kubadilika kwa tabia ya
mke wake, na kusababisha Gaddi awaze sana na kujiuliza maswali mengi pasina
kupata majibu, kama mwandishi anavyoonesha akimtumia Gaddi Bullah; "Kwa
nini Nyambuja ananifanyia hivi? Kuna nini anachokosa kwangu? Yaani mambo yote
niliyomfanyia huu ndio wema anaonilipa kweli?" [Uk 62] Suluhisho la
mgogoro huu ni baada ya Gaddi Bullah kugundua kuwa mke wake alikuwa akiisaliti
ndoa wakaamua kuvunja ndoa yao kama mwandishi anavyosema; “ Wiki moja
baadaye Gaddi na Nyambuja waliachana kisheria….” [Uk 68]
Pia kuna mgogoro mwingine wa
Gaddi Bullah na nafsi yake, chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Gaddi Bullah
kusalitiwa na Dania, suluhisho la mgogoro huu wa nafsi ni Gaddi kuamua kutoweka
na kwenda kuishi Pemba ili kuwa mbali na Dania katika maisha yake yote. kama
mwandishi anavyosema akimtumia Bi. Hanuna; "Gaddi Bullah amefanya yote
hayo ili awe mbali kabisa na huyo rafiki yako na wote mnayehusiana nae."
[Uk 31]
Dania na nafsi yake
Dania na nafsi yake
Chanzo cha mgogoro huu ni baada
ya Dania kusalitiwa na Jerry mpaka Dania akataka kujiua kama mwandishi
anavyosema; “…Sasa hili lilkuwa ni pigo
la mwisho na Dania alivurugikiwa kabisa….alijaribu kujiua…” [Uk 87]
Suluhisho la mgogoro huu ni Dania kuanza uhusiano wa kimapenzi na Gaddi Bullah.
Pia mgogoro mwingine wa Dania na
nafsi yake unajitokeza baada ya Dania kufadhiliwa ini na hatimaye kupona akawa
na mgogoro wa nafsi wa kutaka kujua ni nani hasa mfadhili wake, kama mwandishi
anavyosema; "Ila sasa akili yake ikawa inajiuliza swali moja kila siku.
Mfadhili wake ni nani?" [Uk 139]
Suluhisho la mgogo huu ni hatua
ya Dokta Virani kuamua kumweleza Dania kuwa mfadhili wake ni Bullah. Kama
mwandishi anavyosema; "Gaddi Bullah ndiye mfadhili wako Dania..."
[Uk 140]
Nunu na nafsi yake
Chanzo cha mgogoro huu ni hatua
ya Dania kumsaliti Gaddi Bullah na Gaddi Bullah anaenda nyumbani kwa Nunu
anapata mgogoro wa nafsi juu ya nini atakachomweleza Gaddi, kama mwandishi
anavyosema akimtumia muhusika Nunu; "Mungu wangu! Nitamueleza nini
Gaddi leo? Nitaanzaje? Hivi kwanini Dania ananiweka kwenye mtihani namna hii
lakini?[Uk. 123]
Dokta Virani na nafsi yake
Chanzo cha mgogoro huu ni kukaa
na siri moyoni mwake ambayo walikubaliana na Gaddi Bullah kuwa asimwambie mtu
kuwa yeye ndiye mfadhili wa Dania, Suluhisho la mgogoro huu ni Dokta Virani
kuamua kuitoa hiyo siri, kama anavyosema: "Samahani sana
Gaddi...imenibidi nifanye hivyo...nadhani Dania alipaswa ajue kuwa ni wewe
ndiye uliyejitolea ini lako ili kuokoa maisha yake!" [Uk.144]
Mgogoro kati ya mtu na mtu
Gaddi Bullah na Nyambuja
Gaddi Bullah anakuwa na mgogoro
na Nyambuja ambaye ni mke wake, chanzo cha mgogoro huu ni hatua ya Nyambuja
kubadilika kitabia kama vile kuanza kuchelewa kurudi nyumbani, majibu ya hovyo
na hatimaye kugundua kuwa alikuwa akiisaliti ndoa yao. Suluhisho la mgogoro
Gaddi na Nyambuja wanamua kuvunja ndoa yao kama mwandishi anavyosema; “ Wiki
moja baadaye Gaddi na Nyambuja waliachana kisheria….” [Uk. 68]
Gaddi Bullah na Dania
Gaddi Bullah anakuwa na mgogoro
na Dania, chanzo cha mgogoro huu ni Dania kumkuta Gaddi Bullah akiwa amekaa na
kujitau ofisini kwake na pia Gaddi kupewa cheo cha Dania, na kupelekea Dania
kutokuwa mttifu kwa Gaddi na kuchelewesha kuandika ripoti jambo linalopelekea
Gaddi kumwandikia barua kali ya onyo. Suluhisho la mgogoro huu nia hatua ya
Gaddi kuamua kuichoma moto barua ya onyo na kumaliza tofauti zao kama mwandishi
anavyosema; "...Hilo suala limeisha kama jinsi hizi barua zinavyomalizwa
na huu moto! Tusahau kama lilitokea...tufanye kazi!" [Uk 94]
Mgogoro kati ya Gaddi
Bullah na Jerry
Gaddi Bullah na Jerry wanajikuta
wakiingia katika mgogoro, chanzo cha mgogoro huu ni Jerry kuingilia penzi la
Gaddi Bullah na Dania na kufikia hatua ya kupigana kama mwandishi anavyosema; "Jerry
alimtandika ngumi nzito ya taya....Gaddi Bullah alighadhibika. Alimsukuma Dania
pembeni na kumkabili adui yake..." [Uk. 121] Suluhisho la mgogoro huu
ni Gaddi Bullah kuamua kuondoka na kuachana na Dania. Rejea ukurasa wa 121-123.
