Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Sunday, February 22, 2015

RAIA WA KENYA NA RWANDA RUKSA KUINGIA UGANDA BILA VIZA WALA KIBALI CHA KUFANYIA KAZI. TANZANIA NA BURUNDI WAPIGWA BAN



Serikali ya Uganda imeondoa ada ya kibali cha kufanyia kazi nchini humo pamoja na mahitaji ya viza miongoni mwa raia wa Kenya na Rwanda wanaoingia na kutoka taifa hilo. Uamuzi huo uko sambamba na uidhinishaji wa mtindo wa uhuru wa kutembea chini ya Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Soko la pamoja ambayo iliafikiwa mwaka 2009 na marais Museveni wa Uganda,Mwai Kibaki wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania,Paul Kagame wa Rwanda na Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Kamishna wa udhibiti wa uhamiaji katika wizara ya maswala ya ndani bwana Anthony Namara ameliambia gazeti la Monitor jumamosi kwamba raia wa mataifa hayo mawili pia hawatahitajika kutoa viza ama vibali vyovyote vya usafiri ili kuingia Uganda isipokuwa vitambulisho vyao pekee.
Amesema kuwa Kenya na Rwanda tayari zinaidhinisha mpango huo wa uhuru wa kutembea ambao unalenga kuimarisha utalii katika eneo hili mbali na kuruhusu usafiri wa wataalam katika mataifa haya matatu.
Tanzania na Burundi hayamo katika mpango huu unaoshirikisha vibali vya kufanya kazi na mahitaji ya Viza. 
SOURCE: BBC

