Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Blog ya kijanja kwa ajili ya watu wajanja

Saturday, December 10, 2016

RAIS MAGHUFULI AKUTANA NA MMILIKI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE. HAYA NDIYO WALIYOKUBALIANA...


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
                                  OFISI YA RAIS,
                                               IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
                   11400 DAR ES SALAAM,
                                         TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Rais Magufuli amesema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu  ambao  walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.
''Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema Rais Magufuli.
Dokta Magufuli amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia  kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43  kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora  kuliko kuagiza nje.




Katika kuthibitisha hilo,  tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi  ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya  Tanzania  na kamwe hana  nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Katika hatua nyingine Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wengine walioapishwa na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa  Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).

Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.
10 Desemba, 2016.

Video hapa chini


Friday, December 9, 2016

DARASA KATIKA WIMBO WAKE NI KAMA ANAWACHANA DIAMOND NA KIBA

                           Darasa                                                          Alikiba                                           Diamond

Na. Furaha Venance

1.  Darasa anaanza kuwaponda wasanii ambao wanakomaa katika game lakini mambo yamekuwa magumu kwao. Anawaambia:

Rudi utotoni,
Usipotembea utabebwa mgongoni.

Hapa anawazungumzia wasanii ambao walipata kiki kwa kubebwa na media (kumbuka anayebebwa ni Mtoto). Hivyo anawataka warudi enzi hizo za kubebwa au wawatafute watu wa kuwabeba.

2.      Diamond ni msanii ambaye anajisifu sana kuwa yeye ndiye msanii anayelipwa zaidi kuliko msanii yoyote Bongo, ndiye msanii mwenye nyumba Sauz, ndiye msanii pekee anayelipa kodi zaidi ya mil/ 30 TRA. Mashakibiki wa muziki wanamuonma kama ni msanii mwenye sifa sana na ni kama ameota mapembe kutokana na misifa yake. Darasa anamwambia:

 Wanaoota mapembe waongezee mkia.

3.      Kiba na Diamond wanajisifu kuwa wao ni wakali hadi kufikia kujifananisha na wanyama, Diamond anajiita Mnyama, Simba huku mashabiki wa Kiba wakimwita mfalme huyo Tembo. Darasa anawambia:
Blah blah sitaki kusikia,
siyo Simba, siyo Chui,
siyo mamba, haaha ”

Akiwa na maana kwake hakuna cha samba, chui wala mamba wote hao anawameza ndiyo maana anamalizia na kibwagizo “Haaaaa!” (kumeza).

4.      Diamond ni msanii anayesifika kwa mashauzi, kujigamba n.k. yemwenyewe anajiita mswahili wa uswahilini hasa. Darasa anamwambia:

Pumzi yangu inatosha kujigamba,
Na sina maneno ya kwenye kanga

Hapa anamaana kuwa kazi (pumzi) zake zinatosha kujigamba wala hana maneno ya kwenye kanga (maneno ya uswahili).

5.      Diamond ni msanii anayemiliki wasanii kadha wa kadha. Miongoni mwao kuna Richmavoko, Raymond, Harmonize na Queen Darlin. Kati ya wasanii hawa Harmonize ameonekana kuzua kizaazaa. Wapo wanamuona hatafika mbali, kutokana na kukosa ubunifu wake na kumuiga zaidi Diamond katika muziki hadi maisha yake binafsi. Sasa hapa ni kama Darasa anamuonya Diamond:

Kuzaa unawe kuzaa kizaazaa,
Sinzia na fegi uchome kibanda. 

Akiwa na maana Diamond ni kama amemzaa Harmonize lake badala yake amezua kizaa, akiendelea kumkumbatia (sinzia na fegi) anaweza ua WCB (choma kibanda).

6.     Wapo wanasema kuwa WCB chini ya Diamond hawafanyi muziki zaidi ya kufanya usanii usanii tu. Miongoni wa wasanii wanaosema hivi ni Ommy Dimpoz na Team Kiba. Darasa ni kama anaungana nao na kumwambia Diamond:

Maisha na muziki,
acha maneno weka muziki.

7.  Kwa sasa bila ubishi Diamond ndiye msanii aliyejuu. Huku Kiba akikimbizana kuhakikisha anamshusha msanii huyo. Sasa kaja Ommy Dimpoz naye anataka kuchuana, kukimbizana na Diamond ambaye anaonekana amewaacha, sasa Darasa anawambia wasanii hawa:

Unataka kukimbia na hauna break,
what do you expect?

Hapa ni sawa na kuwaambia wanataka kushindana wakati hawana mbinu za ushindani. Muziki ni kuwekeza mkwanja, ubunifu na kipaji ili ufike unapotaka.

8.     Diamond ni msanii anayesemwa kuwa anajifanya mjuaji sana, mademu anawajua yeye, muziki anajua yeye, maisha anayajua yeye yaani kila kitu anajua yeye. Sasa kuhusu madem, Darasa anamwambia:

Watch yourself, usije ukaji-comfuse…
Vitu vingine havitakagi ujuaji,
utajikuta unatandikia watu jamvi.”