Mgogoro kati ya Bi. Hanuna na
Dania
Chanzo cha mgogoro huu ni Dania
kumsaliti Gaddi Bullah na pia Dania kushirikiana na Jerry kumuweka rumande kama
mwandishi anavyosema;"Hapo Jerry alikuja juu. Alipiga simu polisi na
muda si mrefu Bi. Hanuna alikamatwa na kuwekwa rumande kwa kosa la
shambulizi." [Uk. 127]
Suluhisho la mgogoro huu ni Gaddi
Bullah kumuomba Bi. Hanuna amsamehe Dania kama mwandishi anavyosema akimtumia
muhusika Gaddi Bullah; "Nakuomba...usimchukie Da...Dania
dada...Usimchukie kabisa...si kosa lake." Bi. Hanuna naye anajibu kwa
kusema; "Oh! Gaddi...sasa hata nikimchukia itabadilisha nini..." [Uk.
146]
Mgogoro kati ya Bi. Hanuna
na Nunu
Chanzo cha mgogoro huu ni Bi.
hanuna kukataa katakata kumwambia Nunu mahali alipo Gaddi Bullah, kama
mwandhishi anavyosema akimtumia Bi. Hanuna; "Na kaniapiza kuwa nisithubutu
hata siku moja kuwapeleka au kuwatajia mahala alipo...kwa sababu siwezi kuvunja
kiapo changu na kumsaliti mdogo wangu pekee kwa ajili ya mahayawani kama
nyinyi!" [Uk 31-32]
Sulihisho la mgogoro huu ni Nunu
kuamua kmchukua kwa nguvu [kumteka] Bi. Hanuna na kumpeleka Bi. Hanuna mahali
alipo Dania ili ajionee mwenyewe kwanini Dania anamuhitaji Gaddi Bullah. Rejea
Nunu anapomwambibia Bi. Hanuna; "Na hii ndio sababu pekee iliyonifanya
nikuchukue kwa nguvu na kukuleta hapa Bi. Hanuna...ili uje ujionee mwenyewe
hali hii." [Uk. 55]
Gaddi Bullah rafiki yake
Mgogoro mwingine unaojitokeza
katika riwaya hii ni mgogoro kati ya Gaddi Bullah na rafiki yake, chanzo cha
mgogoro huu ni hatua ya rafiki yake huyo kumsaliti Gaddi kwa mkewe. Rejea
mwandishi anaposema: "Baadaye aliamua kwenda kwa rafiki yake kumpasha
habari habari juu ya masahibu yake. na huko alipata mshituko mkubwa. Mke wake
mwenyewe ndiye aliyemfungulia mlango, tena akiwa khanga moja tu...ilhali rafiki
yake akiwa amejitawanya kwenye sofa akiwa kidari wazi na kaptura tu!"
[Uk. 66]
Suluhisho la mgogoro huu ni Gaddi
kuamua kuondoka kwa dharau na kuwaacha wasaliti wake kama mwandishi anavyosema;
"Alivuta funda kubwa la moshi kutoka kwenye ile sigara na kuwapulizia
moshi ule kwa dharau. Kisha aligeuka na kuondoka bila ya kusema neno lolote
zaidi!" [Uk. 68]
Mgogoro mwingine unaojitokeza ni
mgogoro kati ya kikundi kimoja na kikundi kingine cha watu. Mgogoro huo ni;
Mgogoro kati ya familia ya
Dania na familia ya Jerry.
Chanzo cha mgogoro huu ni Jerry
kushindwa kutokea katika harusi yake na Dania. Rejea Mama Mlole anapomwambia
Gaddi Bullah, "...Lakini Jerry hakupatikana. Ilikuwa kama vile Jerry
ameyeyuka ghafla kutoka kwenye uso wa dunia...Uhasama mkubwa ukazuka baina ya
familia zao." [Uk. 85]
Suluhisho la mgogoro huu ni Dania
anajenga chuki na wanaume wote duniani, anajaribu kujiua na pia anaanza tabia
ya ulevi wa kupindukia kama mwandishi anavyosema akimtumia muhuika Mama Mlole;
"Na matokeo yake akajenga chuki na dunia na wanaume wote hapa
duniani...Alianza kunywa pombe kali tena kwa wingi!" [Uk. 87]
UJUMBE / MAFUNZO
Ujumbe ni yale mafunzo ayapatayo
msoamji wa kazi ya fasihi, kwa maana hiyo basi kile ambacho msomaji wa kazi za
fasihi amejifunza kutoka na kusaoma kazi husika huo ndio ujumbe. Ujumbe
unaojitokeza katika riwaya hii ni;