MBOWE AICHANA TUME YA UCHAGUZI, HAYA NDO MADUDU YA NEC


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameibua tuhuma nzito dhidi ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akisema kuwa wamekaidi ushauri wa kitaalam uliowazuia wasitumie mfumo mpya wa Biometric Voter Registration (BVR) katika uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Mbowe amedai kuwa baada ya kuona zoezi la kuandikisha wapiga kura haliendi kama ilivyotakiwa, NEC walimtafuta mshauri mwelekezi aitwae Darrell Geusz, mtaalam wa masuala ya BVR kutoka Marekani ambaye baada ya kufanyia utafiti ‘hali’ ya Tanzania kuhusu mfumo huo mpya, aliwaambia wakilazimisha wanaweza kusababisha machafuko ya kisiasa nchini.
Kwa mujibu wa Mbowe, mtaalam huyo katika ripoti yake aliyoitoa mwezi Januari mwaka huu, aliiambia NEC kuwa kwa sasa Tanzania haiwezi kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa BVR kwa sababu ya ukosefu wa fedha, vifaa, utaalam na muda kwani mfumo huo ili uweze kufanya kazi inayotakiwa unahitaji maandalizi ya takriban mwaka mmoja.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ameyasema hayo jijini Mbeya wakati alipohutubia matukio mawili tofauti, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika mikoa ya Kanda (ya CHADEMA) ya Nyanda za Juu Kusini yenye mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma na Rukwa.
Mapema asubuhi Mwenyekiti Mbowe alihutubia wakati akifungua kikao cha Baraza la Uongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kisha baadae jioni akahutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Dk. Slaa mjini Mbeya.
“Mshauri huyo mwelekezi ambaye ni mtaalam wa masuala ya BVR kutoka Marekani, amewahi kuisaidia nchi ya Bangladesh ambako waliandikisha wapiga kura milioni 80, aliwaambia NEC kuwa Tanzania hatuwezi kuendesha hili zoezi kwa sasa, hatuna vifaa, hatuna wataalam, hakuna muda wa kutosha, hatuna wataalam, hatuna maandalizi, akawatahadharisha wakilazimisha wanaweza kusababisha machafuko.
“Lakini katika hali ambayo haijulikani, wakiendeleza ukaidi kwa ajili ya kutaka kuibeba CCM, NEC inaonekana kutaka kuendesha zoezi hili bila kuzingatia ushauri wowote wa kitaalam wala kushirikisha wadau ambao ni vyama vya siasa wala haitaki kutoa taarifa za kutosha kwa wananchi ambao ndiyo wapiga kura wenyewe.
“NEC imekuwa ikiendesha suala hili kwa usiri usiri sana, taarifa zao wanapoamua kutoa zimekuwa za kusua sua sana, kwa kushtukiza. Tumekuwa tukidai ushirikishwaji wa kina wa shughuli na mfumo huu bila mafanikio. Tumeomba sana kupata nyaraka ili tuelewe, lakini hawataki. Wanafanya siri kubwa.
“Sasa nasi kwa sababu tunazo njia mbalimbali za kupata taarifa, tumezipata nyaraka ambazo hawataki wadau kwa maana ya vyama vya siasa tuzione.
Kwanza tumepata nyaraka ambayo inaonesha kuwa wakati walikuwa wanasema hawana kitu cha kutupatia ili tuelewe mfumo huu wa BVR, wao labda na CCM yao tangu 2013 walikuwa tayari wanajua kitakachofanyika.
“Lakini pia tumefanikiwa kupata nyaraka nyingine hii hapa. Hawa jamaa wa NEC baada ya kuzidiwa wakaamua kutafuta mshauri mtaalam kutoka Marekani ambaye anasifika duniani, yaani katika masuala ya BVR ni authority, ameandika ripoti yake yenye kurasa 16, amewapatia hadi ushauri wa tahadhari ya madhara ya kiusalama jamaa wa NEC na Serikali ya CCM hawataki kusikia,” amesema Mbowe.
Mbowe ameongeza kusema kuwa wakati mshauri huyo mtaalam wa BVR akiwatahadharisha NEC kuhusu muda, tume imeendelea kusema kuwa zoezi hilo litafanyika na kufanikiwa kwa kipindi cha ndani ya miezi miwili, jambo ambalo Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kuwa serikali inacheza na ‘roho ya amani katika nchi’.
Alisema kuwa mazingira yanayoendelea nchini Tanzania katika suala la mchakato wa hatua mbalimbali za uchaguzi mkuu wa mwaka huu, yanatengeneza hali ya kutokuaminiana miongoni mwa wadau, akisema kuwa hali hii husababisha uchakachuaji na katika nchi zingine imesababisha machafuko ya kisiasa.
NEC na ubabaishaji katika ratiba
Mbowe amesema kuwa tangu mwaka jana NEC imekuwa ikitoa taarifa za kukanganya kuhusu ratiba kamili ya kuanza kuandikisha upya wapiga kura nchi nzima, ambapo iliwahi kusema shughuli hiyo ingeanza Septemba 2014, baadae ikaahirisha hadi Desemba, lakini pia haukufanyika, kisha baadae ikatoa ratiba ya kuanza kazi hiyo Februari 16 mwaka huu, ikianza na mikoa minne ya Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.
Kiongozi huyo amesema kuwa baada ya vyama vya siasa kuibana NEC juu ya ratiba na maandalizi muhimu kuhusu shughuli hiyo huku muda ukikaribia, tume ikawaita wadau na kuwaambia kuwa zoezi limesogezwa mbele ili kuvipatia vyama vya siasa muda wa kuandaa mawakala, hivyo litaanza Februari 23, mkoa mmoja pekee wa Njombe badala ya mikoa minne kama ilivyotangazwa awali.
