Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Wednesday, April 11, 2018

VIDEO--MAGUFULI AMWAMBIA KIKWETE HATAONGEZA HATA DAKIKA 1 MADARAKANI MUD...


UTAFITI ULIWAHI KUBAINI KUWA WATANZANIA WANA IQ NDOGO.

Image may contain: 2 peopleKada wa CCM ajulikanae kwa jina Thadei Ole Mushi ameandika hivi kuhusiana na uwezo wa kufikiri kati ya Watanzania, Wakenya na Waganda. Soma makala haya kisha shusha comment yako chini unakubaliana nae kwa asilimia ngapi?

Na Thadei Ole Mushi.
Kuna utafiti uliwahi kusema kuwa sisi watanzania tuna IQ ndogo kuliko nchi zote za Afrika mashariki. Walidai kwenye swala la Abstract reasoning ni wa mwisho kabisa...... na concur observation hiyo hebu ona:- 

#Nchini Kenya:- Wananchi wanafuatilia kwa karibu sana Mijadala inayoendelea Bungeni na mijadala iliyopo viral ni swala la Ajira kwa vijana, Kilimo na Uwekezaji. Wananchi wanajadili kila kona yanayoendelea Bungeni tafsiri yake ni kuwa Bunge linapata uhai nje na ndani. Wananchi wanaongeza pressure kwenye mambo ya msingi.

Kiuchumi huku njee wanajadili uwekezaji mkubwa wa uanzishwaji wa viwanda vya kuassemble magari vinavyotaka kuanza kujengwa Nchini humo. Nafikiri hata Sisi Watanzania tumejikuta tunatekwa na mijadala ya Kenya.

#Nchini Uganda:- Bunge linaendelea kilichoshika kasi huko ni Bajeti ya wizara ya Kilimo wananchi na wabunge wamengangania iongezwe. Wanajadili makubaliano ya Kilimo ya Msumbiji yafuatwe kama yalivyo. Wananchi wanalipa bunge pressure toka njee na kweli bunge linapata uhai.

#Tanzania:-Asilimia 95 hawajui ni mijadala gani inaendelea Bungeni. Hakuna pressure yoyote ya maana toka kwa wananchi inayoongeza value kwenye Bunge letu. Mwananch Communication wasiporekodi ka clip hatuwezi kujua ni mijadala gani mizito inayotakiwa wananchi waijengee attention na kuiongezea pressure kwa manufaa ya kitaifa.

Kilichobamba huku njee ni mama mtu Mzima kudai kuwa yeye ni Mtoto wa Lowassa taifa Zima limehamia kwenye mjadala huo.

Kila mpango na Sera ya nchi uwe mbovu au mzuri unapigwa mhuri na Chombo hiki. Ukishatoka Bungeni unakwenda kwenye utekelezaji. Huku njee tunajadili mambo mepesi sana.
Hii ndio Tanzania tuna tatizo la msingi mahali.....
Morning Tanzania ngoja tuingie mzigoni kulijenga Taifa.

Ole Mushi.
0712702602

Unakubaliana nae kwa asilimia ngapi?

KAMA WEWE NI MTUMISHI WA UMMA KUPATA SALARY SLIP YAKO YA KILA MWEZI ONLINE