1. Kikulacho kinguoni mwako.
Huu ni ujumbe ama funzo
tunalolipata baada ya kusoma riwaya hii, ujumbe huu tunaupata kupitia muhusika
Gaddi Bullah na rafiki yake, Bullah anasalitiwa na rafiki yake huyo kwa kuamua kuanza mahusiano ya kimapenzi
na mke na kupelekea Bullah kuvunja ndoa kisa rafiki yake, ujumbr huu tunaupata
kupitia muhusika Bullah anaposema, “Na
wewe! Nilidhani kuwa u rafiki yangu! Nilikuwa nakuletea matatizo yangu kumbe
ulikuwa ukinilamba kisogo?” [Uk 67]
2. Mapenzi ni kitovu cha uzembe kazini.
Huu pia ni ujumbe mwingine
unaojitokeza katika riwaya hii, mwandishi anawatumia wahusika Gaddi Bullah na
Dania ambao kutokana na matatizo yanayowasibu katika mapenzi tunawaona
wakiathirika kisaikolojia na hatimae kupungukiwa ufanisi wa kazi, kwa mfano
tunamwona Gaddi akipitisha malipo hewa kwa kukosa umakini na kusabibisha
kushushwa cheo alikadharika Dania nae mapenzi yanamfanya ajitumbukize katika.
ulevi uliokithiri na hivyo kusababisha kutokuwa makini ka0zini kama mwandishi
anavyosema kupitia muhusika Mama Mlole, "Na hapa ndipo utendaji wake
kazini ulipoathirika vibaya sana. Kazi zikawa haziendi kabisa." [Uk
88]
3. Ulevi wa kupindukia ni hatari kwa afya ya binadamu.
Ni ujumbe mwingine tunaoupata
katika riwaya hii. Ili kufikisha ujumbe huu mwandishi ame watumia wahusika
Dania ambaye kutokana na tabia yake ya ulevi wa pombe kali anajikuta akipata
ugonjwa wa ini kama mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika Dokta Virani
anaposema, “Ini lake la kulia
limeathirika kutokana na pombe kali alizokuwa akinywa, wakati wa mfadhaiko wake
uliotokana na madhila aliyofanyiwa na Jerry.” [Uk 105]
Lakini pia tunaona kuwa ulevi
uliokithiri wa uvutaji sigara unaofanya na Gaddi Bullah unamsababishia matatizo
ya mapafu na hatimaye anafariki kwa ugonjwa wa mapafu ambao unatokana na
uvutaji wa sigara uliokithiri.
4. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli.
Ni ujumbe unaojitokea pia katika
riwaya hii, mwandishi katika kufikisha ujumbe huu amewatumia wahusika Dania,
Bullah, Nunu na Boaz. Kwa mfano richa ya Dania kumfanyia unyama Gaddi Bullah
kwa kumsaliti lakini anakuja kumfaa wakati wa dhiki yaani wakati Dania anaumwa
kwa kumfadhili ini kama mwandishi anavyosema akimtumia muhusika Dokta Virani; "Samahani
sana Gaddi...imenibidi nifanye hivyo...nadhani Dania alipaswa ajue kuwa ni wewe
ndiye uliyejitolea ini lako ili kuokoa maisha yake!" [UK. 144]
Lakini pia mwandishi amemtumia
muhusika Nunu licha ya kumshauri Dania kwa nguvu zake zote asirudiane na Bullah
na kutosikilizwa lakini baadaye anakuja kuhangaika kumtafuta Bullah kwa ajili
ya Dania, lakini pia Dania alikuwa tayari kujitolea ini kwa ajili ya rafiki
yake Dania ila tatizo lilikuwa ni damu kama mwandishi anavyosema, “Nunu naye
alijitolea. Vipimo vilionesha kuwa maini yake yote yalikuwa safi na aliweza
kabisa kumtolea Dania ini moja, lakini damu yake ilikuwa haioni kabisa na ile
ya Dania." [Uk. 132]
Pia Boaz alishirikiana bega kwa
bega na Nunu kumtafuta Gaddi Bullah kwa kila hali yote haya yanatupa ujumbe
kuwa rafiki wa kweli ni yule akufaaye kwa dhiki na raha.