“Tukawaambia mnasema tuwaandae mawakala wetu, tuwaandae kuhusu kufanya majukumu yapi hasa na hamtaki kutupatia nyaraka, bado wakaendelea kutoelewa. Tukawaomba hata ratiba ya mkoa huo mmoja bado hawakuweza kutupatia. Yaani ni ubabaishaji tu. Sisi tukaamua kupeleka watu wetu huko mkoa mzima kuanza maandalizi. Tayari tunavyozungumza tuna watu wako field.
“Katika hali ya kushangaza sana, jana tukapokea ratiba yao, wakaongeza maajabu mengine tena. Ratiba yao inaonesha kuwa hata mkoa mmoja wa Njombe pekee wameshindwa kuandikisha mkoa mzima badala yake wataanza na jimbo moja tu la Njombe Kaskazini. Katika jimbo hilo pia hawawezi kuandikisha kata zote kwa wakati mmoja badala yake wataanza na kata mji mdogo wa Makambako.
“Yaani wameshindwa mikoa minne, wakaamua mkoa mmoja, mkoa mmoja hawawezi kuandikisha wilaya zote, hata wilaya moja wameshindwa, wataanza na jimbo moja na katika jimbo hilo wataandikisha kata 12, sio zote kwa pamoja wataanza na kata 9 za mji mdogo wa Makambako, kisha zitafuata kata zingine. Hii ni aibu ya hatari,” amesema Mbowe na kuongeza;
“Yaani wakati mamilioni ya Watanzania wanasubiri kuandikishwa nchi nzima, NEC haiwezi hata kuandikisha wilaya moja kwa wakati mmoja. Halafu eti wameniandikia barua ya mwaliko kwenda Makambako kushiriki hafla ya uzinduzi utakaofanywa na Waziri Mkuu Pinda siku ya Jumanne ijayo, nawauliza viongozi wenzangu niende nisiende.
“Kwa sababu kwenda kwenye uzinduzi huo wa NEC utakaofanywa na Waziri Mkuu ni kubariki uhuni wote huu wanaoufanya.”
Serikali kufilisika, ukosefu wa vifaa vya BVR na kuchezea Sheria
Mwenyekiti Mbowe ameshusha tuhuma nzito kwa Serikali ya CCM akisema kuwa kushindwa kupatikana kwa vifaa vya BVR kwa muda unaotakiwa ili wananchi waanze kuandikishwa kunatokana na serikali hiyo kufilisika, kukosa vipaumbele, kuendekeza ufisadi na matumizi ya anasa huku pia ikilifanya zoezi la uchaguzi kuwa ni tukio la dharura badala ya mchakato wenye maelekezo ya kikatiba.
Alisema kuwa kugeuza uchaguzi kuwa tukio la dharura badala ya takwa la kidemokrasia lenye masharti ya kisheria ni kucheza na haki na matumaini ya Watanzania jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani ya nchi.
“Ili kuandikisha wapiga kura nchi nzima, NEC ilihitaji vifaa…wanaviita BVR kits vipatavyo 15,000 lakini Serikali ya CCM ikawaambia hapana wapunguze, wakapunguza hadi 8,000, katika hivyo 8,000 hadi sasa vipo 250 pekee tangu wakati wa uandikishaji wa majaribio. Hadi sasa vingine havijafika kwa sababu serikali haijalipia, haijalipa kwa sababu imefilisika.
“Pamoja na mazonge haya yote, juzi nimemsikia Mwenyekiti wa NEC, Jaji Lubuva akisema daftari hili hili watakaloandikisha litatumika kwenye Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, huyu mzee tunamheshimu sana lakini wamempatia kazi itakayoondoa heshima yake. Huyu ni mwanasheria, Jaji mstaafu. Sitaki kuamini kuwa hajui kuwa kuhakiki daftari kabla halijaanza kutumika ni hitaji la kisheria.
“Sheria inaagiza kwamba baada ya uandikishaji lazima wapiga kura wahakiki daftari lao kisha sasa ndipo tunapata daftari la kudumu la wapiga kura. Sasa kwa ratiba yao wanamaliza kuandikisha Aprili 29 na kesho yake Aprili 30 kura ya maoni inapaswa kupigwa, sasa sijui anataka kutumabia nini.
“Pamoja na kwamba sisi kama CHADEMA pamoja na wanachama wenzetu wa UKAWA tumewaomba Watanzania kutoshiriki kupiga kura ya maoni ya katiba ili wasitumike kuhalalisha mchakato haramu, lakini hatutakubali sheria ziendelee kuvunjwa tu waziwazi na akina Lubuva kwa sababu ya maelekezo ya ikulu huku NEC ikitumika tu kama kanyaboya,” alisema Mbowe.
Aliongeza kuwa serikali nyingi duniani hukaribisha machafuko na anguko lake kila zinapoanza kuchezea chaguzi mbalimbali. Alisema kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ulijulikana miaka 5 iliyopita kikatiba hivyo maandalizi yake hayawezi kuwa ya zimamoto au dharura.
Alisema sheria ya uchaguzi inaelekeza wazi kuwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linapaswa kuboreshwa mara mbili katikati ya uchaguzi mmoja hadi mwingine, lakini hata takwa hilo la kisheria pia limevunjwa na NEC ambayo imeshindwa kuboresha tangu ilipoandikisha mwaka 2010.
Alisema kuwa serikali inayojua wajibu wake kwa wananchi, ilipaswa kujua vipaumbele vya mwaka huu, ikitambua kuwa kuweka mambo makubwa matatu ndani ya mwaka mmoja, yaani; uandikishaji wapiga kura, kura ya maoni ya katiba mpya na uchaguzi mkuu, ni mambo ambayo haiwezi kumudu kuyatekeleza ndani ya muda mfupi, bila kuwa na fedha.
“Yaani wakati Watanzania wenye sifa wakisubiri nchi nzima, taifa zima linasubiri, katika sintofahamu hii, bado viongozi wetu wanathubutu kudanganya kuwa kura ya maoni itafanyika, huku Waziri Mkuu Pinda akienda kubariki mchezo huu keshokutwa huko Makambako. Hatujui wanapata wapi ujasiri huu wa kuwadanganya Watanzania,”amesema Mbowe.

