Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Monday, July 13, 2015

KUMBE JINA LA MAKONGORO NYERERE LILITINGA KATIKA TANO BORA WATU WAKALIKATA. MWENYEWE ALALAMIKA

Tokeo la picha la makongoro nyerereAliyekuwa mmoja wa wagombea nafasi ya kuteuliwa na chama cha CCM ndugu Makongoro Nyerere ameibuka na kudai kuwa jina lake lilitinga katika tano bora ila kuna mkuda mmoja aliamua kulikata jina lake. Hayo yamesemwa leo hii na Makongoro mwenyewe kupitia akaunti yake ya facebook ameandika yafuatayo:

Nawashukuru sana wajumbe wa kamati ya maadili ya chama cha mapinduzi kwa kuniteua jina langu kuongoza katika team ya awali ya tano bora ya wagombea urais kupitia chama cha mapinduzi. Walitenda haki. Mungu awabariki sana. Namhurumia sana na namsamehe 70 x 7 aliyelikata jina langu katika tano bora ya wagombea urais kupitia CCM bila ya kutoa hata sababu moja kutoka kinywani mwake. Namuomba sana mwenyezi Mungu pia amsamehe. Ramadan Karim.

Unaweza ingia hapa katika akaunti yake kusoma zaidi Charles Makongoro Nyerere

No comments:

Post a Comment