5. Majuto ni mjukuu.
Ujumbe huu unajitokeza pia katika
riwaya hii, mwandishi anamtumia muhusika Dania ambaye kutokana na unyama
aliomfanyia Gaddi Bullah na kutomsikiliza rafiki yake Nunu wakati akimhauri
kuhusiana na Jerry baadaye anakuja kujuta kutokana na maswahibu yaliyomkuta
kama mwandishi anavyosema, “Nilimuona
Jerry ni bora kuliko Gaddi nawe ukaniambia kuwa nilikuwa najidangajnya,
sikukusikia. Sasa nimedhihirisha mwenyewe...hii ndio ile ya mkaidi hafaidi
mpaka siku ya Iddi. Najuta..." [Uk 135]
6. Elimu ni ufunguo wa maisha.
Mwandishi anatupa ujumbe mwingine
kuwa, ili mtu aweze kufanikiwa hana budi kushikiria na kuizingatia elimu kwani
elimu ni ufunguo wa maisha, ujumbe huu katika riwaya hii unajitokeza kwa
muhusika Gaddi Bullah ambaye kutokana na elimu aliyokuwa nayo anapata kazi
nzuri na kuwa na maisha mazuri, kama mwandishi anavyosema; “….kampuni ile
kubwa ya mawasiliano nchini ambayo ilimwajiri mara baada ya kumaliza masomo
yake ya elimu ya juu miaka mitano iliyopita.” [Uk 57]
Ujimbe huu pia unajitokeza
mwandishi anapomtumia muhusika Mama Mlole anaposema; “ Mke anamtaka, lakini
na masomo pia anayataka. Masomo ambayo yangemfungulia milango mipya ya
maendeleo kielimu na kiuchumi.” [Uk 84]
7. Mpende akupendaye
asiyekupenda achana nae.
Hussein Tuwa katika riwaya hii
anaipa ujumbe jamii yake kuwa penda pale unapopendwa na si kumng'ang'ania tu
mtu kwa kuwa moyo wako unataka tu kuwa naye, ujumbe huu tunaupata kupitia kwa
muhusika Dania ambaye licha ya kufanyiwa vituko vya kila aina na Jerry yeye
bado alimuona kuwa ni mtu wa maana na kuamua kumsaliti Gaddi Bullah mwanaume
aliyempenda kwa dhati, lakini baadaye anakuja kung'amua kuwa Jerry hakuwa na
mapenzi ya dhati, ujumbe huu unajidhihirisha Dania anaposema; “Nilimuona
Jerry ni bora kuliko Gaddi nawe ukaniambia kuwa nilikuwa najidangajnya,
sikukusikia. Sasa nimedhihirisha mwenyewe...hii ndio ile ya mkaidi hafaidi
mpaka siku ya Iddi. Najuta..." [Uk 135]
8. Uongozi bora ni chachu ya
maendeleo na maelewano sehemu za kazi.
Hili ni funzo tunalolipata mara
baada ya kusoma riwaya hii, ili kuleta ufanisi wa kazi na maendelea ni wajibu
wa viongozi kubadilika na siyo kuwasubiri wanaowaongoza wakosee ndipo wawape
onyo kali au kuwafukuza, kama mwandishi anavyotuambia akimtumia muhusika Mama
Mlole;"Utawala wa kusubiri mfanyakzi akosee ili umuadhibu siku hizi
umepitwa na wakati, Gaddi! Utawala wa sasa ni wa kumjenga mfanyakazi kitabia na
kimaadili ili asiingie kwenye makosa yatakayosababisha kuchukuliwa hatua za
kinidhamu. Viongozi tunatakiwa tubadilike sasa, Gaddi!" [Uk 93]
Ø
Matumizi ya Lugha.
è
Misemo / Nahau
1.
Jibu lile lilimkata maini. [Uk 36]
2.
Pale walikuwa wamegonga mwamba. [Uk 33]
3.
Anakuhitaji wewe, radhi zako na kumtia moyo. [Uk. 35]
4.
Dania anamuhitaji.. ni suala la kufa na kupona. [Uk.
26]
·
Methali
ü
Ukiyastaajabu
ya Musa utayaona ya Firauni. [Uk. 27]
ü
Hakuna
marefu yasiyo na ncha. [Uk.117]
ü
Ni bora
nusu shari kuliko shari kamili. [Uk. 127]
ü
Mkaidi
hafaidi mpaka siku ya Idi. [Uk.135]
Tamathari za semi
·
Takriri
Hii ni hali ya
kurudiarudia maneno, neon, silabi au sauti zinazolingana katika kazi ya fasihi
ili kusisitiza au kutia mkazo jambo fulani. Mfano wa takriri zinazojitokeza
katika riwaya hii ni:
Jjambo
lililowafanya ndugu wa mumewe kumfukuza kama mbwa kutoka kwenye nyumba ya
marehemu mumewe. [Uk. 60]
Nimesema
sitaki! Sitaki. Sitaki. Sitaki!
Ø
·
Tashibiha.
Hii ni
tamathari ambayo hulinganisha vitu kwa kutumia viunganishi kama, mfano wa, sawa
na, mithili ya, kama vile. N.k. baadhi ya tashibiha zinazojitokeza katika
riwaya hii ni:
ü
Midomo ilikuwa ikimtetemeka kama mgonjwa wa
malaria kali. [Uk 18]
ü
Sasa hapo ilikuwa kama amechokoza nyuki. [Uk 30]
·
Tashititi.
