Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Thursday, August 4, 2016

MKUU WA WILAYA YA MANYONI AJA NA MPYA. WENGI WAMUUNGA MKONO. WAIONA MANYONI MPYA INAKUJA

Na Furaha Venance-Manyoni
Mkuu wa wilaya ya Manyoni ndugu Geoffrey Idelphonce Mwambe (pichani kushoto) ameanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ya Manyoni (Manyoni Development Fund). Mfuko huo ambao una lengo la kuwaunganisha wakazi wa Manyoni unakusudia kujenga Shule za sekondari, hususani za Adavance, kutengeneza madawati, kutatua kero ya maji, afya na maeneo mengine yatakayoonekana kuwa ni muhimu kwa wakati husika.

Mfuko wa Maendeleo ya Wilaya ya Manyoni ni endelevu na uchangiaji wake utakuwa ni wa wananchi wote wa Manyoni na wadau wa maendeleo yetu. Mfuko unalenga kuwaunganisha Wanamanyoni, kujenga Shule za Advanced, kuongeza madarasa, kutengeneza madawati, kushugulikia matatizo ya maji na afya na maeneo mengine muhimu kwa maendeleo ya haraka ya watu wetu.” Alisema mkuu huyo wa wilaya. 

Mfuko huo umeanzishwa Agosti, 1 mwaka huu kwa kuanza kuwakutanisha kundi la wafanyabiashara wa wilaya hiyo. Katika jitihada zake za kuhakikisha mfuko huo unafanya kazi kwa ufanisi, Mkuu huyo wa wilaya ameuchangia mfuko huo jumla ya tsh. Milioni, 15,000,000/= amabazo amechangiwa na waliokuwa watumishi wenzake wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Akizungumzia hili Bwana Mwambe alisema, “…niliitisha kikao na wafanyabiashara wa Manyoni ambapo nimeanzisha Mfuko huu na kuanza kwa kuwachangia watu wa Manyoni jumla ya Sh.15,000,000/= (Shilingi Milioni Kumi na Tano tu) ambazo nimechangiwa na Watumishi wenzangu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.”
 
Aidha mkuu wa wilaya aliwashukuru wakazi wa manyoni hususani wafanyabiashara hao kwa mwitikio wan a kumuunga mkono katika uanzishwaji wa mfuko huo. Katika harambee iliyofanyika siku hiyo ya Agosti 1, jumla ya tsh. Million 4,500,000/= zilichangwa hapo hapo na wafanyabiashara hao na hivyo kuufanya mfuko kuwa na jumla ya tsh. 19,500,000/=
Mkuu wa wilaya anawakaribisha watu wote wenye mapenzi mema na wanamanyoni wote kokote walipo kuunga mkono jitihada hizi kwa ajili ya maendeleo ya Manyoni na watu wake.
Naomba niwakaribishe watu wote wenye mapenzi mema na hususan Wanamanyoni kokote mliko tushirikiane kuijenga Manyoni mpya”amesema mkuu huyo wa Wilaya bwana Geoffrey Idelphonce Mwambe.

Aliongeza kuwa watu wote wenye mapenzi mema kuchangia kwa kutuma michango yao kupitia akaunti namba 50710006932. Taarifa za akaunti hiyo kama ilivyotolewa nay eye mwenyewe ni:
Jina la Akaunti: Manyoni Development Fund
Akaunti Namba: 50710006932
Jina la Benki: NMB
Tawi la Benki: Manyoni

Aidha unaweza kuwasiliana na mkuu wa wilaya huyo kuhusu mfuko huo na namna ya kuchangia kwa  simu Simu: 0784509891 na barua pepe, mwambe.geoffrey@yahoo.com

Maoni ya wananchi
Wananchi wengi wamepongeza jitihada hizi za Mkuu wa Wilaya. “Kama mkuu huyu atapewa ushirikiano wa kutosha, kweli naiona Manyoni mpya.” Alisema bwana Issihaka Mashaka mkazi wa wilaya hiyo.

Aidha mfanya biashara ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa, “…mambo kama haya tulitarajia yafanywe na mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi. Kuona mkuu wa wilaya, tena mtu wa kuja tu ameteuliwa na rais anakuwa na jitihada kama hizi Wanamanyoni tuna bahati sana. Sisi wafanyabiashara tutamuunga mkono.” 

Kwa kipindi kirefu Manyoni tumekosa viongozi wabunifu haina hii. Nawashauri viongozi wengine katika wilaya hii waige mfano wa Mwambe.” Aliongeza mkazi mwingine wa wilaya hiyo.

Wakazi wengi wameshauri pia ili watu waweze kuchangia vizuri, mfuko huo unatakiwa kutangazwa sana lakini pia kuongeza njia nyingine za kuchangia kama vile kutumia mitandao ya simu na kuongeza akaunti za benki yingine kama ya CRDB ili iwe rahisi kwa kila mtu kuchangia.

Mwandishi anapatikana kwa namba zifuatazo:
0755440699
0715335558

No comments:

Post a Comment