Mkuu wa wilaya ya Manyoni ndugu Geoffrey
Idelphonce Mwambe (pichani kushoto) ameanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ya Manyoni (Manyoni
Development Fund). Mfuko huo ambao una lengo la kuwaunganisha wakazi wa Manyoni
unakusudia kujenga Shule za sekondari, hususani za Adavance, kutengeneza
madawati, kutatua kero ya maji, afya na maeneo mengine yatakayoonekana kuwa ni
muhimu kwa wakati husika.
Mfuko wa Maendeleo
ya Wilaya ya Manyoni ni endelevu na uchangiaji wake utakuwa ni wa wananchi wote
wa Manyoni na wadau wa maendeleo yetu. Mfuko unalenga kuwaunganisha
Wanamanyoni, kujenga Shule za Advanced, kuongeza madarasa, kutengeneza
madawati, kushugulikia matatizo ya maji na afya na maeneo mengine muhimu kwa
maendeleo ya haraka ya watu wetu.” Alisema mkuu huyo wa wilaya.
Mfuko huo umeanzishwa Agosti, 1 mwaka huu kwa
kuanza kuwakutanisha kundi la wafanyabiashara wa wilaya hiyo. Katika jitihada
zake za kuhakikisha mfuko huo unafanya kazi kwa ufanisi, Mkuu huyo wa wilaya
ameuchangia mfuko huo jumla ya tsh. Milioni, 15,000,000/= amabazo amechangiwa
na waliokuwa watumishi wenzake wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa
Afrika Mashariki.
Akizungumzia hili Bwana Mwambe alisema, “…niliitisha kikao na wafanyabiashara wa
Manyoni ambapo nimeanzisha Mfuko huu na kuanza kwa kuwachangia watu wa Manyoni
jumla ya Sh.15,000,000/= (Shilingi Milioni Kumi na Tano tu) ambazo nimechangiwa na Watumishi wenzangu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.”
Aidha mkuu wa wilaya aliwashukuru wakazi wa
manyoni hususani wafanyabiashara hao kwa mwitikio wan a kumuunga mkono katika
uanzishwaji wa mfuko huo. Katika harambee iliyofanyika siku hiyo ya Agosti 1,
jumla ya tsh. Million 4,500,000/= zilichangwa hapo hapo na wafanyabiashara hao
na hivyo kuufanya mfuko kuwa na jumla ya tsh. 19,500,000/=
Mkuu wa wilaya anawakaribisha watu wote wenye
mapenzi mema na wanamanyoni wote kokote walipo kuunga mkono jitihada hizi kwa
ajili ya maendeleo ya Manyoni na watu wake.
“Naomba
niwakaribishe watu wote wenye mapenzi mema na hususan Wanamanyoni kokote mliko
tushirikiane kuijenga Manyoni mpya”amesema mkuu huyo wa Wilaya bwana Geoffrey
Idelphonce Mwambe.
Aliongeza kuwa watu wote wenye mapenzi mema
kuchangia kwa kutuma michango yao kupitia akaunti namba 50710006932. Taarifa za
akaunti hiyo kama ilivyotolewa nay eye mwenyewe ni:
Jina la Akaunti: Manyoni Development Fund Akaunti Namba: 50710006932
Jina la Benki: NMB
Tawi la Benki: Manyoni
Aidha unaweza kuwasiliana na mkuu wa wilaya huyo
kuhusu mfuko huo na namna ya kuchangia kwa simu Simu: 0784509891 na barua pepe, mwambe.geoffrey@yahoo.com
Maoni ya wananchi
Wananchi wengi wamepongeza jitihada hizi za Mkuu
wa Wilaya. “Kama mkuu huyu atapewa ushirikiano wa kutosha, kweli naiona Manyoni
mpya.” Alisema bwana Issihaka Mashaka mkazi wa wilaya hiyo.
Aidha mfanya biashara ambaye hakutaka jina lake
litajwe alisema kuwa, “…mambo kama haya
tulitarajia yafanywe na mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi. Kuona mkuu wa
wilaya, tena mtu wa kuja tu ameteuliwa na rais anakuwa na jitihada kama hizi Wanamanyoni
tuna bahati sana. Sisi wafanyabiashara tutamuunga mkono.”
“Kwa
kipindi kirefu Manyoni tumekosa viongozi wabunifu haina hii. Nawashauri viongozi
wengine katika wilaya hii waige mfano wa Mwambe.” Aliongeza mkazi mwingine
wa wilaya hiyo.
Wakazi wengi wameshauri pia ili watu waweze
kuchangia vizuri, mfuko huo unatakiwa kutangazwa sana lakini pia kuongeza njia
nyingine za kuchangia kama vile kutumia mitandao ya simu na kuongeza akaunti za
benki yingine kama ya CRDB ili iwe rahisi kwa kila mtu kuchangia.
Mwandishi anapatikana kwa namba zifuatazo:
0755440699
0715335558