HAWA NDO WASANII 12 WA KIBONGO AMBAO DIAMOND ANAWAZIMIA KINYAMA

People who inspired me... These are the people who INSPIRED me alot in my Music world...they played such a big part in my dreams... jus One word to them "I appreciate" ( Hawa ndio watuwalionifanya nitamani sana nami kuwa Mwanamziki.. Walikuwa na nafasi kubwa sana katika Ndoto zangu... Neno Moja tu kwao "Nawaheshim sana" )


Embedded image permalink 

Saturday, February 21, 2015

KIONGOZI WA VIJANA WA JKT WALIOTISHIA KUANDAMANA YAMKUTA YA ILIMBOKA, ATEKWA, APIGWA NA KUTUPWA PORINI

Dar es Salaam. Utata umezingira suala la kijana George Mgoba, ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) baada ya habari kuwa alitekwa na baadaye kutupwa kwenye Msitu wa Pugu, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar es Salaam lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa, kupigwa na kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo hospitalini hapo kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa maelezo mengi.
Mgoba amekuwa akihamasisha vijana wenzake waliohitimu ya JKT kukusanyika jijini Dar es Salaam na kuandamana hadi kwa Rais ili kumweleza masikitiko yao ya kutopatiwa ajira baada ya kumaliza mafunzo kama walivyoahidiwa wakati wakienda kwenye kambi za jeshi hilo.
“Ndio aliletwa hapa majira ya saa 10:30 akitokea Hospitali ya Amana,” alisema ofisa uhusiano wa MHN, Aminiel Aligaeshi.
“Lakini waganga walipotaka kumtibu alikataa kwa sharti kwamba atibiwe wakati ndugu zake wakiwapo. Ndugu zake walipofuatwa nje, hawakuonekana. Anaonekana ana maumivu sehemu ya mgongoni na anapumua kwa shida.”
Habari zinasema kuwa kuanzia saa 1:00 jioni madaktari walikuwa wakijaribu kumshauri akubali kutibiwa, lakini akakataa na hivyo kuwalazimu madaktari kumtaka asaini fomu ya kukataa matibabu. Hata hivyo hadi saa 2:00 usiku hakuwa amesaini.
Kijana huyo anasemekana kutekwa juzi jioni na watu ambao hawajajulikana na aliokotwa na msamaria mwema ambaye baadaye aliungana na watu wengine kumpeleka Hospitali ya Tumbi.
Hata hivyo, aligoma kutibiwa kwenye hospitali hiyo akitaka ndugu zake wawepo.
Habari zinasema baadaye alisafirishwa kuhamishiwa Hospitali ya Amana kabla ya kuhamishwa tena na kwenda Muhimbili jana saa 9:00 alasiri.
Mfanyakazi mmoja wa Hospitali ya Amana aliiambia gazeti hili kuwa kabla ya askari wa Jeshi la Polisi kumfuata na gari mbili aina ya Land Rover, kundi la vijana wanaosadikiwa kuwa ni wahitimu wa mafunzo ya JKT, liliwasili Amana na kutaka kushinikiza kumchukua Mgoba, lakini uongozi uliwakatalia kwa maelezo kuwa wangetoa ruhusa hiyo kama wangekuwapo ndugu zake.
Alivyotekwa
Mwandishi wetu kutoka Kibaha anaripoti kuwa kijana huyo, anayejielezea kuwa ni mtetezi wa vijana waliohitimu JKT, aliokotwa kwenye kichaka kilichopo Picha ya Ndege mjini humo akiwa amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwiliniKwa mujibu wa mwandishi wetu, kijana huyo aliokotwa asubuhi ya Februari 19 na msamaria mwema ambaye hakutaka jina lake akiwa kwenye kichaka hicho kilicho jirani na baa ya River Road na Shule ya Sekondari ya Tumbi.
Alisema wakati msamaria huyo akipita karibu na kichaka hicho alisikia sauti ya mtu akigugumia na ndipo alipoenda kichakani na kumkuta Mgoba akiwa amefungwa kamba miguuni huku akionekana kuwa na maumivu makali.
Msamaria huyo alisema alipomhoji kilichompata, kijana huyo alimwambia anahisi amepigwa na mhusika wa ajira za JKT kwa sababu alipigiwa simu na mtu anayemfahamu kuwa akafuate majibu ya maombi yake na akiwa njiani alipishana na watu wawili na ghafla alihisi kulewa na baadaye kupoteza fahamu hadi mtu huyo alipomzindua.