Hii ni aina ya
tamathari ya semi ambayo mtu huuliza swali huku jibu lake akilifahamu, mfano wa
tashititi zinazojitokea katika riwaya hii ni:
·
Tashihisi.
Tamathari hii
hufanya vitu ambavyo havina uhai wa kutenda jambo kama binadamu vitende au
vifanye jambo hilo kama binadamu, mfano wa tashihisi zinazojitokeza katika
riwaya hii ni:
·
Tanakali
sauti [Onomotopeia] na Tanakali lafudhi.
Tanakali sauti [Onomotopeia]
Hii ni aina ya
tamathari ambayo sauti ya kitu fulani huigwa ili kwa lengo la kuburudisha au
kuipa dhamira uzito falani. Mfano wa tanakali sauti zilizotumika katika riwaya
hii ni:
Tanakali lafudhi.
·
Tafsida
Hii ni aina ya
tamathari za semi ambazo hutumika ili kupunguza ukali wa maneno, mfano wa
tasfida zilizotumika katika riwaya hii ni:
·
Sitiari
·
Mdokezo
Matumizi ya Taswira.
5.
Matumizi ya ucheshi.
Ø
Matumizi ya Lugha.
MANDHARI
Kwa kiasi kikubwa riwaya hii
imetumia mandhari ya Dar-es-salaam, ambapo ndipo panatajwa kuwa ni makao
makuu ya Kampuni ya mawasiliano ambayo Gaddi Bullah na Dania ndipo walipkuwa
wakifanyia kazi. Rejea mwandishi anaposema; " Ni mwezi mmoja sasa
ulikuwa umepita tangu ahamishwe kwenye ofisi hii iliyopo jijini Dar-es-salaam,
ambayo ndiyo makao makuu ya kampuni ile kubwa ya mawasiliano nchini." [Uk.
57]
Katika Jiji hili la Dar-es-salaam
pia kuna mandhari nyingine ndogondogo zinajitokeza kama vile Mbezi,
Oysterbay, Magomeni, Sinza kwa Remmy, Tabata. n.k
Mbezi, mwandishi
anaeleza kuwa ndipo mahali Gaddi Bullah alipojenga nyumba yake ya kifahari na
kuiuza baada ya kupatwa na matatizo ya kusalitiwa na mpenzi wake. Rejea
mwandishi anaposema; "Alikuwa na miradi iliyomuingizia pesa ya kutosha,
ikiwemo nyumba nzuri na ya kifahari maeneo ya mbezi..." [Uk. 58]
Oysterbay, ni
mandahri inayotajwa katika riwaya hii ambapo ndipo wanapoishi wa zazi wa Dania
yaani Mzee Theobald na mkewe katika nyumba ya kifahari. [Rejea ukurasa 47-49]
Katika riwaya hii maneo ya Mbezi
na Oysterbay ni mandhari ambayo mwandishi ameyatumia ili kuonyesha
matabaka katika jamii yake kwa kuonesha sehemu na namna ambavyo watu wenye
kipato cha juu wanaishi, na hivyo mandhari haya yote mwandishi ameyatumia
kufikisha dhamira ya matabaka katika jamii.
Vilevile, Magomeni kumetajwa kama
sehemu aliyokuwa akiishi Bi. Hanuna katika nyumba yao ya urithi, lakini pia
Tabata imetumika kama sehemu anayoishi Dania katika nyumba aliyojengewa na baba
yake, Sinza kwa Remmy ndipo alipokuwa anaishi Jerry katika nyumba ya kupanga.
Arusha pia ni mandhari nyingine
inayojotekeza katika riwaya hii, Arusha ndipo alipokuwa akifanyia kazi Gaddi
Bullah katika kampuni ya mawasiliano kabla ya kuamishiwa Dar-es-salaam, pia
Arusha na huko ndipo Gaddi Bullah alipokutana na Nyambuja na kufunga ndoa kama
mwandishi anavyosema; "...Pale mjini Arusha...ndipo Gaddi Bullah
alipokutana na binti yule aliyekuwa na sura ya kuvutia, mwili wa kutamanisha na
haiba iliyovuta hisia za mapenzi kwa kila rijali..." [Uk. 59]
Sehemu nyingine zinazotajwa
katika riwaya hii ni, Mkuranga anakohamia Bi. Hanuna baada ya kuhama
kule Magomeni kama mwandhishi anavyosema akimtumia muhusika Boaz; "Bi.
Hanuna alijengewa nyumba nyingine na mdogo wake huko Mkuranga..."[Uk. 20]
Lakini pia mandhari ka Pemba imetumika
pia ambako ndipo Gaddi Bullah alipokimbilia kujificha huko na ndipo
anapofia.[Rejea ukurasa wa 140-148]
Mwandishi pia ametumia Marekani
ambako Jerry anaenda kusoma baada ya kupata ufadhili wa shirika fulani, lakini
pia inatajwa Afrika ya kusini ambako Dania alienda kutibiwa. [Uk. 83 na 88]
Mandhari nyine zilizotumika ni, nyumbani,
ofisini, mgahawani, hospitalini. n.k
Nyumbani tukianzia na kule
Arusha, mwandishi anaonyesha matatizo ya kifamilia nyumbani hususani katika
ndoa kama tunavyoona kwa Nyambuja na mumewe. pia nyumbani kwa rafiki yake Gaddi
Bullah tunaona Gaddi akimfumania mke wake na rafiki yake. [Rejea Uk. 60-68]
Nyumbani kwa Dania,
tunaona akifumaniwa na Gaddi Bullah, na vilevile kupigana kwa Gaddi na Jerry.
