Umoja wa Mataifa Jumatano umetaja mataifa 38 "yanayo aibisha"
yakiwemo China na Russia kwa kile walichodai kuwa ni ulipizaji kisasi au
vitisho dhidi ya wale wanaoshirikiana na umoja huo kwa ajili ya
kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu.
Miongoni mwa unyanyasaji ulotajwa ni pamoja na mauaji, mateso na kukamatwa kiholela kwa watu hao.
Ripoti ya kila mwaka iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UN Antonio
Guterres imetaja pia kuwepo na kampeni kuwafuatilia, kuwatendea maovu,
na kuwaaibisha hadharani watetezi wa haki za binadam na waathiriwa.
Mataifa hayo 38 yanajumuisha 29 yenye kesi mpya na mengine 19 yakikabiliwa na kesi zinazoendelea.
Ripoti inaeleza kwamba mataifa mengi yanadaiwa kuwafungulia mashtaka
wanaharakati wa haki za binadamu kwa ugaidi au kushirikiana na mataifa
ya kigeni kuhujumu hadhi na usalama wa taifa, ikiwa ni njia ya
kuwatishia wasiendelee kushirikiana na UN katika uchunguzi huo.
Kesi hizo mpya zinazochunguzwa ziko Bahrain, Cameroon, China,
Colombia, Cuba, DRC, Djibouti, Misri, Guatemala, Guyana, Honduras,
Hungary, India Israel, Krygyszstan, Maldives.
Nyingine ni Mali Morocco, Myanmar. Ufilipino, Rwanda. Saudia Arabia,
Sudan Kusini, Thailand, Trinidad na Tobago, Uturuki, Turkmeni na
Venezuela.
Chanzo: VOA
No comments:
Post a Comment