“Wakati nashangaa, watu wengine waliokuwa wakipita hapo na baadhi ya waliokuwa wakipata huduma mbalimbali kwenye baa hiyo, nao walisogea jirani tulikokuwa na tukakubaliana tutoe taarifa polisi na askari kweli walifika na gari na kumchukua hadi kituoni cha Polisi cha Tumbi,” alisema msamaria huyo.
Alieleza kuwa baadaye walichukua maelezo ya kijana kisha akapelekwa hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Wakati tukio hilo likiendelea, ndipo taarifa zikaanza kusambaa katika maeneo kadhaa ya mji wa Kibaha zikieleza kuwa kiongozi wa vijana waliohitimu JKT nchini, amelazwa Tumbi baada ya kupigwa.
Taarifa hizo zilisababisha vijana kadhaa wanaodaiwa kuhitimu JKT, ikiwamo kambi ya Ruvu kufika hospitalini hapo kwa lengo la kumjulia hali mwenzao.
Taarifa zilizopatikana ndani ya hospitali hiyo zimeeleza kuwa kazi ya kutoa huduma ya kwanza kwa Mgoba ilikuwa ngumu kwa madaktari kutokana na kwanza majeruhi mwenye kuwa anachunguza kila kitu alichokuwa anafanyiwa, na pili kusisitiza kuwa hayupo tayari kuchomwa sindano wakati huo hadi hapo watakapofika ndugu zake.
“Ni kweli kama unavyosema huyu kijana kweli hata mimi nilikuwa nashangaa alivyokuwa msumbufu, maana ukichukua tu bomba la sindano anahoji hiyo sindano ya nini, nikamwambia tulia tunakutibu. Nilishangaa alinisihi nisimchome sindano, bali nifanye usafi wa majeraha,” alisema daktari mmoja ambaye pia hakutaka jina lake litajwe.
Aliendelea kusema kuwa kama tiba ni muhimu kwa wakati huo, basi aruhusiwe aende nyumbani akatibiwe huko na kwamba hadi wakati huo hakujua kuwa majeruhi huyo ni Mgoba.
Taarifa za uhakika zinabainisha kuwa majeruhi huyo alifikia wodi ya wagonjwa wa dharura na alifanyiwa vipimo mbalimbali, ambavyo vilionyesha kuwa hakuwa madhara makubwa ndani ya kichwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na akamtaka mwandishi kuwasiliana na msemaji wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni.
“Nakuambia mimi sijui kama huyu ni mwenyekiti wa vijana waliohitimu wa JKT, bali ninachoweza kukuambia ni kwamba kweli kijana huyo aliokotwa katika kichaka Picha ya Ndege na kama ilivyo ada tulimpeleka Tumbi akapate tiba kwanza kama ilivyo kwa majeruhi wengine, kwa hiyo suala ya yeye kusema yupo kwa ajili ya kuwatetea vijana wenzake waliopita mafunzo JKT ni jambo jingine. Amekuambia wewe mimi sijui… kama wewe unajua basi ni wewe,” alisema Matei.
Mbali ya baadhi ya vijana kutinga Tumbi wakati alipofikishwa hapo, pia taarifa hizo zilisababisha shughuli za biashara katika baadhi ya maeneo kusimama kwa dakika kadhaa ambapo watu walikuwa wakijikusanyika kuulizia ukweli wa suala hilo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Meshack Shimweta hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kuwa alikuwa nje ya ofisi.
Tukio la utekaji lilimtokea mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka mwaka 2012 wakati akiongoza mgomo wa matabibu hao kudai maboresho ya maslahi yao.
Ulimboka alichukuliwa na mtu mmoja kwenye klabu ya Viongozi Kinondoni na baadaye kupigwa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande ambako aliokotwa na msamaria mwema.
Katika hatua nyingine, Serikali imesema haikuwahi kuahidi kwamba kila anayepita Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) lazima apate ajira.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene alisema vijana hao walidai ajira Ikulu kwa kisingizio kwamba Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue aliahidi kupatiwa ajira alipokutana nao.
Mwambene alisema siyo nia ya Serikali kupeleka vijana JKT kwa lengo la kupata ajira ila kuwajenga kimaadili na uzalendo kwa nchi yao ili wawe raia wema.