0fisini, pia
imetumika kama mandhari katika riwaya hii, mwandishi ametumia mandhari hii
kuonesha wizi unaofanyika katika ofisi mbalimbali, rejea kupitishwa ka vocha ya
malipo hewa huko ofisi za Arusha, migogoro kazini kama inavyojitokeza kwa Dania
na Gaddi Bullah, lakini pia suala la uongozi bora kama tunavyoweza kuliona kwa
Mama Mlole. [Rejea ukurasa wa 68, 71-74 na 93.]
MUUNDO. [Plot]
Muundo ni namna visa na matukio
hufuatana kwa mtiririko. Hivyo tunaweza kusema pia muundo ni mfuatano wa
masimulizi katika kazi ya fasihi. Katika riwaya hii mwandishi ametumia muundo
changamani yaani visa na matukio katika riwaya hii ameanza kati, mwanzo halafu
mwisho.
Kwamfano ameanza kati, ambapo
tunamwona Nunu na Boaz wakiwa katika harakati za kumtafuta Gaddi Bullah huku
msomaji akiwa bado kung'amua ni sababu gani ambayo inawafanya akina Nunu
kumsaka Gaddi Bullah? [Angalia kuanzia ukurasa wa 1-56]
Baada ya kuanza na kisa cha
katitikati, katika sura ya pili hadi ya tisa mwandishi anaanza kuelezea kisa
cha mwanzo na kurudi tena katikati, hapa tunaelezwa habari za Gaddi Bullah na
ndipo sababu za Gaddi kutafutwa kinaelezwa. Halafu anamalizia na kisa cha
mwisho kujitolea ini kwa Gaddi na kufariki kwake.
Pia katika kuyapanga matukio yake
katika riwaya hii, mwandishi ameigawa kazi yake katika sura/sehemu ambazo
amezipa namba kuanzia sura/sehemu ya kwanza [1]
hadi kumi [10].
Sura ya 1. Nunu na
Boazi wakimtafuta Gaddi Bullah bila mafanikio na hatimaye kumteka dada
yake [Bi. Hanuna] na kumpeleka hadi
nyumbani kwa akina Dania. [Uk. 1-56]
Sura ya 2 hadi ya 8.
Mwandishi anaanza mwanzo, hapa tunaona kukutana kwa Gaddi Bullah na Nyambuja na
kuoana, Gaddi kusalitiwa na huyo mke wake, kuvunja ndoa yake, Kuamishiwa
Dar-es-salaam, kukutana na Dania na kuanza uhusiano wa kimapenzi na kusalitiwa
na Dania na hatimaye Gaddi Bullah kutoweka. [Uk 57-128]
Sura ya 9 hadi ya 10, Dania
anaanza kuumwa ini, Dania anakimbiwa na Jerry kwa mara ya pili, Dania anaandika
barua akimuomba Nunu aipeleke kwa Gaddi Bullah, Gaddi anajitolea ini kumfadhili
Dania, Gaddi anaanza kuumwa, Dokta Virani anatoa siri juu ya mfadhiri wa Dania,
Gaddi anafariki dunia na ndio mwisho wa riyawa hii. [Uk 129-148]
MTINDO [Setting]
Mtindo ni jinsi msanii
anavyotumia ufundi, umahiri na hisia zake katika kutenda au kueleza jambo
fulani. katika riyawa hii kuna mitindo mbalimbali ambayo mwandishi ameitumia ni
kama vile;
Vipengele vya mtindo
vilivyotumika katika riwaya hii.
Monolojia [Masimulizi]
Kwa kiasi kikubwa mwandishi
ametumia lugha ya masimulizi katika kuelezea visa/matukio, sifa na tabia za
wahusika katika kuikamilisha kazi yake.
Diolojia [Majibizano]
Mwandishi katika kazi yake hii
ametumia pia lugha ya majibizano, mfano;
Nunu:
"Aaah Bi. Hanuna, tusamehe...tusaidie tafadhali...ni muhimu sana
kwangu
kuonana na Gaddi..."
Bi. Hanuna. "Sio juu
yangu kutoa msamaha juu ya hilo Nunu! au unataka kuniomba
nimsaliti mdogo wangu?
Eeenh? [Uk. 32]
Matumizi ya Barua ndani ya
riwaya.