Hapa ni kama anamwambia kungonoka na madem wa kila aina haitaki ujuaji asijejikuta anaaga dunia kwa ngoma. Si unajua tena mtu akifariki kinachofuata ni kutandika majamvi msibani! (pia inaweza kuwa kuwapa watu maneno ya kusema na kukukalia kitako kukusema).

9.  Kuna hili linasemwa na teamkiba hasa Ommy Dimpoz kuwa wapo wasanii wanaonunua views youtube ili ionekana nyimbo zao zinabamba. Hapa ni kama alikuwa analengwa Diamond na timu yake. Lakini hili ni kama watu hawajalielewa kwa maana kwamba Ommy hajaeleweka. Sasa Darasa anawaona watu wasioelewa hili ni kama machizi vile. Anamwambia Ommy na teamkiba, “Kumuelewesha chizi utajipa kazi.” Anaendelea kuwaambia wasanii kupata views nyingi wafunge mkanda, wakaze kamba, kwa maana ya kutoa ngoma kali. Au wafuate nyao za kununua views waone kama hawajachana msamba (kupotea kwenye game) kama asemavyo:

 Funga mkanda na kaza kamba,
Ama ufuate nyayo uchane msamba.

10.  Mwisho anazigeukia media na watu wanaotaka kuipoteza Hip Hip na wasanii wake. Anawambia:
Wanataka tupotee kwenye map,
tunapeleka game to the top top…
We don’t stop.

Huu ni mtazamo tu...inaweza kuwa si kweli
Mwl. Venance
0715 335558 (whatsapp) 
follow me instagram @fullraha17

Wednesday, December 7, 2016

AJIRA ZAMWAGWA SEKTA YA AFYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO TANGAZO LA KAZI MRADI WA AJlRA YA DHARURA KATlKA SEKTA YA AFYA 

uhuruggggggggggggggggg

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata kibali cha mpango wa Ajira ya dharura kwa wataalamu wa "fani za Tabibu na Wauguzi. Mpango huu utaendeshwa chini ya mradi, kwa ufadhili wa fedha za Mfuko wa CDC, Award No. 5U2GGH001062-03 kwa muda wa miaka miwili

Mradi utaajiri watumishi 192 ambao watapangiwa kufanyakazi kwenye halmashauri za wilaya 40 zenye uhaba mkubwa wa watumishi wa kutoa huduma za afya hasa kwa waathirika wenye virusi vya UKIMWI. Watumishi hawa watalipwa mishahara na stahiki nyingine kwa kufuata taratibu na kanuni za serikali. Watumishi wanaotakiwa ni Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant) 95 wenye ngazi ya Astashahada (Certificate in Clinical Medicine) na Wauguzi (Enrolled Nurses) 97 wenye ngazi ya Astashahada (Certificate in Nursing and midwifery). 

Wizara inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa watanzania wenye sifa zilizotajwa hapo juu, wawe na cheti cha kumaliza kidato cha nne pamoja na cheti cha taaluma aliyosomea kutoka kwenye chuo kinachotambuliwa na serikali. Barua ya maombi ioneshe wilaya ambayo mtumishi atapenda apangiwe kufanyakazi kati ya wilaya zilizopendekezwa hapo chini. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/12/2016

Maombi yote yatumwe kwa:- 

Katibu Mkuu 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, 
6 Samoral Machel Avenue, 
S.L.P 9083, 11478, Dar es Salaam. 
Tanzania 
05/12/2016


Orodha ya Halmashauri za Wilaya na idadi Watumishi waliopendekezwa.
Na.MkoaHalmashauri  (Wilaya)Tabibu WasaidiziWauguzi WasaidiziJumla
1Arusha1. Arusha CC336
2Dar es Salaam2. Ilala MC336
3. Kinondoni MC336
4. Temeke MC336
3Dodoma5. Dodoma MC235
4Geita6. Geita DC224
5Iringa7. Mufindi DC336
8. Iringa MC224
6Kagera9. Bukoba DC336
10. Muleba DC224
7Kigoma11. Kigoma Ujiji MC235
8Kilimanjaro12. Moshi DC336
9Lindi13. Lindi MC224
10Mara14. Musoma MC224
15. Rorya DC224
11Mbeya16. Chunya DC224
17. Kyela DC336
18. Mbarali DC224
19. Mbeya CC336
20. Mbeya DC336
21. Mbozi DC224
22. Rungwe DC224
12Morogoro23. Morogoro MC336
13Mwanza24. Nyamagana MC336
25. Sengerema DC224
14Njombe26. Njombe TC224
27. Wanging’ombe DC224
15Rukwa28. Sumbawanga DC224
29. Sumbawanga MC224
16Ruvuma30. Mbinga DC224
31. Songea MC224
17Shinyanga32. Kahama DC224
33. Kahama TC336
34. Shinyanga MC224
18Tabora35. Igunga DC224
36. Nzega DC224
37. Tabora MC336
19Tanga38. Korogwe TC224
39. Muheza DC224
40. Tanga CC336
Jumla9597192