Wednesday, February 18, 2015

RAIS KIKWETE APANGUA WAKUU WA WILAYA, WAPYA WAINGIA WENGINE WAACHWA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA FEBRUARY 18, 2015

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi. Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishirini na saba (27) zilizotokana na:
  1. Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3
  2. Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa Wakuu wa Mikoa
  3. Kupangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya 7; na
  4. Kutengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 12
Katika mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais amewateua Wakuu wapya wa Wilaya 27 ili kujaza nafasi hizo wazi.
Aidha, Wakuu wa Wilaya sitini na nne (64) wamebadilishwa vituo vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vya sasa.

Sunday, February 15, 2015

MATOKEO YA KIDATO CHA IV 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA IV 2014 YAMETANGAZWA



KWA MATOKEO YA SHULE ZOTE BOFYA HAPA  MATOKEO KIDATO CHA IV 2014


SHULE KUMI BORA

   JINA LA SHULE                                     MKOA
1. KAIZIREGE -----------------------------KAGERA
2. MWANZA ALLIANCE ----------------MWANZA
3. MARIAN BOYS------------------------- PWANI
4.St. FRANCIS GIRLS---------------------MBEYA
5. ABBEY-------------------------------------MTWARA
6. FEZA GIRLS-------------------------------DAR
7.CANOSSA-----------------------------------DAR
8. BETHEL SABS GIRLS-------------------IRINGA
9. MARIAN GIRLS---------------------------PWANI
10. FEZA BOYS-------------------------------DAR