Rejea barua aliyoandika Nyambuja
kwa Gaddi anaposema:
"Kwako Gaddi,
Samahani sana kwa yote yaliyotokea, na pia
kwa huu uamuzi nilioamua
kuchukua...Gaddi nimependana na mtu mwingine na nimekuwa nikisaliti ndoa
yetu kwa muda mrefu....Nakutakia maisha
mema katika siku zako zilizobaki ukiwa mbali nami.
Kwa heri,
Aliyekupenda kwa
dhati,
Nyambuja." [Uk.65]
Matumizi ya nafsi.
Mwandishi ametumia nafsi zote
tatu, nafsi ya kwanza, pili na tatu.
JINA NA JALADA LA KITABU
Tukianza na jina la kitabu, jina
la kitabu ni Mfadhili, kwa mujibu wa Kamusi ya kiswahili Sanifu [1981]
nenoMfadhili limefasiliwa kuwa ni, "Mtu
anayemfanyia wema mkubwa mtu mwingine" Kwa maana hiyo basi, kwa kiasi
kikubwa jina la kitabu linasadifu yale yanayozungumzwa katika riwaya hii. Kwa
mfano tunaona baada ya Dania kuanza kuumwa na Daktari kuthibitisha kuwa ana
tatizo la ini juhudi za kumtafuta mfadhili
atakayejitolea ini lake lipandikizwe kwa Dania zinafanyika kama mwandishi
anavyosema; "Hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuanza kutangaza kwenye
vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuomba wasamaria wema watakaopenda
kujitolea sehemu ya ini kumfadhili mgonjwa..." [Uk. 134]
Baada ya Juhudi zote kufanyika za
kumtafuta mfadhili kufanyika hatimaye
Mwandishi anaonesha kupatikana kwa mfadhili
huyo, Mwandishi analithibitisha hili anaposema; "Nina taarifa njema
muhimu kwetu sote...hatimaye mfadhili amepatikana!" [Uk 137]
Mwandhishi anamuonesha Gaddi
Bullah kuwa ndiye aliyejitolea ini kumfadhili Dania na hivyo kuokoa uhai wa
Dania, kama mwandishi anavyothibitisha akimtumia muhusika Dokta Virani
anapomwambia Dania; "Gaddi Bullah ndiye mfadhiri wako Dania..."
[Uk 140]
Vilevile jina la kitabu
linasadifu yale yanayozungumzwa katika riwaya kwa sababu tunamwona Dania baada
ya kupona anakuwa akijiuliza kila mara ni nani mfadhili wake? swali ambalo
limekuwa likiusumbua moyo wa Dania, kama mwandishi anavyosema; "Ila
sasa akili yake ikawa inajiuliza swali moja kila siku. Mfadhili wake ni
nani?" [Uk 139]
Pia swala la ufadhili
linajitokeza kwa Jerry amabaye anapata ufadhili wa kwenda kusoma Marekani, kama
Mwandhishi anavyosema; "...Alikuwa
amepata ufadhili wa shirika moja la kimataifa ambalo huwa linapokea maombi
mengi sana ya ufadhili kuliko uwezo uliopo..." [Uk 83]
Pamoja na hayo kuna ufadhili
mwingine unaofanywa na Dokta Virani kwa Bi. Hanuna, baada ya Bi. Hanuna
kukamatwa na polisi na kuwekwa rumande ni Dokta Virani ndiye anayemfadhili kwa
kumtoa kwa dhamana kama mwandhishi anavyosema; "Dokta Virani alipopata
taarifa alihangaika huku na huko kumpatia dhamana, lakini ilishindikana."
Mwandishi anaendelea kusema; "Siku iliyofuata, Dokta Vilani alifanikiwa
kumtoa kwa dhamana." [Uk 127]
Ufadhili unaofanywa na Mama Mlole
kwa Dania na Gaddi Bullah, licha ya kuwa Dania na Gaddi Bullah kuwa na matatizo
ambayo yangeweza kuwafukuzisha kazi, Mama Mlole anafanya juhudi kubwa
kushawishi uongozi wa kampuni ili waweze kuendelea na kazi kama mwandishi
anavyosema akimtumia muhusika Mama Mlole anaposema; "Ndio...na kwa
hatua aliyofikia, ilibidi aachishwe kazi, lakini kwa kumsaidia, nikiwa kama
Afisa Utumishi wa kampuni, nilipendekeza apewe likizo....nilifanya kazi ya
ziada kuushawishi uongo wa kampuni juu ya hili, jinsi nilivyofanya kazi ya
ziada kulishawishi lile jopo la wakaguzi kule Arusha kukupa wewe nafasi
nyingine...badala ya kukufaukuza kazi..."
[Uk 88]
Hivyo basi kwa ushahidi huo
tunaweza kusema jina la kitabu linasadifu yale yote yanayozungumzwa katika
riwaya hii.
FALSAFA YA MWANDISHI.
Mwandishi anaami kuwa katika
mapenzi kuna pande mbili, pande hizo ni utamu na uchungu au tunaweza kusema
raha na karaha, mara nyingi mapenzi yanapoanza huwa moto moto na yenye furaha
kubwa na upendo lakini pindi yanapoanza kupatwa na majaribu ya aina mbalimbali
mapenzi hayo hubadilika na kuwa karaha [chungu].
MTAZAMO WA MWANDISHI.
Mwandishi ana mtazamo wa
kimapinduzi kwa maana anaihitaji jamii yake kubadilika, ameonesha matatizo
mbalimbali katika jamii yake kama vile usaliti, ulevi wa kupindukia, unafiki, uongozi mbaya, mapenzi ya ulaghai.
n.k. ambayo anaitaka jamii yake kubadilika na kuachana nayo.
TATHIMINI
Baada ya kusoma na kuhikiki
riwaya hii, kama Mhakiki, inanilazimu kufanya tathimini japo kwa ufupi, katika
tathimini nitaelezea mwandishi amefaulu katika mambo gani na wap kuna upungufu
katika kazi yake ili iwe msaada kwake na kwa Waandishi wengine mara wasomapo
tahikiki hii. Tukianza na:
KUFAULU KWA MWANDISHI.
Tunapoangalia kufaulu kwa
mwandishi uwa tunaangalia kufaulu kwa mwandishi katika vipengele vya fani na
maudhui, kifani mwandishi amefaulu katika vipengele vifuatavyo, kwanza amefaulu
kutumia lugha ambayo ni rahisi na inayoeleweka na watu wengi na hivyo kufanya
wasomaji wa riwaya hii kuielewa vizuri na kupata dhamira na ujumbe kwa urahisi
kabisa.
Pia mwandishi amefaulu kuwajenga
wahusika wake vizuri na kuwatumia wahusika hao katika kufikisha dhamira na
ujumbe aliokusudia kwa hadhira yake.
Kwa upande wa mandhari mwandishi
pia ameweza amefaulu kutumia mandhari halisi ambazo kwa namna moja ama nyingine
mandhari hayo yamesaidia kujenga dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika
riwaya hii.
Mwandishi amefaulu katika
kuyapanga matukio na visa katika mtindo unaomvutia msomaji kuendelea kukisoma
kitabu bila kuchoka kwa namna ambavyo matukio yamesukwa na kupangwa vizuri.
Jina la kitabu ni kipengele
kingine ambacho mwandishi amefaulu kwani jina la kitabu limeweza kusadifu yale
yote yanayozungumzwa katika riwaya hii.
Katika kipengele cha maudhui
mwandishi amefaulu kuonesha matatizo mbalimbali yanayoisibu jamii yake na
kuenesha njia namna ya kuyamaliza matatizo hayo, matatizo ambayo mwandishi
amejaribu kuyaibua ni kama vile usaliti, ulevi, unafiki. n.k. Vilevile tunaona
mwandishi amefaulu kuonesha namna migogoro inayoweza kutokea na jinsi migogoro
hiyo inavyoweza kutatuliwa kwa kutuo suluhisho kwa mgogo husika.
MAPUNGUFU
Kitu chochote kizuri huwa
hakikosi kasoro au mapungufu, hivyo hata riwaya hii pamoja na uzuri wake lakini
ina mapungufu yake pia, tukianza na mapungufu hayo, kwa mafano mwandishi
ameshindwa kuonesha hatima ya Nyambuja na rafiki yake Bullah walivyofumaniwa
kama waliamua kuendelea na uhusiano au ulikoma palepale na hivyo kupelekea
jamii kuona kuwa wakati mwingine usaliti ni kitu kizuri katika jamii maana
ingekuwa vizuri kama angeonesha madhara au matatizo ya usaliti huo kwao.
Pili, mwandishi pia ameshindwa
kuonesha je! Baada ya Jerry kutoweka kwa mara ya pili na Dania kupona na Gaddi
kufariki dunia je! alirejea tena na kama
hakurejea je! huko alikokwenda yuko salama, kwa hiyo hapa pia mwandishi
alitakiwa kuonesha madhara ambayo Jerry anakumbana nayo ili watu wenye tabia
kama ya Jerry wajifunze kuwa tabia hiyo siyo nzuri hata kidogo.
MAONI YA MHAKIKI
Hii ni riwaya ya aina yake
inayohusu mapenzi na masahibu yanayowapata wapenzi, imejaribu kuelezea kuelezea
matatizo mbalimbali kwa wanandoa na hata matatizo kwa mapenzi ambao hawajaingia kwenye ndoa, ni
riwaya nzuri ambayo inafaa kusomwa na mtu yoyote yule na ikaeleweka vema.
Matukio na visa vyake vimepangiliwa vizuri kiasi kwamba unapoanza kusoma riwaya
hii hutaiweka chini au kuruka kurasa ni riwaya unayotakiwa kuisoma kama
hujaisoma.
Mwandishi ni Mwalimu Shule ya Sekondari Mwanzi-Manyoni (Singida) anapatikana kwa namba zifuatazo:
Mawasiliano: 0715 33 55 58 (whatsapp)
0755 44 06 99
Nifollow instagram: fullraha17
Facebook: Furaha Venance
Nifollow instagram: fullraha17
Facebook: Furaha Venance